Mwanza

1176. LYANGAKALILA.

Akahayile kenako kalolile bhanhu abho bhajaga gujulolilola lipuli umuchalo ja Ndoleleji. Ilipuli linilo ligalekwa na bhichalyo lilidima ng’wibhonde lya kumongo go Mangu.

Abhanhu aho bhalibhona bhagayupela gujulilola ukunhu bhalikumija mpaga nose bhukwila gete. Olihoyi munhu umo uyo agaligima bho gulyegela mpaga ulikinde linti, kunguno ya wigimbi bhokwe bhunubho. Aho lyamona ligangakalila linsangile mpaga upela uko gujile unyaga ugagwa mulilonga. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “lyangakalila.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitulaga bhumani bho gwigimba sagala, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga abhadarahile abhiye kunguno ya wigimbi bhokwe bhunubho. Uweyi apandikaga mamihayo gagwiduma na bhanhu aha kaya yakwe kunguno ya gwitula bhumani bho gubhadalaha abhiye chiniko, umuwikaji bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agaligima ilipuli bho gulikinda linti mpaga lyuntula, ugagwa mulilonga, kunguno nuweyi agitulaga bhumani bho gubhabyeda abhiye mpaga opandika mamihayo gagwiduma na bhanhu aha kaya yakwe yiniyo, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “lyangakalila.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhutumamila chiza ubhutale nubhumani bhokwe umubhutumami bho milimo yabho, kugiki bhadule gwikala chiza na bhichabho, umuwikaji bhobho.

Hesabu 13:30-32.

Zaburi 46:2-3.

KISWAHILI: LIMEMTUKA KWA MAJIGAMBO.

Msemo huo, huongelea watu walioenda kumwangalia Tembo kwenye kijiji cha Ndoleleji. Tembo huyo aliachwa na wenzake kwenye bustani ya Mto wa Mangu alijilisha.

Watu walipomuona huyo Tembo walikimbia kwenda kumuangalia mpaga wakawa wengi sana. Mmoja wa wale watu alijidai kumzoea huyo Tembo kwa kumsogelea mpaga akamchoma mti, kwa sababu ya majivuno yake hayo. Tembo huyo aligeuka na kumfuata kwa majigambo yule mtu ambaye alikimbia kuelekea unakoenda upepo mpaka akaanguka kwenye korongo. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “limemtuka kwa majigambo.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujitia kujua kwa kujigamba hovyo, katika maisha yake. Mtu huyo, huwadharau wenzake kwa sababu ya majivuno yake hayo. Yeye hupata matatizo ya kukosana na watu kwenye familia yake, kwa sababu ya kujidai kujua kwake akiwadharau wenzake hao, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyejigamba kwa kumchola mti Tembo, afukuzwa mpaka agaangukia kwenye korongo, kwa sababu naye hujigamba kwa kuwadharau wenzake mpaka anapata matatizo ya kukosana na watu, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “limemkuta kwa majigambo.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuutumia vizuri uongozi na uwezo wao, katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kuishi vizuri na wenzao, maishani mwao.

Hesabu 13:30-32.

Zaburi 46:2-3.

ENGLISH: IT HAS POMPOUSLY FOUND HIM.

This saying speaks of the people who went to see an Elephant in the village of Ndoleleji. This elephant was left by his companions in the Mangu River garden where it fed itself.

When the people saw it, they ran towards it in order to see it and there were many of them. One of them claimed to be familiar with such Elephant by approaching it. He stabbed it with a tree, because of his arrogance. The elephant turned and proudly followed such man who ran in the direction of the wind until he fell into the canyon. That is why people told him that, “it has pompously found him.”

This saying is compared to a person who makes himself known by being vainly proud, in his life. Such person despises his colleagues because of his pride. He has problems of missing people who can to stay with him in his family, because of his self-deprecating knowledge of those colleagues in his life.

This person resembles the one who boasted about to the point of stabling an elephant by using a tree, who was chased until he fell into a canyon, because he also boasts about disrespecting his colleagues until he gets problems of not getting along with people, in his life. That is why people tell him that, “it has pompously found him.”

This saying imparts in people an idea of using their leadership and abilities properly, in an enactment of their responsibilities, so that they can live well with their people, in their lives.

Numbers 13:30-32.

Psalm 46:2-3.

elephant-335754__480

1173. WIGONZOLA UWINGA.

Gwigonzola ili gwigondagula kunguno ya mapinja mapinja ayo gagatindikaga winga. Bhalihoyi bhanhu abho bhahayaga gwitola umuchalo ja Ngeme. Abhilomeji bha bhikweji abha nhande ijibhili bhagakoyakoya ugwidebha umpango go ng’ombe mpaga nose wimichiwa uwinga bhunubho. Aho wimichiwa, igigela na mbita hagati yingi hangi iyo igabhudija uwinga bhunubho, kunguno bhugasola likanza lilihu noyi na witiwa lulu. Hunagwene abhanhu bhagayomba giki, “wigonzola uwinga.”

Akahayile kenako kagalengajiyagwa ku bhitoji abho bhagiyumilijaga ugugamama wangu amakoye ulu gigela umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagikomejaga gutumama milimo yabho kihamo na guhoya bhuli makanza ulu bhapandikaga makoye, kunguno ya witogwi bhobho bhunubho, umuwitoji bhobho. Abhoyi bhagabhambilijaga abhanhu bhabho ugugamala wangu amakoye gabho kunguno ya wiyumilija bhobho bhunubho, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho bhagikolaga nu winga ubho bhugadijiwa na bhikweji mpaga yugigela na mbita hagati yingi, na witiwa, kunguno nabhoyi bhagapandika makoye bhiyumilija ugugamala wangu bho gutumama milimo yabho kihamo na guhoya kihamo, umuwikaji bhobho bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “wigonzola uwinga.”

Akahayile kenako kalanga bhitoji higulya ya gubhiza na wiyumilija bho guhoya chiza na kutumama milimo yabho kihamo kugiki bhadule gugamala wangu amakoye gabho, na gwikala bho mholele, umiwikaji bhobho.

Luka 14: 15-20.

Mathayo 24:36-38.

KISWAHILI: HARUSI IMEJIVIRIGA VIRIGA.

Kujivirigaviriga ni kucheleweshwa kwa harusi kwa sababu ya mapingamizi mbalimbali. Wakuliwepo watu waliotaka kuoana katika kijiji cha Ngeme. Watu wa pande mbili waliokaa kikao cha kuelewana mahali walishindwa kufikia mwafaka mpaga mwishowe harusi hiyo ilisimamishwa kwa muda. Baada ya kusimamishwa hivyo yalitokea matatizo mengine ambayo aliichelewesha zaidi harusi hiyo, kwa sababu ilichukuma muda mrefu ndipo ikafanyika. Ndiyo maana watu walisema kwamba, “harusi imejivirigaviriga.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa wana ndoa wale ambao huyatatua matatizo yao kwa uvulimilivu, kila yanapotokea, katika maisha yao. Watu hao, hujibidisha kufanya kazi zao kwa pamoja na kuongeza kwa pamoja kila wanapopata matatizo, kwa sababu ya upendo wao huo kati yao. Wao huwasaidia watu wengi katika kuyatatua matatizo yao haraka, kwa sababu ya uvumilivu wao huo, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na ile harusi iliyocheleweshwa na wapangaji wa mahali mpaka yakatokea matatizo wengine yaliyoichelewesha zaidi, kwa sababu nao huyatatua matatizo yao kwa uvumilifu kila yanapotokea, kwa kuongea na kufanya kazi zao kwa pamoja, katika maisha yao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “harusi imejivirigaviriga.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kuwawezesha kuyatatua matatizo yao kwa kuongea na kufanya kazi zao kwa pamoja, ili waweze kuishi kwa amani, maishani mwao.

Luka 14: 15-20.

Mathayo 24:36-38.

ENGLISH: THE WEDDING HAS MESSED UP.

Stagnation is a delay of a wedding due to various hostilities. There were people who wanted to get married at Ngeme village. People from both sides who sat in a meeting to understand each other failed to reach an agreement at the end the wedding was stopped for a while. After that suspension, other problems occurred which further delayed the wedding, because it took a long time to take place. That is why people said that, “the wedding has messed up.”

This saying is compared to married people who solve their problems with patience, whenever they arise, in their lives. Those people, try to do their work together and talk together whenever they have problems, because of their love for each other. They help many people in solving their problems quickly, because of their patience, in their lives.

Those people are like the wedding that was delayed by planners until there were other problems that delayed it even more, because they also solve their problems patiently whenever they occur, by talking and doing their work together, in their lives. That is why people tell them that, “the wedding has messed up.”

This saying teaches people about having patience that is strong enough to enable them solve their problems by talking and doing their work together, so that they can live peacefully in their lives.

Luke 14: 15-20.

Matthew 24:36-38.

bride-5427659__480

1172. KALAGU –  KIZE. UMYAJI ALI NA MAGULU ALIYO UMYALWA ADINA MAGULU – NGOKO NI GI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola kikalile ka ngoko na bhulanhani bho bhana bhayo. Ingoko yiniyo ligashigaga likanza yatela bho gunyela magi na gugalela bho gugabhandila mpaga gapya. Ulu gapya amagi genayo gagatandukaga kafuma kana umu bhuli ligi lyene, kunguno ya bhudiliji wiza ubho ngoko yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “umyaji ali na magulu aliyo umyalwa adina magulu – ngoko ni gi.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli myaji uyo agabhalelaga chiza abhana bhakwe mpaga bhakula, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agiyumilila ugubhalela abhana bhakwe bhenabho bho guhoya nabho bhuli lushigu, kunguno ya bhutogwa bhokwe ukubhana bhakwe bhenabho. Uweyi agabhakujaga mpaga bhadula gung’wambilija chiza aha kaya yake kunguno ya gubhalela chiza chiniko, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nkola iyo iyanyelaga magi yagabhandila chiza mpaga gapya na gufuma kana umu bhuli ligi lyene, kunguno nuweyi agabhalelaga chiza abhana bhakwe mpaga bhadula gung’wambilija chiza aha kaya yake yiniyo, umiwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “umyaji ali na magulu aliyo umyalwa adina magulu – ngoko ni gi.”

Ikalagu yiniyo, yalangu bhabyaji higulya ya kubhalanhana abhana bhabho bho gubhalela chiza, kugiki bhadule gubhambilija chiza umu kaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 1:24-31.

Hekima ya Sulemani 7:6.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

MZAZI ANA MIGUU LAKINI MZALIWA HANA MIGUU – KUKU NA YAI.

Chanzo cha kitendawili hicho, huangalia maisha ya kuku na utunzaji wa vifaranga vyake. Kuku huyo, hufika muda wa kutaga mayai na kuyalea kwa kuyakumbatia vizuri mpaga yanaiva. Mayai hayo yakiiva hupasuka na kutoa kifaranga kila moja kwa sababu ya utunzaji mzuri wa kuku huyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mzazi ana miguu lakini mzaliwa hana miguu – kuku na yai.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mzazi yule ambaye huwalea vizuri watoto wake mpaga wanakua, katika maisha yake. Mtu huyo, huvumilia katika kuwalea watoto wake hao kwa kuongea nao kila siku, kwa sababu ya upendo wake huo kwao. Yeye huwakuza vizuri watoto wake hao, mpaka wanaweza kumsaidia vizuri katika familia yake, kwa sababu ya kuwatunza kwa kuwapatia malezi mema, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule kuku aliyetaga mayaji akayatunza vizuri mpaka yakaiva na kutoa mtoto kila moja, kwa sababu naye huwatunza watoto wake kwa kuwalea vizuri mpaka wanaweza kumsaidia vizuri katika familia yake hiyo, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mzazi ana miguu lakini mzaliwa hana miguu – kuku na yai.”

Kitendawili hicho, hufundisha wazazi juu ya kuwatunza watoto wao kwa kuwalea vizuri, ili waweze kuwasaidia vyema katika familia zao, maishani mwao.

Mwanzo 1:24-31.

Hekima ya Sulemani 7:6.

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

THE PARENT HAS LEGS BUT THE CHILD HAS NO LEGS – THE CHICKEN AND THE EGG.

The foundation of this paradox, looks at the life of chickens and the care of their chicks. The hen spends time to lay eggs and nurture them by hugging them well until when they are ripe. When the eggs are ripe they crack and give out a chick each one because of the good care of her. That is why people say that, “the parent has legs but the child has no legs – the chicken and the egg.”

This paradox is compared to the parent who takes good care of his children as they grow up, in his life. Such person perseveres in raising his children by talking to them every day, because of his love for them. He raises his children well, until they can help him well in his family, because of taking care of them by providing them with good upbringing in life.

This person resembles the hen that laid eggs and took good care of them until they ripen and give birth to each one, because he also takes care of his children by raising them well until they can help him well in his family. That is why people say about him that, “the parent has legs but the child has no legs – the chicken and the egg.”

This riddle teaches parents on how to take care of their children by raising them well, so that they can help them better in their families in their societies.

Genesis 1:24-31.

Wisdom of Solomon 7:6.

 

chicken-1867521__480

1171. ODIMAGA IKANZA.

Akahayile kenako kalolile munhu uyo oli nikanza lya gujila minzi bhuli lushigu. Umunhu ng’wunuyo, wipunaga diyu aja kumongo gujudaha minzi bhuli lushigu, kunguno osangaga mingi masoga ayo gadayugulilwe na mitugo ahikanza linilo. Uweyi agakumuka nose umuchalo jakwe jinijo kunguno ya wipuni bhokwe bhunubho ubho gujila minzi bhuli lushigu. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “odimaga ikanza.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajilanijaga na likanza umubhutumami bho milimo yakwe umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agandyaga gulima ulu lyashiga ilikanza ilya jidiku, kunguno ahayile apandike matwajo mingi aha kaya yakwe. Uweyi agapanaga majiliwa mingi aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya gwigulambija gutumama milimo yakwe bho gujilanija ni kanza chiniko, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo wipunaga gujudaha mingi ogapandika minzi masoga bhuli lushigu, kunguno nuweyi agandyaga gulima ahikanza ilya jidiku bho gujilanija ni kanza mpaga opandika sabho ningi, umubhutumami bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “odimaga ikanza.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bho gujilanija ni kanza bhuli lushigu, kugiki bhadule kupandika sabho ja gubhambilija chiza, umukaya jabho jinijo.

Mhubiri 3:1-8.

Yohana 2:1-5.

Luka 22:14-16.

KISWAHILI: AMESHIKA MUDA.

Msemo huo, huangalia mtu aliyekuwa akienda kuchota maji kila siku. Mtu huyo, alikuwa akijilawa asubuhi na mapema kwenda mtoni kuchota maji kila siku kwa sababu ya kutaka kupata maji safi ambayo hajavurugwa na mifugo wakati huo. Yeye alijulikana sana kwenye kijiji chake kwa sababu ya kutoka kwake asabuhi na mapema kwenda kuchota maji. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “ameshika muda.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huendana na muda katika utekelezaji wa kazi zake, maishani mwake. Mtu huyo, huanza kulima kwa bidii sana wakati wa masika, kwa sababu anapenda kupata mafanikio mengi katika familia yake. Yeye hupata mazao mengi kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya kujibidisha kufanya kazi kwa kuendana na muda hivyo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyejilawa kwenda kuchota maji akayapata yaliyosafi, kwa sababu naye hujibidisha kulima wakati wa masika kwa kuendana na muda mpaga anapata mali nyingi, katika kazi zake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “ameshika muda.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kwa kuendana na muda kila siku, ili waweze kupata mali za kuwasaidia vizuri, katika familia zao.

Mhubiri 3:1-8.

Yohana 2:1-5.

Luka 22:14-16.

 

ENGLISH: HE IS ON TIME.

This saying looks at the person who went to fetch water every day. Such man used to wake up early in the morning to go to the river for fetching water every day because he wanted to get clean water that was not disturbed by livestock at that time. He was well known in his village because of his going out early in the morning to fetch water. That is why people said about him that, “he is on time.”

This saying is compared to a person who goes with time in implementing his works, in his life. Such person starts farming very hard during the spring, because he likes to get a lot of success in his family. He gets a lot of harvests in his family, because of working according to the required time, in his life.

This person resembles the one who went to fetch water in the morning and found it clean, because he also cultivates during the spring in accordance with the time to the point of getting a lot of wealth, in his works. That is why people say about him that, “he is on time.”

This saying imparts in people an idea of having to do their works in accordance with the time every day, so that they can get enough assets to support them well, in their families.

Ecclesiastes 3:1-8.

John 2:1-5.

Luke 22:14-16.

 

people-3127600__480

1170. YAPYAGA INDULU.

Ulusumo lunulo, luhoyelile higulya ya ndulu iyo yapyaga. Indulu yiniyo igikalaga munda ya mitugo nulu ndimu iyo agailujaga inyama yayo ulu yutinikila mumho mugati ahikanza ilya guibhaga inyama yiniyo. Iyoyi igaikenagulaga chiniko inyama ya ndugo gunuyo ulu yubhagwa bho nduhu witegeleja. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “yapyaga indulu.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agapelanaga bho nduhu uguyangulwa nulu okenyiyagwa hadoo duhu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agapelanaga wangu nulu ukenyiyagwa bho kamhayo kadoo duhu, kunguno ya bhukali bhokwe bhunubho. Uweyi agabhakoyaga abhanhu bha ha kaya yakwe kunguno ya gulema guyangulwa bhuli makanza ulu upelanaga, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ndulu iyo igakumiyaga hadoo duhu yatanduka mpaga yayiluja pye inyama, kunguno nuweyi agakenyiyagwa hadoo duhu opelana mpaga olema uguyangulwa umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “yapyaga indulu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka upelanu bho gulema guyangulya ulu bhakenyiyagwa nulu hadoo duhu, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Luka 19:45-48.

Luka 22:47-50.

Luka 14:21.

KISWAHILI: NYONGO IMEIVA.

Methali hiyo, huongelea juu ya nyongo iliyoiva. Nyongo hiyo, hupatikana tumboni mwa mifugo ambayo hufanya nyama iwe chungu endapo itapasukia ndani wakati wa kumchuna huyo mnyama. Yenyewe huiharibu hivyo hiyo nyama yote, asipokuwa na uangalifu mchunaji wa mnyama huyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “nyongo imeiva.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hukasirika upesi mpaka kufikia hatua ya kukataa kuamriwa hata anapokesowa kwa jambo dogo tu, katika maisha yake. Mtu huyo, hukasirishwa haraka na hata kwa jambo dogo tu, na kukataa kuamriwa kwa sababu ya hasira yake hiyo. Yeye huwahangaisha watu wa kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya ukali wake huo wa kukataa kuamriwa na wenzake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ile nyongo ambayo huguswa kidogo na kupasuka mpaka inaiharibu nyama yote, kwa sababu naye hukasirishwa hata na jambo dogo tu, na kukataa kuamriwa, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “nyongo imeiva.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha hasira ya kukasirika upesi kwa sababu ya jambo dogo tu na kukataa kuamriwa, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

Luka 19:45-48.

Luka 22:47-50.

Luka 14:21.

ENGLISH: THE GALL IS RIPE.

This proverb speaks of a ripen gall. The gall is found in a stomach of livestock, which makes the meat bitter if it bursts inside while slaughtering the animal. It itself destroys all the meat, if the slaughterer of such animal is not so careful. That is why people say that, “the gall is ripe.”

This proverb is compared to the person who gets angry quickly to the point of refusing to be ordered even when he is wronged in a small thing, in his life. Such person, gets angry quickly and even in a small thing that he refuses to be ordered because of his anger. He worries the people in his family, because of his harshness in refusing to be ordered by his colleagues, in his life.

This person is like the gall that is touched a little and bursts until it destroys all the meat, because he also gets angry even in a small thing to the point of refusing to be ordered, in his life. That is why people speak about him that, “the gall is ripe.”

This proverb teaches people about stopping getting angry quickly because of a small thing to the point of refusing to be ordered by others, so that they can raise their families well, in their lives.

Luke 19:45-48.

Luke 22:47-50.

Luke 14:21.

 

 

stick-fight-412666__480