114. GUKULILWA GO WELELO

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Olihoi Ntemi umo nsabhi noi, ilina lwake, Kisirani. Untemi ng’wunuyo uli na manumba mingi guti sonda, hangi pye agose gali malihu mpaga ng’wigulya.

Giko, olina na hela nyingi guti masalu ga nghwani. Hangi jose jali muma noti ga igana igana. Kunguno ya bhusabhi bhutale bhunubho, UKisirani agabhiza na kajile ka gukumya noi.

Oliadazwalaga imyenda nghangala ibhili. Adalalaga muchumba jimo nghangala ibhili, oladikalaga na nke nghangala ibhili, oliadalalilaga bhulili bhumo nghangali ibhili.

Uwei ulu uzwala sulubhale ni ngwanda ijikolile ilelo, intondo aguzwala jingi, na atalaishokela hangi iyalelo. Hangi ulu ulala muchumba iji ilelo, nduhu atalishokela hangi ugulala umuchumba jinijo ija lelo.  Uwei uluntola ng’waniki nnebhe ileo limi, agumpeja idilu hilu, na guntola ungi ilimi, adunkumya hangi uolelo ng’wunuyo.

Ulu ulalila bhulili ubhu ilelo, intondo ubhuponya kule na adubhulalila hangi. Nose UKisirani agisanga bhuli lushiku wenhaga myenda mipya, nkima mpya, chumba jipya, bhulili bhupya na gwendelea.

Aliyo pye iyose iyiniyo idanfujije, na ijina bhunghana, umumoyo gokwe adabhizile na bhuyegi, nulu hadoo, kunguno lushigu mpaga lushigu wigwaga ilaka ilebhe umumoyo gokwe. Nawe wiigwa giki ginhu jilebhe jiligaikana ijagubhushikilija ubhuyegi bho bhusabhi bhokwe. Aliyo adamanile ni ginhu ki iginijo, na ku iyiniyo lushigu lulebhe agigisha wiganika noi, kugiki wite kiyi adule gupandika ubheyegi umusi.

Aho wiganika chiniko, agashigila ha wiyanguji bhumo, giki, ubhusabhi ubho alinabho bhutoshije, aliyo ijojiligaikana, umuwikaji bhokwe, angu bhuli bhuhabhi ubho gudula gulinganila nubhusabhi bhokwe.

Na lulu, agiyangula giki, acholwe munhu uyo wina makoye gulebha pye umubhikaji bhakwe, wenhwe kuliwei. Ililagilo linilo ligatimijiwe numulikanza lwenilo.

KISWAHILI: Kuhurumiwa Kwa Ulimwengu

Alikuwapo  Mfalme mmoja tajiri sana, jina lake Kisirani. Mfalme huyu alikuwa na majumba mengi  kama nyota, tena yote yalikuwa marefu hadi angani.

Vile vile, alikuwa na fedha nyingi kama mchanga wa pwani. Tena zote zikiwa katika manoti ya mia mia. Kutokana na utajiri huo mkubwa, Kisirani alikuwa na tabia moja ya ajabu sana.

 Alikuwa havai nguo moja mara mbili, halali chumba kimoja mara mbili, hakai na mke siku mbili, wala halali kitanda kimoja mara mbili. Yeye akivaa suti hii leo, kesho anatupa na kuvaa nyingine, na kamwe hatairudia tena hiyo ya leo.

Aidha Kisirani akilala chumba hiki leo, kesho atalala chumba kingine na hatakigusa tena kile cha leo. Yeye akimwoa binti fulani leo alasiri, atamfukuza mapema alfajiri na kumwoa mwingine alasiri, na kamwe hatamgusa tena huyo wa leo.

Pia akilalia kitanda hiki leo, kesho atakitupilia mbali na kulalia kingine, hatakirudia tena hiki cha leo, nakadhalika. Hatimaye kisirani alijikuta kila siku ana nguo mpya, ana mke mpya, chumba kipya, kitanda kipya, nakadhalika.

Lakini yote hayo, hayakutosha kumfanya atosheke na kwa kweli rohoni mwake hakuwa na raha, hata kidogo, kwani siku hadi siku, sauti fulani ililia rohoni mwake. Naye alihisi kwamba kitu fulani kimekosekana katika kuikamilisha  raha ya utajiri wake.

Lakini hakujua kitu hicho ni nini. Hata hivyo, siku fulani alikaa kitako na kufikiri sana, afanye nini ili apate raha  katika dunia. Na baada ya kufikiri hivyo, alifikia uamuzi mmoja,  kwamba utajiri alionao unatosha, lakini kilichokosekana, katika maisha yake, eti, ni umaskini wa kuweza kulinganishwa na utajiri wake. Basi aliamuru kwamba atafutwe mtu mwenye dhiki kuliko wote katika raia wake aletwe kwake. Amri hiyo ilitimizwa mara moja.

pharaoh-

portrait-child

 

ENGLISH: MERCY TO THE WORLD

Once upon a time, there was a very rich king whose name was Kisirani. The king had many palaces like stars, and they were all tall reaching the sky.

He also had a lot of money as sands of the beach. All his money was in one  hundred notes. As a result of this enormous wealth, Kisirani had one strange character.

 He could not wear the same clothes twice. He could not sleep in the same room twice. He could not sleep with the same wife for two days. He could not sleep in the  same bed twice. It was like this: If he wears this suit today, tomorrow he throws it away, and if he wears different dress, he never repeated wearing any of the clothes.

In addition, if Kisirani sleeps in this room today, tomorrow he would sleep in another room and would not come back it again. When he married a woman this afternoon, he would divorce her early the following morning and could marry another woman in the afternoon.  He would never come back to previous one.

Also, if he lay on this bed today, tomorrow he would throw it away and sleep in another. He would never come back to this another day. Finally, Kisirani found himself every day with new clothes, a new wife, a new room, a new bed, and so on.

But all those, were not enough to make him satisfied and really in his soul there was no happiness. No happiness at all. One day, a voice cried out in his heart. He felt that something was missing despite his wealth.

But he didn’t know what that was. However, he sat down and thought deeply about it. He realized that what was missing, was poverty with which to compared his wealth. So he ordered that a man in distress should be sought among his citizens to be brought to him. The command was fulfilled immediately.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.