Imbuki ya lusumo lunulo yingilile mub’utuuji bho jikolo jigehu mulijisema litale. Ijikolo jinijo jigusaga numo jilili duhu, jidikomile gukwila jokale umujiseme jinijo, nulu gugeha. Untuuji ojo agujisanga gitumo ojituulila jilihoyi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘nkulu adalyaga.’
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho b’agatuulaga sabho jabho mujikolo jitale ja gudula gujilang’hana chiza, nulu jigikala moyi bho makanza malihu jidujimila. Abhanhu bhenabho bhagajisangaga isabho jabho jilihoyi gitumo bhajituulila, kunguno b’adebhile igiki, ‘nkulu adalyaga.’
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gulanghana chiza isabho jabho bho gujituula mubenki iyo idulile gujilanghana chiza.
Zaburi 78:70-72.
1Samweli 16:7.
KISWAHILI: MKUBWA HALI
Chanzo cha methali hiyo chatokea kwenye uwekaji wa vitu vichache kwenye chombo kikubwa. Kitu hicho hubakia kama kilivyo tu, hakiwezi kuongezeka kikalingana na chombo hicho, wala kupungua. Mwekaji wa kitu hicho huvikuta kama kilivyokuwa wakati akikiweka pale. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘mkubwa hali.’
Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wale wawekao mali zao kwenye kitu kikubwa ambacho chaweza kutunza mali hizo kwa usalama, hata kama zitakaa kwa mda mrefu, hazitapotea. Watu hao huzikuta mali zao zikiwa salama kama walivyoziweka, kwa sababu wafahamu kwamba, ‘mkubwa hali.’
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kutunza vizuri mali zao kwa kuziweka kwenye mabenki yawezayo kuzitunza vizuri.
Zaburi 78:70-72.
1Samweli 16:7.
ENGLISH: KEEP YOUR PROPERTIES/ ITEMS IN A BIG CONTAINER
This saying comes from a tendency of putting things in a big container. Things kept in a big container will not decrease or increase to fill the container. The owner of those things will find it intact.That is why people say, “keep your properties in a big container.”
The proverb is comparable to those people who put their belongings in a container that can hold them safely for a long time without losing them. These people find their properties intact.
The proverb teaches people how to take good care of their properties by putting them in banks that can take good care of them.
Psalm 78: 70-72.
1 Samuel 16: 7.