Riddles

495. KALAGU – KIZE. NSIZA ONE ALI NA MIKIMBILI MINGI:- NHUMBI JI GUWA.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola iguwa. Iliguwa lilina nhumbi ningi noyi. Huguhaya giki, ligalenganijiyagwa na nkimbili kunguno ligikolaga chene. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘nsiza one ali na mikimbili mingi:- nhumbi ji guwa.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu, uyo adebhile chiza isumo  yakwe. Umunhu ng’wunuyo, aidebhile ihitoria ya bhabyaji bhakwe, niya bhabyaji bha bhabyaji bhakwe.

Uweyi agabhalanjaga na bhiye ihistoria yiniyo, kugiki bhimane umundugu yabho. Abho bhagandelekaga, bhagadulaga ugubhamana chiza abhadugu bhabho, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘nsiza one ali na mikimbili mingi:- nhumbi ji guwa.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya guidebha historia ya jibyalilwe jabho, kugiki bhadule gwimana chiza, umuwikaji bhobho, kunguyo abhanhu bhali na jibyalilwe jingi noyi.

Mathayo 1:1-17.

Mwanzo 15:1-6.

Luka 3:23-38.

KISWAHILI: KITENDAWILI   –  TEGA.

KAKA YANGU ANA VIUNO VINGI:- MUWA.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia muwa. Muwa huo, una pingili nyingi sana. Ndiyo kusema kwamba, huwa unalinganishwa na kiuno, kwa sababu ya wenyewe kufanana nacho. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘kaka yangu ana viuno vingi:- muwa.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anaelewa vizuri historia ya ukoo wake. Mtu huyo, anaielewa historia ya wazazi wake na ile ya wazazi wa wazazi wake.

Yeye huwafundisha wenzake historia hiyo, ili waweze kuwaelewa ndugu zao. Wale wanaomsikiliza, huweza kuzifahamu vizuri koo zao, maishani mwao. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘kaka yangu ana viuno vingi:- muwa.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuzielewa historia za koo zao, ili waweze kufahamiana vizuri, maishani mwao, kwa sababu watu huwa wana vizazi vingi mno.

Mathayo 1:1-17.

Mwanzo 15:1-6.

Luka 3:23-38.

maguha

miguha1

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

MY BROTHER HAS MANY WAISTS:- SUGARCANE.

The source of this riddle is sugarcane and its joints. Sugarcanes have so many joints that look like waists. Those sugarcane joints are being compared to waists. That is why people came up with a riddle that describes the structure of sugarcane in comparison to waists by riddling that ‘my brother has many waists – sugarcane.’

This saying can be compared to a person who understands his/her family history. That person understands well his/her parent’s history and that of his parents’ parents. He/she can teach history to his/her colleagues so that they can understand their past in terms of family geneology.

This saying teaches people about understanding their family history so that they can get to know each other better in their lives. This comes because people have so many generations that are inter-connected and sometimes cannot be easy to know them.

Matthew 1: 1-17.

Genesis 15: 1-6.

Luke 3: 23-38.

487. KALAGU – KIZE. ANE ANE MPAGA TANGA: – MADANDALI GA MUNDUKA.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola munduka iyo igikalaga na madandali ane. Imunduka yiniyo, idulile gupejiwa mpaga yushiga kule wikanza iguhi, kunguno ya wiyambilija bho madandali gayo, ayane geneyo.

Kuyiniyo lulu, ijisumva ijo jilina magulu ane, jigasiminzaga wangu wangu, nulu jidulile gupela wangu wangu mpaga jusegenela bho likanza liguhi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ane ane mpaga Tanga:- madandali ga munduka.’

Ikalagau yiniyo, igalenganijiyagwa ku bhanhu abho bhagiyambilija kihamo na bhichabho, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhadebhile ugutumama kihamo na bhichabho, gitu umo gagiyambiligijaga amadandali ayane aga munduka genayo.

Abhanhu bhenabho, bhali jigemelo ja gwikala kihamo bho gwiyambilija, umubhutumami bho milimo yabho. Umukikalile kabho kenako, bhagabhalangaga nabhichabho, ahigulya ya gubhiza halumo ijinaguitumama bho wiyambilija imilimo yabho. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayombaga giki, ‘ane ane mpaga Tanga:- madandali ga munduka.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya guitumama imilimo yabho halumo bho gwiyambilija, kugiki bhadule guimala wangu na kupandika matwazo mingi, umuwikaji bhobho.

Uwiyambilija bhunubho, bhudulile gubhinha nguzu ja kunondela Yesu bho bhukamu bhutale, ubho wikomile gubhashisha mpaga ng’wigulu.

Yahane 14:11-14.

Yohane 14:25-26.

Yohane 15:1-5.

2Wafalme 2:11-12.

Matendo ya mitume 4:32-37.

KISWAHILI: KITENDAWILI   –  TEGA.

NNE NNE MPAKA TANGA:- MAGURUDUMU YA GARI.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia gari yenye magurudumu manne. Gari hilo, laweza kuendeshwa mpaka likafika mbali, kwa muda mfupi, kwa sababu ya kusaidiana kwa magurudumu hayo manne.

Kwa hiyo, viumbe vyenye miguu mine, hutembea kwa haraka hata vinaweza kukimbia kwa haraka mpaka vikafika mbali kwa muda mfupi. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘nne nne mpaka Tanga:- magurudumu ya gari.’

Kitendawili hicho, chalinganishwa kwa watu wale wanafahanya kazi zao kwa kusaidiana, maishani mwao. Watu hao, wanaelewa namna ya kuyatekeleza majukumu yao, kwa kusaidiana katika kumoja wao, kama yanavyosaidiana yale magurudumu manne mpaka yanafaulu kulifikisha mbali kwa muda mfupi gari hilo.

Watu hao, ni mfano wa kuigwa katika kuuishi umoja wa kusaidiana katika utekelezaji wa majukumu yao. Maisha yao, huwafundisha wenzao juu ya kuwa na umoja unaowawezesha watu kusaidiana katika kufanya kazi zao. Ndiyo maana watu hao husema kwamba, ‘nne nne mpaka Tanga:- magurudumu ya gari.’

Kitendawili hicho, chafundisha watu juu ya kuzifanya kazi zao katika umoja wa kusaidiana, ili waweze kuzimaliza mapema na kupata mafanikio mengi zaidi, maishani mwao.

Umoja huo, utawasaidia hata katika kumwamini Yesu na kumfuata hadi kumfikia Yeye mbinguni.

Yahane 14:11-14.

Yohane 14:25-26.

Yohane 15:1-5.

2Wafalme 2:11-12.

Matendo ya mitume 4:32-37.

chevrolet

jaguar

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

FOUR FOUR UP TO TANGA- CAR WHEELS.

The source of this riddle is the car and its tyres. The car can be driven for a long distance with the help of its tyres. This four-legged creature can move very fast to the extent of covering a very long distance within a very short period of time. To describe how the car is assisted by its tyres to reach such long distances people tend to use the riddle that ‘four four up to Tanga’ where Tanga is used as a measure of distance; the highest distance from where the car set off the journey.

This riddle can be compared to those people who do their works in collaboration with others. These people tend to understand each other on how to carry out their duties. They help each other in the same way tyres work until they reach their desired goals. Such people can be described as role models for others.

This riddle teaches people about doing their jobs in collaboration. This can help people to finish their works within a short time. In so doing, they will be making their families to have good and peaceful life. This unity can also help them to know how Jesus works in human minds. They can work together in ensuring that they follow Him to heaven after death.

John 14: 11-14.

John 14: 25-26.

John 15: 1-5.

2Kings 2: 11-12.

Acts 4: 32-37.

486. KALAGU – KIZE. NTI GONE GULI NA MATAMBI MPUNGATI; AYANE MADOTO, AYABHILI, MOMU, ILIMO LISAJI:- NG’OMBE.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola ndimu iyo ilitanwa Ng’ombe. Ingombe yiniyo, ili na magulu ane, ha matambi amadoto, ayabhili momu, ha mapembe gayo ing’ombe yiniyo. Ilitambi ilimo lisaji, ugwene hunkila goyo, kunguno gukilalaga gulifilinjiwa ukunu nu kunu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘nti gone guli na matambi mpungati, ayane madoto, ayabhili, momu, ilimo lisaji:- Ng’ombe.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile ugugalekanya chiza amakanza. Umunhu ng’wunuyo, umulikanza lya jidiku amanile igiki isi igikalaga ndoto, agalimaga kunguno lilikaza lya gulima.

Uweyi agisuyaga umulikanza lya chu, kunguno isi igumaga na malima nago gagimaga. Agatumamaga milimo ya gujilanhana chiza ijiliwa ijo ojipandika aho olimaga.

Ilitambi ilisaji, ligikolaga na bhanhu abho bhagajitumamilaga sagara isabho ijo bhagajipandikaga umubhuchoji bhobho. Abhanhu bhenabho, bhagajing’welaga walwa mpaga bhandya guyomba mihayo ya sagala, guti bhanhu bhasaji.

Abhanhu bhenabho, ulu bhuhaya guja gujung’wa walwa, bhagiwilaga giki, bhaje ukubhusaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘nti gone guli na matambi mpungati, ayane madoto, ayabhili, momu, ilimo lisaji:- Ng’ombe.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gugatumila chiza amakanza gabho aga milimo, na gujitumila chiza isabho ijo bhalijipandika, umumilimo yabho yiniyo, kugiki, bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 16:1-4.

Mathayo 24:32-38.

KISWAHILI: KITENDAWILI   –   TEGA

MTI WANGU UNA MATAWI SABA MANNE MABICHI, MAWILI MAKAVU, MOJA KICHAA:- NG’OMBE.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia mnyama aitwaye Ng’ombe. Ng’ombe huyo, ana miguu, minne, ndiyo matawi mabichi, yale mawili ambayo ni makavu, ni pembe zake ng’ombe huyo. Lile moja ambalo ni jehu, ni mkia wake, maana huwa hautulii, kwa sababu huwa unachezeshwa chezeshwa tu. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘mti wangu una matawi saba, manne mabichi, mawili makavu, moja kichaa:- ng’ombe.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye afahamu kutofautisha vizuri majira mbalimbali ya mwaka. Mtu huyo, hufahamu huutumia wakati wa masika kwa kulima, kwa bidii kubwa, kwa sababu wakati huo, ardhi huwa ni mbichi.

Yeye hupumzika wakati wa kiangazi, kwa sababu wakati huo, ardhi huwa ni ngumu na kavu. Huo ni muda wa kuyakusanya mazao yake vizuri, na kuyahifadhi sehemu ambayo yaweza kuyatunza vizuri.

Tawi jehu huonesha wakati wa kiangazi, ambao baadhi ya watu huyatumia mafanikio ya kilimo chao, au mali zao, kwa kunywea pombe. Baadhi yao hulewa mpaka kufikia hatua ya kuanza kuongea maneno yasiyofaa, kama wehu.

Watu hao, hualikana kwenda kunywa pombe wakielezana kwamba, waende kwenye wehu wao. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘mti wangu una matawi saba, manne mabichi, mawili makavu, moja kichaa:- ng’ombe.’

Kitendawili hicho, chafundisha watu juu ya kuutumia muda wao wa kazi vizuri, na kuyatumia mafanikio ya kazi zao hizo vizuri, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Mathayo 16:1-4.

Mathayo 24:32-38.

nzagamba1

cow meat

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

MY TREE HAS SEVEN BRANCHES; FOUR ARE NOT DRY, TWO ARE DRY, ONE IS CRAZY- COW.

The source of this riddle is a cow and its body parts; four legs that help it keep on walking, two horns that are immobile, and a tail that keeps on moving to swip away insects that can tend to attack the cow. Therefore the riddle that ‘my tree has seven branches; four are not dry, two are dry and one is crazy’ communicates how the cow body parts work.

This riddle can be compared to a person who knows how to properly distinguish the different seasons of the year. They can use the spring season for ploughing with great efforts because this is the time when the soil is wet and easy to cultivate. During dry season, they gather their produce from the farm and keep them safely for future use. During summer, people spend what they produced from their farms. They drink local brew to their satisfaction. It is the time where one expects to have extravagance in terms of expenditure.

This riddle teaches people about how to use their time well and make the most of their work so that they can better their families as well as their lives.

Matthew 16: 1-4.

Matthew 24: 32-38.

484. KALAGU – KIZE. ADALALAGA BHUJIKU NA LIMI:- LIMI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola liginhu ilo lilitanwa limi. Ilimi linilo, lidimaga utima kunguno, pye amakanza ligabhizaga lilitumama duhu. Ilyoyi lidanogaga ugutima kunguno, lyabhejiwa chene.  Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘adalalaga bhujiku na limi:- Limi.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu, uyo alina bhukalalwa bho gutumama imilimo yakwe, bho nguvu jakwe pye ijose. Umunhu ng’wunuyo, ogumanilija umili gokwe kutumama milimo yiniyo, bho makanza malilu, kunguno uweyi adanogaga wangu.

Umunhu ng’wunuyo agalenganijiyagwa ni Limi ilo lidanogaga ugutima, kunguno, nang’hwe umunhu ng’wunuyo, adanogaga wangu uguitumama imilimo yakwe yiniyo. Uweyi agabhalangaga nabhiye ahigulya ya guitumama imilimo yabho, bho bhukamu bhutale. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘adalalaga bhujiku na limi:- Limi.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhukalalwa bho guitumama imilimo yabho, bho bhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika, matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

2Wakorintho 4:16-18.

2Wakorintho 5:1-3.

Mathayo 24:35.

KISWAHILI: KITENDAWILI   –  TEGA

HALALI USIKU NA MCHANA:- JUA

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia kitu kinachoitwa Jua. Jua hilo, halisimami kuangaza, kwa sababu lenyewe hufanya hivyo kwa muda wote. Lenyewe halichoki kumulika, kwa sababu liliumbwa hivyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘halali usiku na mchana:- Jua.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye bidii, na hamu ya kufanya kazi zake kwa nguvu zake zote. Mtu huyo, ameuzoesha mwili wake kufanya kazi hizo kwa muda mrefu, bila kuchoka mapema.

Mtu huyo, hulinganishwa na Jua, ambalo huwa halichoki kumulika, kwa sababu naye pia huwa hachoki mapema kuzitekeleza kazi zake hizo. Yeye huwafundisha pia wenzake, namna ya kuyatekeleza majukumu yao, kwa bidii kubwa. Ndiyo maana yeye huwahadithia watu kwamba, ‘halali usiku na mchana:- Jua.’

Kitendawili hicho, chafundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kuzitekeleza kazi zao kwa umakini mkubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

2Wakorintho 4:16-18.

2Wakorintho 5:1-3.

Mathayo 24:35.

Limi

magwa limi

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

HE DOES NOT SLEEP DAY AND NIGHT – THE SUN.

The source of this riddle is the sun that does not rest in its shinning. It shines all the time. The sun was created to shine all the time. That is why people have a riddle to describe this natural happening that ‘he does not sleep day and night – the sun.’

This riddle can be compared to a person who is industrious and eager to do his/her best. That person has conditioned his/her body to work tirelessly, a condition that is comparable to that of the sun that shines day and night.

This riddle teaches people to carry out their duties with great effort and to be diligent in carrying out their tasks with great care so that they can achieve more in their lives.

2 Corinthians 4: 16-18.

2 Corinthians 5: 1-3.

Matthew 24:35.

483. KALAGU – KIZE. OZA ALINAMBA OPI: – MOTO NA FUGO.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola moto na fugo, ahikanza lya bhuzugi. Umubhuzugi bhunubho, uoza ng’wunuyo humoto, uyo gugabhagaka. Uopi hi fugo iyo igazugilagwa ijiliwa. Umoto gunuyo, gugabhizaga guti guliilamba ifugo yiniyo, ulu gulibhaka, kunguno ugoyi gukikalaga hasi, huna yatulwa ifugo ahigulya yago. Ifugo yiniyo, igatulwaga hamashiga adatu, haho guli umoto gunuyo, uyo gugaisebhyaga ifugo yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘oza alinamba opi: moto na fugo.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu, abho bhagikalaga halumo umuwikaji bhobho. Abhanhu bhenabho, bhadilekanijaga umubhutumami bho milimo yabho, kunguno, bhadebhile igiki abhanhu bha makabhila gose, ni rangi jose, bhali sawa ahabhutongi ya yakwe, uyo obhasumba.

Abhanhu bhenabho, bhikolile ni fugo nu moto, ijo jigiyambilijaga ugubisha chiza ijiliwa, kunguno nabho bhagiyambilija halumo ijinaguitumama imilimo yabho yiniyo. Hunagwene, abhanhu bhenabho, bhagabhalangaga na bhichabho, nzila ja gwiyambilija halumo chiniko, bho gwiganila giki, ‘oza alinamba opi: moto na fugo.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwikala bho gwiyambilija halumo, yaya gubhakomanya abhanhu, kunguno ya makabhila, nulu rangi jabho, kugiki bhadule gwikala bho mholele, na kupandika matwazo mingi, umuwikaji bhobho.

1Wakorintho 12:4-11.

1Wakoritho 3:1-8.

KISWAHILI: KITENDAWILI  –  TEGA

MWEKUNDU ANAMBA MWEUSI:- MOTO NA CHUNGU.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia moto na chungu cha kupikia chakula wakati wa upikaji huo. Kinapopikwa chakula, mwekundu huyo, ni moto, na mweuzi, ni chungu ambacho hupikiwa chakula.

Moto huo, huonekana kama unakilamba kile chungu cha kupikia, kwa sababu ya kuwa kinakigusa, unapowaka moto huo, kwa vile, wenyewe huwa chini ya chungu hicho. Chungu hicho, huwekwa kwenye mafiga matatu, ambapo moto huo, huwekwa juu yake. Ndiyo maana watu huhadithiana kwa kusema kwamba, ‘mwekundu ana mlamba mweusi: – moto na chungu.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wale ambao huishi katika umoja wa kusaidiana, maishani mwao. Watu hao, hawatelekezani katika kuyatekeleza majukumu yao, kwa sababu ya kuelewa kwamba, wanadamu wote, wako sawa mbele ya muumba wao, bila kujali kabila au rangi.

Watu hao, hufanana na chungu chakupikia na moto, ambazo husaidiana katika kuivisha chakula, kwa sababu ya kusaidiana kwao na wenzao. Wao hutunza umoja wao huo, katika utekelezaji wa majukumu yao. Ndiyo maana, watu hao, huwafundisha watu juu ya kusaidiana kwa pamoja hivyo, kwa kusema kwamba, ‘mwekundu ana mlamba mweusi: – moto na chungu.’

Kitendawili hicho, chafundisha watu juu ya kuishi kwa kusaidiana katika umoja, bila kuwabagua watu kwa misingi ya ukabhila au rangi, ili waweze kuishi kwa amani, itakayowapatia mafanikio mengi, maishani mwao.

1Wakorintho 12:4-11.

1Wakoritho 3:1-8.

chungu na moto

pot-and fire

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

THE RED ONE IS LICKING THE BLACK FELLOW – FIRE AND POT.

The source of this riddle is fire and the cooking pot during cooking process. The flame of fire is described as red and the pot is black in colour. During cooking process, the red flame is always seen touching the pot, which happens to be placed on the cooking stones. To describe this scenario, people can use the riddle that ‘the red one is licking the black fellow.’

This riddle can be compared to people who live in unity in their lives. Such individuals work together to make sure that a certain activity is done in a required manner. The riddle also gives an impression of fighting against racial segregation by showing how the two antagonistic colours can work together in order to achieve a certain mission. It makes one believe that all human beings are equal before God.

This riddle teaches people about living by helping each other. It also teaches people about fighting against any form of discriminating against people on the basis of race or colour. In so doing, people will be able to live together as one family connected by peace and love.

1Corinthians 12: 4-11.

1Corinthians 3: 1-8.