104. Wikumbwa/Bhulaku Bhubhi (Tamaa/Uroho Mbaya)

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Aho kale agikala munhu umo lina lwakwe Lambwe. Munhu ng’wunuyo a-oliontola nkima o chalo ja kule. Yahaiyagwa giki u Lambwe adadulile ugupanke nkima ogutola umuchalo jakwe.

Olina jika jakwe. Oli atogilwe noi ugulwa nyama. Ulushugu ulo opandikaga nyama ohagigishaga igiki aliilya pye wei ng’winikili. Lambwe wiimililaga wei ahikanza ilizugwa inyama iniyo, ku giki adizigela munhu ose ose oguikumya nulu haho itali ugupya.

Makanza gose u Lambwe ozubhulaga inyama ijitinile manofu haho yandya gupya du wandya gujidakuna bho bhulaku bho gukumya. Abhabehi abho bhikalaga bhuzenganwa na bhabyaji bha ng’wa Lambwe bhagaduma gete ugung’wambilija unsumba ng’wunuyo.

Giko, inhungwa jakwe ijabhubhi jigamanyika bhuli kuli munhu uomu chalo jinijo. Mpaga oho okula wikoma gutola, bhuli ng’wenu uyo agang’wisonga agannema.

Aho obhumana ubhubhi bho nhungwa jakwe, agiyangula gujutola kuchalo ja bhuzenganwa. Gashi nu mu chalo ja bhuzenganwa inhungwa jakwe jali jimanyikile.

Lambwe iganhadikija gusunga lugengo lo guja kule uko agwigela giki ali ngeni gete. Agakoyakoya mpaga ku si ngeni ndebhe, uko agang’wisonga ng’waniki uyo witangwa Mugoli.

Ukubhu nghana Mugoli oli ng’waniki nsoga na o likujo na nhungwa ja wiza. Bhagizunilija gwitola. U Lambwe aho oshoka umu chalo jakwe kihamo na nke okwe u nsoga, gugabhibhakija bhanhu bhingi.

Olinduhu nulu umo umu chalo jakwe uyo wiganikaga giki u Lambwe niodula guntola nkima nsoga giti Mugoli! Wikaji bho ng’wa Lambwe na Mugoli bholi bhusoga na bhanhu bhagakumya pye.

Uwikumbwa bho ng’wa Lambwe ubho guhaya gulwa inyama yose bhugendelea. “Wifunya bhukindile bhusese”, Mugoli adadililile noi inhungwa ja ngoshi okwe kulwa nguno jalinduhu jika jingi umu witogwi bhobho.

Nose bhagapandika bhana bhadatu. Bhuli ng’wana ulu okula, oshiga bhukuji bhulebhe, ochalagwa gujumanyichiwa kuli guku obho. Unimo gogubhachala abhana bhanabho goli go ng’wa Lambwe.

Lambwe obhachala bho ndima abhana bhakwe ukuli nkwiye. Inzila ya guja kunuko igabhita ng’wipolu lya ndimu nhali. Lushigu lumo, Lambwe agaja gujubhagisha bhakwiye, aho oshika koi, agamana igiki ung’wana okwe uumo alianogile ugwikala aha kaya ya ng’wa guku na mama okwe. Agandya gulila. Lambwe agiyangula gushoka nawe.

Aganomba umayu bhukwi jiseme ja gubhukija jiliwa na jifaa jingi ja ng’wanokwe. Mayu bhukwi agamegelegeja bhuli ginhu. Lushigu lo kabhili dilu, Lambwe agandya lugendo lokwe ukunu amukije ung’wanokwe ku ngongo. Ali adibhile ugubhucha inhome, ichimu ni panga.

Aho oshika ung’wiporu linilo agigwa malaka ga noni jilimba ulu luli lumengho lwa giki jabhonaga ndimu. Agogoha noi mpaga wikumbwa gushoka uko ofumaga.

Kihamo ni yiniyo adashokile inuma, kulwa nguno ulugendo lokwe lolilomala mapande adatu ga lugendo, lyalilyasaga ipande limo du mpaga ashige ku kaya.

Agendelea na lugendo lokwe na ukunu inoni jinijo jilongeja guyoganya malaka. Aho olola lwande lumo lo nzila, agibhona Mboku ilalile. Ujipeja inoni jinijo, wiyegela ndimu yiniyo.

Igwandya wiganikaga giki imboku yiniyo yaliilalile oganoga umana igiki gashi yali yamala gucha ikanza idili lihu ilo lyabhitaga. Ku yiniyo, indimu yali itali ugundya ugubhola.

Agandya gwita lusona kuti nu bhulaku bhokwe ubhobholibhomtema umu nyama. Agasola panga yakwe na gutina linofu litale iliginu, agalituula lwande. Lambwe oladamanile igiki imboku yiniyo yaliyabhulagwa na shimba.

Gashi aho likanza alitina inyama yiniyo, ishimba yaliifulile hambeho aho yamalaga gwiguta. Ninga iki yalidikule ugufuma ahenaho, aliyo u Lwambwe adibhonile.

Ninga ulu nioibhona wangu nadagemile ugwegela aha nyama ya mboku yiniyo. Ahenaho, U Lambwe agang’wicha ung’wanokwe na gung’wigasha hasi ukunu uwei ng’winikili agachola manti ga gubegesa moto. Aho obhiza kule hadoo inoni ijo jigashoka na guyoganya umu nyama na gwandya guigombagula inyama yiniyo.

Ishimba nayo igakolwa ugubhona giki inoni jinijo jiliichafula inyama yayo yiniyo. Wangu wangu, ishimba igaja gujujipeja inoni na gwendelea kuilya inyama.

Ung’wana o ng’wa Lambwe bho nduhu gumana agiyegela ishimba bho nduhu bhobha, na gwandya guibabasha giti umo umunhu agibabasijaga imbwa.

U Lambwe aho oshoka ahenaho agibhakila uguibhona ishimba yigundamilaga guidakuna inyama yiniyo. Agahugana ugumona ung’wana okwe aliibabasha ishimba ukungongo bho nduhu bhobha.

U Lambwe agading’wa na lutuga. Adamanile ijagwita. Aho ohaya gung’wegela ishimba igalunduma na gumpeja gitumo yajipegejaga inoni. Ung’wanokwe adibhakile, agendelea du uguibabasha ukungongo.

Ishimba yalidinawasiwasi bhosebhose nu ng’wana ng’wunuyo. Ishimba igendelea gumpeja u Lambwe, nanghwe odubukaga nhambo. Agabhona niyabhiza jidamu ugudula gwibhulaga ishimba yiniyo wei bhung’wene.

Aho oli kule hadoo Lambwe agandya gung’witana ung’wanokwe. Aho ung’witana kuli likanza lilihu, ung’wana agang’wigwa ubhabha okwe huna ugandya gung’wegela.

Aho obhona giki ung’wanokwe aliza, Lambwe agaigwa ingholo yakwe ilitinhinha na bhuyegi. Ikanza iguhi ung’wana agang’wegela, aganfefula na gumhucha kungongo. Wangu wangu agandya lugendo akajije wangu wangu guja kaya. Makanza gose omanaga ulabhula na gulalo inyuma kugiki gumana ulu idanondejije ishimba.

Aho oshika ikaya, unke agakumya aho omona ungoshi adina jilanga nulu jibhukijo ja ng’wana. Aho atali aleshema kubhobha ubho alinabho bhundimilile na ku bhunoge bho lugendo na nzala, Lambwe agandya kunomela unke okwe, pye iyose iyo igampandika umu legendo lokwe. Unke agading’wa na bhukoyakoi na agang’wila ungoshi alekane nu bhulaku bho gulwa nyama bho sagala giti umo yali uko numa.

Kiswahili: Tamaa/Uroho Mbaya

Hapo Zamani palikuwa na mtu mmoja, jina lake Lambwe. Mtu huyo, alikuwa amemuoa mwanamke wa kijiji cha mbali. Inasemekana kwamba Lambwe hakuweza kupata mchumba katika kijiji chake. Alikuwa na kasoro yake, Alipenda mno kula nyama. Siku akipata  nyama, alihakikisha kuwa anaila yote yeye peke yake.

Lambwe alisimamia wakati inapikwa nyama ile, ili asiwepo mtu ye yote wa kuigusa hata kabla haijaiva. Daima Lambwe alichopoa vipande vya nyama mara tu inapoanza kuiva na kuitafuna kwa uchu wa ajabu.

Jamaa wakiokuwa wanaishi jirani na wazazi wa Lambwe walishindwa kabisa kumsaidia kijana huyo. Hivyo, tabia yake mbaya ilijulikana na kila mmoja katika kijiji.

Hata alipopata umri wa kuoa, kila liyemchumbia alimkataa. Lambwe alipotambua utovu wa tabia yake, aliamua kwenda kuoa kijiji cha jirani. Kumbe hata katika vijiji vya jirani habari zake zilisambaa.

Lambwe ilimpasa kufunga safari ya mbali ambako ataonekana ni mgeni kabisa. Alihangaika hadi nchi ngeni fulani, huko alimchumbia msichana mzuri aliyeitwa Mugoli.

Kwa kweli Mugoli alikuwa mrembo na mwenye adabu na tabia nzuri. Wakakubaliana na kuoana. Lambwe aliporejea kijijini kwake pamoja na mke wake mrembo, kuliwashtusha watu wengi. Hakuna hata mmoja pale kijijini alifikiri kuwa Lambwe angeweza kumwoa mwanamke mzuri kama Mungoli! Maisha kati ya Lambwe na Mugoli yalikuwa mazuri na yakawastaajabisha wote.

Tamaa ya Lambwe ya kutaka kula nyama yote iliendelea. Hiari yashinda utumwa, Mungoli hakujali sana tabia ya mumewe kwa sababu vinginevyo hapakuwa na kasoro nyingine katika mapenzi yao.

Hatimaye, walijaliwa kupata watoto watatu. Kila mtoto alipofikisha umri fulani, alipelekwa kutambulishwa kwa babu yake, jukumu la kuwapeleka watoto  hao lilikuwa la Lambwe.

 Lambwe aliwapeleka kwa zamu watoto wake kwa mkwewe. Njia ya kwenda huko ilipita katikati ya pori lenye wanyama wakali. Siku moja, Lambwe  alikwenda kuwasalimia wakwe zake, alipofika  huko, aligundua kuwa mtoto  wake mmoja alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwa babu na bibi. Alianza kumlilia, Lambwe akaamua kurudi naye.

Akamwomba mama mkwe chombo cha kubebea chakula na vifaa vingine vya mwanae. Mama mkwe alimtayarishia kila kitu. Siku ya pili asubuhi, Lambwe alianza safari yake akiwa amembeba mwanae mgongoni. Aidha, hakusahau kubeba rungu, mkuki na upanga.

Alipokuwa katika pori lile alisikia sauti ya ndege wakiimba ikiwa ishara kuwa walimwona mnyama. Aliogopa sana hata akatamani kurudi alikotoka. Hata hivyo hakurudi nyuma, kwani safari yake ilikuwa imefikia robo tatu na ilibakia robo moja tu hadi awasili nyumbani.

Aliendelea na safari yake na huku wale ndege wakiongeza kupaza sauti. Alipoangalia upande mmoja wa njia, alimwona Pofu amelala. Akawafukuza wale ndege, akamsogelea yule mnyama.

Awali alifikiri kuwa pofu yule alikuwa amelala, lakini baadaye  aligundua kuwa kwa kweli alikuwa amekufa si muda mrefu umepita. Kwa hiyo nyama yake ilikuwa bado kuoza.

Mate yakaanza kumdondoka kama uchu wake ulivyomtawala akiona tu nyama. Alichukuwa upanga wake na kukata kipande kikubwa sehemu iliyonona, akaiweka kando.

Lambwe hakufahamu kuwa yule Pofu alikuwa ameuawa na simba. Kumbe wakati akiwa anakata ile nyama, simba alikuwa amejipumzisha kivulini baada ya shibe. Ingawa hapakuwa mbali kutoka pale, lakini Lambwe hakumwona. Laiti angemwona mapema asigethubutu kuusogelea ule mzoga wa pofu.

Hapo, Lambwe akamteremsha mtoto wake na kumkalisha chini huku yeye mwenyewe akienda kutafuta vijiti vya kupekechea moto. Alipokuwa mbali kidogo wale ndege wakarejea na kupiga kelele kwenye ule mzoga na kuanza kudonoa ile nyama. Simba naye alikasirika kuona kuwa wale ndege wakiichafua ile nyama yake. Haraka, simba alikwenda kuwafukuza wale ndege na kuendelea kula nyama.

Mtoto wa Lambwe bila  kujua alimsogelea Simba bila woga, na kumpasapasa kama vile binadamu anavyompapasa Mbwa. Lambwe aliporejea pale alishitushwa kumwona simba ameinamia kutafuna ile nyama.

Alichanganyiwa alipomwona mtoto wake anampapasa Simba mgongoni bila woga. Lambwe akashikwa na kiwewe. Hakufahamu la kufanya. Alipotaka kumsogelea, Simba aliunguruma (alifoka) na kumfukuza kama alivyofukuza ndege.

Mtoto wake hakushituka, bali aliendelea tu kumpapasa mgongoni. Simba hakuwa na wasi wasi wowote na yule mtoto. Aliendelea kumfukuza Lambwe, naye alikuwa akifyatua mbio.

 Aliona ingekuwa vigumu kuweza kumwua yule Simba peke yake. Alipokuwa mbali kidogo Lambwe alianza kumwita mtoto  wake. Baada ya kumwita kwa muda mrefu, mtoto alimsikia baba yake ndipo alipoanza kumsogelea.

Alipomwona mtoto wake akija, Lambwe aliusikia moyo wake ukimdunda kwa furaha. Mara mtoto alipomkaribia, alimyakua na kumbeba mgongoni. Hima akaanza safari chapuchapu kwenda nyumbani. Daima alikuwa akigeuka na kuangalia nyuma ili kuona kama Simba alimfuata.

Alipowasili nyumbani, mkewe alishangaa alipomwona mumewe hana silaha wala mbeleko. Akiwa bado anahema kwa hofu iliyomwandama pamoja na uchovu wa safari na njaa, Lambwe alianza kumweleza mkewe kisa chote kuhusu yale yaliyowapata katika safari yao. Mkewe alishikwa na mfadhaiko na akamkanya mumewe kuachana na uchu wa kula nyama kwa pupa kama ilivyokuwa huko nyuma.

mammal-

English: Bad Desire/Greed

black-

 

BAD DESIRE/GREED KILLS

In the past, there was one man whose name was Lambwe. Such a man had married a woman from a far away village. It is said that Lambwe could not find a girl in his home village. He had his one defect. He loved meat very much. Whenever he found meat, he made sure that he ate all of it alone.

Whenever meat was cooked, Lambwe was in charge. He could closely observe so that no one could touch the meat even before it was cooked. Lambwe always handled the pieces of meat as soon as it began to be cooked. He could grab it with a strange desire.

Relatives living near Lambwe’s parents were unable to help the boy deal with that greed. This strange behaviour was known to everyone in the village.

When he wanted to get married, everyone refused him. When the Lambwe realized his behavior was not accepted, he decided to go to a nearby village. Even in the neighbouring villages his bad news about him spread.

Lambwe had to travel to a distant place where he was a stranger. He struggled until he finally married a beautiful girl named Mugoli.

Mugoli was beautiful and courteous and well behaved.. When Lambwe returned to his village with his beautiful wife, he shocked many people. No one in the village thought that Lambwe could marry a beautiful woman like Mugoli! The life of Lambwe and Mugoli was beautiful and wonderful.

Lambwe’s desire to eat all the meat continued. Optionally conquered slavery, Mugoli did not care about her husband’s behaviour because otherwise there were no other defects.

Finally, they were blessed with three children. When each child reached a certain age, he was taken to the village to be introduced their grandfather. The responsibility of taking the children to the village was Lambwe’s.

Lambwe took his children to his mother-in-law in shifts. The way to the village went through a a big forest with wild animals. One day, Lambwe went to greet his parents–in- law. When he got there, he found out that one of his children had been tired of living with grandparents. He started crying. Lambwe decided to bring him back.

He asked his mother-in-law something for carrying food and other items for his son. His mother-in-law prepared everything for him. The next morning, Lambwe started his journey,carrying his son on his back. In addition, he did not forget to carry a club, a spear and a sword as was the custom.

When he was in the wilderness, he heard the voice of the birds singing as a sign that theyhad seen a beast. He was so frightened that he wished to go back where he came from. However, he did not go back, as his journey had reached three quarters and only one quarter remained for him to  arrive home.

He went on his way with the birds singing even more loudly. As he looked on one side of the rpath, he saw an eland lying.  He drove out the birds, and came to the beast.

At first, he thought that the animal was asleep. But sooner or later he found that it was actually dead not long ago. So his flesh had not yet decayed.

Lambwe started salivating. He took his sword and cut a piece of that fat eland, and put it aside.

Lambwe did not know that the eland had been killed by the lion. But when Lambwa cut the meat, the lion had rested in the shade after eating enough. Although it was not far from there, but Lambwe did not see it. If he had seen it before, he would not have dared to move to the carcass of the eland.

There, Lambwe dropped his baby and laid him down while he was looking for fire sticks as he wanted to make fire in order to roast the eland’s meat. From a distance the birds returned and shouted at the carcass and began to draw the meat. The lion was also angry to see that the birds were defiling its flesh. Immediately, the lion went to chase the birds and continued to eat meat.

Lambwe’s child did not know to approach the lion with fear, and he kept touching the lion as he touches a dog. When Lambwe came back, he was shocked to see the lion chewing the meat.

He was confused when he saw his son touching the lion on the back without fear. He was caught in trauma. He did not know what to do. When he wanted to move, the lion roared ( angrily) and dismissed him as he drove away the birds.

His child did not panic, but he just kept touching the lion on its back. The lion had no trouble with the baby. The lion continued to chase Lambwe whenever he came closer.

 Finally, Lambwe realized that it would be impossible for him to kill the lion alone. Lambwe then decided to call his son from a far. After calling him for a long time, the child heard his father and he slowly approached oblivious of the danger that surrounded them.

When he saw his son coming, Lambwe felt his heart beating with joy. As soon as the child reached him, he snatched him and carried him on his back. He hurriedly started going home. As he walked home, he was always turning back and looking behind to see if the lion was following him.

When he got home, his wife was surprised to see him without weapons and without  a piece of cloth for carrying the child with. While he was still filled with the fear and the fatigue of the journey, Lambwe started to tell his wife all about what had happened on the journey back home. His wife was depressed and she warned her husband that he should stop his excessive desire for eat meat.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.