247. BAHASHA YA NGEGELEHYA (YA MMINZI) IGIPUNDULAGA YENIKILI

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile ngegelehya iyogikikalaga muminzi, na bhahasha. Aliyo lulu ingegelehya yiniyo ilina magulu ayo gadulile nulu gupundula ginhu ijo jikolile na daladasi. Ulu yutulwa mub’ahasha mumho iguipundula duhu. Hunagwene abhanhu bhagahayaga giki, ‘b’ahasha ya ngegelehya igipundulaga yenikili.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyaga kuli munhu uyo agitaga yabhubhi umuchalo. Umunhu ng’wunuyo agamanyichaga ng’winikili gulwa gwiting’wa, nulu guhugana gokwe. Kihamo na gumanyika chiniko, umunhu ng’wunuyo agahalalikaga bho gulema giki aditile uwei ya wabhubhi yiniyo. Aliyo lulu, abhanhu abho bhalimhona bhalimana pye igiki, uwei huyo witaga iyabhu yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘b’ahasha ya ngegelehya igipundulaga yenikili.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya guleka gwita mihayo ya bhub’i kub’ichab’o. Akikalile kenako kagubhambilija ijinagubhiza na widohya bho gudula gwikala bho mholele na bhanhu umuwikaji b’ob’o.

BAHASHA YA KAA (WA MAJINI) HUJITOBOA YENYEWE

Chanzo cha methali hiyo chaangalia kaa aishie majini, na bahasha. Lakini kaa huyo ana miguu ambayo huweza hata kutoboa vitu ambavyo hufanana na karatasi. Kwa hiyo, mtu akimweka kwenye bahasha ataitoboa tu. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘bahasha ya kaa hujitoboa yenyewe.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule atendaye maovu katika jamii. Mtu huyo, hujulikana mwenyewe kutokana na wasi wasi wake, au hofu aliyo nayo. Pamoja na kuwa na wasi wasi au hofu hiyo, mtu huyo hubisha kwa kukataa kuwa yeye hajafanya uovu huo. Huyo ni mtu asiyetaka kukiri kosa lake ingawa kila mtu anajua kwamba mwenye kosa ni yeye.

Pamoja na kukataa kwake, watu wanaomtazama wote huelewa kuwa yeye ndiye aliyetenda uovu huo kutokana na wasi wasi wake alio nao. Kwa hiyo, mtu aliyetenda jambo baya hujibainisha mwenyewe kwa kubabaika kwake. Ndiyo maana watu husema kuwa, ‘bahasha ya kaa hujitoboa yenyewe.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha kutenda maovu katika jamii au kwa wenzao. Kuishi hivyo, kutawasaidia watu hao katika kujijengea unyenyekevu wa kuwawezesha kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.

Luka 18:18-24.

crabs

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.