Kashinje Zacharia

349. GUGEMELWA ICHIMU IDI GUCHING’WA.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhugemelwa bho ng’wa munhu guching’wa ichimu. Ilichimu linilo jiliginhu jugi ijo jidulile gunhemaja munhu. Kuyiniyo lulu, ulu munhu unkanga ng’wiye bho gungemela gunchima ichimu, uyo aligemelwa, adulile gugwa guti giki ochimagwa nili lichimu liniyo.

Gashinaga lulu, ulu munhu ungemela ng’wiye ichimu idi giki onchimaga, onkanga duhu kugiki, ogohe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘gugemelwa ichimu idi guching’wa.’

Akahayike kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalib’ob’a bha gutumama milimo iyo ilimidimu, aliyo lulu imilimo yiniyo idulile gubhinja bhanhu mumakoye. Abhanhu bhenabho bhagawilagwa giki, imilimo yiniyo idadulile gubhabhulaga, kunguno, ugugemelwa ichimu idi kung’wa.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka bhob’a bho uguitumama imilimo iyo ilimidumu, kunguno imilimo yiniyo idulile gub’inja bhichab’o mumakoye. Yigelelilwe abhanhu bhongeje bhukamu bho guitumama na bhuyegi imilimo yiniyo kugiki, bhadule gujib’eja chiza ikaya jabho.

Yohane 18:10-11.

1 Wakorintho 10:13.

KISWAHILI: KUJARIBIWA MKUKI SIO KUCHOMWA

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye tukio la mtu kujaribiwa kuchomwa mkuki. Mkuki ni kitu chenye ncha kali kiwezacho kumdhuru mtu. Kwa hiyo mtu akimtishia mwenzake kwa kumchoma mkuki, aliyetishiwa aweza hata kudondoka akidhani kwamba, amechomwa mkuki.

Kumbe basi, mtu akimjaribia mwenzake kumchoma mkuki huo, sio kwamba, amemchoma, bali amemtishia tu ili agope. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kujaribiwa mkuki sio kuchomwa.’

Msemo huo hulinganishwa kwa watu ambao wana uoga wa kuzifanya kazi zile zilizongumu, lakini kazi hizo, zaweza kuwaokoa wenzao kutoka kwenye matatizo. Watu hao huambiwa kwamba, kazi hizo haziwezi kuwaua, kwa sababu ‘kujaribiwa mkuki sio kuchomwa.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha uoga wa kuzifanya kazi zilizongumu, kwa sababu kazi hizo zaweza kuwaokoa wenzao kutoka kwenye matatizo. Hivyo, yafaa watu hao waongeze bidii ya kufanya kazi hizo, kwa furaha ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao.

Yohane 18:10-11.

1Wakorintho 10:13.

masai

lance

 

ENGLISH: BEING TESTED BY SPEAR DOESN’T MEAN YOU HAVE BEEN PIERCED.

The source of the above saying comes from an incident of someone trying to brandish a spear. The spear is a sharp knot that can hurt a person. So, if a person threatens a fellow by stabbing him/her with a spear, the threatened person may even fall, thinking that he/she is being stabbed.

A person can pretend to be piercing someone but that doesn’t make this another person to be pierced. Rather, threatening him/her. This is why people say, ‘being tested by spear doesn’t mean that you have been pierced.’

The saying can be comparable to people who are afraid to do hard works, without knowing that those tasks can save others from trouble. These people are told that, those jobs can’t kill them, because ‘being tested by spear does’t mean that you have been pierced.’

The saying teaches people to break the fear of doing hard work because those tasks can save others from trouble. Therefore, it is important for these individuals to increase their efforts in such activities in order to create a better ground for future success in life.

John 18: 10-11.

1 Corinthians 10:13.

348. FUMBUKA AGALEKA CHUMA JAKWE ADAFULILE.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kuli munhu uyo witanagwa Fumbuka na b’ufuji bhokwe bho chuma. Ufumbuka olimfuji ochuma uyo wiganikaga giki, niogumala unimo gokwe gunuyo, bho gujifula pye chuma jakwe. Aliyo lulu, aginga kuwelelo haho atali uguimala imilimo yakwe yiniyo iyagub’eja chuma jakwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Fumbuka agaleka chuma jakwe adafulile.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe bho nduhu gunzunya, nulu gung’wisanya Mulungu. Umunhu ng’wunuyo adamanile igiki, Uwelelo adalindilaga munhu mpaga aimale imilimo yakwe, na ang’wizile. Gashinaga, Uweyi alinabhudula bho gung’wizile munhu ose ose, na kumakanza ayo atogilwe weyi.

Yigelelilwe abhanhu bhaitumame imilimo yabho, bho gunzunya na gung’wisanya Weyi, kunguno alina bhudula bho gubhizile makanza gose gose. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Fumbuka agaleka chuma jakwe adafulile.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kunzunya na gung’wisanya Mulungu, umubhutumami bhobho, kugiki bhadule gwikala gitumo atogelilwe Uweyi.

Mathayo 24: 37-39.

Luka 9:59-62.

2 Wakorintho 6:2.

KISWAHILI: FUMBUKA ALIACHA CHUMA CHAKE HAKUTENGENEZA

Chanzo cha msemo huo chatokea kwa mtu mmoja aitwaye Fumbuka na ufuaji wake wa chuma. Fumbuka alikuwa mfua vyuma aliyedhani kwamba angeimaliza kazi yake hiyo, kwa kufua vyuma vyake vyote. Lakini basi, mtu huyo aliaga dunia kabla ya kuimaliza kazi yake hiyo. Ndiyo maana watu wakasema kwamba, ‘Fumbuka aliacha chuma chake hakutengeneza.’

Msemo huyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi zake bila kumwamini wala kumtegemea Mungu. Mtu huyo haelewi kwamba, Mungu hamsubili mtu mpaka amalize kazi zake, ndipo amchukue. Kumbe, Yeye anao uwezo wa kumchukua mtu yeyote na kwa wakati wowote, anaoutaka Yeye.

Yafaa watu wafanye kazi zao kwa kumwamini na kumtegemea Mungu, kwa sababu Yeye anao uwezo ya kuzifanikisha kazi zao hizo, na kuwachukua wakati autakao Yeye. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘Fumbuka aliacha chuma chake hakutengeneza.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kumwamini na kumtegemea Mungu katika kazi zao, ili waweze kuishi kwa kadiri atakavyo Yeye, maishani mwao.

Mathayo 24: 37-39.

Luka 9:59-62.

2 Wakorintho 6:2.

old

 

ENGLISH: FUMBUKA LEFT HIS IRONS; HE DID NOT MAKE.

The origin of the above saying comes from a man named Fumbuka and his iron-making skill. Fumbuka was an iron-smith who thought he would finish his job by processing all his metals. Unfortunately, the man passed on before he could finish his work. This is why people say, ‘Fumbuka left his irons; he did not make.’

The saying is compared to a person who does his work without his/her trust in God. Such a person does not understand that God does not wait for anyone to finish his/her work, and then take him/her. God has the power to take anybody and at any time He wants to.

People should do their jobs by trusting in God because He has the power to accomplish their tasks and take them at the time He wants. This is why people say, ‘Fumbuka left his irons; he did not make.’

The above saying teaches people an idea of putting their trust in God in their daily works. People need to live according to the way God wants them to live.

Matthew 24: 37-39.

Luke 9: 59-62.

2 Corinthians 6: 2.

  

347. NDIMI JA B’ANAKALE JIGALEKA SUMO

Imbuki ya kahayile kenako yingilile ku ndimi ja bhanhu bha kale. Indimi jinijo, galimahoya gabho umuwikaji bhobho. Umumahoya genayo, abhanhu abhingi abha kale b’agayileka mihayo iyo iliyambisila. Iyiniyo hiyo abhanhu abha haha duguyihoyelaga, kunguno ilina bhulangwa bhutale umukati yayo, iyo igitanagwa sumo. Gashinaga guligonhana igiki ‘ndimi ja b’anakale jigaleka sumo.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalegaka mmenho umuwikaji bhokwe. Immenho jinijo kalikalile kakwe ako kagab’ambilijaga abhiye umumakoye gabho, nu mub’uyegi bhobho. Umunhu ng’wunuyo, adebhile ugubhalunguja abhiye abho akagikalaga nabho. Uwikaji bhokwe bhuli shule ya gwilanga higulya ya gwikala bho mholele na abhanhu umuchalo jakwe. Alisawa ni ndimi ija bhanakale ijo jigaleka sumo, kunguno nang’hwe alileka bhulangwa bho gwikala chiza na bhanhu.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka lumenho lo kikalile ka mholele na bhanhu umuchalo jabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji nu mubhutumami bhobho.

Yeremia 6:26.

Waebrania 1:1-2.

KISWAHILI: NDIMI ZA WANAZAMANI ZILIACHA METHALI

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye ndimi za watu wa zamani. Ndimi hizo, yalikuwa maongezi yao ya kila siku. Watu wengi hao watu wa zamani waliacha maneno yenye mafumbo fulani ndani yake, kupitia maongezi hayo. Maneno hayo ndizo methali tuzitumiazo, kwa sababu zina mafundisho makubwa ndani yake. Kumbe ni kweli kwamba, ‘ndimi za wanazamani ziliacha methali.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu ambaye huacha alama maishani mwake. Alama hizo ni namna ya kuishi kwake mtu huyo, ambako huwasaidia wenzake katika kipindi cha furaha na cha matatizo. Mtu huyo afahamu kuwafariji wenzake walioko kwenye matatizo maishani mwao. Maisha yake mtu huyo ni shule ya kujifunza juu ya kuishi kwa amani na watu maishani. Yeye ni sawa na ndimi za wanazamani ambazo ziliacha methali, kwa sababu naye huacha alama ya kujifunza kuishi vizuri na watu.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha alama za kusaidia watu kuweza kuishi kwa amani katika vijiji vyao, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao.

Yeremia 6:26.

Waebrania 1:1-2.

beautiful-elderly

 

ENGLISH: TONGUES OF THE OLD ONES LEFT OUT PROVERBS.

The origin of the above saying comes from tongues of ancestors. Those tongues were speaking words of wisdom in their daily conversations. Many of those ancestors left words with some parables in them. These words are the proverbs we use today because they have a great deal of teaching in them. Then, it is true that ‘tongues of the old ones left out proverbs.’

The saying is compared to someone who leaves a mark on his/her life. The mark or symbols left are a way of living of that person. People can be remembering him/her based on how he/she helped other people on ways to sustain the lives of others in happy and difficult times.

His/her life then becomes a school to learn about how to live in peace with people. He/she is like the old tongues that left out proverbs, a word of wisdom that shapes people’s daily lives. This is why people say, ‘tongues of old ones left out proverbs.’

The above saying teaches people about leaving marks that will help other people to have a decent life and finally have success in life.

Jeremiah 6:26.

Hebrews 1: 1-2.

298. LUTAMBI LUPYA IMALA MAGUTA

Imbuki ya lusumo lunulo ingilile kulutambi ulo lutali lupya. Ulutambi lunulo lugasolaga maguta mingi agagudula guibhacha ikolobhoi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘lutambi lupya imala maguta.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alindimu ugwitegeleja imihayo iyo aliwilwa na bhiye. Ugushiga agadule gwitegeleja umunhu ng’wunuyo, agub’iza omalaga mihayo mingi noyi unomeji okwe, aliyo uweyi agabhizaga ndimu duhu ugwelelwa. Hukwene guhaya giki, unomeji okwe agumala mihayo yakwe duhu, bho nduhu uweyi ugwitegeleja. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga, umunhu ng’wunuyo, giki, ‘lutambi lupya imala maguta.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gudula guidebha chiza imihayo iyo ilihawiza na bhichabho, na guitumamila iyo iliyawiza, umuwikaji bhobho.

Yohana 14:8-9.

KISWAHILI: UTAMBI MPYA HUMALIZA MAFUTA

Chanzo cha methali hiyo chatokea kwenye hali ya utambi mpya. Utambi huo huchukua mafuta mengi ya kutosha kuiwezesha taa kuwaka. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘utambi mpya humaliza mafuta.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu ambaye ni mgumu wa kuelewa kile anachoambiwa na wenzake. Mtu huyo humfanya yule anayemwelewesha amalize maneno mengi, bila kuelewa. Mweleweshaji wake huyo, humaliza maneno mengi bila kumwezesha mtu huyo kuelewa, kile anachomwambia. Ndio maana watu humwambia mtu huyo, kwamba, ‘utambi mpya humaliza mafuta.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuelewa mapema kile wanachoelezwa na wenzao, na kukifanyia kazi kile kilicho chema katika kuwaletea maendeleo, maishani mwao.

Yohana 14:8-9.

kerosene-lamp

ENGLISH: A NEW WICK USES A LOT OF KEROSINE

The above proverb stems from a situation of a new wick.The new wick uses a lot of kerosine to keep the light on. This makes people to say, “a new wick uses a lot of kerosine.”

The proverb is used to refer to someone who does not understand what is being told by his/her companion. Such a person makes whoever is explaining something to him/her to use a lot words in vain.That is why people tell such people that, “a new wick uses a lot of kerosine.”

The proverb teaches people to listen and understand what they are told by their companions and use whaever it is good to bring progress to their lives.

John 14: 8-9.

257. UYO WACHA ADABHONAGA NG’WANA.

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile munhu uyo ocha uleka bhana. Umunhu ulu ucha agab’izaga adina nduguye nulu bhana, kunguno ung’unuyo wingaga igiki agubhagunanha. Gwike lulu, abho bhalekelagwa imhina jinijo habhanabho abho b’agujilela, na bhana bhenabho bhagubhakalalija bhoyi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘uyo ocha adabhonaga ng’wana.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagab’alelaga chiza abhana abho bhachilwa na bhabyaji bhabho. Bhagabhasomishaga na gubhalela chiza abhana abhapina bhenabho.

Abhanhu bhenabho bhagikalaga bhedeb’ile igiki unimo ugogubhalang’hana abhana bhenab’o guligobhapanga guti bhoyi, kunguno abho bhamala gwinga kuwelelo bhadadulile ugubhabhona abhana abhapina bhenabho. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘uyo ocha adabhonaga ng’wana.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu  gudebha gubhalela chiza abhana abho bhachilya na bhabyaji bhabho. Ubhudebhi bhunubho bhugubhambilija abhana abho bhalibhapina, ijinagubhasomisha na bhubhalanga kikalile kawiza umuwikaji bhobho. Hukwene guhaya giki, abhapanga kihamo na bhaduguye bha njimiji, ha bhaleji bha bhana abho bhalib’apina, kunguyo, ‘uyo ocha adabhonaga ng’wana.’

(Zaburi 22:6-7; Yohane 19:26 -27).

KISWAHILI: ALIYEKUFA HAONI MTOTO.

Chanzo cha methali hii chaangalia mtu aliyefariki akaacha watoto. Mtu akifa huwa hana ndugu wala watoto, kwa sababu huyo hawezi kuwasaidia. Hivyo, walioachiwa yatima hao, wakiwemo ndugu za marehemu, ndio wale watakaowalea watoto hao. Yatima hao watawaangalia na kuwategemea hao walio hai. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘aliyekufa haoni mtoto.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wale wawaleao vizuri watoto yatima. Watu hao huwasomesha na kuwapatia malezi yawezayo kuwasaidia watoto hao katika maisha yao. Watu hao, waelewa kuwa, jukumu la kuwalea watoto yatima ni la watu walio hai kama wao kwa sababu wazazi wa watoto hao, walishafariki dunia, hivyo hawawezi kuwaona yatima hao. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘aliyekufa haoni mtoto.’

Methali hiyo hufundisha watu  kupokea jukumu la kuwalea watoto yatima. Upokeaji wa jukumu hilo, utawasaidia watoto yatima wengi katika kupata watu wa kuwasomesha na kuwapatia malezi yawezayo kuwasaidia kuishi maisha mema. Ndiyo maana watu kusema kwamba, watu walio hai ikiwa ni pamoja na ndugu zake marehemu, ndio walezi wa watoto hao yatima, kwa sababu, ‘aliyekufa haoni mtoto.’

Zaburi 22:6-7.

 

african-child1

cross1

ENGLISH: THE DEAD PERSON DOES NOT SEE A CHILD.

The origin of this proverb is the deceased who left children. When a person dies, he has no brothers or children, because he cannot help them. As such, those who have been left behind, including the relatives of the deceased, are the ones who will raise the orphaned children. The orphans will expect help from those who are alive. That is why people say, ‘The dead person does not see a child.’

The proverb is used comparatively to commend those who properly raise orphans. These people provide the orphans with education and the care that they need in their lives. Those people take the responsibility of providing the orphans with education and upbringing that can help them in their future lives.

Those people understand that the responsibility of raising the orphaned children is under those who are alive because their parents passed away and, hence, cannot see the orphans. That is why people say, ‘The dead person does not see  achild.’

This proverb instills in people the sense of accepting the responsibility of raising orphans. Accepting such a responsibility helps the orphans to get people who can support provision of their education and care for better lives. That is why people say that, the living people, including the relatives of the deceased, are the guardians of the orphans, because, ‘The dead person does not see a child.’

(Psalm 22: 6-7).