111. JIGANO JA BHANA BHADATU

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Bhaliho bhayanda bhadatu bha hakaya imo bhajaga gujutega noni bhuli dilu. Nyanda wabhenabho obhizaga ulu opuja inoni yang’wila giki “nilekege nkoyi nalagugunana gubhujakale,” wilekela.

Pye indimu ujitang’ang’hya. Nose ab’iye bhuyunjija ugulya ijo bhapujaga bhaling’wila giki, “ubhebhe ugajilekelaga ulu opuja. Nose wifugula uguyutega na uja ng’wipolu ugab’ona ng’waniki umo bhitogwa.

Nabhuja kung’wawe ya ng’waniki ng’wenuyo. Aho bhashiga ho, namhala uhaya, “napandika nkwilima.” Uwilwa gujufega ipolu itale gete kulushigu lumo. Nang’hwe uja ugandya ugufega. Uliduma linti limo gwike, wandya gulila ohaimanila jiza mhuli jung’wambilija ugulifega lyose.

Uwilwa guja gujub’ib’a ngunda gutale go heka 10. Aho oshoga unkwiye ung’wila “noloha ugulima, jaga ugajikong’onhe imbiyu jane jib’ize gitumo jalijili. Nang’hwe agaja ugita gitumo owililagwa. Aho oshika uduma umo witile. Gwimanila jiza noni jung’wambilija ujisolela imbiyu jose uchala kaya, unkwiye utogwa gete.

Lukangala ulu unkwiye ung’wila ng’wanone nab’onaga giki izile utole ahenaha nguno yose iyo naliguwila ulishigilija, ihaha lulu jaga lo kwimala uganisumile bhujiku pa ganana unenhele henaha. Nyanda uja aliyo alib’uja ‘nagudula ginehe ugub’udima ubhujiku nagubhutula mu ganana?’

Aho oshiga kwenuko owilagwa, kiza ga sayayi kung’wila, “ilekage iganana ugang’wile ‘nakajaga aliyo ninhage ngata ya lyochi nagabhukije ninhage ni haha.’

Namhala aho owilwa chene uduma umo agudulila ugulib’ilinga ilyochi, na ung’wila unyanda giki, “jaga ugab’ufuge ubhujiku, wenhe kaya iganana na usole unke oko.’

KISWAHILI: Hadithi Ya Vijana Watatu

Walikuwepo wavulana watatu kwenye familia moja. Walioenda kutega ndege kila asubuhi. Mdogo wao kila aliponasa ndege, ndege alimwambia, “niachia rafiki yangu nitakusaidia kwenye siku za mbele.” Alimwachia.

  Wanyama wote aliwaeneza. Mwishowe wenzake walimkataza kula wale waliowanasa wao wakimwambia hivi, “wewe huwa unawaachia unapowanasa.

Mwishowe alizila kutega, akaenda porini. Huko alionana na msichana mmoja wakapendana. Akaenda kwa wazazi wake msichana huyo. Walipofika pale, mzee alisema, “nimepata mkwilima.”

Aliambiwa kwenda kufyeka pori kubwa kabisa kwa siku moja. Naye alienda na kuanza kufyeka. Alishindwa kuukata mti mmoja tu akaanza kulia, kushitukia, wakaja tembo wakamsaidia kulifyeka lote.

Baada ya kuimaliza kazi hiyo, aliambiwa kwenda kumwaga mbegu kwenye shamba kubwa la heka 10. Aliporudi, baba mkwe wake alimwambia, “nimeahilisha kulima, nenda ukaziokote zile mbegu zangu ziwe kama zilivyokuwa.” Naye kama alivyoelezwa alienda. Alipofika alishindwa wakaja ndege wakamsaidia kuziokota mbegu zile zote, akapeleka nyumbani, baba mkwe alifurahi kabisa.

Safari hii baba mkwe wake, alimwambia, “mtoto wangu nimeona kwamba utaoa hapa kwa sababu yote yale ninayokuambia unayatimiza. Sasa basi, nenda kwa mara ya mwisho, ukanikusanyie usiku ujae kwenye kikapu, uniletee hapa.”

Mvulana alienda lakini akijiuliza “nitawezaje kuushika usiku na kuuweka kwenye kikapu?”

Alipofika huko alikoambiwa, akaja Sungura, akamwambia, “kiache kikapu ukamwambie, nimejaza, lakini nipatie kata ya moshi nikabebee, nipatia sasa hivi.”

Mzee alipoambiwa hivyo, alishindwa namna ya kuukusanya huo moshi na akamwambia mvulana hivi, “nenda ukaumwage usiku, ulete nyumbani kile kikapu na umchukue mke wako.”

elderly-egyptian-one

THE STORY OF THREE YOUTHS

There were three boys in one family. They used to go the trap birds every morning. When the youngest trapped a bird, such a bird could tell him, “Leave me, my friend I will help you in the future.” He could leave it.

He did the same it to all animals. Finally, his brothers forbade him to eat what they had caught saying, “You cannot eat what we catch because you leave the animals that you catch.”

He finally abandoned the whole enterprise and went the wilderness. There, he met a girl with whom he fell in love. He went to the parents of that girl. When they got there, the old man said, “I’ve got a son-in-law.”

As a condition before he could be allowed to marry a daughter, the young man was told to go to cut a big forest for one day. He went and started slashing. He failed to cut down one tree and started to crying, not knowing what to do. It happened that the elephants came and helped him to cut all the troubling trees.

After completing the work, the young man was told to go and sow the seeds in a huge piece of land of ten acres. After that, his father in law told him, “I have changed my mind on the idea of cultivating. Therefore, I order you to go and gather up all the seeds you sowed and return them to me as they were.”  When he tried to do that, he failed. Suddenly, birds came and helped him to gather up all the seeds, which he sent home. His father-in-law was very happy for what the young man did.

After the young man had passed all the tests, his father-in-law told him, “My son I have seen that you will marry here because you do all that I tell you. Now, go for the last test. Gather the night in this basket. Bring it to me here. ”

The boy went but wondered, “How can I catch the night and put it in the basket?”

When he got there, he came across the hare shared his assignment with him, the hare told the young man,“Leave the basket with me and then go back and tell him, I have filled it, but give me smoke so as to go and  carry it, right now.”

When the father-in-law was told that, he failed to collect the smoke and in response told the boy, “Go and pour out the night and bring home the basket and then take your wife.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.