Sukuma Proverbs

455. MAKUNZA ADAJAGA NG’WAMASAGINGHI NG’WIYE.

Imbuki ya lusumo lunulo yilolile kikalile ka ng’wa makunja ako kali ka heke. Uweyi olialemile ugukaleka akikalile kakwe, ako kagang’wenheleja kubhiza masaginghi.

Umunhu ng’wunuyo oliadajaga ukuli masaginghi ng’wiye. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘makunja adajaga ng’wa masaginghi ng’wiye.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile igiki, bhuli ginhu jili na jimile jajo. Umunhu ng’wunuyo, agalenganijiyagwa na makunja uyo adajaga ng’wa masaginghi ng’wiye, kunguno nanghwe agajisomelaga iginhu giti numo jili, umujimile jajo.

Uweyi agikalaga akadimilile akajile kakwe kenako, guti nu makunja umo oliakadimililile akajile kakwe. Adajigaluchaga iginhu jinijo, kugiki jifade akimile kakwe uweyi, agajilekaga numo jili. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga, ‘makunja adajaga ng’wa masaginghi ng’wine.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyabhi, bho gujitumila chiza ijinhiwa jabho, kugiki bhadule kupandika matwazo mingi, umuwikaji bhobho.

Yohana 3:12.

1 Wakorintho 12:12.

KISWAHILI: MAKUNJA HAENDI KWA MASAGINGHI MWENZAKE.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia maisha ya makunja yalivyokuwa ya pekee. Yeye alikuwa hataki kuacha mwenendo wake huo wa maisha, ambao ulimfanya aitwe masaginghi, yaani mtu wa pekee.

Mtu huyo alikuwa haendi kwa masaginghi mwenzake, kwa maana ya kuiacha namna yake yakuishi, iliyompatia mafanikio mengi maishani mwake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘makunja haendi kwa masaginghi mwenzake.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule anayeelewa kwamba, kila kitu kina asili yake. Mtu huyo hulinganishwa na makunja asiyeenda kwa masaginghi mwenzake, kwa sababu naye huvisoma vitu hivyo katika asili yake, ili aweze kuuelewa ukweli wa vitu hivyo.

Yeye huwa havibadilishi vitu hivyo, vifuate alivyo yeye, bali huviacha vibaki vilivyo. Ndiyo maana watu humwambia mtu huyo kwamba, ‘makunja haendi kwa masaginghi mwenzake.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na uhuru wa kuvitumia vizuri vipaji vyao, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao.

Yohana 3:12.

1Wakorintho 12:12.

zambia-

ENGLISH: MAKUNJA DOES NOT GO TO HIS FELLOW MASAGINGHI.

The source of this proverb looks at Makunja’s unique life style. He did not want to change his style of life and people labelled him (Masaginghi) a special person. This kind of life made him a successful person. This is why people can use the proverb ‘Makunja does not go to his fellow Masaginghi’ to communicate how one with success in life cannot easily give up in struggle for fear of losing his/her richness.

The proverb can be compared to a person who understands that everything has its origin. Such a person is compared to Makunja who do not go to fellow Masaginghi because he can read by himself and be able to understand the world in its natural state.

The proverb teaches people about the freedom to make the best use of their talents. This can make one have the best kind of life determined by him/her.

John 3:12.

1 Corinthians 12:12.

454. WICHEMBA INGELE WANIJIMBA.

Imbuki ya lusumo lunulo yilolile bhuchembi bho ngele, ubhogubhajimba abhangi. Umunhu uyo alijinja ginhu ulu uichemba ingele iyo agapimilaga, aguyubhajimba abho bhalingulia. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘wichemba ingele wanijimba.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo aling’wiming’holo, umubhusuluja bhokwe. Umunhu ng’wunuyo agabhajimbaga abhanhu abho agabhajingijjga.

Uweyi agalenganijiyagwa na munhu uyo oyichemba ingele yakwe, kunguno, nanghwe abhagapunjaga abhaguji bha jikolo jakwe, bho nyashilimu. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘wichemba ingele wanijimba.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja wiming’holo, umubhusuluja bhobho, kugiki bhadizubhajimba abhaguji bha jikolo jabho.

Amosi 8:4-6.

 1 Wathesalonike 4:6.

ULIKIKATA KIPIMO UMENIPUNJA.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia ukataji wa kipimo anachokitumia mtu katika biashara yake, kwa lengo la kuwapunja wateja wake.

Mtu akikikata kipimo chake hicho cha kufanyia biashara yake, atawapunja wale wanaonunua vitu vyake. Ndiyo maana watu hao wakigundua kwamba anawapunja kwa sababu ya kukipunguza kipimo chake, humwambia kwamba, ‘ulikikata kipimo umenipunja.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mchoyo katika uendeshaji wa biashara zake. Mtu huyo huwapunja wale anaowauzia vitu vyake, kwa kutumia ujanja wa namna mbalimbali.

Yeye hulinganishwa na mtu aliyekikata kipimo chake cha kufanyia biashara, kwa sababu, naye hutumia ujanja wa kuwapunja wale wanaonunua vitu vyake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘ulikikata kipimo umenipunja.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha tabia za uchoyo wa kuwapunja watu katika biashara zao, ili waache kuwadhulumu wateja wao.

Amosi 8:4-6.

1Wathesalonike 4:6.

scale

ENGLISH: YOU HAVE CUT THE SCALE; YOU HAVE GIVEN ME LITTLE.

The source of this saying is the use of scale in business activities. A business person can cut his/her measuring scale in order to generate more profit in his/her business. If some one does so, he/she is likely to chase his/her customers and therefore destructing his/her own business. He/she can be accused of stealing from customers.

This saying can be compared to a person who is greedy in running his/her business. The person manipulates the goods he or she sells using a variety of tactics.

He/she is compared to a person who dismisses his/her business through fooling his/her customers.

The saying teaches people to stop being greed rather stick to principles of trustworthy that can enable them live better with others in the society.

Amos 8: 4-6.

1Thessalonians 4: 6.

450. NDUHU MHAYO NU MHAYO GULIHO.

Imbuki ya lusumo lunulo, yingilile kuwikaji bho bhanhu, na mihayo yabho iyo bhuli ng’wene, aliiganika umung’holo yakwe.

Umuwikaji bho bhanhu bhenabho, ulu bhalihoya bhagashoshaga giki, nduhu mhayo, aliyo gashinaga bhaliganika mhayo, umumioyo jabho. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘nduhu mhayo nu mhayo guliho.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo okenyiyagwa na ng’wiye, uyo agalekejaga bho mihayo duhu, aliyo umung’holo yakwe adalekejije.

Umunhu ng’wunuyo agalemaga nulu gulipwa nu ng’wiye uyo onkenyaga, kunguno ya giki, ongu onhekejaga. Aliyo lulu, umunhu  ng’wunuyo, agandyaga guyunhaya shibhi ukubhanhu, uyo onkenya ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘nduhu mhayo nu mhayo guliho.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gufunya bhulekaja bho ng’hana, ukubhanhu abho bhabhakenya, kugiki bhadule gwikala bho mholele, na bhichabho bhenabho,  umuwikaji bhobho.

Mathayo 6:6:14-15.

 2 Wakorintho 2:10.

 Waefeso 4:32.

 Wakolosai 2:13.

 Wakolosai 3:13.

KISWAHILI: HAKUNA NENO NA NENO LIPO.

Chanzo cha methali hiyo chatokea kwenye maisha ya watu, na maneno yao yaliyomo ndani ya moyo wa kila mmoja. Maisha ya watu hao, yana maongezi ya kawaida yawapatiayo nafasi ya kuyaeleza yale yaliyomo mioyoni mwao.

Lakini watu hao, wakipewa nafasi ya kutoa mawazo yao, hujibu kwa kusema kwamba, hakuna neno wakati, maneno hayo yamo mioyoni mwao.  Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘hakuna neno na neno lipo.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye amekosewa na mwenzake, ambaye humsamehe mwenzake huyo, kwa maneno tu, lakini moyoni huwa bado ana hasira.

Mtu huyo, hukataa hata kupewa fidia kutoka kwa yule aliyemkosea, akidadi eti, amemsamehe. Lakini basi, mtu huyo huanza kumsema vibaya kwa watu, yule aliyemkosea. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘hakuna neno na neno lipo.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kutoa msamaha wa kweli kwa watu walio wakosea, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.

Mathayo 6:6:14-15.

 2 Wakorintho 2:10.

 Waefeso 4:32.

 Wakolosai 2:13.

 Wakolosai 3:13.

south-africa

ENGLISH: NO WORD AND A WORD IS THERE.

The source of this saying is people who happen to have concealed hatred towards others who have done something wrong to them. Such people tend to say that they have forgiven them while deep in their hearts they still have grievances. When asked if they have forgiven they reply by saying that they don’t have any more words to mean forgiveness while they don’t mean what they say. Such people are being described using the saying that ‘no word a word is there.’

This saying can be compared to a person who has wronged another person and asks for forgiveness. That person can pretent to have forgiven him/her to the extent of even refusing taking any sort of compensation, but deep in his/her heart, he/she still harbours feelings of revenge.

The proverb teaches people to give true forgiveness to those who have wronged them. This will enable them to have harmony with others in their lives.

Matthew 6: 6: 14-15.

 2 Corinthians 2:10.

 Ephesians 4:32.

 Colossians 2:13.

 Colossians 3:13.

449. GWISAGILWA NYAMA YIBUPU.

Imbuki ya lusumo lunulo yilolile wisagiji bho nyama yibupu. Inyama yiniyo ilindololo noyi, iyo igagulagwa bho hela ngehu duhu.

Kuyiniyo lulu, uyo aliisagilwe inyama yiniyo adudula ugwilya mpaga wiguta, kunguno ya bhudoo bhoyo bhunubho. Umunhu ng’wunuyo agitindikaga ugujichola iginhu ijo jilina solobho nhale, kunguyo ya ‘gwisagilwa nyama yibupu.’

Ulusumo lunulo lugalenganijjiygwa kuli munhu, uyo agisagilagwa ginhu ijo jidina solobho, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agalekaga uguitumama imilimo iyo ilina solobho, kunguno ya gwisagilwa ginhu jinijo ijo jidadulile nulu ugung’wambilija, umuwikaji bhokwe bhunubho.

Hunagwene agalenganijiyagwa na ‘gwisagilwa nyama yibupu,’ kunguno nang’hwe, wisagililwe ginhu ijo jidina solobho, umuwikaji bhokwe.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwisagilwa ginhu ijo jidulile gubhambilija ijinagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho, kutinda kujimiza makanza gabho bho gulindila ginhu, ijo jidina solobho.

Warumi 8:25.

Zaburi 62:9.

2 Wakorintho 12:11.

KISWAHILI: KUTUMAINI NYAMA YA KONGOSHO.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia hali ya kutumaini nyama ya kongosho. Nyama hiyo ni ndogo sana na nyepezi, ambayo hununuliwa kwa bei ya chini sana.

Kwa hiyo, mtu yule anayeitumaini nyama hiyo hawezi kuila mpaka akatosheka. Mtu huyo, hujichelewesha kutafuta kitu ambacho kinathamani kubwa, kwa sababu ya ‘kutumaini nyama ya kongosho.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutumaini kupata au hutegemea kitu kisicho na thamani katika maisha yake.

Mtu huyo, huacha kufanya kazi za maana, ambazo zinathamini, kwa sababu ya kutumaini kitu hicho ambacho, hakiwezi kumsaidia katika maisha yake.

Ndiyo maana, watu humlinganisha na ‘kutumaini nyama ya kongosho,’ kwa sababu naye hutegemea kitu kisicho na faida maishani mwake.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kutumaini kitu ambacho chaweza kuwasaidia katika kuzijenga vizuri familia zao, maishani mwao, badala ya kupoteza muda wao, kwa kutegemea vitu visivyoweza kuwasaidia katika kuziendeleza familia hizo.

Warumi 8:25.

Zaburi 62:9.

2 Wakorintho 12:11.

meat-cow1

ENGLISH: RELYING ON THE PANCREACE MEAT.

The source of this saying is the pancreace meat that is believed to be very small in size and it is tender thus bought at a very cheap price. Therefore one who eats pancreace meat cannot easily get satisfaction. Instead, he/she is adviced to look for something of great value in order to have satisfaction because reliance on pancreace meat only can make one suffer from hunger.

This saying can be compared to a person who depends on worthless things for his/her survival. Such people are being warned against it by telling them not to ‘rely on the pancreace meat’ as a way to make them hard workers.

This proverb teaches people to hope for something that will help them better build their families. They don’t have to waste their times doing worthless things rather work hard and help their families to develop in different aspects.

Romans 8:25.

Psalm 62: 9.

2 Corinthians 12:11.

447. KWENGU NA KWENGULILA.

Imbuki ya lusumo lunulo yilolile kikalile ka bhanbhu abho bhalibhashilimu pye abhose. Abhanhu bhenabho bhagikalaga bhuli ng’wene alihaya giki, amanile yose kukila ung’wiye, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagabhitanaga, ‘gwengu na kwengulila.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhadidebhaga aha kaya yabho. Abhanhu bhenabho bhadidebhaga kunguno ya bhushilimu bhobho, ubho gwikala bhuli ng’wene andalahile ung’wiye. Hunagwene abhanhu bhagabhitagaga, ‘kwengu na kwengulila.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kuleka bhushilimu bho gubhadalaha abhichabho, kugiki bhadule gwikala bhidebhile chiza, umuwikaji bhobho.

Wagalatia 3:1-5.

KISWAHILI: MJANJA NA MJANJA.

Chanzo cha methali hiyo chaangalia maisha ya watu ambao ni wajanja wote. Watu hao, huishi maisha ya kila mmoja kujikudai kufahamu kila kitu, kupita ng’wenzake. Ndiyo maana watu huwaita watu hao kwamba ni ‘mjanja na mjanja.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu ambao hawawezi kuishi kwa pamoja. Watu hao hawaelewani kwa sababu ya ujanja wao wa kila mmoja kumdharau mwenzake. Tabia hiyo huwapelekea kushindwa kuishi kwa pamoja. Ndiyo maana watu huwaita watu hao, kwamba ni ‘mjanja na mjanja.’

Methali hiyo hufundisha watu, juu ya kuacha ujanja wa kuwadharau wenzao, ili waweze kuelewana vizuri na wenzao, maishani mwao.

Wagalatia 3:1-5.

soccer

ENGLISH: CLEVER AND CLEVER.

The source of this saying is two clever people who happen to be together sometimes. These two individuals happen to compete for knowledge; each one of them claiming to know better than the other.

This saying can be compared to people who cannot live together. Such people do not understand each other because of their individual ability that makes them despise each other. This behaviour leads to failure to live together. That’s why people can describe them using the saying that ‘clever and clever.’

The proverb teaches people about giving up the habit of belittling peers. People should respect individual abilities in order to create a ground for good understanding among members of the society.

Galatians 3: 1-5.