Sukuma Proverbs

686. NDA ITALUMBAGA.

Ulusumo lunulo, lwandija kujigano ja bhanigini ijo jilihigulya ya Nda na Nomo. Inda igalomba jiliwa yiliyomba, ‘ninhage jiliwa natubhaga.’ Unomo gugayinha guliyomba giki, ‘sologa jijaho.’ Inda igikomeja gulomba duhu bho nduhu ugulumbilija. Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba giki, ‘Nda italumbaga.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhahayile gwinhiwa bhuli ikanza bho nduhu ugulumbilija. Guti ni Nda iyo igabokelaga jiliwa ja bhuli mbika bho nduhu ugulumbilija, abhanhu bhanabha bhagacholaga solobho yabho duhu bho nduhu ugubhadilila abhichabho. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, ‘Nda italumbaga.’ Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa  bho 54.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhulumbilija uku bhanhu abho bhali bhinha ginhu jilebhe, kugiki bhadule nabho gutumama milimo ya solobho kubhichabho, kukila guitumama iyo ili na solobho kubhoyi duhu.

“UYesu Kristo adizile aha si henaha guchola solobho yakwe, aliyo agiza kunguno yise. Unangwa adintale noyi gukila ung’walimu okwe, aliyo itoshije unangwa gubhiza guti nu ng’walimu okwe.

Bhasi dudizubhiza bhanhu bha gwilola yise bhinghikili duhu. Igelelilwe difunye kunguno ya bhigusu guti numo UYesu Kristo agifunya kunguno yise.

IEkaristia bhuli bhulumbi. Mujitambo ja Misa duganumbilijaga Mulungu Bhabha kihamo nu Yesu Kristo nu mugati yakwe kuwiza bhose ubho oditila no no no ugudinha ubhupiji wise. Igelelilwe gufunya bhulumbi kuli mulungu bhuli makanza. Dudizubhiza bhanhu abho bhaginhiyagwa bho nduhu ugulumbilija. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukuraba bho 54.

Wafilipi 2:4.

Luka 17:17-18.

Matendo 20:35.

1Wakorintho 13:4.

KISWAHILI: TUMBO HALITOI SHUKRANI.

Methali hiyo ilianzia kwenye hadithi ya watoto inayohusu tumbo na mdomo. Tumbo aliomba chakula akisema, ‘nipatie chakula najisikia njaa.’ Mdomo ulimpatia ukisema, ‘chukua hicho hapo.’ Tumbo aliendelea kuomba bila kushukuru anapopewa.  Ndiyo maana watu wakaanza kusema  kwamba, ‘tumbo halitoi shukrani.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa wale watu ambao wanataka kupewa kila mara bila kutoa shukrani. Kama tumbo ambalo linapokea chakula cha kila aina bila kushukuru, watu hawa wanatafuta faida yao tu bila kuwajali wengine. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, ‘tumbo halitoi shukrani.’ Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 54.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na moyo wa shukrani kwa yale wanayopewa na wenzao, ili waweze kujifunza pia kufanya kazi kwa faida ya wenzao, badala ya kujinufaisha wao wenyewe tu.

“Yesu Kristo hakuja hapa duniani kutafuta faida yake, bali alikuja kwa ajili yetu. Mwanafunzi si mkuu zaidi kuliko mwalimu wake bali inatosha kwa mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake.

Basi tusiwe watu wa kujiangalia sisi wenyewe tu. Yafupasa kujitoa kwa ajili ya wenzetu kama Yesu Kristo alivyojitoa kwa ajili yetu.

Ekaristi maana yake ni kushukuru. Katika sadaka ya Misa tunamshukuru Mungu Baba pamoja na Yesu Kristo na ndani yake kwa mema yote ambayo ametutendea hasa kwa kupatia wokovu wetu. Yatupasa kutoa shukrani kwa Mungu kila wakati. Tusiwe watu ambao wanapewa bila kushukuru.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 54.

Wafilipi 2:4. “Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake.”

Luka 17:17-18. “Watu kumi walitakaswa, sivyo? Wale tisa wako wapi? Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?”

Matendo 20:35. “Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.”

1Wakorintho 13:4. “Upendo hautafuti faida yake binafsi.”

eating food

eating jackfruit

 

ENGLISH: THE STOMACH IS NEVER BE GRATEFUL.

This proverb has its origin on children stories about the stomach and the mouth. In the story, the stomach asked for food saying, ‘Give me food, I’m hungry.’ The mouth whispered, ‘Take it there.’ The stomach ate that food without saying thanks to mouth and asked for more after a while. This is why people came with this proverb that ‘the stomach is never be grateful.’

This proverb can be compared to those people who want to be given all the time without giving thanks. Like a stomach that receives all kinds of food without thanking the one that gave him, these people only look for their benefits without caring others (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 54). This book was written by: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

The proverb teaches people to be thankful for what others give. This can help people learn how to work for the benefit of others, instead of working for their own benefits.

Jesus Christ did not come to this world to seek His benefit, but He came for us. A student is no greater than his teacher but it is enough for the student to become like his teacher.

“So we must not be self-centered. We must give ourselves for our friends as Jesus Christ gave Himself for us.”

The Eucharist means thanksgiving. In the Mass offering we thank God the Father and Jesus Christ and in Him for all the good that He has done for us in particular for our salvation. We should always give thanks to God. We must not be the people who are given thanks (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 54).

 Philippians 2: 4. Luke 17: 17-18. Acts 20:35. 1Corinthians 13: 4.

685. LUFU LWA NG’HABHI LUKALILAGWA BHAGEHU.

Ulusumo lunulo, lwandija ku lufu lo mhunhu ng’habhi o jiji jilebhe. Ulushigu lunulo, bhalihoyi bhanhu bhagenhu noyi aha masugu genayo. Uumo obho agabhuja, ‘ni bhuli bhalihoyi bhanhu bhagehu chiniki ilelo.’ Ung’wikaji o muchalo jinijo, aganshogeja giki, ‘yilikunguno ya gugayiwa nyama aha lufu lo ng’habhi ng’wunuyo.’ Ungeni agayomba, ‘gashinaga abhanhu bhagajaga ukumasugu kunguno ya gulya nyama, kukila ugolecha bhumo bhobho!’ Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba giki, ‘lufu lwa ng’habhi lugalilagwa bhagehu.’

Usulumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagajaga ugujubhalunguja abho bhapandikaga masugu, bho kusolanya kunguno ya gusendamila gupandika ginhu jilebhe. Ihali yiniyo, igeng’helejaga kubhiza bhanhu bhagehu aha lufu lo ng’wa munhu uyo alig’habhi.

Aha lufu lwa nsabhi, bhagajaga hoyi bhanhu bhingi noyi, iki bhagalyaga nyama  nyingi hoyi. Hangi abhadugu wakwe unjimiji, bhagagabhanhaga sabho ijo jalekwa nu njimiji.

Aliyo lulu, aha lufu lwa ng’habhi, bhagashigaga hoyi bhagehu, kunguno ya kugaiwa inyama ya gulya. Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba giki, ‘lufu lwa ng’habhi lugalilagwa bhagehu.’ Rejea Kueneza Injili Kwa Methali, bhukurasa bho 52.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka kubhasolanya abhanhu abhasabhi na mahabhi. “Giko lulu, dudizubhiza na bhusolanya mugati ya bhanhu abho bhali bhasabhi, na bhahabhi, nulu abhanhu abho bhalibhatongeji, nabho bhadina bhutale.

Hangi dudizubhadalaha iki UYesu Kristo alimo umudati yabho pye abhose. No no no, umugati ya bhahabhi, bhajilema, nabho bhadidujije abho ubhutemi bho ng’wa Mulungu bhuli bhobho.

UYesu Kristo, agacha guti munhu ng’habhi noyi, iki umu lufu lwakwe bhalihoyi bhanhu bhagehu, aliyo ulufu lokwe luli lufu lwa nsabhi, ulo lugadusabhyaga aise pye abho danzunya. Bhuli munhu adulile gulya matwajo ayo gagigelaga umunti go nsalabha, ubho bhuli hubhupanga ubho bhulunga kele. Lolaga Kueneza Injili kwa  Methali, 52.

Yakobo 2:1-5.

Luka 10:22.

Waroma 5:10.

Yohane 3:14-15.

KISWAHILI: KIFO CHA FUKARA KINALILIWA NA WACHACHE.

Methali hiyo, ilianzia kwenye kifo cha mtu fukara wa kijiji furani. Siku hiyo, walihudhuria watu wachache sana. Mmoja akauliza, ‘kwa nini watu ni wachache hivi leo?’  Mwenyeji wa sehemu hiyo alimjibu, ‘ni kwa sababu ya kukosekana kwa nyama kwenye kifo cha mtu huyu furaka.’

Mgeni akasema, ‘kumbe watu huenda kulia kwenye msiba kwa sababu ya kutegemea kula nyama, badaya ya kuonesha umoja wao!’ Ndiyo maana watu wakaanza kusema kwamba, ‘kifo cha fukara kinaliliwa na wachache.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wanaoenda kufariji watu wenye matatizo kwa kubagua kwa sababu ya kutegemea kupata faida fulani. Hali hiyo, husababisha kuwepo kwa watu wachache kwenye kifo cha mtu maskini. Kwenye kifo cha tajiri huhudhuria watu wengi mno kwa kuwa hula nyama nyingi. Tena ndugu zake hugawana mali iliyoachwa na marehemu.

Lakini kwenye kifo cha fukara, hufika watu wachache kwa sababu ya kukosa nyama. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kifo cha fukara kinaliliwa na wachache.’ Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukuraka 52.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha ubaguzi kati ya watu matajiri na maskini. “Hivyo tusiwe na ubaguzi kati ya watu matajiri na maskini au kati ya watu wa cheo na wasio na cheo. Tena tusiwadharau kwa kuwa Yesu Kristo yumo ndani ya watu wote. Hasa yumo ndani ya watu maskini wenye kulemaa na wasiojiweza ambao ufalme wa Mungu ni wao.

Yesu Kristo alikufa kama mtu maskini, kwa kuwa kwenye kifo chake walikuwepo wachache, lakini kifo chake hasa ni kifo cha tajiri ambacho kinatutajirisha sisi sote tunaomwamini. Kila mtu aweza kula matunda yanayotokea katika mti wa msalala, yaani  uzima wa milele.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, 52.

Yakobo 2:1-5. “Ndugu zangu, kama waaminio katika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe na upendeleo kwa watu. Kwa maana kama akija mtu katika kusanyiko lenu akiwa amevaa pete ya dhahabu na mavazi mazuri, pia akaingia mtu maskini mwenye mavazi yaliyochakaa, nanyi mkampa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, ‘‘Keti hapa mahali pazuri,’’ lakini yule maskini mkamwambia, ‘‘Wewe simama pale,’’ au ‘‘Keti hapa sakafuni, karibu na miguu yangu,’’ je, hamjawabagua na kuwa mahakimu mioyoni mwenu mkihukumu kwa mawazo yenu maovu?   Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao?”

Luka 10:22. “Vitu vyote vimekabidhiwa mikononi Mwangu na Baba.                                             

Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.”

Waroma 5:10. “Kwa kuwa kama tulipokuwa adui wa Mungu tulipatanishwa naye kwa njia ya kifo cha Mwanawe, si zaidi sana tukiisha kupatanishwa, tutaokolewa kwa uzima Wake”

Yohane 3:14-15. “Kama vile Mose alivyomwinua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu. 15Ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele.”

people-burial

tanzania-jimasai

 

ENGLISH: THE DEATH OF THE POOR IS MOURNED BY FEW PEOPLE

This proverb has its origin from the death of a poor village man. In this poor man’s burial, only few people attended. One of the attendants asked, ‘why mourners are few?’ and the response was, ‘because the dead man was poor therefore, people knew that there would be no meat to eat in his burial.’ This is why people came with such a proverb that ‘the death of the poor is mourned by few people.’

This proverb can be likened to those people who discriminate others because of their social differences. Those people consider themselves as the successful ones in life and therefore they cannot associate with others who appear to be of low profile; poor. People know that, attending the burial of a rich person means having enough food to eat and, on the side of relatives, their attendance to burial means having a share in the distribution of the late’s properties (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 52). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

The proverb teaches people to stop discriminating between rich and poor. As the Holy scripture says, “So we must not discriminate between the rich and the poor. And let us not despise them for Jesus Christ is in all men. Especially the poor and crippled people of whom the kingdom of God belongs.

Jesus Christ died as a poor man, for at his death there were only a few, but his death was actually a rich death that enriches all of us who believe in Him. Every man is able to eat the fruit of the tree of life, namely, eternal life (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 52).

James 2: 1-5. Luke 10:22. Romans 5:10. John 3: 14-15.

684. CHUGA JA NKOGO (IPANDO LYA NGOGO) ITABHANYA BHALOSO. NULU “NUNDI GWANGOKO ITABHANYA BHALOSO.”

Ulusumo lunulo, lwingilile kuli munhu uyo alinhaku ogulya nyama. Alihoyi namhala umo uyo oli adina mino. Uweyi  oliatogilwe gulya nyama ja nofu. Lushigu lumo agalomba nyama kubhiye, aliyomba, ‘ninhagi inyama nalye.’  Abhiye bhang’winha bhaliyomba, ‘solaga yiyi.’

Gashinaga inyama iyo bhagang’winha lyali pando lya ngoko, lulu, nundi go ngoko. Ohayugema ugugulya gunemela kulwa bhudamu bhogo.  Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagandya guyuyomba giki, ‘chuga ja ngoko (ipando lya ngoko) itabhanya bhaloso.’ Nulu ‘Nundi go ngoko itabhanya bhaloso.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina wikumvi bho gulya nyama nsoga bhuli makanza. Umunhu ng’wunuyo, ulu ugayiwa inyama ija jofu agagemaga yoseyose. Uluwinhiwa gugulu go ngoko aguduma ugugubhinza na agukoyakoya noyi ugugudakuna.

Uweyi agikiloaga nu ngosha uyo alina wikumvi bho guja kuli nkima uyo aliowiza. Nang’hwe ulu ugaiwa agakoya koyaga noyi, guti nu ni ogugulu go ngoko. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘chuga ja ngoko (ipando lya ngoko) itabhanya bhaloso.’ Nulu ‘Nundi go ngoko itabhanya bhaloso.’ Lolaga kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 50.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleka bhulaku, nulu wikumvi bho gwita yabhubhi, umuwikaji bhobho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umukikalile kabho.

Yilijidamu noyi ukubhanhu abho bhagatongelagwa na wikumvi bho gwita mihayo ya bhubhi aha welelo, ugugaluka. Ukwene hu guleka uwikaji bho gwita iyabhubhi na gwingila muwikaji bhupya ubho gwita ya wiza. (Matayo 19:23-26).

Umuwikaji wise dulilomba wambilijiwa bho ng’wa Mulungu na jinhilwa ja ng’wa Moyo Ng’wela, kunguno ubho nguzu jise bhung’wene, dududula ugwita josejose. Ulu dunomba Mulungu bho guzunya dugubhedecha, iki ayo gadadulikanile ukubhanhu, gadulikanile ukuli Mulungu. Rejea Kueneza Injili Kwa Methali, bhukurasa bho 50.

Matendo ya mitume 24:24-25.

Marko 10:22.

Marko 4:19.

Tito 2:12.

KISWAHILI: KIKWATO CHA KUKU HUWAHANGAISHA WENYE TAMAA (WANAOPENDA KULA NYAMA KILA WAKATI).

Methali hiyo, yatokea kwa mtu yule ambaye ni mlafi wa kula nyama. Alikuwepo mzee mmoja ambaye hakuwa na meno. Yeye alipenda kula nyama ya minofu. Siku moja aliomba nyama kwa wenzake akisema, ‘nipeni nyama nile.’ Wenzake hao, walimpatia wakisema, ‘chukua hii.’

Kumbe, hiyo nyama waliyompatia yilikuwa ya kwato la kuku, au mguu wa kuku. Alipojaribu kula ikamshinda, kwa sababu ya ugumu wake. Ndiyo maana watu wakaanza kusema kwamba, ‘kikwato cha kuku huwahangaisha wenye tamaa (wanaopenda kula nyama kila wakati).’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye tamaa ya kula nyama nzuri kila wakati. Mtu huyo, akikosa nyama hiyo, huhangaika sana, kwa kujaribu kile anachokiona. Akipewa kwato au mguu wa kuku, hushindwa kuuvunja na huhangaika sana kuutafuna.

Yeye hufanana na mwanamume yule ambaye ni mwenye tamaa ya kwenda kwa mwanamke anayemuona kuwa ni mzuri. Naye akimkosa huhangaika sana katika maisha yake, kama mtu yule aliyeshindwa kula kikwato cha kuku. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kikwato cha kuku huwahangaisha wenye tamaa (wanaopenda kula nyama kila wakati).’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 50.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuachana na tabia ya ulafi au tamaa ya kutenda maovu, maishani mwao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, katika maisha yao.

Ni vigumu sana kwa watu wale ambao wanatawaliwa na tamaa za kufanya anasa za hapa duniani, kugeuka, yaani kuacha maisha ya namna hiyo na kuwa na maisha mapya (Mathayo 19:23-26).

Katika unyonge wetu tunahitaji msaada wa Mungu na vipawa vya Roho Mtakatifu, kwa kuwa kwa nguzu zetu hatuwezi kufanya lolote. Tukimwomba Mungu kwa imani tutafanikiwa kwa kuwa yasiyowezekana kwa mwanadamu, yawezekana kwa Mungu. Rejea Kueneza Injili Kwa Methali, bhukurasa bho 50.

Matendo ya mitume 24:24-25. “Baada ya siku kadhaa Feliksi alipokuja pamoja na Drusila mkewe, ambaye alikuwa Myahudi, alituma aitiwe Paulo na kumsikiliza alipokuwa akinena juu ya imani katika Yesu Kristo. Naye Paulo alipokuwa akinena juu ya haki kuwa na kiasi na juu ya hukumu ijayo, Feliksi aliingiwa na hofu na kusema, “Hiyo yatosha sasa! Waweza kuondoka. Nitakapokuwa na wasaa nitakuita.””

Marko 10:22. “Yule mtu aliposikia hayo, akasikitika sana, akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.”

Marko 4:19. “lakini masumbufu ya maisha haya, udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae.”

Tito 2:12. “Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu, katika ulimwengu huu wa sasa, huku.”

chicken-1

chicken2

chicken3

ENGLISH: CHICKEN LEGS PUNISHED THE GREEDY MEAT EATER.

This proverb comes from a greedy person. Some days back, there was a toothless old person who preferred eating boneless meat. One day he asked for meat from his friends. He said, ‘Give me some meat to eat.’

Instead of giving him boneless meat, they gave him chicken legs. He tried eating it but it was not easy to chew the bones. This is where the proverb ‘chicken legs punished the greedy meat eater’ came into being.

This proverb can be likened to a man who always want to eat good meat. Such a person will be uncomfortable if there is no meat to eat. This person can be compared to a man who always chase for beautiful ladies. At the end of the day, this man is likely to land on a difficult woman who will cause trouble to him (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 50). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

This proverb teaches people to break free from the desire to do evil things in life. This can make one to live in harmony with others in their lives.

It is very difficult for those people who are ruled by the lust of this world to turn around, to give up such a life and to have a new life (Matthew 19: 23-26).

In our weaknesses we need the help of God and the gifts of the Holy Spirit, for in our own strength we cannot do anything. If we ask God in faith we will succeed because whatever is impossible to man, it is possible with God (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 50).

Mark 10:22. Mark 4:19 .Titus 2:12.

683. NTEMI NYIA NA MBOZU.

Ulusumo lunulo, lwingila ku wikaji bho Ntemi o Jisuguma, uyo obhabokelaga abhanhu abho bhalemagwa na bhananzengo bhakwe. Munanzengo umo agamuja UNtemi, “ni bhuli ugabhabokelaga abhanhu abho bhali na kajile kabhi?” UNtemi aganshokeja, “unene nagalyaga na bhanhu bhose, abhawiza na bhabhubhi, kunguno abhenabho pye, bhali bhanhu bhane.” Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba giki, ‘Ntemi nyia na mbozu.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhatongeji, nabho bhagabhabokelaga na gubhalisha bhanhu bha mbiga jose, bho nduhu ubhusolanya. Dugemele, umunhu uyo ali na bhusadu bho mbiji, “mbozu”, umunhu uyo ali nabhubhozu, umunhu uyo ali na nhungwa ja bhubhi, jilema, Namba (Malaya) na yingi guti yiniyo. Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 44.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Abhanhu bhenabho, bhagabhalangaga abhanhu bhabho, inzila ja gubhabokela abhanhu bhose bho nduhu bhusolanya. Abhoyi bhagikolaga nu Ntemi uo Jisuguma uyo obhabokelaga pye abhanhu, kunguno nabhoyi bhagikalaga na bhanhu bhose, bhawiza  na bhabhubhi. Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba giki, ‘Ntemi Nyia na Mbozu.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wizang’holo bho gubhakaribhusha pye abhanhu bho nduhu, bhusolanya bho rangi, ikabhila nabho Lihanga.

Ahanaha Welelo bhulihoyi bhutemi bhubhili. UYesu Kristo, agayomba giki, “nali na nzala uganinha ijiliwa.’ Adayombile higulya ya bhanhu abho bhalibhitila ya bhubhi abhichabho, aliyo agayomba higulya ya bhanhu abho bhadabhadililaga nulu, bhadihoyi moyi, aliyo agayomba giki bhanhu abho bhadadililaga nulu abho bhagayombaga giki, bhadihoyi moyi, na gali makoye ukubhanhu.

Ishibhi idi gubhitila abhanhu yabhubhi duhu, aliyo ili gukija ugutimija iyo igelelilwe bhayitimije, na guyomba giki, bhadiho moyi umumakoye ga bhanhu. Dudizubhiza bhanhu abho dulichola solobho ise, aliyo ibhize solobho ya bhigisu.

Dubhize guti Ntemi Yesu Kristo, uyo agifunya kunguno ya bhigisu, nulu ng’wanishi ubhusolanya. Umuyiniyo, dugumanyika igiki, dulihoyi ng’hana UBhutemi bhotwe, duduleng’wa ahalushigu ulo Nhalikijo. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 45.

Luka 14:13-14.

Methali 31:8-9.

Marko 10:45.

Mathayo 25:34-36.

Zaburi ya 23.

Yohane 10:11.

KISWAHILI: MTEMI HULA NA MWENYE KUOZA.

Methali hiyo, ilianzia kwenye maisha ya Mtemi wa Kisukuma aliyekuwa anawapokea watu waliokataliwa na wananchi wake. Mwananchi mmoja alimuuliza mtemi, ‘kwa nini unawapokea watu wenye tabia mbaya?’ Mtemi alijibu, ‘mimi hula na watu wote wabaya na wema, kwa sababu watu hao wote ni wangu.’ Ndiyo maana watu wakanza kusema kwamba, ‘mtemi hula na mwenye kuoza.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa viongozi na wale wanaowapokea na kuwalisha watu wa kila aina bila ubaguzi. Kwa mfano, mtu mwenye ugonjwa wa ukoma, “mbozu” yaani mtu mwenye hali ya kuoza, mtu mwenye sifa mbaya, kama vile kiwete, Malaya na kadhalika. Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 44.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Watu hao huwafundisha watu wao namna ya kuwakaribisha watu wote bila ubaguzi, kwa njia ya maisha yao. Wao wanafanana na Mtemi wa kisukuma aliyewapokea watu wote, kwa sababu nao pia huishi na watu wote, wema na wabaya. Ndiyo maana watu hao huwaambia watu kwamba, ‘Mtemi hula na mwenye kuoza.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwakaribisha watu wote bila ubaguzi. Kama ‘Mtemi wa Kisukuma”, Mungu ni Baba ambaye hana ubaguzi. Huwapenda na kuwalisha watu wote bila kujali rangi ya mtu au kabila au Taifa.

Hapa duniani kuna falme za aina mbili. Ufalme wa watu ambao wanajali au wanahusika na shida za watu. Yesu Kristo aliposema, “nilikuwa na njaa hukunipa chakula,” hakusema juu ya watu ambao wanawatendea wenzao vibaya, bali alisema juu ya watu ambao hawajali au hawahusiki na shida za watu.

Dhambi sio kuwatendea watu mabaya tu, bali ni kutotimiza wajibu wetu, kutojali na kutohusika na shida za watu. Tusiwe watu ambao tunatafuta faida yetu bali faida ya wenzetu.

Tuwe kama Mtemi Yesu Kristo aliyejitoa kwa ajili ya wenzetu, hata adui ubabuzi. Katika hili tutajulikana kwamba tumo kweli katika ufalme wake na hatutakataliwa siku ya mwisho. Rejea Kueneza Injili kwa Methali, 45.

Luka 14:13-14. “Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu, nawe utabarikiwa kwa sababu hawa hawana uwezo wa kukulipa. Mungu atakulipa wakati wa ufufuo wa wenye haki.””

Methali 31:8-9. “Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea, kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa. Sema na uamue kwa haki, tetea haki za maskini na wahitaji.”

Marko 10:45. “Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai Wake kuwa ukombozi kwa ajili ya wengi.”

Mathayo 25:34-36. “Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wake wa kuume, ‘Njoni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha, nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.’”

Zaburi ya 23.1-6.  “BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza, huihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami, rungu yako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu,  kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.”

Yohane 10:11. ‘‘Mimi ndimi Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema huutoa uhai Wake kwa ajili ya kondoo.”

king1

chief

king2

 

ENGLISH: THE CHIEF EATS WITH ALL PEOPLE.

This saying has its origin on the Sukuma chief who used to receive people who were refused by his citizens. One day, one of his citizens asked him: ‘Why do you receive even bad people?’ The chief replied, ‘I eat with all people; the bad and the good ones because they are all mine.’

This saying can be compared to leaders and those who receive and feed people of all kinds, for example, people with leprosy, lame, prostitutes, and so on (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs’, page 44). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

These people teach their fellows how to welcome all people in their lives.

This proverb teaches people about generosity of welcoming all people with impartiality. As the Sukuma chief, God is an impartial Father. People need to love and feed all people regardless of their race or ethnic or national origin.

There are two kingdoms on earth. A kingdom of people who care for or deal with people’s problems and another kingdom of people who are not concerned about people’s problem. When Jesus Christ said, “I was hungry and you did not give me food,” he was not talking about people who treat others badly, but rather about people who do not care about others or are not concerned about people’s problems.

Sin is not just doing wrong to people, but not fulfilling our responsibility, being careless and not dealing with people’s problems. We shouldn’t be the people we seek for our own benefit but the benefit of our fellow men.

Let us be like the Lord Jesus Christ who gave Himself for all. In this we shall be known that we are truly in His kingdom and will not be rejected on the last day (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 45).

Luke 14: 13-14. Proverbs 31: 8-9. Mark 10:45. Matthew 25: 34-36. Psalm 23. John 10:11.

682. KULYA N’GWA MPANGA TUKIKALAGA HA NGEGU (LUGEGU).

Ulusumo lunulo, lofumila mulyimbo lya Nhingi, Shagembe, uyo agang’wimbila nywani okwe, Nchimani:

“Unene naduduja uguleka ugung’wa uwalwa, Nchimani ng’wana o ng’wa Mulola, muna Kadoto. UMulungu adina mahoya ulu uhaya gugusola. Bhabehi ugulya ng’wa mpanga dugikala ha ngegu. Abho mtogilwe gubyaja sabho na ng’wisabhe guti ng’walagana nu Mulungu. Bhabehi! Nalimuwila, gulya ng’wa mpanga dugikalaga ha ngegu.” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 42.

 Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagatumilaga chiza ijiliwa ijo bhinhiwa nu Mulungu. Giko, abhoyi bhadebhile igiki, bhinhiwa jiliwa na Mulungu, ijo igelelilwe bhajilye haho bhatali bhapanga.

Bhalihoyi bhanhu bhamo abho bhalemile ugulya, nulu, ugujitumila isabho ijaha welelo. Abhanhu bha mbika jinijo, bhadina masala, dugemele, umunhu alina ng’ombe nyingi, aliyo abhana bhakwe na nke okwe, bhagazwalaga sagala sagala.

Hangi, bhadina bhulalo bhusoga. Ulu umo obho usada bhalemile ujinga ng’ombe bhang’wambilije. Hunagwene abho bhadebhile isolobho ya gujitumila chiza isabho jinijo, bhagabhawilaga abhanhu bhenabho, giki, ‘kulya ng’wa mpanga tukikalaga ha ngegu (lugegu).’ Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ubhukurasa bho 42.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu giki, idina solobho uguleka ugulya ijiliwa nulu, uguleka ujitumila isabho ijo bhinhiwa nu Mulungu. “Giko ugukija ugulya ijiliwa ijo dalekelwa nu Yesu Kristo, idina solobho.

UYesu Kristo ng’winikili, agadukomelejaga gulya mili gokwe na gung’wa milinga gakwe, mu Sakramenti ya Ekaristi Nhagatifu. Ulu dutali aha welelo igubhiza mhayo go nyabuli ulu dukija gulya umili gokwe nu gung’wa amilinga gakwe, iki “kulya ng’wa mpanga tukikalaga ha ngegu (lugegu).

Hangi ijililwa iji jidaliyagwa na bhanhu abho bhacha, ukwene huguhaya, abhanhu abho bhali mushibhi, ijoyi jigaliyagwa na bhanhu abho bhali na mioyo yape na guzunya…Ulu duli mushibhi igelelilwe dulumbwe ishibhi haho dutali ugubhokela Ekaristi. Ee, ugalyaga bho nduhu ugukalabha amakono?” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ubhukurasa bho 43.

Mhubiri 5:18-19.

Zaburi 128:1-2.

Mathayo 26:26-28.

Yohane 6: 52-53.

KISWAHILI: MWENYE KULA NI MTU HAI TUNAKAA UKINGONI.

Methali hiyo, imetokea kwenye wimbo wa Manju Shagembe aliyemwimbia rafiki yake Nchimani:

“Mimi siwezi kuacha kunywa pombe, Nchimani bin Mulola, wa Kadoto. Mungu hana maongezi kama akitaka kukuchukua. Jamani kula tukingalia hai, kwani, huwa tunakaa ukingoni. Mnaopenda kuzalisha mali na mtajirike kama mna mapatano na Mungu. Jamani! Nawaambieni, kula tungali hai kwani tunakaa ukingoni.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 42.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wanaotumia vizuri chakula ambacho wamepewa na Mungu. Hivyo, wanafahamu kwamba, wamegawiwa chakula na Mungu ambacho ni lazima wakile wakati wangali wazima.

Wako baadhi ya watu ambao hawataki kula au kutumia mali ya hapa duniani. Watu wa namna hiyo hawana akili, kwa mfano, mtu ana ng’ombe wengi, lakini watoto wake na mke wake huvaa ovyo ovyo.

Tena hawana mahali pazuri pa kulala. Ikiwa mmoja wao amepatwa na ugonjwa hataki kuuza ng’ombe amsaidie. Ndiyo maana wale wanafahamu umuhimu wa kuvitumia vizuri mali walivyo navyo, huwaambia watu hao kwamba, ‘mwenye kula ni mtu hai, tunakaa ukingoni.’ Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa, 42.

Methali hiyo, huwafundisha watu kwamba, haina maana kutokula chakula au kutokutumia mali ambazo wamepewa na Mungu. “Vile vile kutokula chakula tulichoachiwa na Yesu Kristo pia, haina maana.

Yesu Kristo mwenyewe hutuhimiza kula mwili wake na kunywa damu yake katika Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. Ikiwa bado tupo hapa duniani litakuwa jambo la kipumbavu tusipokula mwili wake na kunywa damu yake kwa kuwa. “Mwenye kula ni mtu hai, tunakaa ukingoni.”

Tena chakula hiki hakiwezi kuliwa na watu ambao wamekufa, yaani watu ambao wamo katika hali ya dhambi, bali huliwa na watu wenye mioyo safi na imani…Ikiwa tumo katika hali ya dhambi yatupata kuungama kabla ya kupokea Ekaristi. Je, hula bila kunawa mikono?” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 43.

Mhubiri 5:18-19. “Ndipo nikatambua kwamba ni vema na sahihi kwa mtu kula na kunywa na kutosheka katika kazi yake ngumu chini ya jua katika siku chache za maisha yake Mungu alizompa, kwa maana hili ndilo fungu lake. Zaidi ya yote, Mungu anapompa mtu ye yote utajiri na milki, humwezesha kuvifurahia, kukubali fungu lake na kuwa na furaha katika kazi yake, hii ni karama ya Mungu.”

Zaburi 128:1-2. “Heri ni wale wote wamchao BWANA, waendao katika njia zake. Utakula matunda ya kazi yako, Baraka na mafanikio vitakuwa vyako.”

Mathayo 26:26-28. “Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, ‘‘Twaeni, mle, huu ndio mwili wangu.’’Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa akisema, ‘‘Kunyweni nyote katika kikombe hiki. Hii ndiyo damu yangu ya agano, ile imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”

Yohane 6: 52-53. “Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?’’ Hivyo Yesu akawaambia, “Amini, amini, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu.”

africa uganda

food5

ENGLISH: OUR DAYS TO LIVE ON EARTH ARE NUMBERED, EATING IS IMPORANT.

This saying comes from Manju Shagembe’s song who was singing to his friend Nchimani:

“I cannot stop drinking alcohol, Nchimani, Mulola’son’son, of Kadoto. God has no negotiation if He wants to take you. Eat while still alive, for we are always on the brink. You who want to produce wealth and get rich as if you have agreement with God. Hello! I tell you, “Eating is life to human being” (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 42). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

This saying can be compared to those people who make good use of the food given to them by God. Such people have food that can make them eat throughout their life on earth. This saying also can be compared to someone who has enough riches but does not spend it well for the benefit of his/her children as a result, they can end up dying poorly. In such a scenario of not spending well the riches one has, one can experience things such as failing to have a good place to sleep, and not attending well family members when have problems. That is why those who are aware of the importance of using the resources they  tell those people, ‘The days to live on earth are numbered, eating is important’ (Refer to ‘Gospel Spelling in Proverbs,’ page 42).

This saying teaches people to spend well what they have managed to get in their lives. For Christians, not eating food Jesus left us with is none sense; it makes us die a satanic death.

Jesus Christ Himself urges us to eat His flesh and drink His blood in the Sacrament of the Holy Eucharist. If we are still here on earth it would be foolish for us not to eat His body and drink His blood. “Eating is life to human being who live on the brink.”

And this food cannot be eaten by people who are dead, that is, people who are in a state of sin, but is eaten by people who have a pure heart and faith. Do you eat without washing your hands? ” (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 43).

Ecclesiastes 5:18-19  “ This is what I have observed to be good: that it is appropriate for a person to eat, to drink and to find satisfaction in their toilsome labour under the sun during the few days of life God has given him –this is their lot. Moroever, when God gives someone wealth and possessions, and the ability to enjoy them, to accept their lot be happy in their toil –this is a gift of God.”

Psalm: 128:1-2 “ Blessed are all who fear the LORD, who walk in obedience to him. You will eat the fruit of your of your labour; blessings and prosperity will be yours.”

Matthew 26:26-28 “ While they were eating Jesus took bread, and when he had given thanks, he broke it and gave it to his deciples, saying, ‘take and eat; this is my body.’ The he took a cup, and when he had given thanks, he gave it to them, saying ‘Drink from it, all of you. This is my blood of the covenant, which is poured out for many for the forgiveness of sins.”

John 6: 52-53 “ Then the Jews began to argue sharply among themselves, ‘How can this man give us his flesh to eat?’ Jesus said to them, ‘very truly I tell you, unless you eat the flesh of the son of Man and drink his blood, you have no life in you.’”