Imbuki ya Lusumo lunulo ilolile ihanga na nhuni ya ng’wa munhu. Ilihanga ligalingisilaga wandijo b’o ng’wa munhu, nulu ginhu jileb’e. Inhuni igalingisilaga nhalikijo yakwe umunhu ng’wunuyo, nulu iginhu jinijo.
Kuyiniyo lulu, b’uli jene ijo jilinihanga jidagaiyagwa inhuni, ilingisilile giki, b’uli jene ijilinawandijo jidagayiyagwa inhalikijo.
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kub’anhu abho bhagiganikaga giki, b’agwikala bhulunga kele ehenaha welelo. Kunguno yiniyo lulu, ulu umo ob’o winga kuwelelo, bhagapandikaga wib’akizu bho gudula nulu gucha, kunguno ya wib’akizu b’unubho. Abhanhu bhenabho b’aghibhaga igiki, b’ulijene ijo jilinihanga jina nhuni.
Ijinagongeja, ulusumo lunulo hangi lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagapandikaga mayange, nulu matwajo ayo galikihamo na bhusab’i, gub’iza bhalinhola, gupandika milimo na yingi mingi, umuwikaji b’ob’o. Ulusumo lunulo lugab’izukijaga abhanhu bhenab’o igiki, b’ulijene ijo jilinihanga, jidagayiyagwa inhuni.
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gub’iza na widohya b’o gwikala na bhanhu bho mholele. Uwikaji bhunub’o bhugabhadugijaga b’ingi uguginja amakoye gab’o chiza, nulu gugatumila chiza amatwajo gab’o, kunguno bhuli jene ijo jilinihanga jidakijaga ugub’iza ni nhuni. Hugwene guhaya giki, bhuli jene ijo jilinawandijo, jidagayiyagwa ugub’iza na nhalikijo.
KISWAHILI: KILA KILICHO NA SURA KINA KISOGO
Chanzo cha methali hiyo huangalia sura na kisogo cha mtu. Sura humaanisha mwanzo wa mtu au kitu fulani. Kisogo humaanisha mwisho wake huyo mtu au kitu hicho.
Kwa hiyo, kila kilicho na sura hakikosi kuwa na kisogo, humaanisha, kwamba, ‘kila kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.’
Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wafikirio kwamba wataishi milele hapa duniani. Kwa sababu hiyo, mmoja wao akifariki, watu hao hupata mshituko hata kupelekea kwa baadhi yao kupoteza maisha, kwa sababu ya mshituko huo. Watu hao husahau kuwa ‘kila kilicho na sura kina kisogo.’
Zaidi ya hayo, methali hiyo pia hulinganishwa kwa watu wapatao matatizo au mafanikio, yakiwemo yale ya kupata utajiri, kuwa na afya njema, kupata kazi na kadhalika, maishani mwao. Methali hiyo huwakumbusha watu hao kuwa kila kilicho na sura hakikosi kuwa na kisogo.
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na unyenyekevu wa kuishi na watu kwa amani. Hali hiyo huwawezesha wengi kuyatatua vizuri matatizo yao, na kuyatumia vizuri mafanikio yao, kwa sababu kila kilicho na sura hakikosi kuwa na kisogo. Ndiyo kusema, ‘kila kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.’
ENGLISH: EVERYTHING THAT HAS A FACE HAS A BACK HEAD
The overhead proverb looks at the existence of the face and the back head, both being parts of a human being. On the one hand, the face signifies the beginning of person or thing, and on the other hand, the back head signifies the end of a person or thing. Therefore, everything that has a face also has an end, that is, the back head. This also means that ‘everything that has a beginning has an end.’
The proverb relates to those who think that they will live on earth forever. Thus, when one of them passes on, these people get so devastated to an extent of even losing their own life as well, due to the shock. They forget that ‘everything that has a face has a back head.’
In addition, the proverb is also relates to people who experience both success and problems. Success could be in form of wealth, good health, employment, and so on. The proverb reminds them that everything that has a face also has a back head.
The proverb teaches people about the importance of living with others in humility and in peace. This enables people to solve their problems effectively, and to make the most out of their success, because everything that has a face has a back head. This is to say, ‘Everything that has a beginning has an end.’