Sukuma

998. OB’ILE NANGI.

Akahayile kenako, kamhoyelile Nangi. UNangi ng’wunuyo ali munhu uyo agatumilaga bhuduja na b’umani bhokwe bho gubhalanga bhung’hana abhanhu bhakwe, kugiki bhadule gung’welelwa chiza. Uweyi alinangiji owiza kunguno agabhutumilaga ubhumani bhokwe bho bhubhalangila chiza abhanhu mpaga bhabhumana ubhunhana. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ob’ile Nangi.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agayilelaga chiza ikaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, ajimanile inhungwa ijawiza ijo abhalelelaga abhanhu bhakwe, kunguno ya bhumani bhutale ubho gulela bhanhu ubho alinabho bhunubho. Uweyi agabhambilija bhanhu bhingi ugwikala na nhungwa jinijo ijawiza, kunguno ya guwikalana chiza ubhunhana ubho agabhulangaga bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nangi uyo obhalangaga chiza abhanhu bhakwe, kunguno nuweyi agabhalangaga nhungwa jawiza abhanhu bhakwe bho gujikalana chiza, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, “ob’ile Nangi.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gub’iza ni lange lya nhungwa jawiza ukubhanhu bhabho, bho gujikalana chiza umukikalile kabho, kugiki bhadule kujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Yohana 3:1-21.

Yohana 3:31-36.

Mathayo 18:6.

Mathayo 5:17-20.

KISWAHILI: AMEKUWA MWALIMU.

Msemo huo, humwongelea Mwalimu. Mwalimu huyo ni mtu yule ambaye huutumia uwezo na uelewa wake kwa kuwafundisha watu wake ili waweze kumwelewa vizuri. Yeye ni mwelekezaji mzuri wa watu kwa sababu ya kuutumia ufahamu wake wote kwa kuwaelewesha vizuri watu hao mpaga wanauelewa ukweli huo anaoufundisha. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “amekuwa mwalimu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huilea vizuri familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, anayaelewa maadili mema ambayo huwalelea watu wake, kwa sababu ya ufahamu wake huo mkubwa wa kulea watu. Yeye huwasaidia watu wengi katika kuyaishi maadili hayo mema kwa kuuishi ukweli wa yale anayoyafundisha, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule mwalimu aliyewafundisha vizuri watu wake, kwa sababu naye huwafundisha watu maadili mema kwa kuyaishi vizuri yeye mwenyewe, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “amekuwa mwalimu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na maadili ya kuwalea vizuri watu wao, kwa kuyaishi vizuri maadili hayo, katika maisha yao, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

Yohana 3:1-21.

Yohana 3:31-36.

Mathayo 18:6.

Mathayo 5:17-20.

kenya-school

teacher-

ENGLISH: HE HAS BECOME A TEACHER.

The above saying refers to a teacher. The teacher is the one who uses his abilities and understanding for teaching his people so that they can well understand him. He is a good guide to those whom he teaches because he uses all his understandings for making that people know the truth which he is teaching. That is why people say to him that, “He has become a teacher.”

This saying is equated to a man who raises his family well in his life. He understands the good values ​​that he nurtures his people, because of his great understanding ways of fostering people. He helps many people in living according to the good values ​​enough by practicing the truth of what he teaches to the daily lives.

This man is like the teacher who taught his people well, because he also teaches people good manners by living well with them in his life. That is why people say to him that, “He has become a teacher.”

This saying teaches people about maintaining the values of their societies for ​​ taking good care of their people, by living according to those values in their lives, so that they can nicely raise their families well in their societies.

John 3: 1-21.

John 3: 31-36.

Matthew 18: 6.

Matthew 5: 17-20.

997. KALAGU – KIZE. NINA NG’WEJI MUGATI YA JISEME – MAB’ELE.

Ikalagu yiniyo ihoyelile mab’ele. Amab’ele geneyo gali gape, nulu igab’iza giti gagigengelekaga duhu, umugati ya jiseme. Agoyi gali gape guti ng’weji uyo gugejaga ibhujiku. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “nina ng’weji mugati ya jiseme – Mab’ele.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina ng’holo yape, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, alina ng’holo yape guti mab’ele kunguno nayo ili mugati ya mili go ng’wa munhu ng’wunuyo. Uweyi agamanyikaga kulwa kayombele kakwe na mito gakwe ayo galigawiza genayo, nulu ib’ize giti, ing’holo yakwe igelaga duhu, umuwikaji bhokwe.

Ing’holo ya ng’wa munhu ng’wunuyo, igikolaga na mab’ele ayo gali mujiseme, kunguno nayo iliyape iyo igikalaga mugati ya mili go ng’wa munhu uyo agiyolechaga bho gwikala chiza na bhanhu bhakwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu bhake higulya ya kubhiza na ng’holo jape kugiki bhadule gwikala chiza na bhanhu bhabho, bho kikalile kakwe kenako. Hunagwene agabhawilaga abhanhu bhakwe bhenabho giki, “nina ng’weji mugati ya jiseme – Mab’ele.”

Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’holo yape bho gwiyambilija gugamama wangu amakoye gabho na gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule gwikala chiza na gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Mathayo 25:34-35.

Wagalatia 6:10.

Yakobo 5:19-20.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

NINA MWEZI NDANI YA BAKULI – MAZIWA.

Kitendawili hicho, huongelea juu ya maziwa. Maziwa hayo ni meupe hata kama yakiwa gizani huonekana wazi ndani ya chombo yalimotiwa. Yenyewe ni meupe kama mwezi uangazao usiku. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “nina mwezi ndani ya bakuli – maziwa.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana moyo mweupe kama mazima, katika maisha yake. Mtu huyo, ana moyo mweupe ndani ya mwili wake, kama maziwa yaliyotiwa ndani ya bakuli, ambao huonekana kwa sababu ya wenyewe kumwezesha mtu huyo kutenda mema kwa wenzake. Yeye hujulikana kwa njia kutenda matendo yake mema yaangazao gizani, kwa sababu huwa yanatoka kwenye moyo wake huo mweupe, maishani mwake.

Moyo wa mtu huyo, hufanana na yale maziwa yaliyomo kwenye bakuli, kwa sababu nao ni mweupe uliyomo ndani ya mwili wa mtu ambao hujionesha kwenye maisha mema ya mtu huyo aishiye vizuri na wenzake. Yeye huwafundisha watu wake juu ya kuwa na moyo huo mweupe, ili waweze kuishi na watu vizuri, kwa njia ya maisha yake. Ndiyo maana huwaambia watu wake hao kwamba, “nina mwezi ndani ya bakuli – maziwa.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na moyo mweupe kwa kusaidiana katika kuyatatua matatio yao, na kufanya kazi zao vizuri, ili waweze kuishi vizuri na kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Mathayo 25:34-35.

Wagalatia 6:10.

Yakobo 5:19-20.

 

milk-2

milk-23

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

I HAVE A MOON INSIDE A BOWL – MILK.

This riddle talks about some milk. This milk is white in color even if it is in the dark it is clearly visible inside the container. It is as white as the moon at night. That is why people tell each other that, “I have a moon inside a bowl – milk.”

This puzzle is compared to the person who has a white or good heart in his life. This person has a white heart in his body like milk that has been poured into a bowl, which can be seen because of doing good deeds to his fellows. He/she is known for his good deeds that shine in the dark because they come from his white or clean heart in his life.

The heart of this person is like some milk which is in a bowl, because he also has white or clean heart in his body which is seen in living good life with his colleagues. He teaches his people about having that pure heart, so that they can live well with others in their lives. That is why he tells his people that, “I have a moon inside a bowl – milk.”

This riddle teaches people on how to be pure in heart by helping each other enough to solve their problems, so that they can live well to the point of achieving more successes in their lives.

Matthew 25: 34-35.

Galatians 6:10.

James 5: 19-20.

996. IGUSHAGE NA MUNHU O JIKOLO, UDIZIGUSIJA JIKOLO.

Ulusumo lunulo, luhoyelile higulya ya wigusija bho jikolo na wigusha na munhu ijikolo. Umunhu uyo agigushaga na munhu o jikolo agapandikaga bhuyeji uweyi kihamo nuyo alinajikolo ng’wunuyo, bho gongeja masala gagusab’ila.

Aliyo lulu, umunhu uyo agigusijaga jikolo agajib’ipyaga na gujimala bho gujitumamila sagala, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agapandikaga makoye ga guhab’ika kunguno ya kujigusija sagala ijikolo jakwe jinijo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “igushage na munhu o jikolo, udizigusija jikolo.”

Ulusumo lunulo, lugayombagwa kuli munhu uyo agajikenagulaga bho gujitumila sagala ijikolo jakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajib’ipyaga ijikolo jakwe bho gujigusija sakala na gujigulila maginhu ayo gadina solobho yoseyose, kunguno ya gugayiwa masala na witegeleja bho katumamilile ka sabho jakwe jinijo. Uweyi agajimalaga gujib’ipya na gujikenagula sagala isabho jakwe jinijo kunguno ya gujigusija sagara chiniko, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agajimala gujigusija sagala ijikolo jakwe, kunguno nu weyi agajimalaga isabho jakwe bho gujigusija sagala umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “igushage na munhu o jikolo, udizigusija jikolo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na masala ga gujilang’hanila chiza isabho jabho bho gujitumamila na witegeleja bhutale, kugiki jidule gubhambilija chiza, umuwikaji bhobho.

Mathayo 19:-23-24.

Luka 15:11-13.

KISWAHILI: CHEZA NA MTU MWENYE MALI, USICHEZEE MALI.

Methali hiyo, huongelea juu ya uchezeaji wa mali na kucheza na mtu mwenye mali. Mtu yule ambaye hucheza na mtu mwenye mali hupata furaha ya kujifunza namna ya upataji wa mali wakiwa pamoja na mwenye mali hizo.

Lakini mtu achezeae mali huziharibu na kuzimaliza kwa kuzitumia hovyo katika maisha yake. Mtu huyo, hukumbwa na tatizo la umaskini kwa sababu ya kuzichezea hovyo mali zake hizo. Ndiyo maana watu humuonya kwa kumwambia kwamba, “cheza na mtu mwenye mali, usichezee mali.”

Methali hiyo, hutumiwa kwa mtu yule ambaye huiharibu mali yake kwa kuitumia hovyo, katika maisha yake. Mtu huyo, huviharibu vitu vyake hivyo kwa kuzichezea hovyo kwa sababu ya kukosa akili ya umakini katika matumizi ya mali zake hizo. Yeye huzimaliza mali zake hizo, na kukumbwa na tatizo la umaskini kwa sababu ya kuzichezea hovyo mali zake hizo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyevimaliza vitu vyake kwa kuvichezea hovyo, kwa sababu naye huzimaliza mali zake kwa kuzichezea hovyo, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “cheza na mtu mwenye mali, usichezee mali.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na akili ya kuwawezesha kuzitunza mali zao kwa kuzitumia wakiwa na umakini mkubwa, ili ziweze kuwasaidia vizuri, maishani mwao.

Mathayo 19:-23-24.

Luka 15:11-13.

guitar-1

zulu-youths-

ENGLISH: PLAY WITH SOMEONE WHO HAS WEALTH BUT DO NOT PLAY WITH WEALTH.

The overhead proverb speaks about playing with property and playing with a wealthy person. The person who plays with the person who owns the property finds joy of learning how to acquire the property from such owner of possessions.

Nonetheless a man who squanders his possessions destroys them as well as himself by misusing them in his life. This man, however, suffers from poverty because he wasted his resources. That is why people warn him by saying that, “play with someone who has wealth but do not play with wealth.”

This proverb is applied to the man who squanders his belongings by wasting them in his life. This man, in effect, destroys his possessions by playing with them carelessly because of a lack of common sense in usage of his belongings. He squanders his wealth to point of suffering from poverty because of finishing them in useless matters.

This person is like the one who squanders his possessions by playing with them, because he also squanders his wealth by his carelessness in taking care of them in his life. That is why people say to him that, “play with someone who has wealth but do not play with wealth.”

This proverb instills in people a clue on how to be intelligent enough to take care of their possessions by using them with great care, so that they can nicely help them in their lives.

Matthew 19: -23-24.

Luke 15: 11-13.

agriculture-

995. JA NG’WINIKILI JIGALIYAGWA NA NG’WENEJO.

Ung’winikili jikolo ali munhu uyo adebhile umo ujicholela isabho jinijo. Umunhu uyo agikalaga na jikolo jakwe agajilyagwa weyi bho nduhu uo gunemeja kunguno jili sabho jakwe. Uweyi agabhalemeja abho bhagamonelaga wilu umubhuli bho jikolo jakwe jinijo. Hunagwene agabhawilaga giki, “ja ng’winikili jigaliyagwa na ng’wenejo.”

Ulusumo lunulo, lugayombagwa kuli munhu uyo agabhabhonelaga wilu abhanhu abho bhagalyaga sabho jabho. Umunhu ng’wunuyo, alina nhungwa ja gubhakolwa abhiye abho bhagajilyaga chiza isabho ijo bhajichola bhoyi b’inikili, kunguno ya wilu bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe. Uweyi agitindikaga gutumama milimo yakwe sagara kunguyo ya guhoyela mihayo ya abhiye abho bhagajitumilaga jikolo getumo bhatogelilwe bhoyi bhinikili, umuwikaji bhobho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo omonelaga wilu umunhu uyo alyaga jikolo jakwe, kunguno nuweyi agabhabhonelaga wilu abhasabhi abho bhagajitumilaga isabho jabho gitumo bhatogelilwe bhoyi b’inikili, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ja ng’winikili jigaliyagwa na ng’wenejo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja gubhabhonela wilu abhanhu abho bhagalyaga jikolo jabho, kugiki bhadule gwigulambija gutumama milimo ya gubhenhela matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Yoshua Bin Sira 31:8.

Yoshua Bin Sira 3:8.

 

KISWAHILI: ZA MWENYEWE HULIWA NA MWENYEWE.

Mwenye mali ni mtu anayefahamu jinsi alivyojitafutia mali hizo. Mtu huyo, huzitumia mali hizo kwa kuzila akiwa na uhuru kwa sababu ni haki yake kutumia mali zake kama apendavyo. Yeye huwakataza wale wanaomuonea wivu azitumiapo vizuri mali zake hizo, kwa sababu hawana haki ya kumzuia kuila atakavyo mali yake hiyo. Ndiyo maana huwaambia kwamba, “za mwenyewe huliwa na mwenyewe.”

Methali hiyo, hutumiwa kwa mtu yule ambaye huwaonea wivu wale wanaokula mali zao. Mtu huyo, ana tabia ya kuwachukia watu wanaotumia mali zao hizo kama wapendavyo wenyewe, kwa sababu ya wivu wake huo, katika maisha yake. Yeye hujichelewesha bure kufanya kazi zake kwa sababu ya kuongelea wale wanaotumia mali zao kama wapendavyo, maishani mwao.

Mtu huyo, hufanana na wale waliomuonea wivu yule aliyekuwa akitumia mali yake kama apendavyo, kwa sababu naye huwaonea wivu matajiri wanaotumia utajiri wao kama watakavyo wao wenyewe, maishani mwao. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “za mwenyewe huliwa na mwenyewe.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kuwaonea wivu watu wanaotumia mali zao kama wapendavyo, ili waweze kuutumia muda wao kwa kujibidisha kufanya kazi zao za kuwaletea mafanikio mengi, maishani mwao.

Yoshua Bin Sira 31:8.

Yoshua Bin Sira 3:8.

cow-12

woman-211

ENGLISH: THE PROPERTY OF THE OWNER IS EATEN BY THE OWNER.

A property of owner is something which the one who has it knows how he or she sought it. This owner, in effect, uses it for eating freely because it is his right to spend his property as he/she likes. He/she forbids those who are jealous of him/her when he/she makes good use of it, because they have no right to stop him/her from eating it. That is why he tells them that “the property of the owner is eaten by the owner.”

This proverb is applied to a man who envies those who eat their possessions. This man has a tendency of hating people who spend their property as they like themselves, because of his jealousy in his life. He delays in vain in doing his works because of speaking about those who use their wealth according to their wishes in their lives.

This man resembles those who envied the one who used his wealth as he wished, because he also envies the rich people who use their wealth according to their interests in their lives. That is why he tells people that “the property of the owner is eaten by the owner.”

This proverb teaches people on how to stop being jealous of people who use their wealth as they like, so that they can spend their time for working hard enough to bring them more successes in their lives.

Joshua Bin Sirach 31: 8.

Joshua Bin Sirach 3: 8.

 

african-girl-

994. NOMO GO NTALE GULINA B’UNONU.

Unomo ugo ntale ili mihayo iyo agayiyombaga ulu alifunya ilange ukubhanhu bhakwe. Abhanhu abho bhagayigwaga imihayo yakwe bho gulidimila chiza ililange lwake linilo, bhagapandikaga bhunonu. Ubhunonu bhunubho jili mbango ijo bhagajipandikaga ulu bhalikalana chiza ililange lya ntale obho ng’wunuyo. Hunagwene bhagayombaga giki, “nomo go ntale guli na b’unonu.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhana abho bhali na wigwi bho gwiyikalana chiza imihayo ya myaji obho, umukikalile kabho. Abhana bhenabho, abhayigwaga imihayo ya myaji obho ng’wunuyo na guyikalana gufumila ahabhunigini mpaga ha bhutale bhobho, kunguno ya nhungwa jabho ijawiza jinijo. Abhoyi bhagapandikaga mbango ja gwikala chiza na bhanhu na gub’iza na sabho ningi, umuwikaji bhobho, kunguno ya wigwi bhobho ubho gulikalana chiza ililange lya myaji obho ng’wunuyo.

Abhana bhenabho, bhagikolaga nabho bhagalikalana chiza ililange lya ntale obho, mpaga bhupandika matwajo mingi, kunguno nabho bhali na wigwi bho gulikalana chiza ililange lya myaji bhobho, ilo ligabhenhelaga mpango ja bhusab’i na gwikala chiza na bhanhu bhabho, umuwikaji bhobho. Hunagwene bhagayombaga giki, “nomo go ntale gulina b’unonu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gub’iza na wigwi bho gulidilila ilange liza lya bhatale bhabho na gulikalana chiza, kugiki bhadule kupandika mbango ja gusab’a na gwikala chiza na bhanhu bhabho, umuwikaji bhobho.

Mithali 7:1-3.

Mithali 6:20-23.

1Yohana 3:18.

Mathayo 23:37-39.

Yohana 1:11-12.

Mithali 22:12.

Waefeso 6:1-4.

KISWAHILI: MDOMO WA MKUBWA UNA UTAMU.

Mdomo wa mkubwa ni maneno anayoyaongea mtu huyo anapowapatia maadili mema watu wake. Watu wanaoyasikia maneno yake hao, kwa kuyajali katika kuyaishi maadili hayo mema, hupata utamu. Utamu huo, ni Baraka wanazozipata wanapoyaishi maadili hayo mema ya mkubwa wao huyo. Ndiyo maana husema kwamba, “mdomo wa mkubwa una utamu.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watoto wale ambao wana utii wa kuyaishi maadili ya mzazi wao, katika maisha yao. Watoto hao, huyaishi maneno ya mzazi wao kwa kuishi katika maadii mema kuanzia utotoni hadi ukubwani mwao, kwa sababu ya tabia yao hiyo njema. Wao hupata Baraka za kuishi vizuri na watu wao na kuwa na mali ninyi maishani mwao, kwa sababu ya utii wao huo kwenye maadili ya mzazi wao.

Watoto hao, hufanana na wale walioyaishi maadili ya mkubwa wao, mpaga wakapata mafanikio mengi, kwa sababu nao wana utii wa kuyaishi maadili ya mzazi wao, yanayowaletea Baraka za kuishi na watu wao vizuri. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “mdomo wa mkubwa una utamu.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na utii wa kuyajali maadili ya wakubwa wao na kuyaishi vizuri, ili waweze kupata Baraka za kutajirika na kuishi vizuri watu wao, maishani mwao.

Mithali 7:1-3.

Mithali 6:20-23.

1Yohana 3:18.

Mathayo 23:37-39.

Yohana 1:11-12.

Mithali 22:12.

Waefeso 6:1-4.

elder-1

SON OF THE CHIEF

ENGLISH: “THE MOUTH OF AN ELDER PERSON HAS SWEETNESS.”

The mouth of the elder person has sweetness because of speaking words of wisdom which provide listeners with good manners. People who hear those words learn moral for taking care of their societal members. They become aware of good values enough to find sweetness in applying them to their daily lives. Such sweetness is the blessing which they receive as they live up to their high moral standards. That is why they say that, “The mouth of an elder person has sweetness.”

This proverb is compared to children who are obedient to the moral values ​​of their parents in their lives. These children, in turn, live up to their parent’s words by living a good life from infancy to adulthood, because of their good behaviors. They get blessings of living well with their people because of their obedience to their parent’s values.

These children are like those who lived up to the values ​​of their elders who have had great successes, because they too have the obedience to live up to their parents’ values, which bring them with blessings of living well with their people. That is why they tell people that, “the mouth of an elder person has sweetness.”

This proverb imparts in people a clue on how to be obedient to the values of their socieities enough to live on the morals of their elders by liveing peacefuly with others, so that they may receive blessings of getting rich enough to support their family members in attaining their goals.

Proverbs 7: 1-3.

Proverbs 6: 20-23.

1 John 3:18.

Matthew 23: 37-39.

John 1: 11-12.

Proverbs 22:12.

Ephesians 6: 1-4.