484. KALAGU – KIZE. ADALALAGA BHUJIKU NA LIMI:- LIMI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola liginhu ilo lilitanwa limi. Ilimi linilo, lidimaga utima kunguno, pye amakanza ligabhizaga lilitumama duhu. Ilyoyi lidanogaga ugutima kunguno, lyabhejiwa chene.  Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘adalalaga bhujiku na limi:- Limi.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu, uyo alina bhukalalwa bho gutumama imilimo yakwe, bho nguvu jakwe pye ijose. Umunhu ng’wunuyo, ogumanilija umili gokwe kutumama milimo yiniyo, bho makanza malilu, kunguno uweyi adanogaga wangu.

Umunhu ng’wunuyo agalenganijiyagwa ni Limi ilo lidanogaga ugutima, kunguno, nang’hwe umunhu ng’wunuyo, adanogaga wangu uguitumama imilimo yakwe yiniyo. Uweyi agabhalangaga nabhiye ahigulya ya guitumama imilimo yabho, bho bhukamu bhutale. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘adalalaga bhujiku na limi:- Limi.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhukalalwa bho guitumama imilimo yabho, bho bhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika, matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

2Wakorintho 4:16-18.

2Wakorintho 5:1-3.

Mathayo 24:35.

KISWAHILI: KITENDAWILI   –  TEGA

HALALI USIKU NA MCHANA:- JUA

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia kitu kinachoitwa Jua. Jua hilo, halisimami kuangaza, kwa sababu lenyewe hufanya hivyo kwa muda wote. Lenyewe halichoki kumulika, kwa sababu liliumbwa hivyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘halali usiku na mchana:- Jua.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye bidii, na hamu ya kufanya kazi zake kwa nguvu zake zote. Mtu huyo, ameuzoesha mwili wake kufanya kazi hizo kwa muda mrefu, bila kuchoka mapema.

Mtu huyo, hulinganishwa na Jua, ambalo huwa halichoki kumulika, kwa sababu naye pia huwa hachoki mapema kuzitekeleza kazi zake hizo. Yeye huwafundisha pia wenzake, namna ya kuyatekeleza majukumu yao, kwa bidii kubwa. Ndiyo maana yeye huwahadithia watu kwamba, ‘halali usiku na mchana:- Jua.’

Kitendawili hicho, chafundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kuzitekeleza kazi zao kwa umakini mkubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

2Wakorintho 4:16-18.

2Wakorintho 5:1-3.

Mathayo 24:35.

Limi

magwa limi

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

HE DOES NOT SLEEP DAY AND NIGHT – THE SUN.

The source of this riddle is the sun that does not rest in its shinning. It shines all the time. The sun was created to shine all the time. That is why people have a riddle to describe this natural happening that ‘he does not sleep day and night – the sun.’

This riddle can be compared to a person who is industrious and eager to do his/her best. That person has conditioned his/her body to work tirelessly, a condition that is comparable to that of the sun that shines day and night.

This riddle teaches people to carry out their duties with great effort and to be diligent in carrying out their tasks with great care so that they can achieve more in their lives.

2 Corinthians 4: 16-18.

2 Corinthians 5: 1-3.

Matthew 24:35.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.