274. NCHA ALILE SHANGU NA GUBHOLA.

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile kajikilwe ka ng’wa munhu uyo alinsabhi o ng’ombe. Unsabhi o ng’ombe ng’wunuyo ulu ucha agakumbagwa ndili ndoto ya ng’ombe, kugiki wanguhe ugubhola, nu bhubhi bho lufu, bhushile wangu.

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagajitumilaga chiza isabho jabho umuwikaji bhobho. Abhanhu bhenabho bhadebhile igiki bhalacha bhujileka isabho jinijo. B’agabhalangaga na abhichab’o gwikala bho mholele na bhanhu, umumayange nu mubhuyegi. B’adebhile ugubhalunguja abhanhu abho bhali na mayange, kugiki bhagamale wangu na bhomholele. Hunagwene bhagayombaga ahikanza lya mayange giki, ‘ncha alile shangu na gubhola.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu gwikala bho mholele na bhanhu ijinagutumila chiza isabho jabho. Uwikaji bhunubho bhugub’alunguja abho b’alimumayange, kugiki bhamanile wangu na gwandya kutumama milimo yabho.

(Ufunuo 14:13)

KISWAHILI: AFAYE AMEKULA NI MWEPESI KUOZA.

Chanzo cha methali hii chaangalia namna azikwavyo mtu mwenye utajiri wa ng’ombe. Tajiri huyo akifa, huviringiwa ngozi mbichi ya ng’ombe ili awahi kuoza aepuke ubaya wa kifo mapema.

Methali hii hulinganishwa kwa watu wale watumiao vizuri mali zao maishani mwao. Watu hao hufahamu kwamba watakufa na kuziacha mali hizo. Hivyo, huwafundisha wenzao kuishi kwa amani na watu, wakati wa matatizo na ule wa furaha. Watu hao huelewa pia namna ya kuwafariji watu walio na matatizo, yakiwemo yale ya misiba, ili wayamalize mapema na kwa amani. Ndiyo maana huwaambia walioko kwenye msiba kwamba, ‘afaye amekula ni mwepezi kuoza.’

Methali hiyo hufundisha watu kuishi kwa amani na watu wengine watumiapo vizuri mali zao. Maisha hayo yatawafariji wale walioko kwenye misiba, ili waizoee mapema hali hiyo, kiasi cha kutosha kuendelea na kazi zao, kwa sababu ‘afaye amekula ni mwepezi kuoza.’

 “Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wale wafao katika Bwana tangu sasa.”

 “Naam,’’ asema Roho, “watapumzika kutoka katika taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.’’”

(Ufunuo 14:13).

 

 

stone cross

ENGLISH: HE WHO DIES AFTER EATING DECAYS FAST.

The origin of this proverb is a livestock-rich person’s burial. When such a person dies, he is shrouded in a fresh cow skin, so that he/she may decay fast and do away with the badness of death.

The proverb is used comparatively to commend those people who make good use of their assets. These people know that they will die and leave the assets behind. Thus, they teach their fellows about how to live in peace with people, in times of trouble and in happiness. They also understand how to comfort people who have experienced tragedies, such as disasters, to solve them in time and in peace. That is why people tell those who are in bereavement grief that, ‘he who dies after eating decays fast.’

The proverb teaches people to live in peace and use their property properly. They will comfort those in bereavement so that they can accept the situation and adjust acordingly enough to continue their daily life, because, ‘He who dies after eating decays fast.’

 “And I heard a voice from heaven saying,”Write, Blessed are they that die in the Lord from henceforth.”

 “Yea,” saith the Spirit, “shall rest from their troubles, for their works shall follow them. ‘” (Revelation 14:13).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.