752. GUB´ISA GO NVA GUGAFUMBULAGWA NG`HUNGULU.

Ulusumo lunulo, lulihoyela higulya ya masala ga nva ayo gagafumbulagwa na ng’hungulu. Inva ili na masala ayo gagikolaga hadoni na ga bhanhu kunguno igabhisaga inyama ulu uyisaga. Ulu yukuga nyama yulwa yiguta mpaga yuyisaja, igajagub´isa hanhu kugiki ilize yilwe hangi ulu yutubha.

Ing´hungulu nayo ili noni iyo ili na masala gagupadija aho yabhiyisilaga inva inyama yiniyo. Gashinaga lulu, ulu ub´isa umuna mva iyoyi igajaga yaginjaho yalila ha ng´wape, aho bhadulile nulu bhanhu bhuyibhona na gudebha igiki inva yaliyabhisa nyama. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “gub´isa go nva gugafumbulagwa ng`hungulu.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitaga ginhu bho gwibhisa ijo jigamanyikaga aha numa yaho. Umunhu ung’wunuyo, alina nhungwa ja wiminholo ukubhiye, ijo jigampondaga soni ulu bhandebha bhiye. Uweyi agiganikaga giki alibhakelela abhangi aliyo gashinaga bhayidebhile iyo agiyitaga.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nhi nhungwa ja nva ija gubhisa nyama iyo igafumbulagwa na ng’hungulu, kunguno nuweyi agabhisaga ginhu ijo jigampondaga soni ulu jagiza kumanyika ukubhiye. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “gub´isa go nva gugafumbulagwa ng`hungulu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja wiminholo umuwikaji bhobho, kugiki bhadule gwiyambilija chiza umubhutumami bho milimo yabho. Igelelilwe bhiyambilije kihamo umukikalile kabho, kugiki bhadule kupandika matwajo ga gujibheja chiza ikaya jabho.

Warumi 2:16.

1Wakorintho 14:25.

KISWAHILI: KUFICHA KWA MBWA HULIFICHULIWA KUNGULU.

Methali hiyo, huongelea juu ya  akili za mbwa ambazo hufichuliwa na kungulu. Mbwa ana akili ambayo hufanana kidogo na ile ya wanadamu kwa sababu yeye huficha  nyama anayoisaza. Hivyo, akiokota nyama na kuila mpaka akaisaza, huificha sehemu ili aje aile tena baadaye akijisikia njaa.

Kungulu naye ni ndege mwenye akili za kugundua pale alipoyificha mbwa yule ile nyama. Kumbe basi, mbwa akificha yenyewe huenda kuichukua ile nyama na na kuanza kuila mahali pa wazi. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kuficha kwa mbwa hufichuliwa na kungulu.”

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutenda jambo fulani kwa kujificha ambalo hujulikana baadaye kwa wale aliowaficha. Mtu huyo, ana tabia ya uchoyo kwa wenzake, ambayo humfedhehesha kutokana na aibu anayoipata mbele ya wenzake baadaye siri yake kujulikana. Yeye hufikiri kwamba anawazidi ujanja wengine kumbe wanakielewa kile anachokifanya.

Mtu huyo, hufanana na akili ya mbwa ya kuficha nyama ambao ilifichuliwa na kungulu, kwa sababu naye huficha jambo fulani ambalo humuaibisha baada ya kujulikana kwa wenzake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kuficha kwa mbwa hufichuliwa na kungulu.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya uchoyo maishani mwao, ili waweze kusaidiana vizuri katika utekelezaji wa kazi zao. Wanatakiwa kuwa  na ushirikiano wa pamoja katika kutekeleza majukumu yao ili waweze kupata mafanikio ya kuziendeleza vizuri familia zao.

Warumi 2:16. “Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za mioyo ya wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama isemavyo Injili yangu.”

1Wakorintho 14:25. “nazo siri za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akikiri, “Kweli Mungu yuko katikati yenu!””

crow kunguru

crow kunguru raven-

dog4

crow kunguru raven-1

ENGLISH: WHAT HAS BEEN HIDDEN BY A DOG IS USUALLY UNCOVERED BY A CROW.

This proverb, speaks of the minds of dogs that are exposed by crows. The dog has a mind that is a little similar to that of human beings because it hides the meat in leaves. So, when it picks up the meat and eats it, it hides the part of it so that it can eat again later when it is hungry.

The crow is also a clever bird that discovered where the dog had hidden the meat. However, a crow can take the meat and begin to eat it in an open area. That is why people say that “What has been hidden by the dog is revealed by a crow.”

The proverb above is likened with a man who does something secretly, but which latter on is known to those it had hidden been hidden from. Such person, however, has a greedy attitude toward his colleagues, which humiliates him due to the embarrassment he gets in front of his colleagues later when his secret is known. He thinks he is better than others, but they understand what he is doing.

Such man is like the dog that hid meat which, was exposed by the crow, because he too hides something that embarrasses him after it is known by his peers. That is why people tell him that, “what has been hidden by a dog is usually uncovered by a crow.”

This proverb teaches people about giving up habits of greed in their lives, so that they can help each other better in the execution of their duties. They need to be co-operative in carrying out their responsibilities so that they can achieve success for the good of their families.

Romans 2:16.

1Corinthians 14:25.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.