115. ULUDUKALABHA MINZI UGOGA MININGA

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Jaliho chalo jilebhe, abhanhu gwegela gub’iza bhose, bhalibhashilimuka, aliyo munhu umo duhu olina jika. Oliadamanile ubhumunhu ni ki. Kuyiniyo, ichalo jigankolwa noi uwei kihamo nu nke.

Umunhu ng’wunuyo ilina lwakwe oli Ntwebhudamu. Oliatolile? Ehe, olimunhu obhub’i noi. Kulwa nguno oliadatoshekile nu nke. Limibu wiyungulaga aha naho, agukungilaga bhaniki, kihamo na bhakima bha bhanhu, na gwita nabho bhunwani bhob’ub’i.

Aliyo abhaswahili bhuhayaga, “amasaka gina miso, ni dunia idina siri. Giko, lidab’itile ikanza, ilishinya lwakwe ilib’i ligamanyika. Idi muchalo jakwe duhu, aliyo hangi ni chalo ijizenganilwe najo, nija kule jigamana na bhanhu bhagankolwa noi, nghangala ningi, aliyo pye iyose yale bhule.

Ntwebhdamu adalekile ngilo, ilishinya lwakwe. Kulwa nguno yakwe, uwikaji bho bhaniki bhingi bhugab’ipa, na kaya ningi jigacha. Uluub’ita kwigulilo abhanhu bhanyombaga uwei, uluuja kumbina amimbo gose gang’wimbaga, numu makanisa na mumisikiti yose, ubhulombi bhanombelaga wei.

Hado hado nhuma imbi ja ng’wa Ntwebhudamu jigampandika hangi nu nke (UVumilia) ng’wiyumilija. Agab’ita Jiwambaza, jisego jose jigansega wei, na bhanhu bhuyunsona wei.

Idi yiniyo duhu, unke agab’ita kulwinzi, bhakima bhose bhuyunsiga wei Ung’wiyumilija, giki adinkima, ali ginhu. Na giki uluniolinkima nghana, ungoshi niadakoyakoyile!

Jito jinijo jigang’wingha bhupina bhutale noi uNg’wiyumilija. No no iki uwei alinshilimu, uyo adamanile kukoyakoya. Ahawandya uNtwebhudamu iyakwe yiniyo,  agagema ugumhama ungoshi ng’wunuyo, aliyo agaduma.

Aha ngelelo agiyangula gulilima na guchib’a matu. Ligashiga ikanza lya gwipanga mujiji ja bhujamaa, ng’waka gunuyo Iserikali igita mhayo gumo gogubhalanga abhanhu gitumo igadugija.

Igabhalomela abhanhu yose ya higulwa ya solobho ja gwikala kihamo, na gutumama milimo kihamo. Aha nghalikilo igabhalekela abhanhu bhayangule b’inikili.

KISWAHILI: Usiponawa Maji Utaoga Damu

Kulikuwapo kijiji fulani, watu wake karibu wote walistaarabika ila mtu mmoja tu alikuwa na kasoro. Hakujua uungwana ni nini. Hivyo kijiji kizima kilimchukia sana yeye pamoja na mkewe.

Mtu huyo jina lake ni Kichwangumu. Alikuwa ameoa? Ndiyo, lakini alikuwa mtu mbaya sana. Maana hakutosheka na mkewe. Kutwa kucha alizunguka hapa  na pale akiwavizia wasichana, pamoja na wake za watu, na kufanya nao urafiki mbaya.

Lakini waswahili husema ‘vichaka vina macho, na dunia haina siri.’ Hivyo haukupita muda mchezo wake huo mbaya ulijulikana. Si kijijini pake tu, bali pia na vijiji vya jirani, na hata vya mbali. Kutokana na jambo hilo watu walimchukia sana mara nyingi, lakini yote hayo yalikuwa bure.

Kichwangumu hakuacha kamwe mchezo wake, na kwa sababu yake maisha ya wasichana wengi yaliharibika, na familia nyingi zilivunjika. Ukipita sokoni watu walimsema yeye, ukienda kwenye ngoma, nyimbo zote zilimwimba, na makanisani na misikitini madua yote yalimwombea yeye.

Kidogo kidogo sifa mbaya za Kichwangumu zilimfikia pia mkewe Vumilia. Akipita viwambaza vicheko vilimcheka yeye, na misonyo yote ilimsonya yeye.

Si hayo tu, akipita kisimani wanawake wote wanamteta yeye Vumilia, kwamba si mwanamke, ni kitu. Na kwamba angalikuwa mwanamke kweli mmewe asingelihangaika!

Jambo hilo lilimtia uchungu mkubwa sana Vumilia. Hasa kwa vile yeye ni muungwana, asiyejua kuhangaika. Mwanzoni alijaribu kumrudi mumewe, lakini alishindwa.

Mwishoni aliamua kufumba macho, na kuziba masikio. Sasa ilifika enzi ya operesheni vijiji vya ujamaa. Mwaka huo Serikali ilifanya jambo moja la kuwaelimisha watu kwa kadiri ilivyoweza.

Pia iliwashawishi watu kwa kadiri ilivyoweza, yote kuhusu faida za kuishi pamoja, na kufanya kazi kwa pamoja. Mwishoni iliwaachia watu waamue wenyewe.

 

 superhero

 

ENGLISH: IF YOU DON’T WASH HANDS WITH WATER YOU WILL TAKE BATH WITH BLOOD

There was a village. Its people were civilized except one man. He had a defect. He did not know what being a gentleman meant. So the whole village hated him.

The name of such a person was Kichwangumu (which means hard head). Was he married? Yes, but he was a very bad man. For he was not satisfied with his wife. He went around and around looking for girls, as well as the wives of other people, and made with them bad friendship.

But the Swahili people have a saying “Vichaka vina macho, na dunia haina siri.” That means the bushes have eyes, and the world has no secret. Within a short time, his game was known by people. He was known not only in his village, but also in neighboring villages, and even those in distant places. Because of this, people often hated him.

Kichwangumu never left his game and because him many girls’ lives got spoiled and many families were broken. When you went to the market, the people talked about him. During the traditional dances, , all the songs were about him. In churches and mosques, prayers were for him.

Little by little, the bad conduct of Kichwangumu also reached his wife, Vumilia. As she passed through various areas, people laughed at her, and they looked down upon her.

Not only that, when she went to the wells, all the women gossiped about her saying, she was not a woman, rather she was something. If she were a true woman, her husband would not worry!

This thing made Vumilia very sad especially since she was a gentle lady, she was not worried. At first, she tried to change her husband, but she failed.

At the end, she decided to pretend not to see and not to hear. Now came the era of operation villages of socialism. The government did one thing to educate people as much as possible.

It also persuaded people as much as possible, all about the benefits of living together, and working together. At last it left people to decide for themselves.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.