196. GULALA MHINDA BHUGONDE

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile mhinda. Imhinda gulinfuko gogutulila hela. Umunhu ulu upandika hela, agajitulaga mumhinda yakwe. Imhinda yiniyo, iyo yatulilagwa ihela jinijo, igagololokaga. Aliyo lulu, imhinda yiniyo ulu idinajo imhiya, igigondaga. Gashinaga lulu, ugulala mhinda b’ugonde, mumho gugwisha limibu mpaga ugalala umunhu ng’wunuyo adapandikile ihela ja gutuula umumhinda yakwe.

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo olalaga adalile ijiliwa. Ing’humbi igalenganijiyagwa na mhinda, kunguno umunhu ulutuub’a umunda agigondaga, gitumo igigondelaga imhinda yiniyo, ulu itina ginhu jose jose. Hunagwene abhanhu bhagayombaga ukubhanhu abho bhalalaga bhadalile, giki, bhalala mhinda b’ugonde. Abhanhu bhenabho bhalina nzala ahakaya yabho.

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gub’iza na bhukamu bho gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule ugupandika ijiliwa ja gulya mpaka makanza malihu. Ubhukamu bho gutumama milimo bhunubho b’ugubhambilija  abhanhu bhenabho umugupona jiliwa ja guipeja inzara yiniyo umukaya jabho.

Ijinagongeja, ulusumo lunuyo lolanga bhanhu higulya ya gub’iza ni sungu lya gubhakuliwa bho gub’inha jiliwa abho bhadinabho ub’udula ubho gutumama milimo umuchalo jabho. Yigelelilwe abhanhu bhab’ize ni sungu lya gubhambilija abho bhadadulile ugutumama imilimo, kugiki nabho bhadule gwinga umulikoye lya nzara, bhadizu lala mhinda bhugonde.

1Wafalme 17:11-12.

Luka 15:17-18.

KISWAHILI: KULALA MFUKO UMEJIKUNJA

Chanzo cha methali hiyo chaangalia mfuko wa kutunzia hela. Mfuko huo ni kitu cha kuwekea pesa. Mtu akipata pesa huziweka kwenye mfuko wake. Mfuko huo ni tunzio la pesa hizo ambazo huunyosha zikiwekwa ndani yake.

Lakini basi, mfuko huo ukikosa pesa hujikunja. Kumbe basi, kulala mfuko umejikunja, maana yake ni hali ya mtu kupitisha siku nzima hadi kwenda kulala bila kupata pesa za kuweka kwenye mfuko wake huo.

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu ambaye amelala bila kula chakula. Tumbo hulinganishwa na mfuko, kwa sababu mtu akijisikia njaa tumboni hujikunja, kama ujikunjavyo mfuko huo wakati hauna kitu chochote.

Ndiyo maana watu husema kwa watu ambao wamelala bila kula chakula, kwamba, watu hao wamelala mfuko ukiwa umejikunja. Watu hao hawana chakula, yaani, wana njaa katika familia yao.

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kufanya kazi zao kwa ajili ya kuwawezesha kupata chakula cha kutosha kula katika familiya zao kwa muda mrefu. Bidii hiyo ya kufanya kazi, itawasaidia watu hao katika kupata chakula kingi kiwezacho kuifukuza njaa hiyo katika familia zao.

Zaidi ya hayo, methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na huruma ya kuwapatia chakula watu wasiojiweza maishani mwao ndani ya vijiji vyao. Yafaa watu wawe na huruma hiyo ya kuwasaidia watu hao wasiojiweza kufanya kazi, kwa ajili ya kuwawezesha nao kutoka kwenye tatizo la njaa, wasije wakalala mifuko ikiwa imejikunja.

1Wafalme 17:11-12.

Luka 15:17-18.

male-

ENGLISH: SLEEPING WITH A FOLDED POCKET

The above proverb is about a pocket that is used to keep money. Usually, the pocket gets stretched due to this function. Conversely, the pocket would fold up when it is devoid of money. ‘Sleeping with a folded pocket’ therefore means spending the entire day and night without getting any money to put in the pocket.

The proverb is likened to person who goes to bed without food. The stomach is compared to a pocket, which, like a pouch, folds up when it is empty. This is why it would be said about those going hungry: ‘they are sleeping with a folded pocket’, meaning they are hungry or they lack food in the family.

Such proverb is used to encourage people to work hard so that they may have sufficient and long lasting food supply in their families. The great effort would help them obtain enough food and keep hunger at bay.

In addition, the proverb teaches people to be compassionate enough to share their food with the poor. It is important for people to care for those who may be disadvantaged to save them from hunger or from ‘sleeping with folded pockets.’

1 Kings 17: 11-12.

Luke 15: 17-18.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.