240. MUGULYA MANUNHYIWA NEGELE

Imbuki ya kahayile kenako ilolile ilange lya namhala uyo alikomeleja b’ana b’akwe b’atumame milimo ya yabho na nguvu, kugiki bhadule gupandika jiliwa jingi, b’atizub’iza na gukob’eleja jiliwa ja gwisoleleja. Ijiliwa ijagwisoleleja jinijo jigalenganijiyagwa nijo jiganunhiyagwa na negele.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagafunyaga ilange lya wiza ukubhanhu bhabho. Ililange linilo ligenhaga ukubhanhu bhabho ikujo, bhukamu bho gutumama milimo, na nhungwa ya kudula gwikala na bhanhu chiza umuwikaji b’ob’o.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhalela abhanhu bhao chiza, kugiki bhadizupandika makoye gagugayiwa jiliwa aha kaya jabho. Akalele kenako kagub’inha matwajo mingi agagudula gub’eng’hela upandiki wingi umuwikaji b’ob’o. Kagub’ingija makoye gagwisoleleja jiliwa.

MTAKULA YANUSWAYO NUNDA

Chanzo cha msemo huo huangalia malezi ya mzee yule ahimizaye watoto wake kufanya kazi kwa nguzu, ili waweze kupata chakula kingi kiwezacho kuwaondolea mahangaiko ya kutafutiza chakula kwa kuokoteza. Hali hiyo ya kuhangaika kwa kuokoteza chakula, hufananishwa na chakula kinuswacho na nunda.

Msemo huo hulinganishwa kwa watu wale watoao malezi mema kwa watu wao. Malezi hayo huleta tabia njema ya kujitegemea, hekima, bidii ya kufanya kazi na ufahamu wa kuishi na watu vizuri, kwa watu wao. Malezi hayo huwaondolea watu wao mahangaiko ya njaa kwa sababu ya kukosa chakula.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwalea vyema watu wao ili waweze kujitegemea kwa kufanya kazi kwa bidii ya kutosha kuwapatia chakula na mahitaji yao yote yaliyoyalazima maishani mwao.

Malezi hayo yatawaletea watu wao maendeleo yakuweza kuziendesha vizuri familia zao maishani mwao. Watakuwa na bidii ya kufukuza njaa majumbani mwao kiasi cha kutosha kuepukana na vyakula vya kuokoteza huko na huko.

Mw 3: 17-19

Mw. 2:15.

badgers-negele6

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.