105. Wikumbwa bhugabhulagaga

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Oliho munhu umo, mu chalo jilebhe uyo otegaga  ndimu bho gutumila waya. Lushugu lumo uningi ng’wunuyo agasanga yapujiyagwa mhala na yaliyamala gucha.

Aho waitaligulila uwaya ubho bholibhoibhulaga, aha mhelo yaho agagabhona mashi madoto ga mbogo. Uningi ng’wunuyo agaileka imhala yakwe, na wandya gugalondeja amabhondo ga mbogo.

 Ubhulingisilo bhokwe bholi giki, ulu niodula guipandika niwandya guipeja, na ku namna yose iki mbogo nayo umo ili nhali, ni yanondeja na gumpeja.

Uningi ng’wunuyo agiyamini giki agupela lugendo lukali giki mpaga imbogo nidadulile ugumpandika. Huna niobhita ahenaho aha ntego gokwe, ku giki ndimu yiniyo uluyashiga aha ntego gokwe niyapujiwa.

Aho oja lugendo luguhi, ohaimanila otung’wana bhilolile ni mbogo. Imbogo igandya gunkalihila uningi ng’wuniyo. Gashi uningi uyo aladabhejije imipango yakwe jisoga.

Aho obhona giki imbogo yabhunja bho wangu wangu, uningi agapelela mulinti ku giki ugulinhe apandike gupila. Imbogo igapelela wangu wangu na ku bhukali aho olili yugansanga alikoyakoya gulinha mulinti na gunshindika kule, aliyo idamulagile.

Bhasi, imbogo aho inga uningi widuta guja kaya bho nduhu gubhita gujusola untego gokwe, imhala. Aho jabhita shigu idatu, ihali yakwe yubhiza yabhipa noi, ulushugu ulo katano agazumalika musi.

Abha kale bhagahayaga giki, munhu ilinhadikija gurizika nijo uliojipandika, kukila gubhiza na wikumbwa bhutale. Uyo ahaile yose agagaiyagwa yose.

KISWAHILI: TAMAA HUUA

Kulikuwa na mtu mmoja katika kijiji fulani ambaye alikuwa akitega wanyama kwa kutumia nyaya. Siku moja mwindaji huyo alikuta amenasa paa na tayari amekwisha kufa. Baada ya kumfungua waya uliomuua, pembeni aliona kinyesi kibichi cha Nyati. Mwindaji huyo akamwacha paa wake pale na kuanza kufuata nyayo za Nyati.

Lengo lake lilikuwa kama angeweza kumkuta angeanza kumkimbiza, na kwa vyovyote vile naye nyati alivyo mkali angemfuata na kumkimbiza. Mwindaji alijiamini kuwa atakimbia mwendo kasi sana hata Nyati asingeweza kumkuta. Ndipo angepita pale kwenye mtego wake, ili Nyati yule atakapofika kwenye mtego wake ungemnasa.

Baada ya mwendo mfupi, ghafla akakutana na yule Nyati uso kwa uso. Nyati akaanza kumfokea yule mwindaji. Kumbe mwindaji huyo hakusuka mipango yake vizuri. Alipoona Nyati anamkimbiza kwa kasi, mwindaji alikimbilia kwenye mti ili akwee apate usalama. Nyati alikimbia kasi na kwa hasira hadi pale alipokumkuta anatapatapa kuukwea mti na kumsukumiza mbali, lakini hakuuawa. Basi,  Nyati aliondoka, naye mwindaji akajikokota kwenda nyumbani kwake bila hata ya kupita kuchukua windo lake, yaani Paa. Baada ya siku tatu hali yake ikawa mbaya zaidi, siku ya tano alifariki dunia.

Wahenga wanasema kuwa mtu anapaswa kuridhika na kile alichokipata kuliko kuwa na tamaa nyingi. Mtaka yote hukosa yote.

buffalo

ENGLISH: GREED KILLS

There was a man in a village who was trapping animals by using wires. One day, the hunter found that he had trapped an antelope which was already dead. After unlocking the deadly wire of the trap, he saw fresh stool of the buffalo. The hunter left his antelope there and began to follow the footsteps of the buffalo.

His aim was to make the buffalo run after him while he could be running towards the trap. He thought that the buffalo would eventually be caught in the trap. The trapper was confident that he would run faster than the buffalo.

Within a short distance, he met the buffalo face to face. The buffalo began to chase the hunter. It appears that the hunter underestimated the risk that was ahead of him. When he realized the buffalo ran faster that he estimated, the hunter ran to a tree to save his life. The buffalo reached him trying to climb the tree. The buffalo attacked him but he did not die.

Theafter, the buffalo left and the hunter went to home without even taking his meat of the antelope that he had trapped. After three days his condition worsened, and on the fifth day he died.

The sages have it that one should be satisfied with what he has earned and should not have have much desire. The one who wants all, misses all.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.