256. NUNU ADADIMAGWA SAGALA.

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile noni iyo igitanagwa nunu. Inoni yiniyo ilindalang’hanu gete na idijinogu ugwidima. Kunguno yiniyo, abhanhu bhagayombaga giki, ‘nunu adadimagwa sagala.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhali na masala ga kudebha chiza uguitumama imilimo yabho kugiki bhadizupandika makoye guti gagugaiwa jiliwa nulu gupejiwa mumilimo yabho. Abhanhu bhenabho bhamanile ugubhalanga abhichabho inzila ja gubhiza na bhulalang’hanu bhunubho.

Igabhizaga jidamu noyi abhanhu bhenabho ugupandika makoye guti ga nzala. Bhagikolaga n’i nunu yiniyo iyo idadimagwa sagala. Abhanhu bhenabho b’ajimanile inzila ja gwikinga na bhanishi guti: bhubuli, bho gusoma na gupandika bhumani, masada bho gusoma, masada bho gupandika bhumani  upanga, na bhuhab’i bho gutumama milimo na bhukamu bhutale.

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu  gub’iza na masala ga gwilang’hana na bhanishi mukikalile kabho. Amasala genayo gagubhambilija ijinagutumama milimo yabho bhobhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika jiliwa, jizwalo, na bhulalo bhobho. Ijinagongeja, amasala genayo gagubhambilija ugubhasomisha chiza abhana bhabho kugiki nabho bhapandike maendeleo matale mukikalile kabho.

KISWAHILI: FUMVU HAKAMATWI KIRAHISI.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia ndege ajulikanaye kwa jina la fumvu. Ndege huyo ni mjanja sana na huwa ni vigumu kukamatwa. Kwa sababu hiyo, watu husema, ‘fumvu hakamatwi kirahisi.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wenye akili za kufahamu vizuri namna ya kufanya kazi zao ili wasiweze kupatwa na matatizo mbalimbali yakiwemo yale ya kuishiwa chakula nyumbani, na kufukuzwa kazi. Watu hao wafahamu namna ya kulea vyema pia wenzao kwa kuwafundisha njia za kuwa na ujanja huo wa kukwepa matatizo.

Huwa ni vigumu sana kwa watu hao kukumbwa na matatizo kama vile njaa katika familia zao. Ndiyo maana watu hao hufanana na ndege huyo fumvu ambaye hakamatwi kirahisi. Wao wanazifahamu njia za kupambana na maadui mbalimbali kama vile: ujinga, kwa kupata elimu, magonjwa kwa kupata elimu juu ya afya bora, na umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii.

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na akili ya kuwapatia ujanja wa kujilinda dhidi ya maadui zao. Akili hiyo itawasaidia katika kufanya kazi kwa bidii kubwa, ili kumshinda adui umaskini, kwa kujipatia mahitaji yao kama vile chakula, mavazi na malazi. Zaidi ya hayo, akili hiyo itawasaidia katika kuwasomesha vizuri watoto wao kwa ajili ya kujipatia maendeleo makubwa maishani mwao.

(Luka 4:29-30; Mathayo 10:16-20)

 

nest-bird

ENGLISH: A LAUGHING DOVE IS NOT EASILY CAUGHT.

The origin of this proverb is a bird known as ‘laughing dove’.’ The bird is considered to be very clever, which makes it difficult to catch. That is why people say, ‘A laughing dove is not easily caught.’

The proverb is used comparatively to refer to people who have a good sense of how to do their jobs so that they do not suffer from a variety of problems, including food shortage, and dismissal from such jobs. They know how to properly nurture their peers by teaching them how to avoid such problems.

It is very difficult for such people to experience problems such as hunger in their families. That is why those people are likened to ‘a laughing dove’ which does not easily fall prey to traps. They are aware of ways to defend themselves against their enemies such as ignorance, disease and poverty through hard work and acquisition of education.

This proverb teaches people about having ingenuity and techniques to defend themselves against their enemies. This ingenuity will help them to work hard enough to defeat the enemy such as poverty through obtaining their basic needs such as food, clothing and shelter. In addition, the ingenuity will help them give their children better education for the greater achievements in their lives.

Luke 4: 29-30.

Matthew 10: 16-20.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.