Imbuki ya lusumo lunulo, yingilile kubhubheja bho ngata ya gubhukija nigo ndito. Ingata yiniyo, igambilijaga ugugukikija ntwe kugiki gudizubhunwa nu nigo gunuyo, kunguno gulintale. Hunagwene abhanhu ulubhuhaya gubhucha nigo uyo guli ndito bhagikomelejaga gubheja ngata bho guyomba giki, ‘bhejagi ngata nigo guli ndito.’
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agibhegelejaga chiza ulu alihaya gwita nimo uyo guli ndito. Umunhu ng’wunuyo, ulu uhaya gutumama nimo uyo guli ndito, agajikumingaga pye ijitumamalo ja nimo gunuyo, kugiki adule gugumala chiza.
Uweyi agikolaga nu munhu uyo agabhejaga ngata ulu ohaya gubhucha nigo ndito, kunguno nu weyi agibhegelejaga bho gujikuminga pye ijitumamilo ja nimo uyo ulihaya gugutumama.
Umunhu ng’wunuyo, agabhakomelejaga na bhiye kugiki nabho bhadule gwibhegeleja chiza haho bhatali uguitumama imilimo yabho. Hunagwene agabhawilaga abhiye bhenabho giki, ‘bhejagi ngata nigo guli ndito.’
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya ya gwibhegeleja chiza haho bhatali uguyandya imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, ijinabhutumami bho milimo yabho yiniyo, umuwikaji bhobho.
Mathayo 26:36-46.
Mathayo 11:18.
Waefeso 6:10.
Marko 8:34.
KISWAHILI: TENGENEZENI NZINGA MZIGO NI MZITO.
Chanzo cha methali hiyo, chatokea kwenye utengenezaji wa Nzinga ya kubebea mzigo mzito. Nzinga hiyo, husaidia katika kukizuia kichwa kupata maumivu ya mzigo huo, kwa sababu ya ukubwa na uzito wake. Ndiyo maana watu wakitaka kubeba mzigo mzito husema kwamba, ‘tengenezeni Nzinga mzigo ni mzito.’
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujiandaa vizuri anapotaka kufanya kazi ambazo ni mzito, katika maisha yake. Mtu huyo, huvikusanya vifaa vyote vinavyohitajika katika utekelezaji wa kazi anayotaka kuifanya, ili aweze kuitekeleza vizuri kazi yake hiyo.
Yeye hufanana na mtu yule ambaye hutengeneza nzinga ya kubebea mzigo mzito anaotaka kuubeba, kwa sababu naye hujiandaa vizuri, kwa kuvikusanya vifaa vile vyote vinavyohitajika katika utekelezaji wa kazi zake.
Mtu huyo, huwahimiza pia wenzake ili nao waweze kujiandaa vizuri kila wanapotaka kuyatekeleza majukumu yao, maishani mwao. Ndiyo maana huwaambia wenzake hao kwamba, ‘tengenezeni Nzinga mzigo ni mzito.’
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kufanya maandalizi ya kina, kila wanapotaka kuyatekeleza majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi katika kazi zao, maishani mwao.
Mathayo 26:36-46.
Mathayo 11:18.
Waefeso 6:10.
Marko 8:34.
ENGLISH: PRAPARE A ROUND HEAD PAD, THE LUGGAGE IS HEAVY TO CARRY.
The source of this saying is a luggage one has to carry on his/her head. In order to carry this luggage, one has to prepare himself/herself by having a round head pad in order to prevent direct pain that the luggage can inflict on the head of the one carrying it. This is why people came with the saying that ‘prepare a round pad, the luggage is heavy to carry’ to communicate preparedness in carrying out some duties.
This saying can be compared to a person who prepares well for the difficult task ahead of him/her. This person can gather all what is needed to make sure that he/she fulfills his/her ambition. This person is like the one who prepares a round head pad ready to undertake the duties ahead of him/her. Such a person teaches others the importance of preparing themselves in carrying out their responsibilities.
The saying teaches people how to prepare themselves before they embark on the actual performance of their duties. Preparedness can make someone have achievements in life.
Matthew 26: 36-46, Matthew 11:18, Ephesians 6:10, Mark 8:34.