238. IHINDI HUKO IGAFUMILAGA IMYENDA NA B’AGAJA DUHU B’ALIHOI

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile myenda iyoigafumilaga b’uhindi. Imyenda yiniyo igab’egejiyagwa kunuko. Igab’ejiyagwa mingi kugiki abhanhu bhayigule b’ingi, nulu bhatanhanhile ugwiswala na yhingi isage iyo igashigaga mpaga kusi jingi.

Abhanhu abho bhalihanze ya si iyo igabheja myenda, bhagiganikaga giki, bhuli ng’wene iko igab’egejiyagwa imyenda, aizwalile iyimyenda yiniyo. Aliyo gashinaga nukwene bhalihoyi abho bhagasimizaga duuhu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ihindi huko igafumilaga imyenda nabho bhagajaga duuhu bhalihoyi.

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalimusi iyo ilina b’usab’i, na bhanhu bhayo abhakamu wa milimo bhalibhasab’i. Aliyo kihamo nubhusabhi bho si yiniyo, na bhabhab’i bhalihoyi.

Hangi lulu ulusumo lunuyo lugelenganijiyagwa ku likelesia, kunguno ung’wene jilihoi mbango ningi noyi, aliyo lulu, nabhanhu abho bhadinajo imbango jinijo, bhalihoi moyi.

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhukamu bho bhugub’utumila chiza ubhusab’i ubho bhulihoyi umusi yabho, nulu kubhiza na bhukamu bho gujichola imbango ijo jilihoyi umo bhali. Ubhukamu bhenubho bhugubhenhela matwajo mingi umuwikaji b’ob’o.

Mathayo 6:33

KISWAHILI: HINDI NDIKO ZITOKAKO NGUO NA WANDAO UTUPU (UCHI) WAPO

Chanzo cha methali hiyo chaangalia nguo ambazo hutoka hindi. Nguo hizo hutengenezwa huko kwa wingi ili kuwawezesha watu wengi kuzipata kwa kuzinunua, ikiwezekana kila mmoja azipate, na zingine kufikia hatua ya kuuzwa nje ya nchi.

Watu walioko nje ya nchi hiyo hufikiri kwamba, kila mmoja anavaa nguo kwenye nchi ile itengenezayo nguo hizo. Lakini kumbe, wapo watu watembeao uchi. Ndiyo maana watu husema kwamba, hindi ndilo zitokako nguo na waendao uchi wapo.

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu waishio ndani ya nchi yenye utajiri mwingi, na wenye bidii ya kuutumia utajiri huo, wamekuwa matajiri. Lakini pamoja na nchi hiyo kuwa na utajiri mwingi hivyo, waishio bila kupata mahitaji ya lazima yakiwemo yale ya nguo, chakula na malazi, wapo.

Zaidi ya hayo, methali hiyo hulinganishwa na Kanisa kwa sababu ndani yake kuna baraka na neema nyingi. Lakini pamoja na uwepo wa baraka hizo ndani yake, watu waishio bila baraka hizo wapo.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kuutumia utajiri uliomo ndani ya nchi yao vizuri, au kuwa na bidii ya kuzipata na kuzitumia baraka na neema zilizoko ndani ya Kanisa. Bidii hiyo itawawezesha kupata mafanikio mengi maishani mwao. “Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake na haya yote mtaongezewa” (Mathayo 6:33).

weaving clothes

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.