Research sponsored by Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs,Sayings and Stories)
Mbuki ya lusumo lwenulu ililola munhu uyo alisiminza nu ungi uyo wigashije, ijinabhuchoji bho sabho. Uyo agusimizaga agalenganijiyagwa na munhu uyo agutumamaga milimo. Gashinaga lulu, ung’wunuyo agujipandika isabho.
Aliyo umunhu uyo wigashije duhu, agalenganijiyagwa nuyo adatumamaga imilimo, ung’wunuyo adujipandika isabho, agubhimba ng’humbi.
Ulusumo lwenulo lulilanga bhanhu higulya ya gubhiza bhatumami bha milimo, kugiki b’adule ugujipandika isabho. Kunguno, Isabho jigapandikagwa bho gujichola ijinagutumama milimo, idibhogwigasha na gulijindila duhu.
Ijina gongeja, ulusumo lwenulo lulilanga bhanhu higulya ya gub’iza na wiyumilija umubhutumami bho milimo yabho. Iyiniyi ili kunguno ya giki, abhanhu abho bhagacholaga na wiyumilija bhagapandikaga isabho umub’lamu b’ob’o.
Yeremia 29:13.
Marko 11:24.
Luka 7:9-10.
KISWAHILI: YULE ATEMBEAE ATAPATA YULE ALIYEKAA ATAVIMBA TUMBO
Chanzo cha methali hiyo kinaangalia mtu yule atembeae, na mwingine yule aliyekaa tu, katika utafutaji wa mali. Yule atembeae hulinganishwa na mtu yule afanyaye kazi kwa bidii. Kumbe basi, huyo atapata Mali.
Lakini mtu yule aliyekaa tu, hulinganishwa na yule asiyefanya kazi, huyo hatapata mali, atavimba tumbo.
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa wafanyakazi wenye bidii, ili kwamba, waweze kupata mali. Kwa sababu, Mali hupatikana kwa kuzitafuta katika kufanya kazi kwa bidii, siyo kwa kukaa, na kuzisubiri tu.
Zaidi ya hayo, methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu katika utafutaji wa mali. Hii ni kwa sababu, watu ambao hutafuta kwa uvumilivu hupata mali maishani mwao.
“Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” (Yeremia 29:13).
“Kwa sababu hiyo nawaambia, yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea nayo yatakuwa yenu.” (Marko 11:24).
“Yesu aliposikia maneno haya alimshangaa sana, akaugeukia ule umati wa watu uliokuwa unamfuata, akawaambia, “Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli.” Nao wale watu waliokuwa wametumwa kwa Yesu waliporudi nyumbani walimkuta yule mtumishi amepona.” (Luka 7:9-10).
ENGLISH: THE ONE WHO WALKS WILL FIND, THE ONE WHO STAYS WILL HAVE A SWOLLEN STOMACH
The source of the above proverb is looking at the person who walks, and the other one who stays in, in the search of property. The one who walks is likened to the one who works hard. Such person will get the property, he/she will be successful in life. But the person who stays, is likened to the one who does not work, he/she will not get wealth. He/she will have his/her stomach swollen.
The proverb teaches people to be hard workers so that they can earn wealth in the future. This is due that to fact that, property is obtained by looking for it, in hard working, not by just staying, and waiting for it. Additionally, the proverb teaches people about being patient in searching for properties. This is due to the fact that, people who patiently look for quantifiable achievement normally get profits in their lives.
“You will seek me and find me; when you seek me with all your heart” (Jeremiah 29:13). “Therefore I tell you, whatever you ask in prayer, believe that you have received it, and it will be yours.” (Mark 11:24). “When Jesus heard this he marveled at him, and turned and said to the multitude that followed him, “I tell you, not even in Israel have I found such faith.” And when those who had been sent returned to the house, they found the slave well.” (Luke 7:9-10).