Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile bhulumbi bho bhasiminzi abho bhinhagwa magulu. Uwinhiwa bho magulu bhunubho, bhuli bho guzugilwa jiliwa abhanhu abho bhalimugendo bhenabho. Ijiliwa jinijo, jigabhinhaga nguzu ja gudula gusiminza mpaga bhushika uko bhajile.
Hunagwene abhasiminzi bhenabho, ulu bhuzugilwa jiliwa aha kaya ndebhe, bhujilwa mpaga bhiguta, bhagalagaga bho gulumbilija giki, ‘wabheja watwinha magulu. Watukungila jilatu.’ Ulu bhuyomba chiniko, bhagandyaga gusiminza bhajile umulugendo lwabho.
Lusumo lunulo, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali na wizanholo bho gubhakalibhusha abhageni na gulumbilija ulu witilagwa ya wiza na bhiye, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunuyo, agikalaga na bhanhu chiza bho gubhagalila abho bhalimugendo, kugiki bhadule gwifula aha ng’wakwe, na gupandika jiliwa ija gudula gubhinha nguzu chiza. Uweyi agabhabhonelaga isungu abhanhu abho bhali na makoye, umuwikaji bhobho.
Umunhu ng’wunuyo, wikolile nu ngaliji obhageni uyo agabhazugilaga jiliwa, kunguno nuweyi agabhakalibhushaga abhageni aha ng’wakwe na gubhagalila chiza. Uweyi agabhalangaga nabhiye ahigulya ya gubhiza bhizanholo bho gubhagalila jiliwa abhageni bhabho.
“Ulusumo lunulo lugatumilagwa na bhanhu abho bhalifunya bhulumbi aho bhamala gulya. Ugudinha magulu lunu ugutubhegeja jilatu mumho: “Oduzugilaga jiliwa ijo jadinhaga nguzu ja gusimizila.”” Hunagwene abhageni bhenabho bhaganumbaga bho guyomba giki, ‘wabheja wa twinha magulu. Watukungila jilatu.’ Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 46.
‘Kueneza Injili kwa methali’ jili jitabho ijo jigandikwa na Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey, M.M., ijojigachapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Lusumo lunulo, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza na wizanholo bho gubhakalibhusha abhageni aha kaya jabho, kugiki bhadule gubhinha nguzu ja gubhashisha uko bhajile.
“Ekaristi mumho gulumba. UmuEkaristia duganumbaga Mulungu ku wiza bhose ubho oditila.
Ulu ijiliwa jigadinhaga nguzu ja gusiminza dushiga ukodujile bho nduhu makoye, Ekaristia igadinhaga nguzu ja gushiga kuli Mulungu bho nduhu makoye. Umu Sakramenti ya Ekaristia UYesu Kristo odinhaga magulu, odubhegejeaga jilatu, giki odinhaga jiliwa ijagudulagudushia ng’wigulu bho nduhu makoye.
Kuyiniyo dadakilwa kunhumbilija USebha Wise UYesu Kristo na gung’wila: “Obheja, Baba, odinha magulu, odubhegeja jilatu.”” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 46.
Yohane 6:54.
kutoka 16:35.
Kumbukumbu 8:10.
Zaburi 139:14.
2 Wathesalonike 1:3.
KISWAHILI: ASANTE UMETUPATIA MIGUU. UMETUTENGENEZEA VIATU,
Chanzo cha methali hiyo, chaangalia utoaji wa shukrani wa wasafiri waliopewa miguu. Upewaji huo wa miguu, ni wa watu waliyoko safarini kukaribishwa kwenye mji fulani na kupikiwa chakula. Chakula hicho, huwapa nguvu za kuendelea tena na safari yao kiasi cha kutosha kuwafikisha kule waendako.
Ndiyo maana wasafiri hao huishukuru familia hiyo, na kuiaga kwa kusema kwamba, ‘asante umetupatia miguu. Umetutengenezea viatu.’ Baada ya kusema hivyo, huendelea na safari yao ya kwenda kule waendako.
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule mwenye ukarimu wa kuwakaribisha wageni na kuwashukuru wale waliomtendea wema, maishani mwake. Mtu huyo, huishi na watu vizuri kwa kuwatunza wale walioko safarini, ili waweze kupumzika kwake na kuwapatia chakula chakuwaongezea nguvu vizuri. Yeye huwahurumia wale walioko kwenye matatizo mbalimbali, maishani mwao.
Mtu huyo, hufanana na mtunzaji wa wageni anayewapikia chakula, kwa sababu naye huwakaribisha wageni na kuwaandalia chakula nyumbani kwake. Yeye huwafundisha pia wenzake juu ya kuwa na ukarimu wa kuwakaribisha wageni wao, na kuwaandalia chakula.
“Methali hii hutumika kwa watu ambao wanatoa shukrani baada ya kula. Kutupa miguu au kututengenezea viatu ina maana: “Umetupikia chakula ambacho kinatupa nguzu za kusafiri.” Ndiyo maana wageni hao, humshukuru kwa kusema kwamba, ‘asante umepatia miguu. Umetugengezea viatu.’ Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 46.
Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti, Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwakaribisha wageni kwenye familia zao, ili waweze kuwapatia nguvu za kuwawezesha kuendelea na safari yao, hadi kuwafikisha kule waendako.
“Maana ye Ekaristi ni kushukuru. Katika Ekaristi tunamshukuru Mungu kwa mema yote ambayo ametutemdea.
Kama chakula hutupa nguvu ya kusafiri tufike tunakokwenda bila shida, Ekaristi hutupa nguvu ya kufika kwa Mungu bila shida. Katika Sakramenti ya Ekaristi Yesu Kristo ametupa miguu, ametutengenezea viatu, yaani ametupa chakula kinachotuwezesha kufika mbinguni bila shida. Kwa hiyo yatupasa kumshukuru Bwana Wetu Yesu Kristo na kumwambia: “Asante, Baba, umetupa miguu, umetutengenezea viatu.”” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 46.
Yohane 6:54. “Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho.”
kutoka 16:35. “Waisraeli wakala mana kwa miaka arobaini, mpaka walipofika katika nchi iliyokaliwa na watu. Walikula mana mpaka walipofika mpakani mwa Kanaani.”
Kumbukumbu 8:10. “Wakati mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni BWANA Mungu wenu kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa.”
Zaburi 139:14. “Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha, kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu.”
ENGLISH: THANK YOU FOR GIVING US FEET; YOU MADE US SHOES.
The source of this saying is thanksgiving for travelers after being well received by their host and being given food. The food they get is considered as feet to mean more strength that can enable them to continue walking until they reach their set destination. As a way to appreciate their host for the kindness they can use the saying that ‘thank you for giving us feet; You made us shoes.’
The saying can be likened to a generous person who welcomes strangers and extends thanks to those who have done good in his/her life. The person lives with the people well by taking care of those on the journey. He/she does so by providing them with accommodation and food. People of this nature teaches others about kindness and hospitality to others.
This proverb can be applied to people who express gratitude after eating. Giving us feet or shoes means “You have cooked a meal that gives us strength to continue walking until we reach the planned destination.” This is why visitors can thank someone saying, ‘Thank you for giving us feet; You have made shoes for us’ to show their appreciation. You can also refer to Kueneza Injili kwa Methali which is translated as Spreading the Gospel in Proverbs, page 46. written by Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M. and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.
The proverb teaches people to be hospitable to their visitors. They need to provide them with whatever help they can manage. In so doing, they help them gain more strength to continue with their journey.
Human beings have to thank God for the gift of Eucharist. In the Eucharist we thank God for all the good that He has done for us.
As food gives us the strength to travel to our destination without difficulty, the Eucharist gives us the power to reach God without difficulty. In the sacrament of the Eucharist Jesus Christ has given us feet, made us shoes, that is, He has given us food that enables us to get to Heaven without difficulty. So we should thank our Lord Jesus Christ and say: “Thank you, Father, you have given us feet; you have made us shoes.” Refer to Kueneza Injili kwa Methali page 46.
John 6:54. Exodus 16:35. Deuteronomy 8:10. Psalm 139:14.