141. NG’WILIMYA LIMYA AGAPANDIKAGA MANOG’HO

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Mbuki ya lusumo lwenulu ililola munhu nimi. Umunhu unimi ung’wene agiyumilijaga ahab’ulimi bhokwe wenubho, mpaka ogushisha unimo gunuyo ahikanza lya gubisha ijilhiwa. Ahenaho agub’iza opandikagaga amanong’ho; nguno agubisha ijiliwa giti Mandege, Busiga, Numbu na jingi ningi giti jinijo.

Ukubhanhu, akahayile kenako kagalenganijiyagwa na munhu uyo alitumama nimo gosegose bho wiyumilija mpaka ogushisha unimo gunuyo aha ng’halikijo yago.

Ubhulangwa bho kahayile kenako ukubhanhu, b’uli higulya ya wiyumilija umubhutumami bho milimo. Ilichiza ugugutumama unimo bho wiyumilija mpaga gugushisha aha ng’halikoko yago.

 Hangi akahayile kenako, kalilanga bhanhu, higulya ya gub’iza b’akamu umugutumama imilimo.  Ijina b’ukamu b’unubho, ubho gutumama imilimo, b’adulile guishisha imilimo yiniyo aha ng’halikilo yajo, bho makanza maguhi.

KISWAHILI: ANAYELIMA HUPATA FAIDA.

Maana ya methali hii inaangalia mtu anayelima. Mkulima huyo huvumilia katika kufanya kazi hiyo ya kulima mpaka kufikia hatua ya kupata mazao yaliyokomaa, hapo atakuwa amepata faida.

Maana atapata mazao ya vyakula kama vile: mahindi, mtama, viazi na vinginevyo vingi kama hivyo.

Kwa watu, msemo huo hulinganishwa na mtu yule anayefanya kazi yeyote kwa uvumilivu, mpaka kufikia hatua ya kuifikishisha kazi yake hiyo kwenye mwisho wake.

Fundisho la msemo huo kwa watu, uko juu ya uvumilivu katika kufanya kazi. Ni vizuri kufanya kazi kwa uvumilivu mpaka kuifikisha kazi hiyo kwenye mwisho wake.

Msemo huo pia hufundisha watu juu ya kuwa na bidii katika kufanya kazi. Ndani ya bidii hiyo ya kufanya kazi, watu wataweza kuimaliza kazi hiyo kwa muda mfupi zaidi na kupata faida ya kazi hiyo.

“Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana. Iweni na furaha katika tumaini, katika dhiki iweni na saburi, dumuni katika maombi.” (Waroma 12:11-12).

“Kwa kuwa vitu vyote vitayeyuka hivyo, ninyi je, imewapasa kuwa watu wa namna gani? Inawapasa kuishi maisha matakatifu na ya kumcha Mungu, mkingojea na kuhimiza kuja kwa hiyo siku ya Mungu, ambayo siku hiyo mbingu zitachomwa moto na kutoweka na vitu vya asili vitayeyuka kwa moto.” (2Petro 3:8-11).

“Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.” (Wagalatia 6:9).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s