Folklore

672. HANGAYA YABHELEKA.

Imbuki ya kahayile kenako, yingilile ku Sonda iyo igafumaga dilu makingilima Isonda yiniyo, uluyafuma  igamanyichaga giki ubhujuku wela, kugiki abhanhu bhaje ku milimo iki wizaga bhupe. Ubhupe bhunubho, bhugolechaga ikanza lya gwandya kutumama milimo, kunguno bhuli ng’wene agadulaga ugubhona chiza. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Hangaya yabheleka.’

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ntumami ogwipunha dilu oja ukumilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agalitumilaga chiza ilikanza ilya Limi, bho gwanguha gujigulambija gutumama milimo yakwe yiniyo. Uweyi adebhile isolobho ya gulitumila chiza ilikanza lyake lya Limi linilo. Isolobho jinijo, jilikihamo na gwipandikila matwajo mingi, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolola ni sonda iyo igabhelekaga dulu, kunguno nuweyi agipunhaga dulu makingilima, ogigulambija gutumama milimo yakwe, iyo igang’winhaga matwajo mingi, umuwikaji bhokwe.

Uweyi agabhinhaga nabhiye bhulangwa bho gulitumila ilikanza lya limi jinagwigulambija uguitumama imilimo yabho yiniyo chiza, umukikalile kabho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘Hangaya yabheleka.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gulitumila ilikanza lyabho ilyalimi bho gwigulambija guitumama na bhukamu bhutale imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo agagujibheja chiza ikaya jabho.

Luka 1:73.

Mathayo 16:3.

2 Wakorintho 6:1.

Luka 2:32.

Waebarania 1:1…

KISWAHILI: SAYARI/NYOTA IMETOKEA.

Chanzo cha msemo huo, chatokea kwenye Nyota ile inayotoka asubuhi na mapema. Nyota hiyo, ikitokea huonesha kwamba usiku umekucha, ili watu waende kufanya kazi kwa vile mwanga umekuja.

Mwanga huo, huonesha wakati wa kuanza kufanya kazi, kwa sababu ya kila mmoja kuweza kuona vizuri. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘Sayari/Nyota imetokea.’

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mfanya kazi anayeamka asubuhi na mapema, na kwenda kufanya kazi zake, katika maisha yake. Mtu huyo, huutumia vizuri muda wake wa mchana, kwa kujibidisha kuyatekeleza  kwa bidii majukumu yake hayo. Yeye anafahamu faida ya kuutumia vizuri muda wake huo wa mchana. Faida hizo, ni pamoja na kujipatia mafanikio mengi, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na Nyota ile inayotokeza asubuhi, kwa sababu naye hujilawa asubuhi na mapema kwenda kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yake, yanayompatia mafanikio mengi, katika maisha yake.

Yeye pia huwapatia mafundisho wenzake, ya kuutumia muda wao wa mchana, katika kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao vizuri, katika maisha yao. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘Sayari/Nyota imetokea.’

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuutumia muda wao wa mchana kwa kujibidisha kuyatekeleza kwa bidii kubwa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio ya kuziendeleza vizuri familia zao.

Luka 1:73.

Mathayo 16:3.

2 Wakorintho 6:1.

Luka 2:32.

Waebarania 1:1…

star

star2

bhakima bhatumami

 

ENGLISH: THE MORNING STAR HAS APPEARED.

The source of this saying is the morning star that communicates that a new day has come. When this star appears it sweeps away darkness and invites light to mean that people have to wake up and continue with their daily activities. This scenario of making people wake up and proceed with their daily routine can be described using the saying that ‘the morning star has appeared.’

This saying can be compared to a person who wakes up early in the morning and goes to work. Such a person values time and knows when to wake up and what to do. People of this nature are likely to have achievements in life because of the way they are organized in their responsibilities. They also teach others about valuing time.

The saying teaches people about how to use their time in their daily activities. People have to work hard in order to achieve success in life.

Luke 1:73. Matthew 16: 3. 2 Corinthians 6: 1. Luke 2:32. Hebrews 1: 1.

671. MVA NYIBHELEJA HUNA NG´WI YA MAGI.

Imbuki ya lusumo lunulo, ilolile wibhembu bho mva iyo igang’waga magi. Imva yiniyo, igibhelejaga bho gwiyolecha giki iliya wiza ukuli nsugi oyo, kugiki akije uguibadija igiki igang’waga maji. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘mva nyibheleja huna ng’wi ya magi.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ng´wibhembu, aliyo ubho mgati adi o wiza, aling´wibheleja duhu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agiyolechaga ukubhanhu giki ali ntengeke, aliyo gashinaga alinkenaguji, umugati yakwe. Uweyi agikalaga bho gwibheleja duhu, kugiki abhanhu bhakije ugumbadija agiki aliobhubhi.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni mva yiniyo inyibheleja, aliyo hing’wi ya magi, kunguno nuweyi alina wibhembu bho gwibheleja hanze dulu, umgati yakwe, agiganikaga mihayo ya bhukenaguji, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘mva nyibheleja huna ng’wi ya magi.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleka gwita mihayo bhubhi, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umuwikaji bhobho.

Yohana 12:43.

Luka 6:26.

Luka 11:43.

KISWAHILI: MBWA MNYENYEKEVU NDIYE MNYWAJI WA MAYAI.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia unyenyekevu wa mbwa, ambaye ndiye mnywaji wa mayai. Mbwa huyo, hujionesha kama ni mwema kwa nje tu, ili asijulikane kuwa ndiye mnywaji wa mayai hayo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘mbwa mnyenyekevu ndiye mnywaji wa mayai.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mnyenyekevu kwa nje, lakini kwa ndani siyo mzuri, maishani mwake. Mtu huyo, ni mpenda sifa kwa kujionesha kuwa yeye ni mwema, lakini kumbe ni mharifu, maishani mwake. Yeye huishi maisha ya kujionesha kuwa ni mwema ili watu wasimtambue kuwa ni mharifu.

Mtu huyo, hufanana na yule mbwa mwenye unyenyekevu wa kujionesha, lakini kumbe ndiye mnywaji wa mayai, kwa sababu naye hujionesha kwa nje kuwa ni mwema lakini kumbe kwa ndani, ndiye mharifu, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘mbwa mnyenyekevu ndiye mnywaji wa mayai.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kutenda uovu, katika maisha yao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.

Yohana 12:43. “Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.”

Luka 6:26. “Ole wenu watu watakapowasifu, kwani ndivyo baba zao walivyowasifu manabii wa uongo.””

Luka 11:43. “Ole wenu Mafarisayo, kwa sababu ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni.”

dog

dog1

dog2

 

ENGLISH: THE HUMBLE DOG IS THE EGG EATER.

The source of this proverb is the humbleness of a dog that, in fact, is the bad one. This kind of dog will always appear very humble to the extent of not predicting anything bad coming from it. But, as this proverb describes, this type of dogs are even worse than the ones that can demonstrate their theft in public. This is why people came with the proverb that ‘the humble dog is the egg eater.’

 This proverb can be compared to a person who is humble in his/her appearance but the reality is he/she is not. He/she can pretend to be well mannered and therefore good to others while the reality on the ground is, he/she is a bad person. Such people are compared to humble dogs that hide their true colours of being egg eaters.

The proverb teaches people to stop doing bad things in their lives. It also teaches people to live in peace with others.

John 12:43: “They loved the praise of men more than the praise of God.”

Luke 6:26: “Woe to you when men praise you, for so did their fathers to the false prophets.”

Luke 11:43; “Woe to you Pharisees, because you love to sit in the synagogues and be greeted with respect in the marketplaces.”

670. MABHELE MANOGU ISAB´A ILAMBU.

Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile bhulogu bho gupandika mabhele na bhudamu bho gusabha ng’ombe. Amabhele gali manogu, kunguno umunhu adulile guja ha ng’wa nsab’i ugagalila.

Aliyo lulu, umunhu ng’wunuyo adadulile ugulombe ng’ombe na gwunhiwa ya bhule, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘mabhele manogu isab’a ilambu.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agigulambijaga kutumama milimo yakwe, mpaga ojipandika isabho, umuwikaji bhobho. Umunhu ng’wunuyo, agalimaga bho bhukamu bhutale ahikanza lya mbula, mpaga ojibisha ijiliwa.

Ijiliwa jinijo, agajilyaga na mpaga ojijinja ijingi ijo jigang’wenhelaga sabho. Uweyi agabhalangaga na abhanhu bhakwe ahigulya ya guitumama imilimo yiniyo bho wigulambijaga bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, alijigemelo ikubhiye ijagutumama milimo bho wigulambija mpaga gupandika matwajo mingi, kunguno ya bhukamu bhokwe, umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu agabhawilaga giki, ‘mabhele manogu isab’a ilambu.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho, bho bhukamu bhutale, umukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika sabho ijagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Waebrania 12:14.

Luka 13:24.

2 Petro 1:10.

KISWAHILI: MAZIWA MARAHISI UTAJIRI MGUMU.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia urahisi wa kupata maziwa, na ugumu wa kupata ng’ombe. Maziwa ni marahisi kwa sababu mtu anaweza kwenda kwa tajiri na kupewa maziwa hayo ambayo huyatumia kama mboga.

Lakini basi, mtu huyo hawezi kwenda kwa tajiri kuomba ng’ombe wa bure na kupewa, maishani mwake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘maziwa marahisi utajiri mgumu.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujibidisha kufanya kazi mpaga anapata mali, maishani mwake. Mtu huyo, hulima kwa bidii kubwa wakati wa mvua, mpaga anafaulu kupata chakula.

Chakula hicho, hukitumia kama chakula kwenye familia yake, na kingine hukiuza kwa ajili ya kujipatia mali. Yeye huwafundisha pia watu wake juu ya kuyatekeleza majukumu yao, kwa bidii hiyo, katika maisha yake.

Mtu huyo, ni mfano wa kuigwa kwa wenzake, katika kujibidisha kufanya kazi mpaga kufikia hatua ya kuyapata mafanikio mengi, kwa sababu ya bidii yake hiyo, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, ‘maziwa marahisi utajiri mgumu.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufayatelekeza majukumu yao kwa bidii kubwa, katika maisha yao, ili waweze kupata mafakinio ya kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Waebrania 12:14. “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana.”

Luka 13:24. “Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba, kwa maana, nawaambia, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.”

2 Petro 1:10. “Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuuthibitisha wito wenu na uteule wenu, kwa maana mkifanya hivyo, hamtajikwaa kamwe.”

cow milk-

cow-1

cow-2

 

ENGLISH: IT IS EASIER GETTING MILK THAN GETTING A COW.

The source of this proverb is the value of milk in relation to the value of cow. When you visit someone, you can easily get milk as present, but not cow. This is associated with value; milk is less valued while cows have more value. This is why people can say ‘it is easier getting milk than getting a cow.’

This proverb can be compared to a person who works hard to earn a living in his life. This person can spend well the rain season to cultivate his/her farm with an expectation to have good harvest at the end of season. Such a person teaches others that it is easier succeeding in life if deliberate efforts are taken seriously.

The proverb teaches people to work hard to carry out their responsibilities with great efforts in their lives. In so doing they can become very successful in life.

Hebrews 12:14: “Strive for peace with all men, and for the holiness without which no one will see the Lord.”

Luke 13:24: “Strive to enter by the narrow door; for many, I tell you, will seek to enter and will not be able.”

2 Peter 1:10: “Therefore, brethren, be the more zealous to confirm your call and election, for if you do this you will nevel fall.”

669. WAPI ADABHELAGA.

Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile bhupi bho ng’wa munhu. Umunhu uyo aliopi ng’wunuyo, nulu agab’iza alio wiza, aliyo ukubhangi, aguhayiwa giki ali opi noyi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘wapi adabhelaga.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijagwa kuli munhu uyo alina ng’holo ya wiza, umukikalile kakwe, aliyo ilihanga lwake lililya bhubhi. Umunhu ng’wunyo, agitaga mihayo ya wiza ukubhuye iyo ilikihamo niya gubhambilija abhanhu abho bhali mumakoye. Uweyi agikalaga na bhanhu chiza bho nduhu ugubhakomanya, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wuniyo agikolaga nu wapi uyo adabhelaga, kunguno nuweyi ali ni hanga libhi, aliyo ing’holo yakwe iliyawiza, iki agabhambilijaga abhiye abho bhalimukoye.

Aliyo lulu, kihamo ni ng’holo yakwe iyawiza yiniyo, abhangi bhagang’wilaga giki, alini hanga libhi noyi, guti nu opi uyo aliyowiza, aliyo agawilagwa, giki, ‘aliopi noyi.’ Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘wapi adabhelaga.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’holo ya wiza ya gwikala na bhanhu bho nduhu ugubhakomanya, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umuwikaji bhobho.

Zaburi 22:6-8.

Wimbo ulio bora 1:5-6.

Ayubu 30:30.

Maombolezo 4:8.

2 Wakorintho 4:16.

KISWAHILI: MWEUSI HAWI MZURI.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia weusi wa mtu. Mtu huyo ambaye ni mweusi, hata kama atakuwa mzuri, lakini kwa wengine, atasemwa kuwa ni mweusi mno. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘mweusi hawi mzuri.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana moyo mzuri, katika maisha yake, lakini sura yake ni mbaya. Mtu huyo, hutenda matendo mema kwa wenzake, yakiwemo  yale ya kuwasaidia wale walioko kwenye matatizo. Yeye huishi na watu vizuri bila ubaguzi, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na mweusi, ambaye huambiwa kuwa ni mweusi mno hata kama sura yake ni mzuri, kwa sababu naye sura yake ni mbaya, lakini moyo wake ni mzuri, kwa vile huwasaidia wenzake walioko kwenye matatizo.

Lakini pamoja na moyo wake huo kuwa mzuri, wengine humwambia kuwa ana sura mbaya mno, kama anavyoambiwa yule mtu mweusi. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘mweusi hawi mzuri.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na moyo mwema wa kuishi na watu bila kuwabagua, katika maisha yao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.

Zaburi 22:6-8.

Wimbo ulio bora 1:5-6.

Ayubu 30:30.

Maombolezo 4:8.

2 Wakorintho 4:16.

 

nkima ahakaya

masai-nkima

winga bho samburu

 

ENGLISH: A BLACK PERSON DOES NOT BECOME DECENT.

The source of this proverb is blackness. A person with black colour is always looked at in relation to negativity. Much as he/she can be beautiful, people will say but he/she is black. This is why people always say ‘a black person does not become decent.’

This proverb can be likened to a person who has a good heart in his/her life. However much this person might be helping others, people will end up looking at the bad side of him/her. He/she can have good appearance and presentable but, as long as he/she is black, people will begin hating him/her.

This proverb teaches people to live positively with others without prejudice. This will help them to be in harmony with others in their lives.

Psalm 22: 6-8. Song of Solomon 1: 5-6. Job 30:30. Lamentations 4: 8. 2 Corinthians 4:16.

668. DUBHELELILE GWIKALA NA NG´HANJO.

Imbuki ya lusumo lunulo, yingilile ku kikalile ka bhuzwaji bho ng’hanjo. Ing’hanjo yiniyo, jilijiswalo ijo jijilanijije gwingila kumabhega mpaga kumagulu, kunguno ya kugugwikoja umili go nzwaji oyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘dubhelelile gwikala na ng’hanjo.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina kaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunubho, againhaga ilange lya gwigulambija gutumama milimo iya guibheja chiza ikaya yakwe yiniyo. Uweyi adebhile uguilela chiza ikaya yakwe, kunguno ya bhukamu bhokwe ubho guitumama chiza imilimo yakwe, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu munhu uyo abhelelile gwikala na ng’hanjo, kunguno nuweyi agaibhejaga chiza ikaya yakwe, bho guinha ilange lyawiza, kugiki bhiyikole chiza, guti bhazwalile ng’hanjo, abhanhu bhakwe.

Uweyi alijigemelo ja gubheja kaya chiza ukubhiye, kunguno ya kikalile kakwe ako kalikawiza kenako. Hunagwene agabhawilaga abhanhu bhakwe giki, ‘dubhelelile gwikala na ng’hanjo.’ Ing’hanjo yiniyo, ili kaya iyo ili nilange lya wiza.

Usulumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kubheja kaya jabho chiza, bho gwigulambija guitumama chiza imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Wagalatia 3:26-27.

Marko 16:1-5.

Yohana 14:1.

KISWAHILI: INAFAA TUWE NA KANZU.

Chanzo cha methali hiyo, chatokea kwenye maisha ya uvaaji wa kanzu. Kanzu hiyo, ni vazi lilishonwa jumla kutoka mabegani hadi miguuni, kwa sababu ya kuuwezesha kufanana mwili wa mvaaji huyo wa kanzu. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘inafaa tuwe na kanzu.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, huipatia malezi mema familia yake hiyo. Malezi hayo, ni pamoja na yale ya kujibidisha kuyatekeleza majukumu yale yawezayo kuiendeleza vizuri familia yake. Yeye anafahamu namna ya kuilea vizuri familia yake hiyo, kwa sababu ya bidii yake ya kuyatekeleza vizuri majukumu yake.

Mtu huyo, hufanana na mtu anayependeza kuwa  na kanzu, kwa sababu naye huijenga vizuri familia yake kwa kuipatia malezi mema, ili waweze kuwa na maadili mema yanayofanana kama kuvaa kanzu. Yeye ni mfano wa kuigwa kwa kuwa na familia yenye malezi mema, kwa sababu ya maisha yake hayo yaliyo mema. Ndiyo maana yeye huwambia watu wake kwamba, ‘inafaa tuwe na kanzu.’ Kanzu hiyo, ni maskani au familia yenye mazezi mema.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujenga familia njema, kwa kujibidisha kuyatekeleza vyema majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Wagalatia 3:26-27.

Marko 16:1-5.

Yohana 14:1.

work eritrea

work2

south-africa working

 

ENGLISH: WE SHOULD HAVE A ROB.

The source of this saying is the wearing of garment. Garment is a type of cloth one puts on and it covers the whole body from shoulders to feet thus making the whole body being uniformly covered. That is why people say ‘we have to have a rob’ to mean uniformity.

This saying can be compared to a person who has a family and he/she is able to provide it with all what is necessary for the family to survive. This includes upbringing them and commitment to fulfill all family responsibilities. Such a person can be taken as an example to others on how to care for their famiies.

This saying teaches people how to build a good family. It makes people become successful in their lives.

Galatians 3: 26-27. Mark 16: 1-5. John 14: 1.