349. GUGEMELWA ICHIMU IDI GUCHING’WA

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhugemelwa bho ng’wa munhu guching’wa ichimu. Ilichimu linilo jiliginhu jugi ijo jidulile gunhemaja munhu. Kuyiniyo lulu, ulu munhu unkanga ng’wiye bho gungemela gunchima ichimu, uyo aligemelwa, adulile gugwa guti giki ochimagwa nili lichimu liniyo.

Gashinaga lulu, ulu munhu ungemela ng’wiye ichimu idi giki onchimaga, onkanga duhu kugiki, ogohe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘gugemelwa ichimu idi guching’wa.’

Akahayike kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalib’ob’a bha gutumama milimo iyo ilimidimu, aliyo lulu imilimo yiniyo idulile gubhinja bhanhu mumakoye. Abhanhu bhenabho bhagawilagwa giki, imilimo yiniyo idadulile gubhabhulaga, kunguno, ugugemelwa ichimu idi kung’wa.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka bhob’a bho uguitumama imilimo iyo ilimidumu, kunguno imilimo yiniyo idulile gub’inja bhichab’o mumakoye. Yigelelilwe abhanhu bhongeje bhukamu bho guitumama na bhuyegi imilimo yiniyo kugiki, bhadule gujib’eja chiza ikaya jabho.

Yohane 18:10-11.

1 Wakorintho 10:13.

KISWAHILI: KUJARIBIWA MKUKI SIO KUCHOMWA

Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye tukio la mtu kujaribiwa kuchomwa mkuki. Mkuki ni kitu chenye ncha kali kiwezacho kumdhuru mtu. Kwa hiyo mtu akimtishia mwenzake kwa kumchoma mkuki, aliyetishiwa aweza hata kudondoka akidhani kwamba, amechomwa mkuki.

Kumbe basi, mtu akimjaribia mwenzake kumchoma mkuki huo, sio kwamba, amemchoma, bali amemtishia tu ili agope. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kujaribiwa mkuki sio kuchomwa.’

Msemo huo hulinganishwa kwa watu ambao wana uoga wa kuzifanya kazi zile zilizongumu, lakini kazi hizo, zaweza kuwaokoa wenzao kutoka kwenye matatizo. Watu hao huambiwa kwamba, kazi hizo haziwezi kuwaua, kwa sababu ‘kujaribiwa mkuki sio kuchomwa.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha uoga wa kuzifanya kazi zilizongumu, kwa sababu kazi hizo zaweza kuwaokoa wenzao kutoka kwenye matatizo. Hivyo, yafaa watu hao waongeze bidii ya kufanya kazi hizo, kwa furaha ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao.

Yohane 18:10-11.

1Wakorintho 10:13.

masai

lance

One comment

  1. Msemo huu Ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku, Kwani unatuimarisha na kutupa nguvu. Magumu tunayokutana nayo katika mahangaiko yetu kamwe yasitufanye tukakata tamaa, yanakuja ili kutuimarisha.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.