101. Ubhuhabhi Bhuli Bhone?

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Aho kale oliho munhu umo uyo uli na bhana bhatandatu. Aliyo, oli nhabhi na munhu o wikaji bho makoye. Mpaga ng’waka gumo ikaya yakwe igagaiwa imyenda ya guzala. Hangi nzala igabhisonga. Abhanhu abhangi bhamonaga kudi hali ya kawaida du ugubhiza na wikaji bhunubho.

Lushugu lumo umbehi ng’wunuyo agiyangula gujumana kugiki alekane na makoye ganayo. Agashiga ng’wipolu, agalinha mliti liliihu mpaga mumatambi galwo. Ghafula agilekala gugwa mpaga hasi kugiki ache.

Umbehi ng’wunuyo agagwa hasi puuu! Agasaga henaho ku likanza idoo, halafu agibhuja: “Naminyika?” Agashosha, yaya! Agakumya nibhuli adachile.

Aho wibhona giki atali alimpanga, agagungumka na gulina hangi mpaka hi gulwa ya matambi ga higulwa gete, na gwiponya hasi. Agagwa hangi puuu! Ni chiniko, adaminyikile nulu gucha gitumo aliwiyangulila.

Ohayimanila wigela munhu uyo obhizaga aguyelaga ng’wipolu linilo. Agamona alihaya gulina lukangala lo kadatu, agamuja, “Wina bhulingisilo ki ung’wigulwa ya nti nhihu gunuyo?

“Unene nalinhabhi na wikaji bhone bhuli bho makoye noi. Nalihaya gwibhulaga umu namalaga gulina mpaga ng’wigulwa ya nti gunuyo na gwiponya mpaga hasi na kucha.”

“Naligwikumbilija ndugu one, udizita chiniko gete nulu hadoo. Bokelaga ihela iji, udulile nulu gwita bhusuluja na gupandika matwajo, na giko ugwipandikila jako kihamo na bhana bhako.

Aliyo izukaga giki aho ulasabhe, nagwiza gusola untaji uyo nalinagwina bho nduhu kulomba jagongeja jose jose.

Ahanaho umunhu ng’wunuyo aganumbilija noi unfazili okwe na agaleka gete ubhulingisilo bhokwe ubho gwibhulaga. Aho alibhiza agushokaga kukaya yakwe alinago nu ntaji, agandya gwita bhusuluja.

Nanhana ubhusuluja bhokwe bhugazunya wangu wangu na agabhiza nsabhi. Huna agazenga numba nsoga na gugula ng’ombe. Agasabha noi.

Aho yabhita miaka ikumi, mfazili okwe agaja kugiki adule gunshokeja ihela jinijo ijo agang’winha kugiki wandije bhusuluja. Aliyo, adinhilwe. Unfazili ng’winuyo agendelea kunhomba mpaga igabhita miaka makumi abhili.

Naho yashika imyaka makumi abhili yiniyo, agendelea hangi, aliyo alatali alendelea guntula tarehe. Huna bhagishisha kumabhanza. Ubhulamuji ahabhofunyiwa iganhadikija gunshokeja ihaki yakwe kunhingo lwande.

 

 Kiswahili: Je, Umaskini Ni Wangu?

Hapo zamani palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na watoto sita. Lakini, alikuwa maskini na mtu mwenye maisha ya shida. Hata mwaka moja familia yake ilikosa nguo za kuvaa, pia waliandamwa na njaa. Watu wengine walimwona ni kama kawaida yake tu kuwa na maisha hayo.

Siku moja bwana huyo alijishauri kwenda kujiua ili aondokane na taabu hizo. Alipofika porini, akapanda juu ya mti mrefu mpaka kwenye matawi yake. Ghafla akajiachia na kuanguka hadi chini ili afe.

Bwana huyo alianguka chini puuu! Akabaki palepale kwa muda kitambo, halafu akajiuliza: ‘Nimeumia?’ Akajijibu, La! Alishangaa kwa nini hakufa. Baada ya kujiona kuwa bado yu hai, akainuka na kupanda tena hadi juu kwenye matawi ya juu kabisa, na kujitupa chini. Alianguka tena puuu!

Hata hivyo, hakuumia wala kufa kama alivyonuia. Mara alitokea mtu aliyekuwa anatembea mule porini. Alimwona anataka kupanda safari ya tatu, akamwuliza, “Una malengo gani  juu ya mti mrefu huu?’

“Mimi ni maskini na maisha yangu ni ya shida sana. Nakusudia kujiua baada ya kupanda hadi juu ya mti huu na kujitupa hadi chini na kufa. “Chonde sana ndugu, kamwe usifanye  hivyo hata kidogo. Pokea hapa fedha hizi Unaweza kuanzisha biashara na kupata faida, na hivyo kujipatia riziki yako pamoja na wanao.

Lakini kumbuka kwamba baada ya kutajirika, nitafika kuchukua mtaji niliokupatia bila ya kudai riba yoyote. Hapo yule mtu akamshukuru sana mfadhili wake na akaacha kabisa lengo lake la kujiua. Alipokuwa anarudi nyumbani kwake akawaza kuwa, alifika porini akiwa maskini lakini anarejea nyumbani akiwa na mtaji.

Akaanza kufanya Biashara. Ni kweli biashara yake ilichanganya na haraka akanza kuwa tajiri. Ndipo alijenga nyumba nzuri na  kununua ng’ombe. Akatajirika sana.

Baada ya miaka kumi kupita, yule mfadhili wake akaja ili aweze kumrudishia zile fedha alizomwezesha kuanzisha biashara. Lakini hakupewa.

Yule mfadhili aliendelea kumdai hadi ikapita miaka ishirini. Hata ilipofika miaka ishirini alimwendea tena, lakini bado aliendelea kumpiga tarehe. Ndipo wakafikishana mahakamani. Hukumu ilipotolewa, ilimpasa kumrejeshea haki yake kwa shingo upande.

male-

 ENGLISH: IS POVERTY MINE?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.