Imbuki ya lusumo lunulo, yingilile kubhubheja bho lina. Ubhubheja bho lina bhenabho, bhuli bhogutumama milimo iyo yiliyawiza aha kaya. Gashinaga lulu, uyo alemile ugutumama imilimo uyawiza yiniyo, agaikolanijaga na bhubheja bho lina duhu, kunguno uweyi alingokolo uguitumama imilimo iyo idulile guibheja chiza, ikaya yakwe. Hunagwene umunhu ng’wunuyo, agayombaga giki, ‘natizile gubheja lina.’
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alingokolo ugumama imilimo guti iyagulima, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, atogilwe gwigasha hakaya bho nduhu nimo gosegose, kunguno ya bhugokolo bhokwe. Uweyi adulile nulu gulikolola iligembe lyakwe, kunguno ya kuchola wasa bho gwifula, kugiki ulu bhalitumama abhiye, uweyi amane ulibheja iligembe linilo.
Umunhu ng’wunuyo, agakoyiyagwa na nzala aha ng’wakwe, kunguno ya kugaiwa ijiliwa bhuli makanza. Uweyi agikalaga bho gwilombeleja ijiliwa ukubhanhu abho bhagigulambijaga uguitumama chiza imilimo yabho.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo ayilemile imilimo iya wiza, kunguno nuweyi alemile uguitumama imilimo yakwe, iyo idulile gung’wingija amakoye, umuwikaji bhokwe. Abhanhu abho bhandebhile igiki alingokolo ugulima, bhagankomelejaga gutumama milimo chiza. Aliyo uweyi agalemaga bho guyomba giki, ‘natizile gubheja lina.’
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo, umukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi agagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Luka 11:46.
Mathayo 23:3-4.
Yohana 4:38.
KISWAHILI: SIKUJA KUTENGENEJA JINA.
Chanzo cha methali hiyo, chatokea kwenye utengenezaji wa jina. Utengenezaji huo, ni wa kuutumia muda katika kuufanyia kazi njema. Kumbe basi, yule asiyetaka kuzifanya kazi hizo njema, huzifananisha kazi hizo kama utengenezaji jina tu, kwa sababu ya uvivu wake wa kuzitekeleza kazi zile ziwezazo kuiendeleza vizuri familia yake. Ndiyo maana mtu huyo, hukataa kufanya kazi kwa kusema kwamba, ‘sikuja kutengeneza jina.’
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mvivu wa kuyatekeleza majukumu yale yawezayo kuijenga vizuri familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, hupenda kukaa nyumbani bila kufanya kazi yoyote, kwa sababu ya uvivu wake wa kufanya kazi. Yeye hujisingizia kama anatengeneja jembe wakati wa kufanya kazi ya kulima, kumbe anatafuta muda wa kupumzika. Pia aweza hata kulilegeza jembe lake, ili apate muda wa kupumzika wakati analitengeneza jembe lake hilo, maishani mwake.
Mtu huyo, husumbuliwa na tatizo la njaa nyumbani kwake, kwa sababu ya kukosa chakula. Yeye huishi kwa kuomba chakula kutoka kwa wale wanaolima kwa bidii, maishani mwao.
Mtu huyo, hufanana na yule asiyetaka kufanya kazi, kwa sababu naye ni mvivu katika kufanya kazi, maishani mwake. Watu wanaoifahamu tabia yake hiyo ya uvivu, humuonya ili aweze kuiyacha tabia hiyo. Lakini yeye hukataa kwa kusema kwamba, ‘sikuja kutengeneza jina.’
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao vizuri, ili waweze kupata mafanikio mengi yanayotosha kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.
Luka 11:46.
Mathayo 23:3-4.
Yohana 4:38.
ENGLISH: I DID NOT COME TO MAKE A NAME.
The source of this saying is a person who would like to be known because of his/her own abilities in doing something. This person will have to spend much of the time doing what he/she thinks at the end of the day will make his/her name. On the contrary, lazy people can ridule those hard working people by telling them that they didn’t come to make a name. Such lazy people can do whatever they think can make them not spend much energy in doing their works.
This saying can be likened to a lazy person who avoids his/her family responsibilities. Such a person can just stay home without working and, at the end of the day, he/she suffers for not having food to sustain his/her family. People of this nature can have several tricks of avoiding work. They can deliberately sit down and beginning nursing a child while his/her fellows go on with working, they can also losen the handle of the hoe deliberately in order to rest, and so many other means of justifying their restiness. When these lazy people are asked as to why they do so the simple answer can be ‘I didn’t come to make a name.’
The proverb teaches people to work hard in order to fulfill their responsibilities. In so doing they will be able to supply their families with needs and at the right time.
Luke 11:46. Mathew 23: 3-4. John 4:38.