Ulusumo lunulo, lwingilile kuli munhu uyo alinhaku ogulya nyama. Alihoyi namhala umo uyo oli adina mino. Uweyi oliatogilwe gulya nyama ja nofu. Lushigu lumo agalomba nyama kubhiye, aliyomba, ‘ninhagi inyama nalye.’ Abhiye bhang’winha bhaliyomba, ‘solaga yiyi.’
Gashinaga inyama iyo bhagang’winha lyali pando lya ngoko, lulu, nundi go ngoko. Ohayugema ugugulya gunemela kulwa bhudamu bhogo. Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagandya guyuyomba giki, ‘chuga ja ngoko (ipando lya ngoko) itabhanya bhaloso.’ Nulu ‘Nundi go ngoko itabhanya bhaloso.’
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina wikumvi bho gulya nyama nsoga bhuli makanza. Umunhu ng’wunuyo, ulu ugayiwa inyama ija jofu agagemaga yoseyose. Uluwinhiwa gugulu go ngoko aguduma ugugubhinza na agukoyakoya noyi ugugudakuna.
Uweyi agikiloaga nu ngosha uyo alina wikumvi bho guja kuli nkima uyo aliowiza. Nang’hwe ulu ugaiwa agakoya koyaga noyi, guti nu ni ogugulu go ngoko. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘chuga ja ngoko (ipando lya ngoko) itabhanya bhaloso.’ Nulu ‘Nundi go ngoko itabhanya bhaloso.’ Lolaga kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 50.
Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleka bhulaku, nulu wikumvi bho gwita yabhubhi, umuwikaji bhobho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umukikalile kabho.
Yilijidamu noyi ukubhanhu abho bhagatongelagwa na wikumvi bho gwita mihayo ya bhubhi aha welelo, ugugaluka. Ukwene hu guleka uwikaji bho gwita iyabhubhi na gwingila muwikaji bhupya ubho gwita ya wiza. (Matayo 19:23-26).
Umuwikaji wise dulilomba wambilijiwa bho ng’wa Mulungu na jinhilwa ja ng’wa Moyo Ng’wela, kunguno ubho nguzu jise bhung’wene, dududula ugwita josejose. Ulu dunomba Mulungu bho guzunya dugubhedecha, iki ayo gadadulikanile ukubhanhu, gadulikanile ukuli Mulungu. Rejea Kueneza Injili Kwa Methali, bhukurasa bho 50.
Matendo ya mitume 24:24-25.
Marko 10:22.
Marko 4:19.
Tito 2:12.
KISWAHILI: KIKWATO CHA KUKU HUWAHANGAISHA WENYE TAMAA (WANAOPENDA KULA NYAMA KILA WAKATI).
Methali hiyo, yatokea kwa mtu yule ambaye ni mlafi wa kula nyama. Alikuwepo mzee mmoja ambaye hakuwa na meno. Yeye alipenda kula nyama ya minofu. Siku moja aliomba nyama kwa wenzake akisema, ‘nipeni nyama nile.’ Wenzake hao, walimpatia wakisema, ‘chukua hii.’
Kumbe, hiyo nyama waliyompatia yilikuwa ya kwato la kuku, au mguu wa kuku. Alipojaribu kula ikamshinda, kwa sababu ya ugumu wake. Ndiyo maana watu wakaanza kusema kwamba, ‘kikwato cha kuku huwahangaisha wenye tamaa (wanaopenda kula nyama kila wakati).’
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye tamaa ya kula nyama nzuri kila wakati. Mtu huyo, akikosa nyama hiyo, huhangaika sana, kwa kujaribu kile anachokiona. Akipewa kwato au mguu wa kuku, hushindwa kuuvunja na huhangaika sana kuutafuna.
Yeye hufanana na mwanamume yule ambaye ni mwenye tamaa ya kwenda kwa mwanamke anayemuona kuwa ni mzuri. Naye akimkosa huhangaika sana katika maisha yake, kama mtu yule aliyeshindwa kula kikwato cha kuku. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kikwato cha kuku huwahangaisha wenye tamaa (wanaopenda kula nyama kila wakati).’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 50.
Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuachana na tabia ya ulafi au tamaa ya kutenda maovu, maishani mwao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, katika maisha yao.
Ni vigumu sana kwa watu wale ambao wanatawaliwa na tamaa za kufanya anasa za hapa duniani, kugeuka, yaani kuacha maisha ya namna hiyo na kuwa na maisha mapya (Mathayo 19:23-26).
Katika unyonge wetu tunahitaji msaada wa Mungu na vipawa vya Roho Mtakatifu, kwa kuwa kwa nguzu zetu hatuwezi kufanya lolote. Tukimwomba Mungu kwa imani tutafanikiwa kwa kuwa yasiyowezekana kwa mwanadamu, yawezekana kwa Mungu. Rejea Kueneza Injili Kwa Methali, bhukurasa bho 50.
Matendo ya mitume 24:24-25. “Baada ya siku kadhaa Feliksi alipokuja pamoja na Drusila mkewe, ambaye alikuwa Myahudi, alituma aitiwe Paulo na kumsikiliza alipokuwa akinena juu ya imani katika Yesu Kristo. Naye Paulo alipokuwa akinena juu ya haki kuwa na kiasi na juu ya hukumu ijayo, Feliksi aliingiwa na hofu na kusema, “Hiyo yatosha sasa! Waweza kuondoka. Nitakapokuwa na wasaa nitakuita.””
Marko 10:22. “Yule mtu aliposikia hayo, akasikitika sana, akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.”
Marko 4:19. “lakini masumbufu ya maisha haya, udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae.”
Tito 2:12. “Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu, katika ulimwengu huu wa sasa, huku.”
ENGLISH: CHICKEN LEGS PUNISHED THE GREEDY MEAT EATER.
This proverb comes from a greedy person. Some days back, there was a toothless old person who preferred eating boneless meat. One day he asked for meat from his friends. He said, ‘Give me some meat to eat.’
Instead of giving him boneless meat, they gave him chicken legs. He tried eating it but it was not easy to chew the bones. This is where the proverb ‘chicken legs punished the greedy meat eater’ came into being.
This proverb can be likened to a man who always want to eat good meat. Such a person will be uncomfortable if there is no meat to eat. This person can be compared to a man who always chase for beautiful ladies. At the end of the day, this man is likely to land on a difficult woman who will cause trouble to him (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 50). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.
This proverb teaches people to break free from the desire to do evil things in life. This can make one to live in harmony with others in their lives.
It is very difficult for those people who are ruled by the lust of this world to turn around, to give up such a life and to have a new life (Matthew 19: 23-26).
In our weaknesses we need the help of God and the gifts of the Holy Spirit, for in our own strength we cannot do anything. If we ask God in faith we will succeed because whatever is impossible to man, it is possible with God (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 50).
Mark 10:22. Mark 4:19 .Titus 2:12.