Imbuki ya kalagu yiniyo, yililola kajisumva ako kagitanagwa kagi. Akagi kenako kali kajisumva ako kali kadoo noyi. Akoyi katogilwe gudanha hose hose aho kalatogelwe. Giko lulu, ulu kudan’ha gagutwalwa hose hose uko kalajanwe bho nduhu nabhuli. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘kagadamhilaga mondoka bho dalali:- Kagi.’
Ikalagu yiniyo, yigalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali nomolomo umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga usambaja mihayo ya bhulongo ukubhiye, guti ni umo igadanhilaga hosehose ingi yiniyo.
Unomolomo ulu wigwa mhayo adalendaga aha ng’wakwe, kunguno agab’izaga uyunga bhuli kwenye nulu bhuli hene guja ulomaloma. Uweyi adugije nulu gub’ulaga kaya ja bhanhu, kunguno ya bhulisanya bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘kagadamhilaga mondoka bho dalali:- Kagi.’
Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya kuleka bhulomolomo, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala chiza, na bho mholele na bhichabho, umukikalile kabho.
Walatia 5:16-26.
1Timotheo 1:10.
Ayubu 24:25.
Yakobo 3:5-6.
Zaburi 116:11.
KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.
HUPANDA GARI BILA KULIPIA NAULI: – INZI.
Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia kiumbe anayeitwa Inzi. Inzi huyo, ni kiumbe kidogo sana. Yeye hupenda kutua popote anapotaka. Hivyo basi, akitua mahali hata kwenye gari hupelekwa popote bila nauli. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘hupanda gari bila kulipia nauli:- Inzi.’
Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni muongo, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa anasambaza maneno ya uongo kwa wenzake, kama inzi yule anayetua kila sehemu na kuacha uchafu.
Muongo akisikia neno fulani huwa hatulii nyumbani kwakwe, kwa sababu yeye hudhurura kila sehemu akieneza uongo wake. Yeye anaweza hata kuvunja mji wa watu waliokuwa wanapendana katika maisha yao, kwa sababu ya uongo wake. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘hupanda gari bila kulipia nauli:- Inzi.’
Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuacha uongo katika maisha yao, ili waweze kuishi vizuri na kwa amani na wenzao, maishani mwao.
Walatia 5:16-26.
1Timotheo 1:10.
Ayubu 24:25.
Yakobo 3:5-6.
Zaburi 116:11.
ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.
IT RIDES A CAR WITHOUT PAYING FARE – FLY.
The source of this riddle is an insect known by the name of fly. A fly is a small insect that can land anywhere. It can land on a certain animal and therefore enjoy travelling with that particular animal wherever it wants to go. This is why people came with this riddle that ‘It rides a car without paying fare – fly’ to communicate the behaviour of flies of landing on other animals and enjoying ride pricelessly and in so doing, these flies can transmit diseases from one person to another.
That riddle can be compared to a person who is a liar in his/her life. This person can tend to travel from one point to another to spread his/her lies. Like a fly, this person doesn’t get settled in one place. He/she thinks about moving from one place to another to spread his/her rumours that might have disastrous effect to others.
This riddle teaches people about trustworth and respecting others. This can make people have a good and peaceful life with other members around them.
Leviticus 5: 16-26, 1Timothy 1:10, Job 24:25, James 3: 5-6,Psalm 116: 11.