602. KALAGU – KIZE. MABEHI GITONGEKAGA: – NG’HINGI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, yilolile bhusimbilwa bho ng’hingi.  Ing’hingi jinijo, jili miti iyo igatemagwa na gubhutwa chiza. Ijoyi jigasimbilagwa bho guhelelwa na gatunganyiwa, jawiza guti bhanhu bhitongekaga, kugiki jidule ugiulanghana chiza inumba. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘mabehi gitongekaga:- ng’hingi.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu abho bhali na ng’wigwano goguyilang’hana chiza ikaya yao. Abhanhu bhenabho, bhagikalaga bhuhoya kihamo, ijinaguyibheja bho guilanghana chiza ikaya yao yiniyo. Ubhutogwa bhobho, bhugabhinhaga nguzu ja gutumama milimo yabho bho gwiyambilija chiza bhuli makanza.

Abhanhu bhenabho, bhayilanghanile ikaya yabho guti ni ng’hingi umo jiyilang’hanhilile inumba, kunguno nabho bhali na ng’wigwano go gutumama milimo yabho bho gwiyambilija kihamo. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagiganilaga giki, ‘mabehi gitongekaga:- ng’hingi.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’wigwano go gwikala na witogwi bho gwiyambilija kihamo ijinaguitumama imilimo yabho, umukikalile kabho, kugiki bhadule kujilang’hana chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Matendo 2:4.

Matendo 4:32-37.

Wagalatia 6:2.

KISWAHILI:  KITENDAWILI – TEGA.

JAMAA WAMETANGULIZANA:– NGUZO.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia usimikwaji wa nguzo. Nguzo hizo, ni miti ile ambayo hukatwa na kutengenezwa vizuri. Zenyewe huwa zinachimbiwa kwa kufuata msitari na kushikamanishwa kwa kufungwa pamoja, zikawa kama jamaa waliotangulizana, ili ziweze kusaidiana katika kuilinda vizuri nyumba hiyo. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘jamaa wametangulizana:- nguzo.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wale ambao wana uelewano wa kuilinda vizuri familia yao. Watu hao, huishi kwa ushirikiano wa kupanga mipango ya kuwawezesha kuindeleza kwa kuilinda vizuri familia yao hiyo. Upendo wao, huwapatia nguvu za kuyatekeleza majukumu yao, kwa kusaidiana pamoja katika uelewano wao.

Watu hao, huilinda familia yao, kama zile nguzo zinavyoilinda nyumba hiyo, kwa sababu nao wana ushirikiano wa kusaidiana kwa kuyatekeleza majukumu yao, kwa pamoja. Ndiyo maana watu hao huhadithiana kwamba, ‘jamaa wametangulizana:- nguzo.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na uelewano wa kuishi maisha yenye upendo wa kusaidiana pamoja katika kuyatekeleza majukumu yao, ili waweze kuzilinda vizuri familia zao, maishani mwao.

Matendo 2:4.

Matendo 4:32-37.

Wagalatia 6:2.

nhingi4

nhing3

nhingi

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

GENTLEMEN HAVE PRECEDED ONE ANOTHER – POLES.

The source of this riddle is the pattern of poles used in constructing a house. Poles are trees one can cut and arrange them in a manner that makes them make a house for one to stay in. They are always arranged in a certain pattern and tightened together with strings or nails so that they offer enough support for the house to appear in a good structure. This proper patterning of poles made people to come up with this riddle ‘Gendlemen have preceded one another – poles’ to communicate the way poles appear in making the house have a good structure.

This riddle can becompared to those people who work together in making sure that their families are taken care of. These people tend to formulate their plans together and implement them in a manner that enables them to have success in their families. As the poles protect the house and give shape of the house, these people function as pillars of strength and solidarity in the society.

This riddle teaches people about harmony and helping each other in fulfilling their responsibilities.

Acts 2: 4, Acts 4: 32-37,Galatians 6: 2.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.