103. Wibhakizu (Hofu) Bhugenhaga Lufu

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Ikale iyo oliho msumba umo witanagwa Kisho. Unsumba uyo olina bhumani (maarifa) noi. Bhabha okwe oliamanyikile mu lina lwa Mapali, agantogwa noi u Kisho.

Aganchala ung’wanokwe agandye shule kugiki asome. Kisho agayega noi ugupandika wasa bhunubho bho guja gujelimiaka ku shule. U Kisho aho omala chiza ielimu ya msingi agachagulwa guja ku sekondari.

Agita chiza umu masomo gakwe mpaka agamala jidato ja kane. Hangi ulinsumba uyo agitogwa noi ku bhutalamu bho mubhusafi bho mili na myenda. Makanza gose aliabhelelile gete gete. Oli na nhungwa ja gudilila bhutalatibhu bho afya bhose ya gwikala na afya ya wiza na wikaji bhulihu.

Lushugu lumo, aho bhalyaga aganomba ntumami okwe ang’wenhele minzi ga gung’wa. Untumami uyo agamana hape gete igiki Kisho alatogilwe gung’wa minzi umo glasi uyo ilinsafi na idina jika.

Umtumami agang’wenhela minzi umu glasi nsafi noi. Aho Kisho omala ugung’wa aminzi, agabhulucha ginhu jilebhe jigasagila umugati ya glasi yiniyo.

U Kisho agajikisia giki iginhu jinijo jali ighi lwa ngoku, wangu wangu agaja ku kusitali gujumhona Daktari. “Bhebhe daktari, nagang’wa minzi mabhi. Naliganikila giki nang’waga maghi ga ngoku. Hambo hambo naligulomba ugafunye wangu wangu amaghi genayo gafume umunda yane.

Udaktari agakumya noi ugwigwa mihayo yiniyo. Aganomela u Kisho. “Udizubhiza na bhuhangayiki. Nadiganikaga igiki uguding’wa na bhusatu bhose bhose.

Ulu ulading’we na bhusatu bhosebhose nzugu aha wangu wangu kugiki upandika bhulaguzi!” UKisho adazunije ubhulomeji bho ng’wa Daktari. Agang’wila u Daktali, “Bhuli nagalangwa kushule ihatari ya maghi ga ngoku. Ku yiniyo, nadizunilijaza nu bhebhe. Hambo hambo daktari itaga iyoudulile ugugafunya amaghi genaya ni lelo iyi, badala ya gulindila mpaga ntondo nandya gusata.”

“Nahene, jijaha ijidonge ja gung’wa, jibhili lushulu mara gadatu. Udulile guja kaya.” Agayomba udaktari.

Aho alimunzila ajile ikaya, u Kisho agiigwa giki umunda jigandwa gulunduma. Uding’wa wibhakizu. Bhukoyakoyi bhugendelea mpaga adahayile ugulwa ijiliwa ija mhindi yiniyo, nulu gung’wa minzi adagemile.

Aho oja gujulala adapandikile itula bhujiku pe alimiso. Aho wela du, Kisho agaja hangi kusitali. Aho daktari opandika ubhulomeji bhulihu gufuma kuli Kisho, agamana giki unsumba ng’wunuyo alina wibhakizu (hofu) noi.

“Jaga ugenhe kalishi (choo) na mine kugiki dudule gujipima, daktari aganomela u Kisho. Udaktari agakomeleja giki opimaga, gashi adapimile josejose.

Agashoka ukunu odimaga glasi yina ighi giti ilo ololibhona u Kisho uko kaya yakwe. Udaktari agang’wolekaja u Kisho iglasi yiniyo na gung’wila, “Lolaga aha ni lighi linilo ilo uliolibhona ilikanza ilo ong’waga minzi. Lwafumaga kunguno ya bhugota ubho ubhumilile. Ihaha udizubhiza na wibhakizu (hofu) hangi.  Jaga gukaya yako na bhuyegi.” “Lo! Obheja noi daktari,” agalumbilija u Kisho ukunu abhizile na bhuyegi bhutale. Agashoka kaya na gwendelea gwikala guti kawaida bho nduhu wibhakizu (hofu).

Udaktari uyo ulu nadatumilile maarifa ga gung’wingija ihofu, Kisho niwendelea gusata ikanza ilihu mpaga gwenheleja nulu gucha kulo hofu.

Kiswahili: Hofu Huleta Mauti

Zama hizo kulikuwa na kijana mmoja aliyeitwa Kisho. Kijana huyo alikuwa na maarifa sana. Baba yake alijulikana kwa jina la Mapali, alimpenda sana Kisho. Alimpeleka mwanaye shule ili apate kusoma.

 Kisho aliifurahia sana nafasi ya kwenda kuelimika shuleni. Alipohitimu vizuri elimu ya msingi alichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari. Alifanya vizuri katika masomo yake hadi alipohitimu kidato cha nne.

Aidha alikuwa ni kijana aliyejipenda sana kwa usafi wa mwili na mavazi, daima alikuwa mtanashati kweli kweli. Alikuwa na tabia ya kuzingatia kanuni zote za afya kwa ajili ya kuishi na afya bora na maisha marefu.

Siku moja, wakati anapata chakula, Kisho alimwomba mtumishi wake ampatie maji ya kunywa. Yule mtumishi alifahamu wazi kabisa kuwa Kisho alipenda kunywa maji katika glasi safi isiyo na doa.

Mtumishi huyo alimletea  maji katika glasi safi sana. Baada ya Kisho kuyanywa aligundua kitu fulani kilibaki ndani ya ile glasi. Alihisi kuwa kile kitu kilikuwa ni yai la konokono,  haraka akaenda hospitali kuonana na daktari. “Bwana daktari, nilikunywa maji machafu. Nahisi nimemeza mayai ya konokono. Tafadhali nakuomba uyatoe haraka mayai hayo kutoka tumboni mwangu.”

Daktari alishangaa sana kusikia maneno yale. Akamweleza Kisho, “Usiwe na wasiwasi. Sidhani kuwa utashikwa na ugonjwa wowote. Endapo utashikwa na ugonjwa wowote njoo hapa haraka ili upate matibabu!” Kisho hakuamini maelezo ya daktari. Akamwambia yule daktari, “Mbona nilifundishwa shuleni hatari ya mayai ya konokono. Kwa  hiyo, sikubaliani nawe. Tafadhali daktari fanya kila unaloweza kuyatoa mayai hayo leo hii, badala ya kungojea hadi nimeanza kuumwa.”

“Haya, hapa ni vidonge vya kumeza, viwili kutwa mara tatu. Unaweza kwenda nyumbani.” Alipokuwa njiani kurejea nyumbani, Kisho alisikia tumbo lake likianza kuunguruma. Akashikwa na hofu.

Wasiwasi huu uliendelea hata hakutaka kula chakula jioni ile, wala kunywa maji. Alipokwenda kulala, hakupata lepe la usingizi usiku kucha. Kulipokucha tu,  Kisho alikwenda tena hospitalini. Baada ya daktari kupata maelezo marefu kutoka kwake, alitambua kuwa kijana huyo alisongwa sana hofu.

“Nenda kalete choo na mkojo ili tuweze kuvipima,” daktari alimwelekeza Kisho. Daktari alisingizia kuwa amepima, kumbe hakupima chochote. Akarudi huku ameshika glasi yenye yai kama lile aliloliona Kisho kule nyumbani kwake. Daktari alimwonyesha Kisho ile glasi na kusema, “Tazama hapa ni lile yai ulilolimeza wakati ukinywa maji. Limetoka kwa sababu ya zile dawa ulizomeza. Sasa usiwe na hofu tena. Nenda nyumbani kwako kwa furaha.” “Lo! Asante sana daktari,”  Alishukuru Kisho huku akiwa na furaha kubwa. Akarudi nyumbani na kuendelea kuishi kama kawaida bila hofu.

Kama daktari yule asingetumia maarifa ya kumtoa hofu, Kisho angeendelea kuugua muda mrefu hata kusababisha kufa kwa hofu.

FEAR CAUSES DEATH

There was a young man named Kisho. Such a young man had a lot of knowledge and skills. His father was known as Mapali. The father loved Kisho very much. When school going age, his father took Kisho to school.

 Kisho enjoyed the opportunity for going to school very much. When he completed primary education, he was selected to join secondary education. He did well in his studies until he graduated at Form Four level of education.

In addition, Kisho was a very young man who loved being smart and clean. He was always smart. He had a tendency to adhere to all health principles. He liked health living and long life.

One day, when he got food, Kisho asked his servant to give him a drink of water. The servant knew very well that Kisho liked to drink water in clean glasses.

The servant brought water in very clean glasses. After Kisho drank, he found something left in the glass. He felt that something was like the snail’s egg, quickly went to hospital to see a doctor. “SDoctor, I drank dirty water. I feel screaming snail eggs in my stomach. Please, hurry up, take these eggs from my stomach.”

The doctor was very surprised to hear the words. Then he told Kisho, “Don’t worry. I don’t think you will get any disease. If you get any illness, come here quickly for treatment!” But he did not believe the doctor’s explanation. He said to the doctor, “I have been taught at school the danger of snail eggs. So, I disagree with you. Please do whatever you can to remove these eggs today, rather than waiting until I get ill.”

“Here, here are tablets for swallowing, two to three times. You can go home”, the doctor instructed him. On his way home, Kisho heard his stomach starting to ache. He was very terrified.

This concern continued. In the evening, he did not want to eat food.  He did not want to drink water either. When he went to bed, he could not sleep all night. Just before dawn, Kisho went back to hospital. After the doctor had received a long explanation from him, he realized that Kisho was only scared.

“Go to the toilet and bring your urine so that we can examine it,” the doctor told Kisho. The doctor pretended to have tested the urine. He came back holding a glass containing egg mixed with water. The doctor showed Kisho the glass and said, “Look, here is the egg you swallowed when you drank water. It has come out because of the medication you are taking. Now don’t be afraid again. Go home happily.” “Oh! Thank you very much doctor,” he thanked Kisho, with great excitement. He returned home and continued to live as usual without any fear.

If the doctor did not use the knowledge of giving fear, Kisho would continue to be sick for a long time even causing death.

comic-

 ENGLISH: FEAR BRINGS DEATH (FEAR LEADS TO DEATH)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.