Imbuki ya lusumo lunulo yingilile kuwikaji bho jisumva ukuwelelo na bhuli b’ojo. Ijisumba jinijo jigab’izaga na shigu ningi ija gulwa ijiliwa. Aliyo lulu, ulu shigu ulo gucha, luli lumo duhu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘jagulya ningi lwa gucha lumo.’
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhulamu b’o ng’wa munhu ubho agikalaga nabho aha welelo. Umunhu ng’wunuyo agikalaga ulya bho shigu ningi, kwingila ha gub’yalwa gokwe, ha b’ukuji na wikaji b’okwe bhose. Uweyi adebile igiki, ishiku ija gulya jinijo jili ningi, aliyo lulu, ulushigu ulo gucha, luli lumo duhu. Agabhalangaja nabhiye ugujitumila chiza ishigu jabho ija gulya jinijo. Hunagwene agab’awilaga abhiye giki ‘jagulya ningi lwa gucha lumo.’
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gulya jiliwa ukunhu bhalitumama milimo yabho na gugab’ana ijiliwa jabho na bhichabho, kugiki bhadule gujitumila chiza ishigu jab’o ijaguya jinijo, kunguno ulushigu ulo gucha luli lumo duhu.
Muhubiri 5: 18-19.
Luka 17:17-20.
Tajiri mpumbavu
KISWAHILI: ZA KULA NI NYINGI YA KUFA NI MOJA
Chanzo cha methali hiyo chatokea kwenye maisha ya kiumbe ulimwenguni na ulaji wake. Kiumbe hicho huwa kina siku nyingi za kula chakula. Lakini basi, siku ya kufa kwa kiumbe hicho ni moja tu. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘za kula ni nyingi ya kufa ni moja.’
Methali hiyo hulinganishwa kwenye maisha ya mwanadamu alivyo na siku nyingi za kula, lakini siku yake ya kufa ni moja tu. Mtu huyo huwa anakula mara nyingi katika siku zake hizo, ambazo ni za kuanzia kuzaliwa kwake, kukua na kuishi kwake. Yeye hufahamu kwamba anazo siku hizo nyingi za kula, lakini siku yake ya kufa ni moja. Hivyo huwafundisha watu wake juu ya kuzitumia vizuri siku hizo za kula ili waweze kuacha historia nzuri watakapokufa. Ndiyo maana huwaambia kwamba, ‘za kula ni nyingi ya kufa ni moja.’
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kula chakula huku wakifanya kazi na kuwagawia wahitaji chakula chao, ili waweze kuzitumia vizuri siku zao, kwa sababu siku ya kufa ni moja.
Muhubiri 5: 18-19.
Luka 17:17-20.
ENGLISH: THERE’RE A NUMBER OF DAYS FOR EATING BUT ONE DAY FOR DEATH.
This saying comes from the real life of creatures that they have a number of days they can spend in eating but they have only one day for their death.
This saying can be compared to a man’s life with many days of eating, but having only one day for death. Under normal circumstances, human beings take food from birth to death which means several days (reference is made to human beings who live for quiet a long time). But, when it comes to death, it is only just a minute.
This saying, therefore, teaches people how to make good use of those eating days so that they can leave a certain legacy in life. It also teaches people to work hard and be able to donate food to the needy people because, in doing so, they will be preparing their own environment of being remembered in future.
Ecclesiastes 5: 18-19.
Luke 17: 17-20.