Imbuki ya lusumo lunulo ilolile kalile ka shimba. Ishimba ilindimu iyo idalyaga ndimu iyo ichile. Iyoyi igalyaga indimu iyo yib’ulagaga yoyi njinikili. Kuyiniyo lulu, ishimba igatumilaga nguzu ningi ijaguipeja indimu yiniyo mpaga yib’ulage kugiki ipandike jiliwa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘shimba igalyaga maguzu gayo.’
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagalyaga jiliwa ijo bhajipandika bho gutumila nguzu jabho. Abhanhu bhenabho bhagatumama milimo yabho, bho bhukamu bhutale mpaga bhajipandika isabho ijobhagajilyaga umuwikaji bhobho. Abhanhu bhenabho bhagabhakomelejaga abhichabho gwikomeja gutumama milimo bho guyomba giki, ‘shimba igalyaga maguzu gayo.’
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu gwikomeja gutumama milimo, kugiki bhadule gujipandika isabho ijaguyulya jiliwa ja maguzu gabho.
(1 Wathesalonike 4:11 – 12)
KISWAHILI: SIMBA HULA NGUVUZE.
Chanzo cha methali hiyo chaangalia ulaji wa simba. Simba ni myamapori ambaye hali mzoga. Yeye hula mnyama ambaye amemuua yeye mwenyewe kwa nguvu zake. Kwa hiyo, mnyama huyo hutumia nguvu nyingi katika kumfukuza mnyama yule aliyemlenga, mpaka ampate na kumuua, ili apate chakula chake. Ndiyo maana watu husema, ‘Simba hula nguvuze.’
Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wale ambao hula chakula walichokipata wao kwa kutumia nguvu zao wenyewe. Watu hao hufanya kazi zao kwa bidii kubwa, mpaka kufikia hatua ya kupata mali wailayo maishani mwao. Watu hao huwahimiza pia wenzao kuongeza bidii ya kufanya kazi zao, kwa kusema kwamba, ‘Simba hula nguzuze.’
Methali hiyo hufundisha watu kuongeza bidii katika kufanya kazi ili waweze kupata mali ya kula chakula kitokanacho na jasho lao. Bidii hiyo itawaletea maendeleo katika familia zao.
(1 Wathesalonike 4:11 – 12).
ENGLISH: THE LION EATS ITS STRENGTHS.
The origin of this proverb looks at the lions’ eating habits. A lion is a wild animal that does not eat a corpse. It eats an animal that it has killed with its own efforts and strenghts. Thus, the animal spends most of its energy on chasing the targeted prey, until it finds and kills it, in order to get its well deserved food. That is why people say, ‘A lion eats its strengths’.
The proverb is used comparatively to refer to those people who eat food from their own sweat as a result of using their own strengths. These people work very hard, to the point where they get the wealth they need in their lives. The same people also encourage their peers to work hard, saying, ‘The lion eats its strengths.’
The proverb teaches people to increase their effort in working hard so that they can earn a living from their sweat. The effort will bring prosperity to their families.
(1 Thessalonians 4:11 – 12)