Imbuki ya lusumo lunulo yingile kuligasho lya gulenganija mihayo ya bhanhu abho bhidumaga. Ulu gwigela mhayo nheb’e ab’andugu b’agwib’ilinga nagugub’ugilija chiza mpaga gushiga b’agumane umhayo gunuyo.
Ijigasho jinijo jigakengelaga bho witegeleja b’utale ubho bhudulile gugulenganija chiza umhayo gunuyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ijikome jigamelaga mihayo.
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalinab’utogwa bho gub’ambilija abhichab’o abho bhidumile. Abhanhu bhenabho bhagitaga jigasho ijagudula guikengela chiza imihayo iyobhidumilile abhanhu bhenabho mpaga gushiga hikanza lyagub’ayangula. B’agab’ugilijaga kugiki b’adule ugundeb’a unhubhi na gunhugula adizushokela ugunkenya ung’wiye.
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutogwa bhogwita jigasho ja gudula gubhayangula abhanhu abho bhidumaga. Ijigasho jinijjo, jigabhambilijaga ugwita bhukengeji ubhogudula guyimala chiza imihayo iyo bhidumila abhichibho bhenabho. Ijigasho jinijo jigenhaga wikaji bho mholele, kunguno ijikome jigakomelaga mihayo.
1 Kor 6:1-4.
KISWAHILI: KIKAO HUTATUA MATATIZO
Chanzo cha methali hiyo chaanzia kwenye kikao cha kuwapatanisha watu waliokosana. Likitokea neno au tatizo fulani, wanandugu hukusanyika kwa ajili ya kulichunguza vizuri neno hilo mpaka walipatie ufumbuzi.
Kikao hicho hufanya utafiti kwa umakini mkubwa uwezao kulitapatia ufumbuzi tatizo hilo. Ndiyo maana watu husema kwamba, kikao hutatua matatizo ya watu.
Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wenye upendo wa kuwasaidia wenzao waliokosana. Watu hao hufanya kikao kiwezacho kufanya utafiti mzuri juu ya ukweli wa maneno ya wale waliokosania ili waweze kuwaamua bila upendeleo wowote. Wanakikao hao huulizia kwa makini ili waweze kumfahamu yule aliyemkosea mwenzake na muonya itakiwavyo, asije akarudia kosa lile.
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na upendo wa kuwawezesha kuitisha kikao cha kuweza kuwapatanisha watu waliokosana. Kikao hicho huwasaidia watu katika kufanya utafiti wa kuwawezesha kulifahamu tatizo kwa undani juu ya kile walichokosania wenzao hao. Kikao hicho huleta maisha ya amani kwa watu waliokosana kwa sababu ya kulifanyia utafiti wa kuweza kulitatua tatizo hilo.
1 Kor 6:1-4.
ENGLISH: A MEETING RESOLVES PROBLEMS
The above proverb looks at a situation whereby people get to have their differences resolved through dialogue. This means that, ideally, whenever a problem arises, kinsmen gather to deliberate on it for possible solutions.
The sitting conducts due diligence with great care, ensuring that the best solution is arrived at. This is the reason why it is said that ‘a meeting resolves problems.’
The proverb is compared to people who possess the compassion to help others overcome their differences. They undertake thorough investigation to get to the bottom of the conflict, and then give an impartial judgment. Through careful probing, the meeting identifies the offender and warns him/her accordingly, lest he/she should repeat the mistake.
The proverb teaches about the greatness of sparing time to organize sessions to help resolve people’s differences. Such sessions allow for sufficient fact-finding in order to better understand the source of conflict between the victims. As a result of all the effort in getting to the root of the misunderstanding, a peaceful co-existence among the people is assured.
1 Cor 6: 1-4.