688. MASHIGA NILI, NULU, MAHIGA NILI.

Ulusumo lunulo, lwandija kumahoya ga bhanhu bhabhili ayo gahoyela mashiga. Uumo agamuuja ung’wiye, ‘amashiga ni kiyi?” Ung’wiye aganshokeja aliyomba, ‘amashiga gali mawe, nulu, madafari adatu ayo gagatumilagwa gujidimila ijisema ija guzugila ahaliko. Ahasi yago, gugabhachiyagwa moto umung’hwi ijo jigasolelagwa moyi. Umoto gunuyo gugagasebhyaga amashiga genayo.

Aliyo lulu, amashiga genayo gagabhizaga manilizu, ulugudubhachiyagwa umoto. Hunagwene abhanhu, ulu bhubhona kaya iduzugaga jiliwa, bhagayombaga giki, ‘mashiga nili, nulu, mahida nili.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa ku kaya iyo idabokelaga chiza abhageni na kubhalisha jiliwa, kunguno abhahenaho, bhadina bhutogwa, nulu, ikaya yiniyo idina jiliwa.

Amashiga ayo gali mawe adatu gagatumamilagwa gudima nungu, nulu fulila, aha liko, gagikalaga manilizu kunguno bhadazugaga ijiliwa ahakaya yiniyo. Hunagwene abhanhu, bhagayiwilaga ikaya yiniyo giki, mashiga nili, nulu, mahiga nili. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 58.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wizang’holo bho gubhakaribhusha abhageni aha kaya jabho, kugiki bhadule gujipandika imbango ijo jigigelaga kunguno ya gubhagola chiza abhanhu bhenabho, umuwikaji bhobho.

“Ugubhakaribhusha abhageni bho wizang’holo umu kaya jise, guli nimo gwize ayise abho duganhondejaga Yesu Kristo. Ishibhi idigwita yabhubhi duhu, aliyo hangi nu kuleka gubhitila yawiza abhigisu, guleka uguitumama imilimo yise, na guleka gubhadilila abho bhali na makoye gabho. Ukuhani nu Nawi bhadang’witilile yabhubhi uyo oliotulwa na manyami, aliyo bhagamitilia bho nhudu ugundilila. Bhaditile lyose lyose. Lolaga Kueneza Injili Kwa Methali, bhukurasa, 58.

Mambo ya Walawi 19:34.

Luka 10:31-33.

Waroma 15:7.

Waebrania 13:2.

Mwanzo 18:1-8.

1Wafalme 17:10-16.

Mathayo 25:31-46.

KISWAHILI: MAFIGA BARIDI.

Methali hiyo ilianzia kwenye maongezi ya watu wawili juu ya kazi ya mafika. Mmoja alimuuliza mwenzake, ‘mafiga ni nini?’ Mwenzake alimjibu akisema, ‘mafiga ni mawawe, au matofari matatu yanayotumika katika kushikilia chombo cha kupikia. Chini ya mafiga hayo huwekwa kuni ambazo huwashwa moto unaoleta joto kwenye mafiga hayo. Mafiga hayo huwa baridi kama watu hawapiki chakula.’ Ndiyo maana watu kama wakiona chakula hakipikwi kwenye familia fulani, husema, ‘mafiga baridi.’

Methali hiyo hulinganishwa kwenye familia au kaya ile ambayo haipokei vizuri wageni na kuwalisha chakula, kwa kuwa hawana mapendo au kaya hiyo haina chakula.

Mafiga ambayo ni mawe matatu yatumikayo kutelekea chungu au sufuria jikoni, hukaa baridi kwa sababu hawapiki chakula. Ndiyo maana watu huiambia familia hiyo kwamba, ‘mafiga baridi.’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 58.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwakaribisha wageni katika familia zao, ili waweze kupata Baraka zitokanazo na kuwatunza watu hao, katika maisha yao.

 “Kuwakaribisha wageni kwa ukarimu kwenye kaya zetu ni wajibu wetu sisi tunaomfuata Yesu Kristo. Dhambi sio kutenda mabaya tu, bali pia ni kutowatendea mema wenzetu, kutotimiza wajibu wetu, na kutohusika na shida zao. Kuhani na Mlawi hawakumtendea vibaya yule aliyepigwa na majambazi, bali walipita bila kujali. Hawakutenda lo lote.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 58.

Mambo ya Walawi 19:34. “Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi BWANA Mungu wako.”

Luka 10:31-33. “Kwa bahati nzuri kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine wa barabara, akamwacha hapo hapo. Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipofika mahali pale, alimwona, akapita upande mwingine wa barabara, akamwcha hapo hapo. ‘‘Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri kupitia njia hiyo alipomwona, alimhurumia,”

Waroma 15:7. “Karibishaneni ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowakaribisha ninyi ili kumletea Mungu utukufu.”

Waebrania 13:2. “Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua.”

Mwanzo 18:1-8. “BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.  Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako. Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi  nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.’’ Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.’’

 Hivyo Abrahamu akaharakisha akaingia hemani kwa Sara. Akasema, “Chukua vipimo vitatu vya unga laini haraka, ukande na uoke mikate.”   Kisha akakimbia kwenda kwenye kundi  akachagua ndama mzuri, laini na akampa mtumishi, ambaye aliharakisha kumtayarisha. Kisha akaleta jibini, maziwa na nyama ya yule ndama iliyoandaliwa, akaviweka mbele ya wageni. Walipokuwa wakila, alisimama karibu nao chini ya mti.”

1Wafalme 17:10-16. “Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, mjane alikuwa huko akiokota kuni. Akamwita na kumwomba, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.’’ Alipokuwa anakwenda kumletea, akamwita akasema, “Tafadhali niletee pia kipande cha mkate.” Akamjibu, ‘Hakika kama BWANA wako aishivyo, sina mkate wo wote, isipokuwa konzi ya unga kwenye gudulia na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili kwamba tule kiishe tukafe.’’ Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda nyumbani ukafanye kama ulivyosema. Lakini kwanza unifanyizie mimi mkate mdogo kutoka vile ulivyonavyo kisha uniletee na ndipo utayarishe cho chote kwa ajili yako na mwanao. Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo BWANA, Mungu wa Israeli: “Lile gudulia la unga halitakwisha wala ile chupa ya mafuta haitakauka hadi siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi.’’ Akaondoka na kufanya kama Eliya alivyomwambia. Kwa hiyo kukawa na chakula kila siku kwa ajili ya Eliya, yule mwanamke na jamaa yake. Kwa kuwa lile gudulia la unga halikwisha na ile chupa ya mafuta haikukauka, sawasawa na lile neno la BWANA alilosema Eliya.  ”

Mathayo 25:31-46. Hukumu ya mwisho. “Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake. Mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi. Atawaweka kondoo upande wake wa kuume na mbuzi upande wake wa kushoto.

“Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wake wa kuume, ‘Njoni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha, nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.’

“Ndipo wale wenye haki watakapomjibu wakisema, ‘Bwana, ni lini tulikuona una njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakunywesha? Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukiwa uchi tukakuvika? Tena ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukakutunza au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’ 

“Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin, amin ninawaambia, kwa jinsi mlimvyotendea mmojawapo wa hawa ndugu Zangu walio wadogo, mlinitendea Mimi.’ “Kisha atawaambia wale walio upande Wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele alioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake. Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu hamkuninywesha, nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha, nilikuwa uchi hamkunivika, nilikuwa mgonjwa hamkunitunza na nilikuwa gerezani nanyi hamkuja kunitembelea.’

“Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au uchi , au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’ “Naye atawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’ “Ndipo hawa watakapoingia kwenye  adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.’’”

cooking-pot-

cooking

cooking1

ENGLISH: COLD THREE COOKING STONES.

 The proverb started in a two-person conversation about the work of the three cooking stones. One asked the other, ‘What are the three cooking stones?’  The other answered, ‘these are the three stones, or bricks which are used in holding the cooking tool.’

The cooking pot sits on those three stones in the traditional African fireplace. These three cooking stones of equal size and placement easily support the clay or metal cooking pot. They are positioned very carefully. 

Underneath or between them firewoods are put, which are set on fire. The three stones need each other; they work together. If one takes away one stone and the pot falls down. They however, get cold if people don’t cook food. That’s why when people discover that food is not cooked at a particular family, they say, ‘cold three cooking stones.’

The balance between their standing close together yet apart is a symbol of community life. This is one the Sukuma Proverb that is used to teach about the values of unity, community and working together.

It is found in the Small Christian Communities (SCCs) Book: During a SCC Workshop a very effective teaching on of unity and working together is to demonstrate African proverb.

It has the following teachings:

  1.   A creative way of teaching the importance of SCCs is to describe the three cooking stones on which SCCs are “cooked” as spiritual values, acts of mercy, and concrete projects.
  2.   The metaphor of the one cooking pot and three stones can be used in different ways to describe the Catholic Church.  That is, one church but three parts: priests, religious and laity.
  3.   The image of the cooking pot and the three stones is an important analogy for the Trinity: that is one God and three Divine Persons, namely Father, Son and the Holy Spirit.
  4.   A Sukuma, Tanzania proverb:  The three stones that support the cooking pot are cold (literally mafiga baridi in Swahili) means that there is no fire and thus no food is being cooked, which is a sign of the lack of hospitality, welcome and love. 

The cold stones are a sign of the lack of good relationships within the home itself and with people living outside. Three-cooking stones used for holding a pot or kitchen pan, stay cool because they do not cook food. That is why people tell such family, ‘cold three cooking stones.’ Refer to ‘Kueneza Injili kwa Methali’; which can be literally translated as ‘Spreading the Gospel through Proverbs, page 58.

Such book was written by researchers who are: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Joseph Healey M.M., published by Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

The proverb teaches people about generosity of welcoming strangers into their families, so that they can receive the blessings that come from caring for them, in their lives.

 “The generous hospitality of our families is the responsibility of those who follow Jesus Christ. Sin is not only doing wrong, but also not doing good to others, not fulfilling our obligations, and not dealing with their problems. The priest and the Levite did not harm the victim, but they passed away regardless. They did nothing. ” Refer to “Kueneza Injili kwa Methali” which means, ‘Spreading the Gospel through Proverbs’, page 58.

Leviticus 19:34.

Luke 10: 31-33.

Romans 15: 7.

Hebrews 13: 2.

Genesis 18: 1-8.

1Kings 17: 10-16.

Matthew 25: 31-46.

One comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.