740. LYAB´IMBILILE HAB´I.

Ulusumo lunulo, lwingilile kuli munhu uyo agab’imbila lib’ute, kulwande lo mili gokwe ulo adadulile uguloyomba sagala. Ilib’ite linilo, lyalib’imbilile kulwande lo mbisila yakwe. Uweyi agacha soni uguyomba hab’utongi bho bhanhu aho lib’ilimbile. Hunagwene agayomba bho mbisila giki, “lyab’imbilile hab’i.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo opandikile ikoye itale umuwikaji bhokwe, ilo adadulile ugulimala ubho gutumila nguzu yakwe duhu. Umunhu ng’wunuyo, agalombaga wambilijiwa bho gufumila kubhiye na kuli Mulungu uyo adulile gung’wingija wangu ilikoye linilo. Uweyi adebhile igiki uwambilijiwa bhunubho, bhudulile gulimala ilikoye lyakwe linilo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oliob’imbila lib’ute litale kulipande lya mili gokwe ilo agabhona soni uguliyomba sagala, kunguyo nuweyi ligankoyaga mpaka olomba wambilijiliwa, bho dugula gulyinja ilikoye lwakwe linilo. Hunagwene nang’hwe agabhawila abhanhu giki, “lyab’imbilile hab’i.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gub’iza na masala ga gwiyumilija umumakoye ayo bhalinago, na gulomba wambilijiwa bho gugamala wangu amakoye genayo, kugiki bhadule gwikala chiza na bho mholele na bhichabho, umuwikaji bhobho.

1Wakorintho 12:20-31.

KISWAHILI: LIMEVIMBIA PABAYA.

Methali hiyo, ilianzia kwa mtu aliyevimba jipu katika sehemu ya mwili wake ambayo hawezi kuitaja hovyo, kwa sababu ya kuona aibu. Jipu hilo, lilivimbia kwenye sehemu zake za siri. Yeye hujikia aibu kuitaja mbele za watu sehemu hiyo. Ndiyo maana yeye huitaja kwa mafumbo akisema, “limevimbia pabaya.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule aliyepata tatizo kubwa maishani mwake, ambalo hawezi kulitatua kwa kutumia uwezo wake tu. Mtu huyo huomba msaada kutoka kwa wezake na kwa Mungu awezaye kumtatulia tatizo hilo. Yeye anaelewa kwamba, msaada huo unaweza kulitatua kwa haraka tatizo lake hilo.

Mtu huyo hufanana na yule aliyevimba jipu kwenye sehemu zake za siri akashindwa kuitaja mbele za watu sehemu hiyo kutokana na kuona aibu, kwa sababu naye alishindwa kulitatua tatizo lake hilo mpaka akaomba msaada kutoka kwa wenzake na kwa Mungu mwenye uwezo wa kulitatua tatizo hilo kwa haraka. Ndiyo maana naye alisema kwamba, “limevimbia pabaya.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na akili ya kuvumilia matatizo na kuomba msaada wa kuweza kuyatatua, ili waweze kuishi vizuri na kwa amani na wenzao, maishani mwao.

1Wakorintho 12:20-31. “Kama ulivyo, kuna viungo vingi, lakini mwili ni mmoja. Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na ninyi!” Lakini badala yake, vile viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa dhaifu, ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana. Navyo vile viungo vya mwili tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee. Wakati vile viungo vyenye uzuri havihitaji utunzaji wa pekee. Lakini Mungu ameviweka pamoja viungo vya mwili na akavipa heshima zaidi vile vilivyopungukiwa, ili pasiwe na mafarakano katika mwili, bali viungo vyote vihudumiane usawa kila kimoja na mwenzake. Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja wenu ni kiungo. Mungu ameweka katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za masaidiano, karama za maongozi, aina mbalimbali za lugha. Je, wote ni mitume? Je, wote ni manabii? Je, wote ni walimu? Je, wote wanafanya miujiza? Je, wote wana karama ya kuponya? Je, wote hunena kwa lugha mpya? Je, wote wanatafsiri? Basi tamanini sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonyesha njia iliyo bora zaidi.”

malawi1

malawi3

malawi4

ENGLISH: I HAVE AN ABCESS SWOLLEN AT A BAD PLACE.

This proverb began with a man who had a boil on a part of his body that he could not mention because he felt embarrassed to do so. For sure, this abscess was on his genitals. So he felt ashamed to mention it in public. That is why he spoke using a proverb saying that “I have an abscess swollen on a bad place.”

This proverb is likened with a man who has a serious problem in his life which he cannot solve by simply relying only on his own strengths. Such a person will have to ask for help from his peers and from God who can solve the problem. He understands that such support can quickly solve his problem.

This man is like the one who had a swollen boil on his genitals but failed to show it in public because he was ashamed. This person failed to solve his problem until he asked for help from his colleagues and from God who was able to solve it very quickly.

This proverb teaches people how to have stability to endure problems and ask for help to solve them, so that they can live peacefully with others.

1 Corinthians 12: 20-31.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.