491. JITINDE JA NGALU

Imbuki ya kahayile kenako, yilolile linti ilo lyateng’wa lyubhiza igunguti. Iligunguti linilo, ligabhizaga lidimu guti linti lya gembe. Hunagwene ligitanagwa ‘jitinde ja ngalu,’ kunguno ya bhudimu bholyo bhunubho.

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu, uyo alina nguzu ja gutumama milimo chiza. Umunhu ng’wunuyo, adulile gugubheja chiza nimo gose gose. Uweyi agabhizaga aidulile milimo mingi, kunguno ya nguvu ijo alinajo, nu witegeleja bhokwe. Uwitegeleja bhunubho, bhugang’wambilijaga uguidebha na guitumama chiza imilimo iyo, aginhiyagwa.

Umunhu ng’wunuyo, agalenganijiyagwa ni jitinde ija ngalu ijo jilijidimu, kunguno nang’hwe alindimu ugunoga ulu aliitumama imilimo yakwe. Akikalile kakwe, kagabhalangaja abhanhu higulya ya gubhiza na nguzu ya kuitumama chiza imilimo yabho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga umunhu ng’wunuyo, giki ali ‘jitinde ja ngalu.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza na nguvu ja gudula kuitumama chiza imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwayo mingi, umuwikaji bhobho. Amatwajo genayo, gagubhambilija abhoyi ugujibheja chiza ikaya jabho.

Mathayo 16:13-20.

Mathayo 21:42.

KISWAHILI: KISIKI KILICHO IMARA

Chanzo cha msemo huo, chaangalia mti uliokatwa ukabakia kisiki. Kisiki hicho, huwa kigumu kama mti wa mninga. Ndiyo maana watu hukiita, ‘kisiki kilicho imara,’ kwa sababu ya uimara wake huo.

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu, yule ambaye ana nguvu za kumwezesha kufanya kazi zake vizuri. Mtu huyo, aweza kufanya kazi yoyote ile vizuri. Anao uwezo wa kuzitekeleza kazi hizo, kwa sababu ya nguvu zake na umakini wake. Umakini huo, humsaidia katika kuzielewa na kuzitekeleza vizuri kazi anazopewa na watu mbalimbali.

Mtu huyo, hulinganishwa na kisiki kilicho imara ambacho ni kigumu sana, kwa sababu, naye ni mgumu kushoka anapofanya kazi zake. Maisha yake, huwafundisha wenzake juu ya kuwa na nguvu za kuwawezesha kuyatekeleza vizuri majukumu yao. Ndiyo maana watu humwita, ‘kisiki kilicho imara,’ kutokana na uimara wake wa kuyatekeleza kwa umakini majukumu yake.

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na nguvu za kuwawezesha kuyatekeleza majukumu yao vizuri, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao. Mafanikio hayo, yatawasaidia watu hao katika kuzijenga vizuri familia zao.

Mathayo 16:13-20.

Mathayo 21:42.

jitinde

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.