289. JAWIZA JIDAMALAGWA/ABHASOGA BHADAMALAGWA

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile jisumbwa ja ng’wa Mulungu. Ijisumbwa jinijo jili jabhuli mbika. Bhuli jene jili na wiza bhojo, ubhobhujikilile ijingi. Aliyo lulu gashinaga, jilihoyi ijawiza hangi kukila ni jinijo, ijo umunhu ujikumilijaga, giki jilijawiza kulilanija pye. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘jawiza jidamalagwa.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajidalahijaga ijo alinajoa bho gujibhona giki angu jidijawiza, nulu jilijabhubhi, ulu ojibhona jingi ijo jilijawiza gukila ijo alinajo. Aliyo lulu umunhu ng’wunuyo aho ojibhonaga ijo alinajo ihaha, ojihayaga giki, jilijawiza gukila pye ijingi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘jawiza jidamalagwa,’ kunguno uweyi wiganikaga giki, ojimala pye ugujibhona, ijawiza jinijo.

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya guridhika nijo bhalinajo umuwikaji bhobho, bho gujibhona giki jilijawiza, kunguno ijawiza jidamalagwa.

Luka 12:16-21.

Luka 16:19.

KISWAHILI: VIZURI HAVIMALIZWI/WAZURI HAWAMALIZWI

Chanzo cha methali hiyo chaangalia viumbe vya Mungu. Viumbe hivyo ni vingi, na pia ni vya kila aina. Kila kimoja kina uzuri wake uliotafauti na ule wa kingine. Lakini basi, vipo vilivyo vizuri zaidi ya vingine, ambavyo mtu alishaviona mara ya kwanza, na kudhani kwamba, hicho ni kizuri kuliko vyote. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘vizuri havimalizwi.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu ambaye huvidharau vile alivyo navyo, baada ya kuviona vingine kuwa ni vizuri kuliko alivyo navyo. Lakini mtu huyo, alipoviona kwa mara ya kwanza vile alivyo navyo, alivifikiria kuwa ni vizuri kupita vyote, alivyoviona wakati huo. Yeye alifikiria kwamba, alivishamaliza kuviona vyote vilivyo vizuri, kumbe haikuwa hivyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘vizuri havimalizwi.’ 

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuridhika na vile walivyovichagua maishani mwao. Kuridhika huko, kutawawezesha watu hao, kuyaishi vizuri maisha yao waliyoyachagua, au kuishi kwa amani na wenza wao waliowachagua, maishani mwao, kwa sababu ‘vizuri havimalizwi, au wazuri hawamalizwi.’

Luka 12:16-21.

Luka 16:19.

flowers

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.