Kashinje Zacharia

585. KALAGU – KIZE. NG’OMBE YANE YAGUSHEMELA MKAYA AMAPEMBE HANZE:- LYOCHI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, yingilile ku lyochi ilo ligafumaga hanze ulu munhu alizuga jiliwa umukaya. Ilyochi linilo, lililyapi ilo ligalolelagwa na bhuli ng’wene. Ilyoi ligabhizaga jimanyikijo ja bhuzugi bho jiliwa ahakaya yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘ng’ombe yane yagushemela mkaya amapembe hanze:- lyochi.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitaga ya wiza umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agolechaga imihayo iyo agiiganikaga kubhitila mu miito gakwe ayo galigawiza.

Amiito gakwe agawiza genayo, gagikolaga ni lyochi ili ligolechaga giki jiliwa jilizugwa ahakaya iyo lilifumilila iyochi linilo. Umungu ng’wunuyo, agabhalanjaga nabhiye ahigulya ya gubhiza na miganiko gawiza, kugiki amiito gabho, gadule gubhiza masoga. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘ng’ombe yane yagushemela mkaya amapembe hanze:- lyochi.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na miganiko ga wiza, na gujidebha inhungwa ja bhanhu bhabho, bho gugalola amiito gabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, bho gwikala bho mholele na chichabho, shigu jose.

Mathayo 12:33-37.

Mathayo 7:16-20.

Luka 6:43-45.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

NG’OMBE WANGU WA KUKAMULIA NDANI PEMBE ZIKIWA NJE:– MOSHI.

Chanzo cha kitendawili hicho, chatokea kwenye moshi unaotokea nje ya nyumba wakati mtu anapika chakula ndani yake. Moshi huo, ni mweusi ambao huonekana kwa kila mmoja.

Wenyewe ni ishara inayotambulisha wakati wa kupikwa kwa chakula katika familia hiyo. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘ng’ombe wangu wa kukamulia ndani pembe zikiwa nje:- moshi.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutenda matendo mema katika maisha yake. Mtu huyo, huonesha mawazo anayoyafikiria moyoni mwake, kwa kutenda matendo hayo mema.

Matendo yake hayo, hufanana na moshi unaonesha kupikwa kwa chakula katika familia ile ambayo moshi huo unatokea. Mtu huyo, huwafundisha wenzake juu ya kuwa na mawazo mema ili matendo yao yaweze kuwa mema pia. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘ng’ombe wangu wa kukamulia ndani pembe zikiwa nje:- moshi.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na mawazo mema na kuzifahamu tabia za watu wao, kwa kuyaangalia matendo yao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, katika kuishi kwa amani na wenzao, siku zote.

Mathayo 12:33-37.

Mathayo 7:16-20.

Luka 6:43-45.

lyochi2

lyochi

lyochi1

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

MY COW IS BEING MILKED FROM INSIDE BUT HER HORNS ARE OUTSIDE – SMOKE.

The source of this riddle comes from smoke that comes from one’s house when cooking food. When the smoke comes from one’s house it is an indication that there is a possibility of having food in that particular family. That is why people came with the riddle that ‘my cow is being milked from inside but her horns are outside – smoke’ to communicate the sense of seeing smoke outside someone’s house when cooking.

This riddle can be compared to a person who does good things in his/her life. The person’s actions can be likened to a smoke that shows how rich is the person in terms of his/her thoughts. This person teaches others about how to be good to others.

This riddle teaches people about having positive ideas and being aware of the behaviour of people by observing their actions. This can help to know each other well and take care of the society in a manner that shows peace and co-existence with others.

Matthew 12: 33-37, Matthew 7: 16-20, Luke 6: 43-45.

584. NDULU YAKOMANGA.

Imbuki ya kahayile kenako, yilolile ndimu iyo igitanagwa ndulu. INdulu yiniyo, igasiminzaga lugendo lo gukangilija. Iyoyi igajaga bhutongi bho nduhu ugwigedyagedya, nulu gulabhula inuma. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ndulu yakomanga.’

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe bho nguzu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambija bho guja bhutongi duhu, ijinabhutumami bho miliyo yakwe yiniyo, guti numo igigulambigijaga guja bhutongi, indulu yiniyo.

Uweyi agabhizaga jigemelo ja wiza ukubhiye ijinagutumama milimo bho bhukamu bhutale, kunguno adahayile ugwigedyagedya; umubhutumami  bhokwe, bhunubho.

Akikalile kakwe umunhu ng’wunuyo, kagabhalanjaga abhanhu ahigulya ya guidilila bho guitumama chiza imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwazo mingi, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, ‘ndulu yakomanga.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija guitumama imilimo yabho, bho nguzu na bhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umubhutumami, nu muzunya bhobho, umukikalile kabho.

Waroma 12:11.

2Petro 3:14.

Wagalatia 6:9.

Ufunuo 3:19.

KISWAHILI: PUNDA MILIA ALIEKAZA MWENDO.

Chanzo cha msemo huo, chaangalia mnyama anayeitwa pumda milia. Punda milia huyo, hutembea mwendo wa kuharakisha. Mwenyewe hukaza mwendo kwenda mbele tu, bila kusimama, wala kurudi nyuma. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘punda milia aliyekaza mwendo.’

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatekeleza majukumu yake kwa nguvu, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha katika utendaji wake wa kazi, kwa kusonga mbele tu, kama afanyavyo punda milia. Utendaji huo humwezesha kupata mafanikio mengi, katika maisha yake.

Mtu huyo, huwa mfano wa kuigwa kwa wenzako katika kuyatekeleza majukumu yao, kwa bidii, kwa sababu yeye hataki uvivu katika utekelezaji wa majukumu yake.

Maisha yake mtu huyo, huwafundisha watu juu ya kuzijali kazi zao kwa kuzitekeleza kwa bidii, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika maisha yao. Ndiyo maana watu humwita, ‘punda milia aliyekaza mwendo.’

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao, kwa nguvu na bidii kubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika utumishi wao, na katika maisha yao ya kiroho, maishani mwao.

Waroma 12:11.

2Petro 3:14.

Wagalatia 6:9.

Ufunuo 3:19.

ndulu2

 

ENGLISH: A SERIOUS WALKING ZEBRA.

The source of this saying is an animal by the name of Zebra. This animal is featured by being a fast walker and when it is set to reach somewhere it goes straight without turning back until it reaches its final destination. It is through the seriousness of the zebra that people came with the saying that ‘a serious walking zebra.’

The saying can be compared to a person who performs his/her duties in a serious manner in his/her life. This person keeps on working hard until he/she achieves his/her goals. Such a person can become a role model to others who would like to be responsible in their duties for the aim of achieveing better life. This person also teaches others about hard work and respect for work.

The saying teaches people to strive to carry out their responsibilities with great effort so as to achieve great success in life.

Romans 12:11, 2 Peter 3:14, Galatians 6: 9, Revelation 3:19.

583. KALAGU – KIZE. NANSANGA UMAMA ALIZWA NOGE – IKEMEKELO LYA MUNHU.

Imbuki ya kalagu yiniyo, yingilile ku bhub’eja bho jitwilo ja mujiliwa ijo jigitangwa munhu. Ikale umunhu goli nduhu. Giko lulu, abhachoji bhago, b’akemekaga gayutina minzi gaza, hado hado, ayo gagabhizaga guti munhu alizwa noge. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘nansanga umama alizwa noge:- ikemekelo lya munhu.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agacholaga nzila ningi ija gugamalila amakoye ayo alinago. Umungu ng’wunuyo, agagatumilaga chiza amasala gakwe mpaga ojipandika nzila ija gugamalila amakoye genayo, aha ng’wakwe.

Uweyi agikolaga nu nkemeki o munhu, kunguno nuweyi agagatumilaga chiza amasala gakwe, ijinagugamala amakoye ga ha ng’wakwe. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘nansanga umama alizwa noge:- ikemekelo lya munhu.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gudebha guchola nzila ija gugingija amakoye ayo bhaligo, umuwikaji bhobho, kugiki  bhadule gujibheja chiza ikaya jabho.

Mathayo 5:13-16.

Mathayo 25:31-45.

Luka 10:25-37.

KITENDAWILI – TEGA.

NIMEMKUTA BIBI ANATOKWA DAMU PUANI:- CHUJIO LA CHUNVI.

Chanzo cha kitendawili hicho, chatokea kwenye utengenezaji wa chumvi. Chumvi hiyo, ni kitu kinachoongeza radha kwenye chakula. Zamani chumvi haikuwepo. Hivyo basi, watafutaji wake, walikuwa wakichuja maji yaliyochuluzika kwa kudondosha maji mekundu kama mtu anatokwa damu puani. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘nimemkuta bibi anatokwa damu puani:- chujio la chumvi.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujibidisha kutafuta njia za kutatua matatizo aliyo nayo, maishani mwake. Mtu huyo, hutumia vizuri akili zake, hadi anafikia hatua ya kupata utatuzi wa matatizo hayo, nyumbani kwake.

Yeye hufanana na mchujaji huyo wa chumvi, kwa sababu naye hutumia akili zake katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo aliyo nayo, hapo kwake. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘nimemkuta bibi anatokwa damu puani:- chujio la chumvi.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuelewa namna ya kutafuta njia za kuwatatulia matatizo yao, maishani mwao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao.

Mathayo 5:13-16.

Mathayo 25:31-45.

Luka 10:25-37.

salt1

salt

salt2

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

I FOUND MY GRANDMOTHER BLEEDING ON THE NOSE – A SALT SIEVE.

The source of this riddle comes from salt production. Salt is one of the key substances that add flavor in food. There was a time when salt was very scarce and people could struggle looking for it. They could use traditional methods of getting salt. For example, they could pour water on the soil believed to have salt and begin sieving using sieves in order to get salt.

In an attempt to get salt, the sieve could drop down red liquid that comes from the soil mixed with water, the same way one could experience a person bleeding from his/her nostrils. It is through this process of getting salt using traditional method that the riddle ‘I found my grandmother bleeding on the nose – a salt sieve’ came into being.

This riddle can be compared to a person who struggles to find solutions to his or her problems in his or her life. This person can make use of his/her mind in order to make sure that he/she gets what he/she wants. Such a person is likened to a salt marsh because he/she can squiz himself/herself in order to ensure that he/she solves his/her problems.

This riddle teaches people about understanding how to find solutions to their problems in their lives.

Matthew 5: 13-16, Matthew 25: 31-45, Luke 10: 25-37.

582. YANISONGA GUTI NZILA YA MADATULA.

Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile wisongwi bho makoye ubho wiyikolile ni nzila ya madatula. Inzila ya madatula lilipande ilo nzila ningi jigagelelaga hoyi. Uyo upandika ginhu, lulu mayange mingi, agiikolaga ni nzila yiniyo. Hunagwene umunhu ng’wunuyo, agayombaga giki, ‘yanisonga guti nzila ya Madatula.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo, agamanaga upandika mayange guti ga lufu, nulu ga sada bhuli makanza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhizaga alimumayange genayo, ayo gaganyanjaga noyi, umukikalile kakwe.

Uweyi abhizaga guti ali hanzila iyo gagabhitilaga amakoye aga bhuli mbika, kunguno ya guchilwa hamo na bhadugu bhakwe, nulu gusada weyi, ahakaya yakwe yiniyo. Umunhu ng’wunuyo, agiganikaga guti giki, amakoye genayo, gagandebhaga weyi duhu. Hunagwene agayombaga giki, ‘yanisonga guti nzila ya Madatula.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kubhiza na wiyumilija umumakoye gose, kugiki bhadule gupandika nzila ijo jidulile gugamala chiza amakoye genayo, umukikalile kabho.

KISWAHILI: YAMENISONGA KAMA SEHEMU ZINAPOSHIA NJIA NYINGI.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia ulengwaji wa mfululizo wa matatizo unafanana na sehemu ile ambayo njia nyingi huishia hapo. Sehemu hiyo, ni makutanio ya njia nyingi ambazo huishia hapo. Kwa hiyo basi, hali hiyo ya kusongwa na matatizo mengi, hufanana na sehemu hiyo zinashia njia hiyo nyingi. Ndiyo maana mtu huyo, husema kwamba, ‘yamenisonga kama sehemu zinapoishia njia nyingi.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hupata matatizo kama vile yale magonjwa, na vifo mara nyingi, maishani mwake. Mtu huyo, huishi katika matatizo mengi ambayo humsumbua sana, katika maisha yake.

Yeye huwa kama yuko kwenye sehemu ile ambayo matatizo ya kila aina hufikia, kwa sababu ya matatizo hayo humkumba yeye tu. Ndiyo maana mtu huyo husema kwamba, ‘yamenisonga kama sehemu zinapoishia njia nyingi.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu katika matatizo wanayokumbana nayo, maishani mwao, ili waweze kupata njia  za kuyatatulia matatizo yao, katika maisha yao.

nzila

kaniki1

kanigini1

ENGLISH: I’M BEING PESTERED BY MANY PROBLEMS LIKE THE ONE END OF SEVERAL ROADS.

The source of this saying is many problems one encounter in life. These problems are likened to one end of several roads. The part of the road that marks the end of it can have several roads with different challenges. And, being the final destination, this part of the road should be able to withstand those challenges. This is why people came with the saying that ‘I’m being pestered by many problems like the one end of several roads.’  

This saying can be compared to people who suffer from problems such as illnesses and deaths many times in their lives. They suffer to the extent of making them appear like being at the one end of the road that has several roads.

This proverb teaches people to be patient when they face problems in their lives. Patience will enable them to have a peace of mind in their lives.

581. KALAGU – KIZE. B’ITOLELA B’AKALI PYE:- MHULI NA MHELA.

Imbuki ya kalagu yiniyo, yililola ndimu ibhili: Mhuli na Mhela. Imhuli ili ndimu nhale na nhali noyi, kunguno ulu yusaya igabhapandagilaga abhanhu, nulu abhana ndimu abhangi. Iyoyi udulile nulu gubhaluta abhanhu bho nkondo goyo, kunguno ilina nguzu ningi.

Imhela nayo ili ndimu iyo igikalaga ing’wene ng’wene duhu, kunguno ili ndimu nhali noyi nayo. Gashinaga imhuli ni mhela jili mhali pye. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘bhitolela bhakali pye:- Mhuli na Mhela.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagamanaga bhuyoga ahakaya yabho. Abhanhu bhenabho, bhuli ng’wene alemile uguhang’wa, kunguno ya gwibhona gokwe, igiki adulile pye iyose, umukikalile kakwe. Abhoyi bhagibhonaga giki bhali nguvu na bhukali bho gubhalebhya pye abhichabho, kunguno bhadabhudebhile ubhudula bho ng’wa Mulungu unsumbi o jose.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga na mhela na Mhuli, kunguno nabho, bhuli ng’wene agibhonaga giki alinkali kulebha abhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, ‘bhitolela bhakali pye:- Mhuli na Mhela.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya guleka nhinda ja gwihaya bhukali, kunguno ubhukali bhobho bhudadulile gubhushigila ubhukali bho ng’wa Mulungu, unsumbu o jose, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 11:28-30.

Mithali 3:5-8.

2Wakorintho 13:10-11.

Waebrania 4:12.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

WAMEOLEANA WAKALI WOTE:- TEMBO NA KIFARU.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia wanyama poli wawili ambao ni Tembo na Kifaru. Tembo ni mnyama mkubwa na mkali sana, kwa sababu yeye akikasilika huweza hata kukanyaga watu, na kuwaua. Yeye huweza hata kuwabeba  watu hao, na kuwatupa kwa mkondo wake, kwa sababu ana nguvu nyingi.

Kifaru naye ni mnyama ambaye hupenda kuishi peke yake, kwa sababu ya ukali wake. Kumbe Tembo na Kifaru ni wanyama wakali wote. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘wameoleana wakali wote:- Tembo na Kifaru.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wale ambao hawamalizi kelele kwenye familia yao. Watu hao, kila mmoja hataki kuambiwa kitu na mwenzake, kwa sababu ya kujiona kwamba anaweza yote, katika maisha yake. Wao hujifirikia kuwa na nguvu na ukali wa kuwazidi wenzao wote, kwa sababu  hawaufahamu uwezo wa Mungu ambaye ndiye Muumba wa vyote.

Watu hao, hufanana na Tembo na Kifaru, kwa sababu nao, hujiona kila mmoja kuwa ni mkali kupita wenzake, katika maisha yao. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘wameoleana wakali wote:- Tembo na Kifaru.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuacha kiburi cha kujidai ukali, kwa sababu ukali wao hauwezi kuufikia ukali wa Mungu aliyeumba vyote, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.

Mathayo 11:28-30.

Mithali 3:5-8.

2Wakorintho 13:10-11.

Waebrania 4:12.

mhuli2

mhela2

 

HARSH ANIMALS HAVE MARRIED EACH OTHER – ELEPHANTS AND RHINOS.

The source of this riddle is the two animals, elephant and rhino. An elephant is characterized by being big and fierce to other animals. When it gets angry it can trample on people and kill them. It can also use its tusk to throw away people or any other animal.

A rhino is another wild animal that likes to live a lonely life because of its harshness. The sharing of this attitude of being harsh made people come up with this riddle that ‘harsh animals have married each other – elephant and rhino’ to justify how related behavior of people can affect others in the society.

This riddle can be compared to quarrelsome people in the society. Such people always do not listen to others and they would like to do everything on their own. They always feel superior to others. Unfortunately, they don’t know that God is powerful than any other animal on earth. He is the creator of everything.

This riddle teaches people about giving up the pride of self-indulgence because their severity cannot reach the fierceness of God who created all things. By not praising themselves, people will have peace with each other in the society.

Matthew 11: 28-30, Proverbs 3: 5-8, 2 Corinthians 13: 10-11, Hebrews 4:12.