proverbs

320. UDIZUNIDIMILA MUB’ANA B’A MBULI

Imbuki ya lusumo lunulo yingilile kuli ndimi o mbuli. Undimi ng’wunuyo agajikomanyaga imbuli inhale, na bhana bha mbuli heke. Bhuli jene agajidimaga heke ni jingi. Kuyiniyo lulu, imbuli inhale igalemaga ugudimilwa mub’ana bha mbuli, nulu igab’iza ilinamili gudoo na ginehe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘udizunidimila mub’ana bhana bha mbuli.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alidalahijiwa na bhiye kunguno ya mili gokwe gudoo, aliyo alimunhu ntale. Umunhu ng’wunuyo agalemaga ugusanjiwa mub’anigini. Hunagwene agayombaga giki, ‘udizunidimila mub’ana b’a mbuli.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja kub’adalahija abhanhu, kugiki bhadule ugutumama milimo yabho chiza, mu kaya jabho.

Zaburi 31:18.

1 Petro 2:16-17.

KISWAHILI: USINICHUNGIE KWENYE WATOTO WA MBUZI

Chanzo cha methali hiyo chatokea kwa mchungaji wa mbuzi. Mchungaji huyo huwatenga mbuzi wakubwa na watoto wao, upande mwingine. Kila kundi hulichungia sehemu tofauti na lingine. Kwa hiyo basi, mbuzi mkubwa hukataa kuchungiwa kwenye kundi la watoto, hata kama atakuwa na umbo dogo namna gani. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘usinichungie kwenye kundi la watoto wa mbuzi.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule anayedharauliwa na wenzake kwa sababu ya umbo lake kuwa dogo, ijapokuwa yeye ni mkubwa kiumri. Mtu huyo hukataa kuchanganywa kwenye kundi la watoto, kwa kusema kwamba, ‘usinichungie kwenye watoto wa mbuzi.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kuwadharau watu maishani  mwao, ili waweze kufanya kazi vizuri, katika familia zao.

Zaburi 31:18.

1 Petro 2:16-17.

goats

 

ENGLISH: NEVER PASTURE ME AMONG SMALL GOATS/GOAT’S KIDS

The source of this proverb is a person who pastures goats. The person who tends goats usually separates kids from old goats. Each group is pastured separately. So, an old goat will refuse to be pastured in the same group as kids no matter how small it is in shape.That is why people say, ‘never pasture me among goat’s kids.’

The proverb is analogized to an adult person who is despised by his/her peers because of being small in appearance. The person usually refuses to be treated as a child by saying, “never pasture me among goat’s kids.”

The proverb teaches people to stop the habit of despising other people in their lives.

Psalm 31:18.

1 Peter 2: 16-17

319. LELO YA CHIMA NKUNDI

Imbuki ya lusumo lunulo, yingilile kunkundi uyo gochimagwa ginhu guminyiwa hatale. Unkundi gunuyo gugolechaga b’uminyiwa bho ng’wa munhu uyo ang’wisanije. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘lelo yachima nkundi.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alioludugu, uyo wenhaga mamihayo matale. Abhaduguye b’agasatagwa noyi, kunguno ya gulombwa gufunya nsango kugiki bhabhone guimala imahayo yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘lelo yachima nkundi.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya guleka gwita mamihayo gabhub’i kubhichabho, kunguno amamihayo genayo, gagachimaga nkundi, ukumioyo ya bhichabho bhenabho.

Wagalatia 6:10.

KISWAHILI: LEO IMECHOMA KITOVU

Chanzo cha methali hiyo chatokea kwenye kitovu kilichochomwa kitu fulani kikaumia sana. Kitovu hicho, huonesha jeraha la mauvumi ambalo mtu huyo amelipata kutoka kwa yule amtegemeae, au ameumizwa mtu wa karibu naye. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘leo imechoma kitovu.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu ambaye ameleta matatizo kwa ndugu zake. Ndugu zake mtu huyo huumia sana, kwa sababu ya kuwaletea shida ya kutakiwa kuchanga mali zikiwemo pesa, kwa lengo la kuyatatua matatizo hayo. Ndiyo maana watu husema, ‘leo imechoma kitovu.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha kuwaletea matatizo ndugu zao, au wenzao, kwa sababu, matatizo hayo huchoma vitovu vya mioyo ya wenzao hao, kwa maana ya kuwaumiza sana.

Wagalatia 6:10.

vintage

 

ENGLISH: THE NAVEL HAS BEEN STABBED TODAY

This proverb comes from a person whose navel has been stubbed badly. The navel represents injury caused by a closely-related person. That is why people say, “the navel has been stubbed today.” The proverb is compared to a person who has caused serious problems to his/her relatives. The relatives of that person suffer because of being asked to pay money or something else in order to resolve the problem their relative caused to them. That is why people say, “the navel has been stubbed today.”

The proverb warns people against causing problems to their brothers or their people because problems cause pain to people.

Galatians 6:10.

318. FUGO NHALE IDAMALAGA NGUKULU

Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile nkukulu ijo jisagilile, mu fugo ya guzugila b’ugali. Ifugo yiniyo igab’izaga na masagilwa ga jiliwa ukusi yayo ijo bhagajilekelaga abhali bha jiliwa jinijo. Amalekelwa genayo hayo gagitanagwa ngukulu. Ingululu jinijo jigadamilaga hasi ya fugo yiniyo. Kuyiniyo lulu, umunhu uyo alasange jashilaga ijiliwa, adulile nulu gupala ngukulu ulya. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘fugo nhale idamalaga ngukulu.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinsab’i o mitugo, nulu o jose jose. Unsab’i ng’wunuyo nulu jigacha imitugo, jidushila pye, kunguno jigigelaga nulu ngehu ijagupila. Umunhu ng’wunuyo, agab’izaga na ginhu ja gufunya ukub’iye guti jikolo nulu miganiko ayo gadulile gubhambilija abhiye bhenabho. Hunawene abhanhu ulu bhalinomba ginhu bhagayombaga giki, ‘fugo nhale idamalaga ngukulu.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza b’izanholo ukubhanhu abho bhali na makoye. Uwizanholo b’unubho, bhugubhambilija abhanhu bhenabho ijinakupandika nzila ja guginja amakoye genayo.

Yohane 6:13.

KISWAHILI: CHUNGU KUKUBWA HAKIMALIZI UKOKO

Chanzo cha methali hiyo chaangalia chungu cha kupikia ugali, chenye ukoko. Chungu hicho huwa na mabaki ya chakula ndani yake kwa chini, ambayo hubakishwa na walaji wa chakula hicho. Mabaki hayo hung’ang’ania chini ambayo huitwa ukoko. Ukoko huo huwa mgumu kutolewa ndani ya chungu hicho. Kwa hiyo basi, mtu atakayekuta chakula kimeliwa, huweza kukwangua walau ukoko huo na kula. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘chungu kikubwa hakimalizi ukoko.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu ambaye ni tajiri wa mifugo au wa kitu chochote kile. Mtu huyo huwa na kitu cha kutoa kwa wenzake wanaomuomba kama vile mali, au mawazo yawezayo kuwasaidia wenzake hao. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘chungu kikubwa hakimalizi ukoko.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwasaidia wenye shida mbalimbali. Ukarimu huo, utawasaidia watu hao katika kupata njia za kuyatatulia matatizo hayo.

Yohane 6:13.

camping-cooker

 

ENGLISH: A BIG POT IS NOT WITHOUT CRUST

The source of this proverb is a big pot. A big pot always has crust at the base left by people who ate the food. The crust sticks below the base of the pot and it is difficult to remove it. Therefore, a person who finds the food has been eaten may scrape the crust and eat. That is why people say, “a big pot is not without crust.”

The proverb is analogized to someone who has many livestocks or anything else. Even if all the livestocks die, such a person will have few left behind. The person usually has something to give to those who approach him/her for help.That is why people say, “a big pot is not without crust.”

This proverb teaches people about being generous to other people with problems. Such generosity will help them to find ways to solve their problems.

John 6:13.

316. SHIMBA NG´OSHA IDAGAIYAGWA B´UYENZE

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile shimba iyo iling´osha. Ishimba yiniyo, igikalaga na jimanikijo jayo, ijo jigitanagwa b´uyenze. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ´shimba ng´osha idagaiyagwa b´uyenze.´

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu ngosha, uyo amanyikile chene bho guilang´hana chiza ikaya yakwe. Ubhulang´hani bho kaya yakwe, umunhu ng´wunuyo, wikolile na b´uyenze bho guimanyikija ishimba yiniyo, igiki iling’osha. Umunhu ng´wunuyo agabhalangaga abhanhu bhakwe inzila ja gwikala chiza na bhichabho. Hunagwene abhanhu bhayombaga giki, ´shimba ng´osha idagaiyagwa b´uyenze.´

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gudilila milimo yabho, bho gwikala chiza na bhichabho. Uwikaji bhunubho, bhubhamanyiche ikigi, abhoyi bhali bhanhu bha nhungwa ja wiza, umukikalile kabho.

Mithali 30:30.

Ufunuo 5:5.

KISWAHILI: SIMBA DUME HAKOSI SHALUBU

Chanzo cha methali hiyo chatokea kwenye simba dume. Simba huyo huwa na alama ya kumtambulisha kuwa yeye ni dume, iitwayo shalubu. Kila simba dume anashalubu. Ndiyo maana watu husema kwamba, ´simba dume hakosi shalubu.´

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu mwanaume ajulikanaye hivyo kwa kuitunza vizuri familia yake. Utunzaji huo wa familia yake, hufanana na shalubu la yule simba, limtambulishalo kuwa yeye ni dume. Mtu huyo huwafundisha  pia watu wake namna ya kuishi vizuri na watu. Ndiyo maana watu husema kwamba, ´simba dume hakosi shalubu.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kujali kazi zao kwa kuishi vizuri na wenzao. Maisha hayo, yatawatambulisha, maishani mwao, kuwa wao ni binadamu wenye tabia njema.

Mithali 30:30.

Ufunuo 5:5.

lion1

lion

 

ENGLISH: A MALE LION IS NOT WITHOUT MANE

The source of this proverb is the lione’s mane. The lion’s mane is one of the features used to identify a male lion. Every male lion has it. That is why people say, “a male lion is not without mane.”

The proverb is likened to a man who is known for taking good care of his family. The care of his family is like the lion’s mane; it identifies him as a real man. Such a person also teaches his people how to live well with other people. That is why people say, “a male lion is not without mane.”

The proverb teaches people about caring for their jobs and living well with their people. Such kind of life will make them to be identified as good people.

Proverbs 30:30.

Revelation 5: 5.

315. LUGULU LUTALE LUDAGAIYAGWA MOMA

Imbuki ya lusumo lunulo yingilile kukigelele ka lugulu. Ulugulu lunulo mumo lugalihila lugagaiyagwa aho tub´izu na halihu. Ahatub´izu igitanagwa halyoma. Ubhutub´izu uwingi bhugitanagwa moma. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ´lugulu lutale ludagaiyagwa moma.´

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuwikaji bho bhanhu umowikalelile na lugulu lunulo ulutale, ulo lulina moma. Amoma genayo gikolile nikanza lya makoye, umuwikaji bho bhanhu. Amakoye genayo, mumo gagakulila ukubhanhu, bhadugaiwa inzila iyagugamalila. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ´lugulu lutale ludagaiyagwa moma.´

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gwilunguja umumakoye, na guchola nzila ja gugamalila, bho nduhu gugwa nholo.

1Wakorintho 10:13.

KISWAHILI: MLIMA MKUBWA HAUKOSI MAKOLONGO

Chanzo ch methali hiyo chatokea kweye muonekano wa Mlima. Mlima huo haukosi kuwa na sehemu za kushuka na kupanda, hata uwe mrefu kiasi gani. Sehemu za kushuka huitwa makolongo au mabonde. Ndiyo maana, watu husema kwamba, ´mlima mkubwa haukosi makolongo.´

Methali hiyo hulinganishwa kwenye maisha ya watu ifananavyo na mlima mkubwa wenye makolongo. Makolongo hayo hufanana na wakati wa matatizo katika maisha ya watu hao. Matatizo hayo hata yawe makubwa kiasi gani, watu hawatakosa njia za kuyatatulia au kuyamaliza. Ndiyo maana, watu husema kwamba, ´mlima mkubwa haukosi makolongo.´

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kufarijiana wakati wa matatizo, na kutafuta njia za kuyatatulia matatizo hayo, bila kukata tamaa.

1 Wakorintho 10:13.

mountains

climb

 

ENGLISH: A HIGH MOUNTAIN IS NOT WITHOUT UPS AND DOWNS

This proverb stems from the nature of mountains. Mountains usually have ups and downs; no matter its height. The downs are called valleys. That is why people say, “a high mountain is not without ups and downs.”

The proverb is likened to people’s life; it has ups and downs just like a high mountain. The downs are similar to time of crisis in the lives of those people. People always find ways to solve the crisis no matter how serious they are. That is why people say, “a high mountain is not without ups and downs.”

The proverb teaches people to comfort one another in times of trouble and help each other in finding ways out of problems.

1 Corinthians 10:13.