728. NAMUGI ADAB´IHAJA.

Akahayile kenako, kalolile munhu uyo alintale, nulu uyo ali namugi aha kaya yakwe. Olihoyi namhala umo uyo adimaga mitugo na bhana bhakwe. Lushigu lumo agajimija ng’ombe ubhabhuja abhana bhakwe, “nani uijimijije ing’ombe?” ung’wana ushosha, “ima lulu.” Unamhala ubhawila, “jaji mugaichole mpaga muyibhone.” Aho bhagaibhona bhudebha igiki unamhala huyo aijimija ng’ombe yiniyo, bhuyomba giki, “namugi adab’ihaja.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumilaga bhutale bhokwe bho gubhaluhya abhanhu bhakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhutumilaga ubhutale bhunubho bho gubhubhisa ubhunhana, kunguno ya kulang’hana ikujo lwakwe. Uweyi agitaga giko bho gubhasayila salaga abhanhu bhakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu namhala uyo agajimija ng’ombe ubhasayila na gubhaluhya abhana bhakwe, kunguno nu weyi agabhaluhyaga abhanhu bhakwe bho gubhubhisa ubhung’hana. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “namugi agab’ihaga.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhutumila chiza ubhutale bhobho, kugiki abhanhu bhabho bhadule gwikala na mholele ya gubhambilija guitumama chiza imilimo yabho. Abhanhu bhenabho igelelilwe bhabhize ni kujo kubhanhu bhose.

Zaburi 2:1-12.

Waebrania 6.1-4.

Ayubu 32:6b-7.

KISWAHILI: MZEE WA FAMILIA HAKOSEI.

Msemo huo, huangalia mtu yule ambaye ni mwenye madaraka au baba wa familia. Alikuwepo mzee mmoja aliyekuwa anachunga mifugo na watoto wake. Siku moja, alipoteza ng’ombe akawauliza watoto wake, “nani amepoteza ng’ombe?” Mmoja wa watoto akajibu, “simfahamu?” Akawambia, “nendeni mukamtafute mpaka mmuone.” Walipomuona waligundua kwamba, baba yao ndiye aliyempotea huyo ng’ombe, wakasema, “mzee wa familia hakosei.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatumia madaraka yake kwa kuwakandamiza watu wake. Mtu huyo, hutumia madaraka au nafasi yake hiyo katika kuuficha ukweli, kwa lengo la kulinda heshima yake mbele ya watu. Yeye huwalaimu hovyo watu wake.

Mtu huyo, hufanana na mzee mwenye watoto aliyepoteza ng’ombe akawasingizia watoto wake, kwa sababu naye huitumia nafasi yake ya ukubwa katika kuwakadamiza wale walioko chini yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba,  “mzee wa familia hakosei.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuitumia vizuri nafasi yao ya uongozi, ili waweze kuishi kwa amani ya kuwezesha kuyatekeleza vizuri majukumu yao. Watu hao, wanatakiwa kuwa na heshima kwa watu wote wanaoishi nao.

Zaburi 2:1-12. “Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na mataifa kula njama bure? Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya BWANA na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. Wanasema, ‘‘Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.’’ Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, “Nimemweka Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.’’ Nitatangaza amri ya BWANA : yeye aliniambia, “Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa Baba yako. Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa mali yako. Utawatawala kwa fimbo ya kifalme ya chumana kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.’’ Kwa hiyo, ninyi wafalme, iweni na hekima, mwonyeke, enyi watawala wa dunia. Mtumikieni BWANA kwa hofu na mshangilieni kwa kutetemeka. Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.”

Yoshua Bin Sira 3:12-14. “Mwanangu, umsaidia baba yako katika uzee wake, wala usipate kumhuzunisha siku zote za maisha yake. Akiwa amepungukiwa na ufahamu umwie kwa upole, wala usimdharau iwapo wewe u mzima sana; kwa maana sadaka apewayo baba haitaswahauliwa, na badala ya dhambi itahesabiwa kwa kukuthibitisha; ”

Waebrania 6.1-4. “Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Kristo na tusonge mbele ili tufikie utimilifu, si kuweka tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, yaani, mafundisho kuhusu mabatizo, kuwekea watu mikono, ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. Mungu akitujalia tutafanya hivyo. Kwa kuwa ni vigumu kuwarejeza tena katika toba wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho Mtakatifu.”

Ayubu 32:6b-7. “Mimi ni mdogo kwa umri, ninyi ni wazee, ndiyo sababu niliogopa, sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua. Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’”

hunters nature

familiy africa

ENGLISH: THE FATHER OF THE FAMILY DOES NOT MAKE MISTAKES.

This saying refers to the person who is in charge of something or the father of the family. There was an old man who was tending cattle and his children. One day, he lost a cow and asked his children, “Who has lost this cow?” One of the children replied, “I don’t know” He told them, “Go and look for her until you find her.” When they saw her, they realized that their father was the one who had lost the cow, and they said, “The father of the family does not make mistakes.

This saying is used to refer to a person who uses his power to oppress his people. That person uses his position to conceal the truth, with the aim of protecting his dignity before the public eye. He falsely accuses his people.

Such man is like the father who had children and lost his cattle, but never admitted that he had done so instead he shifted the blame to his children. That is why people have a saying, “The father of the family does not make mistakes”

This saying, teaches people how to make good use of their leadership position, so that they can live in peace to enable them to carry out their responsibilities effectively. Such people have to be respectful to all the people who live with them.

Psalm 2: 1-12, Joshua Bin Sira 3: 12-14, Hebrews 6.1-4, Job 32: 6b-7.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.