113. GWIYUMILIJA MAKOYE

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Umuchalo jise agikala munhu umo uyo akatola nkima nsoga noi. Aho bhikala miaka mingi, bhagapandika ng’wana umo ng’waniki, ilina lwakwe, Nanyale.

UNanyale oli ng’wana o mili gowiza na nihanga lisoga. Uling’wana oafya na bhuyegi bhuli lughigu. Bhab’yaji bhakwe bhagantogwa noi, bhuli lughigu bhang’winhaga ginhu jawiza, bhang’winhaga magi, machungwa, pipi, myenda misoga, jilatu na jingi ningi.

Nanyale agakula ubhiza mtale. Lughigu lumo agapandika masugu, unina agazumalika, usaga wei na se. Agatumama milimo yose ya gufula, kupyagula numba, na gunzugila use. Use agampinihalila noi ung’wana  okwe ng’waniki ng’wunuyo.

Nanyale agandya gukonda kunguno ya miganiko na milimo. Use akamtola mkima ungi. UNanyale oliadantogilwe unina okwe uo kab’ili, kunguno olinkali noi. Oliadatumamaga nimo gosegose, oliatogilwe gwigasha du, bhuli nimo otumamaga Nanyale.

Nalulu, lughigu lumo Nanyale aginhiwa nimo go gusha bhulezi. Agazunya, adalemile. Hangi, bhuli ikanza ilo agagenhiha use, uNanyale opandikaga makoye noi. Uluwandya ugusha wimbaga:

“Sheku sheku umaji, Sheku sheku anganite,  Sheku sheku bwo atajaga,  Sheku sheku ngupya, Sheku sheku ngupya.”

 “Uliyomba ginehe?” Unina uokabhili agamuja.

“Naduyombaga ginhu,” uNanyale agashosha.

“Nigwaga noi, na lulu, ulu ulashokele nagugutula mapi.” UNanyale adayombile ginhu, agendelea gusha. Aho lwabhita ikanza iguhi, agashokela ilwimbo lwake:

 “Sheku sheku umaji, sheku sheku anganite, sheku sheku bwo atajaga, sheku sheku ngupya, sheku sheku ngupya.”

Ubhulingisilo bho lwimbo linilo, ili giki, “nalipandika makoye, umayu olianitogilwe. Oli adaniluhyaga giki, napandika makoye, napandika makoye. Sheku lilililaka lya liwe lwa gushela.

Aho omala ugusha ubhufu bhokwe, agatulwa mapi ga kubhushu. Nanyale agagwa sagali. Gashinaga aho alimba unina o kabhili olibihi nanghwe.

Nanyale agimila bho polepole. Agalisola iliwe lwakwe wandya gusha. Jisoji jingi jazwaga. Unina uokabhili ng’wenuyo, agamuuja, “nagaguwila udizimba ilwimbo lilinilo ulishogela?” UNanyale adashoshije. “Udigwaga, naliyomba niwe nulu munhu?”

Nanyale adashoshije. ‘Paaa!’ Agang’wongegeja ipi lwa kabhili. Nanyale adadililile, agendelea gusha. Jisoji jigahuma noi gulebha igwandya. Unina uokabhili aho obhona giki uNanyale adushoshaga, aginga uneka.

Oliamanile ugwiyumilija adalekile ugusha. Use aho oshoka agansanga uNanyale agushaga ukunu agulilaga. “Mayu ung’wana oko alililila khiyi?” Use agamuja unina uokabhili, “Nadaminile mujage ng’wana oko. Ulinibhuja unene? Nayi unene naliNanyale?” Agashosha unke.

 “Sheku sheku umaji, Sheku sheku angatile, Sheku sheku bwo atajaga, Sheku sheku ingupya, Sheku sheku ingupya”.

Nanyale agashokela ilyimbo lwakwe. Uligwa imihayo ya ng’wana oko?” Unke agang’wila ungoshi, huna gwene nagantula. Agendelea, “ulualing’wizuka unina, na lulu aje aganhimbule, nayi adujibhonaga ijigila?”

Use o ng’wa Nanyale agakumya na hangi wandya gulila. Agampinhihalila ung’wana okwe ung’waniki ung’wunuyo. UNanyale oling’waniki ng’wiyumilija. Kihamo na gupandika bhuluhi  wingi giko adabhinzikile moyo.

Use agampeja unke okwe nu lushigu lunulo. Agasaga na ng’waniki ung’wana okwe ng’wunuyo, bho miaka mingi.

Nose uNanyale agapandika ngosha utolwa. Agikala wikaji bho bhuyegi noi. Mpaga agagibha amakoye goze ga ng’wa nina uokabhili.

Kiswahili: Kuvumilia Taabu

Katika kijiji chetu aliishi mtu mmoja ambaye alioa mke mzuri sana. Baada ya kuishi miaka mingi, walipata mtoto mmoja msichana, jina lake Nanyale. Nanyale alikuwa na umbo zuri na sura nzuri pia.

Alikuwa mtoto mwenye afya njema na furaha kila siku. Wazazi wake walimpenda sana. Kila siku walimpa vitu vizuri. Walimpa mayai, machungwa, peremende, nguo nzuri, viatu na vingine vingi.

Nanyale alikua akawa mkubwa. Siku moja alipata msiba, mama yake alikufa. Akabaki yeye na baba yake. Alifanya kazi zote za kufua, kufyagia nyumba na kumpikia baba yake. Baba alimhurumia sana binti yake.

Nanyale alianza kukonda kwa sababu ya mawazo na kazi hizo nyingi. Baba yake akamwoa mwanamke mwingine. Nanyale hakumpenda mama huyo wa kambo, kwa sababu alikuwa mkali sana. Hakufanya kazi yoyote, alipenda kukaa tu. Kila kazi aliifanya Nanyale.

Basi siku moja Nanyale alipewa kazi ya kusaga ulezi. Nanyale alikubali, hakukataa kwa sababu alimwogopa mama yake. Baba yake alikuwa amesafiri, na kila aliposafiri baba yake, Nanyale  alipata taabu sana. Alipoanza kusaga aliimba:

“Sheku sheku umaji, sheku sheku anganite, sheku sheku bwo atajaga, sheku sheku ngupya, sheku sheku ngupya.”

“Unasemaje?” Mama wa kambo alimwuuliza.

“Sisemi kitu,” Nanyale alijibu.

“Nimesikia sana, basi ukirudia nitakuchapa makofi.” Nanyale hakusema kitu, aliendelea kusaga. Baada ya muda kidogo alirudia kuimba wimbo wake:

“Sheku sheku umaji, sheku sheku anganite, sheku sheku bwo atajaga, sheku sheku ngupya, sheku sheku ngupya.”

Maana ya wimbo huo ni kwamba, ‘napata taabu, mama yangu alinipenda. Hakuwa ananitesa hivi, napata taabu, napata taabu.’ Sheku ni sauti ya jiwe la kusagia. Alipomaliza kusaga unga wake, alipigwa kofi usoni. Nanyale akaanguka chali, kumbe wakati ule alipokuwa akiimba  mama huyo wa kambo, alikuwa karibu naye.

Nanyale  alinyanyuka polepole, akachukua jiwe lake akaanza kusaga, huku machozi yakimtoka kwa wingi. Mama wa kambo alimwuuliza, “nilikuambia usiimbe wimbo huo unarudia?” Nanyale hakujibu, “husikii, nasema na jiwe au mtu?” mama yule aliuza. Nanyale hakujibu kitu, “Paaa!” Alimwongezea kofi la pili. Nanyale hakujali alindelea kusaga.

Machozi yalimtiririka zaidi kuliko mara ya kwanza. Mama wa kambo alipoona kuwa, Nanyale hamjibu, aliondoka akamwacha. Nanyale alijua kuvumilia,  hakuacha kusaga.

Baba yake aliporudi alimkuta Nanyale anasaga huku akilia. “Mama, mtoto wako analilia nini?” Baba alimwuuliza mama wa kambo, “Sijui mwuulize mtoto wako. Unaniuliza mimi? Kwani mimi ni Nanyale?” Mkewe alijibu.

 “Sheku sheku umaji, Sheku sheku angatile, Sheku sheku bwo atajaga, Sheku sheku ngupya, Sheku sheku ngupya”.

Nanyale alirudia wimbo wake. “Unasikia maneno ya mtoto wako? Mkewe alimwambia mumewe, ndiyo maana nampiga.” Akaendelea, “kama anamkumbuka mama yake, basi aende akamfufue, kwani haoni kaburi?” Baba yake Nanyale alisikitika akaanza kulia pia. Alimhurumia binti yake. Nanyale alikuwa binti mvumilivu. Ingawa alipata mateso mengi hakukata tamaa.

Baba yake alimfukuza mke wake siku hiyo hiyo, akabaki na binti yake kwa miaka mingi. Mwishowe Nanyale alipata mchumba akaolewa. Aliishi maisha ya raha sana. Hata alisahau taabu zote za mama wa kambo.

sculpture-

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.