Sukuma Proverbs

578. NGEGEMEJI IDIKOJAGA.

Imbuki ya lusumo lunulo, yililola nzagamba ya Ng’ombe iyo idapandaga inhima. Inzagamba yiniyo, igamanaga yugegemela bho gujilimhila ng’hima, nugupanda nduhu. Iyiniyo, idudula ugwikoja nulu ng’wana (ndilanha). Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ngegemeji idikojaga.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga nimo bhogususanya, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adiko gubyedecha nimo gosegose, kunguno ya gwikala bho nduhu ugutumama chiza imilimo yakwe.

Uweyi agikolaga ni nzagamba iyo igagegemelaga duhu, bho nguhu ugupanda, kunguno nuweyi agasusanyama uguitumama imilimo yakwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ngegemeji idikojaga.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kutumama milimo bho nduhu ugususanya, umukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Mathayo 7:15-20.

Mathayo 7:21-28.

Waroma 12:11-12.

Yakobo 2:14-17.

KISWAHILI: ANAYESITASITA HAWEZI KUFANIKISHA KUPATA MTOTO ANAYEFANANA NAYE.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia fahari wa ng’ombe ambaye apandi majike. Fahari huyo, ni dume la ng’ome ambalo haliwezi kupata majike, badala yake lenyewe huishia kujalibia tu, bila kuyapanda. Yeye hawezi kuwa na ndama anayefanana naye. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘anayesitasita hawezi kufanikisha kupata mtoto anayefanana naye.’

Methali hiyo, hufananishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi kwa kusitasita, maishani mwake. Mtu huyo, hawezi kufanikiwa katika kazi yoyote ile, kwa sababu ya kuishi bila kuyatekeleza vizuri majukumu yake.

Yeye hufanana na fahari ambaye husitasita kupanda majike, kwa sababu naye husitasita kuyatekeleza majukumu yake. Mtu huyo, hajiwekei mikakati ya kufanya kazi kwa badii hadi kuzimaliza. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘anayesitasita hawezi kufanikisha kupata mtoto anayefanana naye.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyatekeleza majukumu yao kwa ukamilifu hadi kuyamaliza, ili waweze kupata mafanikio mengi katika maisha yao.

Mathayo 7:15-20.

Mathayo 7:21-28.

Waroma 12:11-12.

Yakobo 2:14-17.

nzagamba ngegemeji

bull

buli1

 

ENGLISH: HE WHO HESITATES WILL NEVER GET A CHILD THAT RESEMBLES HIM.

The source of this proverb is a bull that is hesitant to mount a cow. This bull fails to mount the cow, instead, ends up trying to mount it. Such a bull is not likely to have a calf that resembles it (the bull). This is why people can describe such a bull using the proverb that ‘he who hesitates will never get a child that resembles him.’

The proverb is likened to a person who works with hesitation in his/her life. Such a person will not be able to succeed in life because he or she is not living up to his or her responsibilities. He/she is like a bull that fails to fulfill its responsibilities. This person also does not make plans to work to the end.

This proverb teaches people to carry out their tasks to the fullest. This will enable them to have achievements in life.

Matthew 7: 15-20. Matthew 7: 21-28. Romans 12: 11-12. James 2: 14-17.

577. NG’HALA NINGI JIDISIMBILAGA MYOB’O.

Imbuki ya lusumo lunulo, yililola ndimu iji jigitanagwa Ng’hala. Indimu jinijo, jigikalaga mu mang’ob’o. Bhuli Ng’hala igikalaga mung’ob’o goyo uyo yagusimba yoyi. Aliyo lulu, ulu jigwa ng’wichajo oyogolwa, pye jigafumaga gujung’wambilija. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ng’hala ningi jidisimbilaga myob’o.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhali na ng’wigwano go gwiyambilija wangu ulu ng’wichabho opandikaga makoye. Abhanhu bhenabho, bhiyiigwile chiza mukikalile kabho, kunguno bhuli ng’webe agatumamaga imilimo yakwe chiza, ukunhu alumanile nabhiye ijinagubhamilija abho bhapandikaga mayange.

Abhoyi bhagikolaga ni ng’hala, ijo jidisimbilaga myob’o, aliyo bhuli yene igajaga wangu ugujubhambilija abhichabho abho bhapandikaga makoye, kunguno nabhoyi bhali na ng’wigwano ugogwiyambilija chiza, umumakoye gabho. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ng’hala ningi jidisimbilaga myob’o.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’wigwano go gwiyambilija umumakoye gabho, bho gudima malagilo ga ng’wa Mulungu na ga Kanisa, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umukikalile kabho.

Mathayo 7:13-14.

Luka 13:22-24.

1Timotheo 6:11-12.

Luka 12:58.

KISWAHILI: VICHECHE WENGI HAWACHIMBIANI MAPANGO/MASHIMO.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia wanyama wanaoitwa vicheche. Vicheche hao, huishi kwenye mapango au mashimo mbalimbali ambayo kila mmoja amendaa. Kila mmoja huishi kwenye shimo lake alilolichimba. Lakini basi, vicheche hao wakisikia kwamba mmoja wao amevamiwa, wote hutoka mashimoni mwao, kwenda kumsaidia mwenzao. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘vicheche wengi hawachimbiani mashimo/mapango.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wale ambao wana uelewano mzuri wa kusaidiana haraka wanapoona kwamba mwenzao amepata matatizo. Watu hao, wanaelewana vizuri katika maisha yao, kwa sababu kila mmoja wao hufanya kazi zake, huku akiwa tayari kwenda kuwasaidia wenzake wenye matatio, kwa haraka inavyo wezekana.

Wao hufanana na vicheche wanaojitegemea katika kuyatekeleza majukumu yao, huku wakiwa tayari kwenda kuwasaidia wenzao waliopata matatizo, kwa sababu nao wana uelewano wa kusaidiana vizuri katika maisha yao. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘vicheche wengi hawachimbiani mashimo/mapango.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uelewano wa kusaidiana vizuri katika kutatua matatizo mbalimbali, kwa kuzishika amri za Mungu na za Kanisa, maishani mwao, ili aweze kuishi kwa amani na wenzao katika maisha yao.

Mathayo 7:13-14.

Luka 13:22-24.

1Timotheo 6:11-12.

Luka 12:58.

ng'hala3

ng'hala2

 

ENGLISH: MEERKATS DO NOT DIG HOLES FOR EACH OTHER.

The source of this proverb is the wild animal known by the name of meerkat. These animals always live in caves or pits, which each one of them digs. Each of these meerkats live in its cave/pit but when it comes that one of them is attacked by an enemy, all of them living around can come out to defend their fellow. This is why people came with this proverb to mean that meerkats do not dig caves/pits for others rather they dig them for their own but protection against enemies is the responsibility of each one of them.

This proverb can be compared to those people who have a good understanding of helping each other as soon as they find out that someone is in need of help. These people understand others well and they are able to help them. These people are highly needed during times of crisis.

The proverb teaches people about the need of helping each other in solving problems. It also teaches people to abide by God’s and Church’s commandments by ensuring that needy people are helped accordingly.

Matthew 7: 13-14. Luke 13: 22-24. 1Timothy 6: 11-12. Luke 12:58.

573. INGI AHO YUNYELA IGALEKAGA BHANA.

Imbuki ya lusumo lunulo, ililola kikalile ka ingi, na kibyalile kayo. Ingi yiniyo, igagwilaga lulu mujiliwa yaleka bhana moyi. Abhana bhayo tugabhizaga tugino tudodo tope, uto tudulile guibhoza nulu nyama iyo yagwilagwa ni ingi yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ingi aho yunyela ikalaekaga bhana.’

Ulusumo lunulo, lugalenaganijiyagwa kuli munhu uyo ali nomolomo umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agayombaga mihayo ya bhulomolomo iyo igabhipyaga kaya ja bhanhu.

Uweyi agikolaga ni ngi iyo igalekaga bhana abho bhagabhipyaga jiliwa ja bhanhu, kunguno nuweyi imihayo yakwe ya bhulomolomo yiniyo, igalisanyaga bhanhu, mpaga nose bhabhulaga kaya jabho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga umunhu ng’wunuyo giki, ‘ingi aho yunyela igalekaga bhana.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleka bhulomolomo umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umuwikaji bhobho.

Kutoka 23:1.

Walawi 9:11.

Mathayo 7:15-18.

2Watorintho 4:2.

Yakobo 1:26.

KISWAHILI: INZI AKITUA POPOTE HUACHA WATOTO.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia maisha ya inzi na kuzaliana kwake. Ingi huyo, hutua hata kwenye chakula na kuacha watoto. Watoto hao, huwa funza wadogo wadogo ambao huweza hata kuharibu nyama ambayo wameachwa juu yake na inzi. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘inzi akitua popote huacha watoto.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni muongo katika maisha yake. Mtu huyo, husema maneno ya uongo ambayo husababisha hata kugawanyika kwa wanafamilia, kwa sababu ya uchonganishi wake.

Yeye hufanana na inzi ambaye huwaacha watoto kila anapotua ambao huharibu chakula cha watu, kwa sababu naye hugonganisha watu hata kufikia hatua ya kuvunjika kwa mji wao, kwa sababu ya uongo wake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘inzi akitua popote huacha watoto.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kusema uongo matika maisha yao, ili waweze kuishi kwa amani na watu  wao, maishani mwao.

Kutoka 23:1.

Walawi 9:11.

Mathayo 7:15-18.

2Watorintho 4:2.

Yakobo 1:26.

ngi

ngi1

ngi2

 

ENGLISH: EVERYWHERE A FLY LANDS IT LEAVES ITS EGGS

The source of this saying is the life of a fly. Everywhere a fly lands it leaves eggs. These eggs can grow into larvae that can destroy something, for example, meat and other related things. To warn people against entertaining such insects, one can use the saying that ‘everywhere a fly lands it leaves its eggs/larvae.’

The saying can be compared to a person who is a liar in his or her life. This person is likely to affect family members by making false statements. In such a context of false statements, one can experience division among family members. Such a person who is a liar can be compared to a fly that always leaves impact wherever it lands.

This proverb teaches people to break the habit of lying in their lives. Rather, they have to be trusthworthy so that they can have peace with others in the society.

Exodus 23: 1. Leviticus 9:11. Matthew 7: 15-18. 2Corinthians 4: 2. James 1:26

572. INGILI YA BHANA IDALUMAGWA MATIMBA.

Imbuki ya lusumo lunulo, yililola ndimu iyi igitangwa ngili. Indimu yiniyo, igikalaga ikingilwe na bhana bhayo umumagulu gayo. Kuyiniyo lulu, abhana bhayo bhenabho, bhagagashigijaga amatimba gayo, kugiki gadizulung’wa na ginhu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ingili ya bhana idalumagwa matimba.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina bhana bhingi abho bhagang’wimbilijaga, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agagunanagwa na bhana bhenabho, ulu opandikaga makoye.

Uweyi agikolaga ni ngili iya bhana iyo idalumagwa matimba, kunguno nuweyi, agalanghanagwa na bhana bhake bhenabho, bho gwambilijiwa umumakoye gakwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘ingili ya bhana idalumagwa matimba.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhalela chiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gubhambilija chiza, ijinagubhinja umumakoye, umukikalile kabho.

Mathayo 28:16-20.

Marko 3:14-19.

Zaburi 127:3-5.

KISWAHILI: KIFARU MWENYE WATOTO HANG’ATWI MIGUUNI.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia mnyama poli anayeitwa ngili. Mnyaga huyo, huwa na watoto ambao huzunguka miguuni pake. Kwa hiyo basi, watoto hao huizuia miguu yake kung’atwa na kitu chochote. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘ngili mwenye watoto hang’atwi miguuni.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana watoto wengi wa kumsaidia katika maisha yake. Mtu huyo, hupata msaada wa kuyatatua matatizo mbalimbali maishani mwake.

Yeye hufanana na ngili mwenye watoto waizuiao miguu yake kung’atwa na kitu, kwa sababu naye ana watoto ambao humsaidia anapopata matatizo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘ngili mwenye watoto hang’atwi miguuni.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwalea vyema watu wato, ili waweze kuwasaidia vizuri katika kutatua matatizo mbalimbali, katika maisha yao.

Mathayo 28:16-20.

Marko 3:14-19.

Zaburi 127:3-5.

ngili2

ENGLISH: THE RHINOCEROS THAT HAS BABIES IS NOT BITTEN ON HER LEGS.

The source of this proverb is the wild animal known by the name of Rhinoceros. This wild animal, when has children, its children will always surround their mother thus keeping their mothers’ legs always protected against any insect that is likely to harm them through their legs. It is through this kind of protection that people came up with this proverb that ‘the wild boar with children is not bitten on legs’ to communicate the power of children in protecting their mothers against enemies.

The proverb can be compared to a person who has children to support in his or her life. This person is capable of getting help from his/her children in his or her life. This person can be likened to wild boar with children who keep its feet from getting stuck. Children ensure the survival of their mother.

This proverb teaches people on how to take care of their children with hope that these children will help their parents when they are old enough to sustain their lives.

Matthew 28: 16-20. Mark 3: 14-19. Psalm 127: 3-5

571. AHA NHEGA BHADASAYAGA.

Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile ligusha lya gutula Nhega. INhega yiniyo, igatulagwa yaja gwigulya guti boli. Ulu yutulwa chiniko, idulile guntula oseose ulu ishokile aha hasi. Uyo ilantule inhega yiniyo, adizusaya, kunguno adakililwe gwiyumilija duhu nulu agatulanijiwa na ng’wiye. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘aha nhega bhadasayaga.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyumilija ulu opandikaga makoye, umubhutumami bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agaidililaga na witegeleja bhutale imilimo yakwe, kunguno iyiniyo, hiyo igang’winhaga sabho ja gudula gung’wambilija uguilanghana chiza, ikaya yakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nabho bhaligusha na nhega, kunguno nuweyi agalabhukagaga ulu aliitumama imilimo yakwe, wiyumilija chiza mpaka oyimala. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga uweyi giki, ‘aha nhega bhadasayaga.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kubhiza bhiyumilija umubhutumami bho milimo yabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umubhumami bhobho bhunubho, umuwikaji bhobho.

1Wakorintho 10:13.

1Wathesalonike 1:6.

2Timotheo 4:4-8.

KISWAHILI: KWENYE MCHEZO WA TIARA HAWAKASIRIKI.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia mchezo wa tiara. Tiara hiyo, hupigwa na kwenda juu kama mpila. Ikipigwa hivyo, yaweza kumpiga yeyote, inaporudi chini. Yule itakayempiga asikasirike, kwa sababu ya yeye kutakiwa kuvumilia tu, kama sheria ya mchezo huo inavyodai. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘kwenye mchezo wa tiara hawakasiriki.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvumilia anapopata matatizo katika utekelezaji wa majukumu yake. Mtu huyo, huzijali kwa kuzitekeleza vizuri kazi zake, kwa sababu hizo, ndizo zinazompatia mali za kumwezesha kuiendesha vizuri familia yake.

Mtu huyo, hufanana na wale wachezao tiara, kwa sababu naye huvumilia anapoumia wakati wa utekelezaji wa majukumu yake. Yeye huyatekeleza majukumu hayo kwa uvumilivu mkubwa, hadi mwisho. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘kwenye mchezo wa tiara hawakasiriki.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika kazi zao hizo, maishani mwao.

1Wakorintho 10:13.

1Wathesalonike 1:6.

2Timotheo 4:4-8.

africa-tanzania

ligusha1

 

ENGLISH: IN NHEGA’S GAME PLAYERS DO NOT GET ANGRY

The source of this saying is the nhega game. In the game, when the nhega is struck it goes up like a ball and when it falls down it can hit anyone around. The rules of this game say that anyone hit by the nhega is not supposed to become angry. This is why people are being forewarned that if one wants to play this game he/she is supposed to abide by the game rules by not becoming angry when hit by the nhega.

The saying can be compared to a person who perseveres when he/she experiences difficulties in performing his/her duties. This person cares for himself/herself and he/she does his/her works well. He/she does so because he/she knows that it is this job that makes his/her family survive. Therefore, he/she has to tolerate whatever condition he/she faces in the work place. Patience is what makes him/her live well in the society.

This saying teaches people to be patient in carrying out their responsibilities. In so doing, they can achieve more in life.

1 Corinthians 10:13. 1Thessalonians 1: 6. 2Timothy 4: 4-8