Author: Sukuma legacy

235. IGELE LYA B’AKENGEJI B’A NDOLELEJI

IGELE LYA B’AKENGEJI B’A NDOLELEJI

Ligele lya bhakengeji b’a Ndoleleji bhalimba lyimbo lya kubhab’ilinga abhanhu guja gujusalila bho gufuada inzila ya guja kubhupanga na guileka iyo ijile kubhujimiji.

KISWAHILI: KIKUNDI CHA KAMATI YA UTAFITI NDOLELEJI

Kikundi cha Kamati ya utafiti Ndoleleji wakiimba wimbo wa kuwaalika watu kwenda kusali kwa kuifuata njia iendayo kwenye uzima wa milele, na kuiacha ile endayo kwenye upotevu.

ENGLISH: NDOLELEJI RESEARCH COMMITTEE GROUP

Ndoleleji Research Committee Group singing a song that invites people to pray by following the way that leads to eternal life instead of that which misleads them. Video

IMG_20190717_114717_9

234. NTUMAMILA JAKWE ADILAMBAGA MAKONO

Imbuki ya kahayile kenako ilolile munhu uyo alitumamila sabho jakwe. Umunhu ng’wunuyo agajitumamilaga na wisandazu bhutale isabho jinijo, kunguno adebhile umo ojikoyakeyelaga ugujipandika.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagaitumamaga imilimo bhobhukamu mpaka bhajipandika isabho. Abhanhu bhenabho bhagajitumamigala isabho jinijo bho wisandazu bhutale, kunguno jilisabho jabho.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhukamu bho gutumama milimo kugiki bhadule gupandika sabho jabho. Isabho jinijo hijo bhagujitumamila na wisandazu, kunguno untumamila jakwe adilambaga makono.

Mathayo 20:1-16.

Walawi 19:13.

Kumbukumbu 24:15.

KISWAHILI: MTUMIA ZA KWAKE HAJILAMBI MIKONO

Chanzo cha msemo huo huangalia mtu atumiaye mali zake. Mtu huyo huzitumia mali hizo kwa uhuru mkubwa, kwa sababu afahamu jimsi alivyozihangaikia katika kuzipata.

Msemo huo hulinganishwa kwa watu wale wafanyao kazi kwa bidii sana mpaka kufikia hatua ya kupata mali. Watu hao huzitumia mali hizo kwa uhuru mkubwa kwa sababu ni zao wenyewe.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kutosha kufanya kazi ziwezao kuwapatia mali na mafanikio makubwa maishani mwao. Mali hizo huwapa nafasi ya kuzitumia kwa furaha, kwa sababu atumiaye mali zake hajilambi mikono.

Mathayo 20:1-16.

Walawi 19:13.

Kumbukumbu 24:15.

interesting-

ENGLISH: ONE WHO USES HIS/HERS DOES NOT LICK HIS/HER HANDS

The above saying is about a person who exploits his/her wealth. Such a person uses his/her wealth with great freedom because he/she knows how he/she struggled to amass it.

The saying relates to people who work very hard to enable them acquire richness. Such people exploit these riches with a lot of freedom because they belong to them after all.

The saying teaches people about being diligent enough to do work that can give them wealth and great success in their lives. Ownership guarantees one the sense of security and gives them the opportunity to use their property happily, because ‘one who uses his/hers does not lick hands.’

Matthew 20: 1-16.

Leviticus 19:13

Deuteronomy 24:15.

233. IJO JINIHANGA JILINIGUDI

Imbuki ya Lusumo lunulo ilolile ihanga na nhuni ya ng’wa munhu. Ilihanga ligalingisilaga wandijo b’o ng’wa munhu, nulu ginhu jileb’e. Inhuni igalingisilaga nhalikijo yakwe umunhu ng’wunuyo, nulu iginhu jinijo.

Kuyiniyo lulu, b’uli jene ijo jilinihanga jidagaiyagwa inhuni, ilingisilile giki, b’uli jene ijilinawandijo jidagayiyagwa inhalikijo.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kub’anhu abho bhagiganikaga giki, b’agwikala bhulunga kele ehenaha welelo. Kunguno yiniyo lulu, ulu umo ob’o winga kuwelelo, bhagapandikaga wib’akizu bho gudula nulu gucha, kunguno ya wib’akizu b’unubho. Abhanhu bhenabho b’aghibhaga igiki, b’ulijene ijo jilinihanga jina nhuni.

Ijinagongeja, ulusumo lunulo hangi lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagapandikaga mayange, nulu matwajo ayo galikihamo na bhusab’i, gub’iza bhalinhola, gupandika milimo na yingi mingi, umuwikaji b’ob’o. Ulusumo lunulo lugab’izukijaga abhanhu bhenab’o igiki, b’ulijene ijo jilinihanga, jidagayiyagwa inhuni.

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gub’iza na widohya b’o gwikala na bhanhu bho mholele. Uwikaji bhunub’o bhugabhadugijaga b’ingi uguginja amakoye gab’o chiza, nulu gugatumila chiza amatwajo gab’o, kunguno bhuli jene ijo jilinihanga jidakijaga ugub’iza ni nhuni. Hugwene guhaya giki, bhuli jene ijo jilinawandijo, jidagayiyagwa ugub’iza na nhalikijo.

KISWAHILI: KILA KILICHO NA SURA KINA KISOGO

Chanzo cha methali hiyo huangalia sura na kisogo cha mtu. Sura humaanisha mwanzo wa mtu au kitu fulani. Kisogo humaanisha mwisho wake huyo mtu au kitu hicho.

 Kwa hiyo, kila kilicho na sura hakikosi kuwa na kisogo, humaanisha, kwamba, ‘kila kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wafikirio kwamba wataishi milele hapa duniani. Kwa sababu hiyo, mmoja wao akifariki, watu hao hupata mshituko hata kupelekea kwa baadhi yao kupoteza maisha, kwa sababu ya mshituko huo. Watu hao husahau kuwa ‘kila kilicho na sura kina kisogo.’

Zaidi ya hayo, methali hiyo pia hulinganishwa kwa watu wapatao matatizo au mafanikio, yakiwemo yale ya kupata utajiri, kuwa na afya njema, kupata kazi na kadhalika, maishani mwao. Methali hiyo huwakumbusha watu hao kuwa kila kilicho na sura hakikosi kuwa na kisogo.

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na unyenyekevu wa kuishi na watu kwa amani. Hali hiyo huwawezesha wengi kuyatatua vizuri matatizo yao, na kuyatumia vizuri mafanikio yao, kwa sababu kila kilicho na sura hakikosi kuwa na kisogo. Ndiyo kusema, ‘kila kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.’

 

elephant-richness

meditate-

ENGLISH: EVERYTHING THAT HAS A FACE HAS A BACK HEAD

The overhead proverb looks at the existence of the face and the back head, both being parts of a human being. On the one hand, the face signifies the beginning of person or thing, and on the other hand, the back head signifies the end of a person or thing. Therefore, everything that has a face also has an end, that is, the back head. This also means that ‘everything that has a beginning has an end.’

The proverb relates to those who think that they will live on earth forever. Thus, when one of them passes on, these people get so devastated to an extent of even losing their own life as well, due to the shock. They forget that ‘everything that has a face has a back head.’

In addition, the proverb is also relates to people who experience both success and problems. Success could be in form of wealth, good health, employment, and so on. The proverb reminds them that everything that has a face also has a back head.

The proverb teaches people about the importance of living with others in humility and in peace. This enables people to solve their problems effectively, and to make the most out of their success, because everything that has a face has a back head. This is to say, ‘Everything that has a beginning has an end.’

232. NHOLE NA GUKULIKILE

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kulinkima na ngosha abho bhalihaya gwitola. Uumo obho agung’wilaga ung’wiye giki, ‘nhole nagukulikile.’ Umuguyomba chiniko alolecha giki, ulubhitola bhagwikala kihamo mpaga pye ishigu ja witoji bhobho. Agayombaga chene unkima uyo aling’wila ungosha uyo alihaya guntola giki, wikale nag’hwe mpaka gushiga kub’ugikulu bhokwe. VIDEOYustina from Ndoleleji Research group presents a song about a joyful marriage

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhitoji abho bhagikalaga kihamo umushigu jabho jose. Abhanhu bhenabho bhamanile ugwiyumilija kihamo na bhichabho umuwitoji bhobho, umumakanza gose, agamakoye nagabhuyegi pye shigu ja bhulamu bho witoji bhobho.

Akahayile kenako kalanga bhitoji higulya ya gubhiza na wiyumilija ubho gudula gubhambilija ugwikala kihamo umushigu jabho jose. Uwiyumilija bhunubho bhugulanga bhana bhabho higulya ya gwikala na nhungwa ja wiza ija gudula gwikala bho mholele na bhanhu, umubhulamu b’ob’o.

Waefeso 5:21-24.

Marko 10:1-9.

 

KISWAHILI: NIOE NIKUZEEKEE

Chanzo cha msemo huo chatokea kwa mwanamke na mwanaume ambao watalajia kuoana. Mmoja wao humwambia mwenzake kwamba, ‘nioe nikuzeekee.’ Kwa kusema hivyo, huonesha kwamba, wakioana wataishi pamoja mpaka uzeeni mwao. Husema hivyo mwanamke akimwambia mwanaume yule atakaye kuoana naye, kwamba waishi naye mpaka kufikia umri wa uzee wao.

Msemo huo hulinganishwa kwa wana ndoa wale waishio pamoja siku zote za maisha yao. Watu hao, wafahamu namna ya kuvumiliana pamoja na wenzao katika raha na shida, siku zote za maisha ya ndoa yao.

Msemo huo hufundisha watu wa ndoa juu ya kuwa na uvumilivu wa kuweza kuwasaidia katika kuishi kwa pamoja siku zote za ndoa yao. Uvumilivu huo huwafundisha pia watoto wao juu ya kujijengea tabia njema ya kuishi kwa amani na wenzao maishani mwao.

Waefeso 5:21-24.

Marko 10:1-9.

lovely black marriage

ENGLISH: MARRY ME I GROW OLD FOR YOU

The overhead saying is based on marriage intent of a man and a woman. One tells the other, ‘Marry me I grow old for you.’ By saying this, they express the intention or wish that the two will stay together until their old age. Usually, this is what the woman tells the man who is going to marry her, as a solemn wish to live and grow old with her.

The saying is comparable to married couples who live together all the days of their lives. Such people know how to accommodate their partners in times of comfort and in distress throughout their married life.

The saying teaches about the virtue of patience for a steadfast marriage life for couples. Such patience is also useful in building good habits in children for a harmonious relationship with their peers.

Ephesians 5: 21-24.

Mark 10: 1-9.

231. IHADIKE LIDAKOMELAGWA KAYA

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kulinamugi uyo agaigasijaga ikaya yakwe bhobhukali. Ikaya yiniyo igasalambanaga kunguno ya bhukalihilwa bhunubho. Hunagwene agawilagwa na bhiye giki, “ihadike lidakomelagwa kaya.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagabhakalihilaga abhanhu abhahakaya jabho. Abhanhu bhenabho bhadabhizaga na bhutongeji bhowiza ukubhanhu bhabho bhenabho. Ubhukali bhunubho bhugabhasalambanyaga abhanhu abhahakaya jabho jinijo, kunguno ya wikaji bhenubho. Gashinaga lulu, goligong’hana igiki, ilihadike lidakomelagwa kaya.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gub’iza na nhungwa ja gubhatongela chiza abhanhu bhahakaya jabho. Ubhutongeji ubhowiza bhunubho, bhugubhinha wiyabhi abhanu bhabho ubhogudula gutumama milimo yahahakaya yiniyo bho mholele na nduhu uguhadikijiwa.

Filimoni 1:14.

Yohane 8:31-32.

KISWAHILI:AMRI YA HAIJENGI FAMILIA

Chanzo cha msemo huo chatokea kwa mzee wa familia aliyeishi kwa kuwalazimisha watu wake katika kutekeleza majukumu ya pale. Familia hiyo ilisambalatika kwa sababu ya watu wake kukalipiwa mara kwa mara na mzee huyo. Ndiyo maana watu humwambia mzee huyo kwamba, amri haijengi familia.

Msemo huo hulinganishwa kwa watu ambao huwakalipia watu walioko kwenye familia zao. Ukali huo huwajengea hofu watu wao mpaka kufikia hatua ya kusambalatika pale nyumbani. Watu hao huwa hawana uongozi mzuri kwa watu wao. Ndiyo maana watu humwambia mtu huyo kwamba, amri haijengi familia.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na tabia ya kuweza kuwaongoza vizuri watu wao hao. Uongozi huo ndiyo ule ulio mzuri uwapao watu wao uhuru wa kutosha kuwawezesha kufanya kazi zao kwa amani na uhuru wa kujituma zaidi badala ya kusubiri kulazimishwa.

Filimoni 1:14.

Yohane 8:31-32.

entrepreneur1

ENGLISH: A COMMAND DOES NOT BUILD A FAMILY

The above saying examines how a family cannot be built through duress by the family elder, who forces people to carry out their duties. Such a family would crumble because of the constant harsh words or commands used by the elder to reproach people as they work. That is why people would tell such an elder that ‘a command does not build a family.’

The saying is comparable to people who use harsh language to admonish others in their families. Such hostility breeds fear in people to the point of breaking the home. And this is a symptom of poor leadership qualities in the elders. That is why such a leader or elder is told, ‘a command does not build a family.’

The saying teaches people about the character of leading others well. Sound leadership allows people sufficient freedom to enable them carry out their duties peacefully and freely rather than by compulsion.

Philemon 1:14.

John 8: 31-32.