116. MIZWI YA BAHATI

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Ilikanza ilo aho itunge igabyalwa umuzi iyi, yali itina manana nulu kapande ki nana. Giko igalilolela iligulya giki yulimilila mate na idadulile ugulala.

Ijiseme ijaheke ijo yaliinhiwa gujipandika gali magulu duhu. Giko lulu, ulugendo lokwe ulo musi lolilo jina bhambu duhu, uluululinganija nulo noni ijo jayelayelaga ung’wigulwa.

Aliyo ninga ya bhulebhu bhunubho itunge yaliyagina guti nyama ya kukomela. Giko majihumbi ga ndimu ganingaga jikali kugiki gameje makubhi ga mhindi na nsuji go kuwalwa.

Ihali yiniyo igantuula utunge mumayange matale. Giko nhangala ng’wingi agaikala wibhisaga limimbu, kugiki adizibola na liso lya ng’wanishi okwe. Agihadikija gwita giko kulwa ubhanga bhokwe ng’winikili.

Lushigu lumo itunge igalota jiloti jisoga guti sukari. Najo ni giki angu yazwaga manana umumbazu jayo. Ni giki, angu ung’wanishi aho ohaya guyidima iyoi egisekeleja yulala ng’wigulwa yuyelayela bho mholele na kumfiila makololelwa ung’wanishi ukunu ahasi.

Naho omisa utunge agadimwa gete na miganiko ga higulya ya jiloti jinijo. Agagikumva noi amanana genayo ayo agagigetela umujiloti jinijo. Aliyo adamanile igiki ihaha jalihei, nhabhi agikumbwa noi alale ng’wigulya giti umo agalotela ubhujiku wenubho.

Aliyo adamanile igiki aguduja ginehe ugwita chiniko. Kwandija lushugu lunulo utunge agayubhuchola ubhuyeji bho nduhu ugubhubhona, limibu, agiganika umo agupandikila amanana alale. Aliyo yose yali milimo ya bhule. Giko aho nhalikilo, agabhiza adina gungi ugogwita, ubhiza na gogub’inzika moyo, na makanza genayo oliokonda guti lushinge.

  Aliyo utunge uyu oliadijisumbwa bhung’wene umusi uyo alimuhali ya gub’inzika moyo, kulwa nguno uliho na ungi umusi munumu uyo oliyob’inzika moyo, ujisumbwa ng’winuyo, nu ntemi o noni.

Uwei ilikoye ilitale ilo lyankoyaga lyalilimo. Ung’wigulya uko jigadoselaga inoni, na manana gajo, bhugigela bhusatu bhutale noi, na majihumbi ga noni, jigayujimija bhupanga bho mioyo yajo bhuli lushigu.

KISWAHILI: MIZIZI YA BAHATI

Wakati  Popo alipozaliwa katika dunia hii, hakuwa na mbawa wala kipande cha ubawa. Hivyo alilitazama anga hivi hivi akalimezea mate na asiweze kuruka.

Chombo cha pekee cha usafiri alichokuwa amejaliwa kukipata ni miguu tu. Hivyo mwendo wake aridhini ulikuwa ni wa Kinyonga tu, ukiulinganisha na ule wa ndege waliokuwa wakirandaranda angani.

Lakini licha ya unyonge huo, Popo alikuwa amenona kama nyama ya kubanika. Hivyo maelfu ya wanyama walimwinda vikali ili wamfanye kitoweo cha jioni na susa ya kilabuni.

Hali hiyo ilimweka Popo katika wasiwasi mkubwa. Hivyo mara nyingi ilimbidi kujificha mchana kutwa, ili asigongane na jicho la adui. Alilazimika kufanya hivyo kwa usalama wake mwenyewe.

Siku moja popo aliota ndoto nzuri kama sukari. Nayo ni kwamba, eti ameota mabawa kwenye mbavu zake. Na kwamba, eti adui alipotaka kumkamata, yeye alitabasamu akaruka juu angani akarandaranda kwa amani na kumtemea kikohozi adui aliyeko chini.

Hata alipoamka Popo alitekwa kabisa na mawazo kuhusu ndoto hiyo. Alizitamani sana zile mbawa alizopigia mbwembwe katika ndoto usiku ule. Lakini hakujua kwamba sasa zilikuwa wapi, maskini, alitamani sana aruke angani kama alivyofanya ndotoni usiku ule. Lakini hakujua kwamba atawezaje, kufanya  hivyo.

Maskini Popo, tangu siku hiyo aliitafuta raha kama hiyo, asiione, kutwa kucha, alichemsha ubongo jinsi  atakavyopata au kukopa mbawa aruke. Lakini yote yalikuwa kazi bure. Hivyo mwishoni akawa hana jingine la kufanya ila kukata tamaa, na wakati huo alikuwa amekwisha kukonda kama sindano.

Lakini Popo huyu hakuwa kiumbe pekee katika dunia aliyekuwa katika hali hiyo ya kukata tamaa, kwani alikuwapo pia kiumbe mwingine hapa duniani aliyekuwa amevunjika moyo pia na kiumbe huyo ni mfalme wa ndege. Yeye tatizo kubwa lililokuwa limemtatiza ni moja. Huko angani wanakoringia ndege na vibawa vyao, kulizuka ugonjwa mbaya sana, na maelfu ya ndege walikuwa wakipoteza maisha ya Roho zao kila siku.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s