245. UYO ALIKUNHUMA HUG’WENE UWAGUGWEGELA UMOTO

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile makoye ayo munhu alinago. Umunhu ng’wunuyo agacholaga inzila ijaguginja amakoye genayo. Aliyo lulu, akomile gub’isanya bhanhu bhangi bho gwiganika giki bhagung’wambilija ugugamala amakoye genayo. Hunagwene abhanhu abho bhadeb’ile igiki umunhu ng’winuyo alindilile wambilijiwa bho gufumila kub’angi, b’agayombaga giki, ‘uyo alikunhuma hung’wene uwagugwegela umoto.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhadatumamaga chiza imilimo yabho kunguno ya gwisanya nulu gwisagilwa gugunanhwa na bhichab’o. Kunguno yiniyo, abhanhu bhenab’o bhagikalaga na makoye ganeyo ku makanza malihu. Ijinagubhahugula abhanhu bhagab’awilaga giki, ‘uyo alikunhuma hug’wene uwagugwegela umoto.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya guleka gwisanya, nulu gwisagilwa b’ugunanhwa bho gufumila kubhanhu bhangi. Igelelilwe bhuli ng’wene agatumile amasala gakwe chiza, ijinagwiingija amakoye ayo alinago. Ili hambohambo kwiyumilija guginja makoye guti ga nzala bho kutumama milimo na bhukamu bhutale.

KISWAHILI: ALIYENYUMA NDIYE ANAYEUSOGELEA MOTO

Chanzo cha methali hiyo chaangalia matatizo ambayo mtu anayo maishani mwake. Mtu huyo hutafuta njia mbali mbali ziwezazo kumwondolea matatizo yake hayo. Lakini basi, huweza pia kutegemea watu wengine kwa kuwasubiri wao waje kumwondolea matatizo hayo.

Matokeo yake, ni pamoja na kubaki kwenye matatizo hayo kwa muda mrefu. Ndiyo maana watu wamfahamuo kwamba mtu huyo amebaki na matatizo bila kujishughulisha mwenyewe, humwambia kwamba, ‘aliyenyuma ndiye anayeusogelea moto.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu ambao huwa hawafanyi kazi zao vizuri kwa sababu ya kutegemea kusaidiwa na watu wengine. Watu hao kubaki wakisumbuliwa na matatizo hayo kwa muda mrefu. Hawautumii vizuri muda wao  katika kujilete maendeleo. Basi, katika kuwaambia waache tabia hiyo, wenzao husema, ‘aliyekonyuma ndiye anayeusogelea moto.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kutegemea au kusubiri kusaidia na watu wengine katika kutatua matatizo yao. Yafaa kila mmoja aitumie akili yake vizuri katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yake. Ni afadhali kwa mfano kuondoa tatizo la njaa, kwa mtu huyo kutumia muda wake vizuri katika kulima kwa bidii kubwa kiasi cha kutosha kumletea maendeleo kwenye familia yake.

 Kwa hiyo, methali hiyo hufundisha kuwa, mtu mwenye shida ndiye anyeshughulika kutafuta utatuzi wa shida yake hiyo. Yafaa kila mmoja atumie akili na muda wake vizuri katika kuongeza juhudi za kufanya kazi ili kutatua matatizo aliyo nayo.

Lk 8:18.

fire-

African people-

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.