586. KALAGU:- KIZE. LITULA NA LITULA: – MAGOHE.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola bhutumami bho ngohe. Ingohe jinijo, jigaitumamaga imilimo yajo bho gugobya, na gulanghana liso bho gugalemeja abhapalala ugwingila moyi. Ijoyi ulu munhu ugobya jigitulanyaga bho gwikumya. Ingohe jinijo jigisuyaga aha makanza ayo munhu olalaga du. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘litula na litula:- Ngohe.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe gwingila dilu mpaga mhindi. Umunhu ng’wunuyo, agayilanghana bho guitumama chiza imilimo yakwe yiniyo, guti ni ngohe umo jigatumamilaga mpaga olala umunhu, hunajifula.

Uweyi agabhizaga jigemelo ja gutumama milimo bho bhukamu bhutale, ukubhiye, kunguno ya kikalile kakwe kenako, aka gutumama milimo gwingila dilu mpaga mhindi. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘litula na litula:- Ngohe.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhukamu bho guitumama imilimo yabho, umu makanza gose aga limi, na gwisuya ibhujiku, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho. Kuhiniyo, ijito ja gugobya go ngohe jinijo, jalanga bhanhu gutumama milimo bhuli makanza, na gwisuya ahikanza ilya bhujiku.

1Wakorintho 3:9-15.

1Wakorintho 15:10.

1Wathesalonike 2:9.

2Wathesalonike 3:8-10.

KITENDAWILI: – TEGA.

PIGANO  NA PIGANO: – KOPE ZA MACHO.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia utendaji kazi wa kope. Kope hizo, hufanya kazi zake kwa kufunga na kufungua macho, na kuyalinda macho kwa kuzuia takataka zisiingie ndani yake. Zenyewe, hupigana kwa kugusana mtu anapofumba na kufumbua macho yake. Kope hizo, hupumzika wakati wa mtu kulala. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘pigano na pigano:- kope za macho.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi zake kuanzia asubuhi, hadi jioni. Mtu huyo, huzilinda kazi zake hizo kwa kuzitekeleza vizuri, kama kope za macho zinavyoyalinda macho, mpaka wakati wa mtu kulala.

Yeye huwa mfano wa kuigwa kwa wenzako katika kufanya kazi kwa bidii kubwa, kwa sababu ya maisha yake hayo, ya utendaji wa kazi kuanzia  asubuhi hadi jioni. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘pigano na pigano:- kope za macho.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na bidii za kuyatelekeza vizuri majukumu yao wakati wa mchana, na kupumzika wakati  wa usiku, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika maisha yao. Kwa hiyo, kitendo cha kupigana kwa kope za macho, hufundisha watu kuyatekeleza majukumu yao, kila wakati, na kupumzika wakati wa usiku.

1Wakorintho 3:9-15.

1Wakorintho 15:10.

1Wathesalonike 2:9.

2Wathesalonike 3:8-10.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.