102. Mayu Njomba Na Ng’wanokwe

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Jaliho chalo jimo umo wikalaga munhu na nke okwe. Bhanhu bhingi bhagantogwa unke okwe ku kajile kakwe ka wiza nihanga lwakwe isumba. Uwikaji bho bhanhu abhabhili bhenobho bholi wiza na bho nduhu jika jose jose.

Unhimo gobho ugutale guli ilima, kihamo na nhimo uyo, abhanhu bhenabho bhasugaga mitugo na, hangi bhali na nhimo go bhulingi umu makanza malebhe aga ng’waka.

Umayu agaja kungunda gujulimila, ungoshi agaja ng’wipolu gujulinga. Bhuli lushugu oshokaga ahakaya na nyama na yagutosha gulila. Ku yiniyo, numba yabho idagaiwe jiliwa ja nyama nulu kamo.

Lushugu lumo dilu, bhabha agafuma guja gujulinga kudi na kadijile kakwe. Agalinga na gubhulaga nyama, aho obhiza alishoka ku kaya yake, agatung’wana na Shimba umunzila.

Ku bhuhodari bhokwe agikenya ni shimba yiniyo kwi kanza lilihu. Shimba igaminya na gung’witila malonda mingi umumili. Aliyo ku bhuhodari bhokwe umunhu ng’wunuyo agadula gwibhulaga ishimba yiniyo. Mininga mingi gagafuma, mpaga agaduma uguja, agaduma mpaga uyoganya. Agachola lwande bihi na henaho wilaja na gulwala.

Unke okwe aho obhona giki mhindi yingila na ngoshi okwe adigelaga agabhiza na mashaka, ubhitana abhazenganwa na gubhawila inhulu ja ngoshi okwe.

Bhanhu pye bhagikuminga bhandya gunchola. Bhagafuata inzila iyo oyibhitilaga bhuli lushugu. Aho bhashiga aho aliwikeneja ni shimba, bhandya gubhona mhengho ja mininga, bhadasegenelile, bhibhona ishimba ilalile umimba goyo ha lwande na nzila.

Bhagiyegela ku bhobha, bhaliganika giki ili mhanga. Aho bhayiyoganija ishimba igendelea kulala du na idibhakilile, nose bhumana igiki yali ichile.

Hali yiniyi igabhatinbya ngholo, bhagandya gunchola ung’wichabho. Hamhelo hadoo ya shimba yiniyo bhagansanga ung’wichabho ali nsatu gete. Aho bhagema ugunyombya, agaduma ugubhashogeja mhayo.

Bhagamhucha gunchala kuli nfumu. Unfumu agikomeja gunhagula, aliyo agaduma. Umunhu ng’wunuyo nu lushugu lunulo agazumalika. Unke agasunduhala noi na agalia ku jisoji jitale.

Ijililo jakwe jigakula ku nguno agalekwa alinchilwa umu hali ya bhudito. Ku nguno ya bhusunduhazu bhunubho, unkima ng’wunuyo agaduma uguyomba na munhu oseose.

Abhazenganwa bhagagema ugunyombya aliyo he! Adayombile hangi, bhuli ikanza aho ohayaga gulomba ginhu jilebhe otumilaga makono bho ishara du. Mpaka aho wifungula ng’wana okwe ngosha adayombile na munhu oseose nulu adayombile mhayo gose gose.

Wandikala ilina lwa ng’wanokwe agang’witana Nhekwa (mpina). Mpina agalanghanwa mpaga ubhiza ntale. Aho oshikila ikanza lwa kusoma shule, agachalwa agasome kihamo na bhana abhangi abho bhalibha mzengo gunuyo.

Agasomishiwa na gulipilwa ada na mayu okwe ku nguno ya ng’wa mayu ng’wunuyo ya gulugala uguyomba, aginhiwa lina lwa mayu njomba. Bhuli uyo agahaya gunomba ginhu, otongejaga lina lwa mayu njomba…Umayu ng’wunuyo agikala wikaji bhokwe kudi munhu ungi oseose. Ijika jakwe jali gukija guyomba du. Ung’wanokwe ulu ohaya ginhu otumilaga ishara du.

Bhuli lushugu aho otung’wana na bhiye ukushule bhanomelaga mihayo mingi higulwa bhamayu bhabho. Bhangi bhagahaya, mayu aganibhuja mambo mbalimbali ayo dugilanga ukushule, nagabhabhila pye na bhagayega noi.

Adamanile inguno iyo yang’wita umayu okwe abhize njomba. Bhuli ikanza aho agalomelwa ijenheleja ja ng’wa mayi okwe gubhiza na jika jinijo adishangile na guzunya gete.

Mpina ohayaga giki umayu okwe oladahayaga du uguyomba nawe, hangi wiganikaga giki umayu okwe adantogilwe. Bhuli ikanza aho oshoka gufuma kushule wikalaga na bhupina, na oladinabhuyegi nulu hado. Umayu unjomba ningiki obhizaga adayombaga, aliyo agagema kung’wolekeja ung’wana okwe hali ya bhuyegi. Ung’wanokwe agaduma uguimana ihali ya ng’wa mayu okwe.

Lushugu lumo umpina agiganika na gwiyangula giki hambohambo gucha gukila ugwikala umu hali ya jina chiniko. Aho wiganika noi agahaya gwinija, aliyo agabhona idichiza, halafu agagubhona nti nhihu na hangi gutale noi uyo golibihi na lilonga lilihu noi.

Agagulola unti gunuyo agabhona giki gusoga noi. Bhasi agiyangula gugulinha na halafu gwiponya mulilonga gufuma kwigulwa yaho. Aho agulinhaga, abhiye bhagamona kulwa nguno yali mhindi na pye bhalibhashokile kaya gufuma kushule. Hangi ku bahati ya wiza unti gunuyo guligudikule sana gufuma ku nzila iyo bhaibhitilaga, bhagamuja, “Mpina, ulita ki umunumo nti?” Umpina agashosha ku jilaka ja bhukali, “Nalihaya gwiponya mulilonga na gucha.”

“Kulwa nguno ki?” Bhagamuja. Ushosha, “Umayu one adanitogilwe, bhuli hene aho nahaya gung’wila ya kushule, guti umo bhalitila abhichane, adushoshaga ginhu, aliyo gwidika bho ntwe du. Ihali yiniyo ilinidacha noi, ihaha nalihaya nibhulage du.”

Abhiye bhagibhakila bhandya gushoka kuja gujung’wila ung’walimu obho. Ung’walimu oliatali ng’widalasa alimalija gusahihisha milimo ya bhana. Oli atali uguja ikaya, “jigela kiyi bhaning’wi?” Agabhuja.

Abhana bhanabho bhagang’wila, giki umpina ulinhaga munti nhihu alihaya gwiponya ng’wikolongo ache. “Nibhuli alihaya gwita chiniko?” Agabhuja. Oyombaga angu opelanaga kulwa nguno umayu okwe adantogagwa, adahayile uguyomba nawe. “Lo! Lo! Yikoye ili, nahene dujagi wangu wangu,” ung’walimu agayomba na kunu alihangaika ku bhobha na wasiwasi.

Habhali jigabhitiwa wangu wangu kubha ng’walimu bhose, ng’walimu úntale na bha ng’walimu bhiye, kihamo na bhana aho bhigwa, bhagapela bho wangu wangu noi bhajile ku nti gunuyo.

Aho bhashika ahenaho bhagabhasanga bhanhu bhingi noi bhikumingaga na bhuli umo obho olakalalile miso gwigulwa ya nti. Ung’walimu agishepeleja mpaka agashiga aha ishina lwa nti. Adegelile sana kulwa nguno ililongo linilo lwalilwagohya.

Ahasi ya lilonga linilo galihoi mawe mingi noi na gali mugi sana. “Mpina hambohambo ikaga wangu wangu ng’wanone,” ng’walimu okwe agang’wikumbilija.

Unene nadikaga nulu hado, niyangulaga gucha, na lelo hi nhalikilo yane. “Ehe, nalina ukunuko nti kugiki uniwile ilikoye lwako?” Ulu ulina du, unene niponya haho na haho! Hambo hambo ukije ugulinha, mpina agashosha.

Ung’walimu ng’wunuyo agikanika wangu wangu, agabhatuma bhana wangu wangu kujung’witana umayu okwe Mpina. Abhana bhanabho bhagapela  sana, bhagashika bhaganomela umayu njomba, inhulu jose. Nanghwe adadilile, aginga lukangala lumo.

Aho oshika ahenaho, agalangamila kwigulwa agamona ung’wana okwe, umpina. Amiso gabho aho galumana umayu njomba agalila jisoji, ningeki agamona Mpina, adayombile mhayo gosegose.

“Aha! Mayu nubhe wiza, ilelo ugwibhonekeja lufu lone guti umo ugibhonekeja ulufu lo ng’wa bhabha one,” Mpina agang’wila umayu okwe ku bhupina.

Umayu njomba adavumiliye, “Ng’wa—Ng’wa—na-na—ng’wanone, ika—ika—ikaga.” “Lo! Umayu njomba aliyomba,” abhana abhangi ahenaho hasi ya nti, bhashangilia ku yomba ningi. “Mayu uliyomba?” Mpina agabhuja ku bhuyegi. “Ehe, nalikulomba wike wangu wangu duje kaya.” Mayu ihaha nagwika wangu wangu.

“Unene nadufumula hangi.” Umayu unjomba, aganyegela u Mpina. U Mpina aho wigwa ilaka lwa mayu okwe, ku wangu wangu lukangala lo gwandya agika wangu wangu.

Aho oshika ahasi agampelela na gunkumbatila umayu okwe na kunu jisoji jilidika. Umayu okwe aganfumuja na bhagaja bhose kukaya yabho na bhuyegi. Bhanhu bhose bhagabhona ja gukumya ja ng’wa Mulungu. Gwandija lushugu lunulo Mpina agikala nu mayu okwe guti bhiye.

Kiswahili: Mama Bubu Na Mwanawe

Kulikuwako na  kijiji kimoja alichoishi mtu na mkewe. Watu wengi walimpenda mke wake kwa tabia yake nzuri na pia kwa uzuri wake wa sura. Maisha ya watu hawa wawili yalikuwa mazuri na yasiyo na kasoro yoyote.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kilimo, pamoja na kazi hiyo watu hawa walifuga wanyama na pia walishughulika na kazi ya kuwinda katika nyakati fulani za mwaka.

Mama anapokwenda shambani kupalilia, mumewe alikwenda mwituni kuwinda. Kila siku alirudi nyumbani na nyama ya kutosha kwa kitoweo. Kwa hiyo nyumba yao haikukosa chakula cha nyama hata mara moja.

Siku moja asubuhi Baba alitoka kwenda kuwinda kama kawaida yake. Aliwinda na kuua mnyama, alipokuwa anarejea nyumbani kwake, alikutana na Simba njiani. Kwa uhodari wake alipigana  na Simba yule kwa muda mrefu. Simba alimuumiza na kumtia majeraha mengi mwilini. Lakini kwa uhodari wake mtu yule alifanikiwa kumuua Simba yule. Damu nyingi zilimtoka hata akashindwa kwenda, alishindwa pia hata kupiga kelele, alitafuta mahali karibu na pale akajilaza na kuugua.

Mkewe alipoona kuwa jioni iliingia na Bwana wake hakuonekana alijawa na hofu akaalika majirani na kuwaeleza habari za mumewe. Watu wote walikusanyika wakaanza kumtafuta.

Waliifuata njia aliyokuwa akiitumia kila siku, walipofika mahali alipokuwa akipigana na Simba, walianza kuona alama za damu, na punde tu wakamwona Simba amekufa kando ya njia. Walimsogelea kwa woga, wakidhani kuwa yu hai. Walipompigia kelele Simba aliendelea kulala tu na wala hakushituka, mwisho walitambua kuwa amekufa.

Hali hii iliwatia moyo wakaanza  kumtafuta mwenzao. Kando kidogo ya Simba yule walimwona mwenzao yuko hoi kabisa. Walipojaribu kumsemesha, alishindwa kuwajibu neno. Walimbeba wakampeleka kwa mganga wa jadi.

Mganga alijitahidi kumtibu, lakini alishindwa. Na yule mtu siku ile ile akafariki. Mkewe alisikitika sana na kulia kwa machozi  makuu. Kilio chake kiliongezeka kwa sababu aliachwa mjane katika hali ya uja uzito. Kwa ajili ya huzuni zile, yule mwanamke alishindwa kusema na mtu yeyote.

Majirani walijaribu kumsemesha lakini wapi! Hakusema tena, kila alipotaka apewe kitu fulani alitumia ishara tu. Hata alipojifungua mtoto  wake wa kiume hakusema na mtu wala hakusema neno lolote. Aliandika jina la mtoto wake akamwita Mkiwa.

Mkiwa alilelewa mpaka akawa mkubwa. Alipofikia makamo ya kusoma shuleni, alipelekwa kusoma pamoja na watoto wengine waliokuwa wakitoka katika kijiji chao.

Alisomeshwa na kulipiwa ada na mama yake, kwa kuwa yule mama alifunga kusema, alipewa jina la mama bubu. Kila aliyetaka kumwomba kitu alitanguliza jina lake na kusema, mama bubu, naomba….

Mama yule aliendesha maisha yake kama mtu mwingine yeyote, kasoro yake kubwa ilikuwa ni kutosema tu. Mtoto wake alipomtaka kitu alitumia ishara tu.

Kila siku alipokutana na wenzake shuleni walimweleza mambo mengi kuhusu mama zao. Wengine walisema, mama aliniuliza mambo mbalimbali tuliyojifunza shuleni, nilimweleza yote na alifurahi sana.

Mkiwa hakujua sababu iliyomfanya mama yake awe bubu. Kila alipoelezwa kisa kamili cha kasoro hiyo hakuridhika wala hakuamini kabisa. Mkiwa alidhani kuwa mama yake hakutaka tu kuzungumza naye, pia alidhani hakupendwa na mama yake.

 Kila aliporudi  kutoka shuleni alikuwa mwenye huzuni na asiye  na raha hata kidogo. Mama bubu ingawa hakuwa anasema, lakini alijaribu kumwonesha mtoto wake hali ya furaha, mwanawe alishindwa kutambua hali ya mama yake.

Siku moja Mkiwa aliwaza na kukata shauri kuwa heri kufa kuliko kuishi katika hali ya namna ile. Baada ya kufikiri sana alitaka kujinyonga, lakini akaona si vema. Baadae aliuona mti mrefu na tena mkubwa sana uliokuwa karibu na genge refu sana.

Aliutazama mti ule akaona kuwa ni mzuri sana. Basi alikata shauri kuupanda na halafu kujitupa gengeni toka juu yake.  Alipokuwa anaupanda, wenzake walimwona kwa sababu ilikuwa jioni na wote walikuwa wanarudi nyumbani kutoka shuleni. Tena kwa bahati nzuri mti ule haukuwa mbali sana kutoka njia waliyokuwa wakipita, walimuuliza,  “Mkiwa, unafanya nini humo mtini?” “Nataka kujitupa gengeni na kufa.” Mkiwa alijibu kwa sauti  ya ukali. “Kwa sababu gani?” Walimuuliza, “Mama yangu hanipendi, kila ninapotaka kumweleza mambo ya shuleni, kama mnavyofanya wenzangu, hajibu kitu bali huitika kwa kichwa tu. Hali hii inaniudhi sana, sasa nataka nijiue tu.” Alieleza.

Wenzake walishituka wakaanza kurudi kwenda kumwambia mwalimu wao, mwalimu alikuwa bado yungali darasani anamalizia kusahihisha kazi za watoto. Alikuwa bado  hajaondoka kwenda nyumbani, “shauri  gani vijana?” Aliuliza. Watoto wale walimweleza, “Mkiwa amepanda mti ule mrefu anataka kujitupa  gengeni afe.” “Kwa nini anafanya hivyo?” Mwalimu aliuliza. “Amesema ati amekasirika kwa sababu mama yake hampendi, hataki kusema naye.” Watoto walieleza. “Lo! Lo! Hatari hii, haya twendeni upesi,” mwalimu alisema na huku akihangaika kwa woga na wasiwasi.

Habari zilipitishwa upesi upesi kwa walimu wote, Mwalimu mkuu, walimu wenzake pamoja na watoto waliposikia, walikimbia kwa haraka sana kuelekea kwenye mti ule.

Walipofika pale waliwakuta watu wengi sana wamekusanyika na kila mmoja wao alikuwa kakazia macho juu ya mti. Mwalimu alipenyapenya mpaka akafika shinani mwa mti, hakusogea zaidi maana genge lile lilikuwa linatisha.

Chini ya genge lile palikuwa na mawe mengi sana tena yenye ncha kali sana, “Mkiwa tafadhali shuka haraka mwanangu,” Mwalimu wake alimsihi. “Mimi sitashuka hata kidogo, nimekata shauri la kufa, na leo ndiyo mwisho wangu.” Mkiwa alijibu. “Je nipande huko mtini ili uniambie shida zako?” Mwalimu aliuliza. “Ukipanda tu,  mimi nitajitupa mara! Afadhali  usipande.” Mkiwa alijibu.

Mwalimu yule hodari alifikiri upesi, akawatuma watoto haraka kumwita Mama yake Mkiwa. Watoto wale walikimbia sana, walipofika walimweleza mama bubu habari zote.

Naye hakuchelewa, aliondoka mara. Alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwona mtoto wake Mkiwa, macho yao yalipogongana Mama bubu alilia machozi, ingawa alimwona Mkiwa, hakusema neno lolote.

“Aha! Mama nawe umekuja, leo utashuhudia kifo changu kama ulivyoshuhudia kifo cha baba yangu,” Mkiwa alimwambia Mama yake kwa uchungu. Mama bubu hakuvumilia, Mwa- – – – Mwa- – – -na – na- – mwana- – ngu, shu – – shu- -shuka. “Lo! Mama bubu anasema,” watoto wengine pale chini ya mti walishangilia kwa kelele nyingi. “Mama unasema?” Mkiwa aliuliza kwa shauku, “ndiyo ninakuomba shuka haraka twende nyumbani.” Mama bubu alisema. “Mama sasa nitashuka haraka.” Mkiwa alisema.

“Mimi sitanyamaza tena.” Mama bubu alimhakikishia Mkiwa. Mkiwa aliposikia sauti ya Mama yake kwa haraka mara ya kwanza alishuka haraka. Alipofika chini alimkumbatia mama yake na huku machozi tele yakimtoka, Mama yake alimtuliza na wakaenda wote nyumbani kwa furaha. Watu wote waliona maajabu ya Mungu. Tangu siku hiyo, Mkiwa aliishi na mama yake kama wenzake.

mozambican-women

 ENGLISH: DUMB MOTHER AND HER SON

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.